Tetesi: Bunge kupitia POAC, ingilieni NSSF inamufa

Tetesi: Bunge kupitia POAC, ingilieni NSSF inamufa

Walifashili miradi mikubwa na kuwekeza kwenye hiyo miradi wamilikisheni wadau wenu
 
Kuna ubabaishaji mwingi sana nssf nimekuwa mwanachama kwa miaka 19 sijawahi kufaidika na chochote kwenye mfuko huu. Nimepoteza ajira yangu sasa naangaika kupata fao la kukosa ajira kwa miezi minne nikusumbuliwa bila kupata chochote. Kila nikienda napangiwa tarehe ingine. Inauma sana aisee

Sent using Jamii Forums mobile app
Hawana pesa ya kukulipa wako hoi, majibu yao kwa miaka miwili sasa ni wako kwenye uhakiki!
 
Hela za wastaafu Ni nyingi kiasi cha wao kushindwa on time?
Ndivyo ilivyo hawana kitu, kilamwezi hutuma ujumbe kwa wastaafu wa kutoweza kulipa mpaka kabla ya mwezi kuisha, ila hawana uhakika wa tarehe! Maana wanategemea makusanyo.
 
Chadema wana hekima wapo 10 tu,wanaelemewa na wapumbavu 340 wa CCM wakiongozwa na mgonjwa wa akili Ndugai.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakuna mbunge yeyote anayejali wananchi wote lao moja na Ukitaka kujua hilo unakumbuka wakati maslahi yao ya posho yaliguswa wote wslichachamaa kupinga hilo jambo haikujulikana nani mpinzan wote waligeuka na kuwa kitu kimoja
 
Ni jambo lisiloeleweka kwanini Bunge kupitia kamati husika linashindwa kuichunguza na kuikagua NSSF ambayo kwa sasa ni mahututi. Kwa muda wa miaka miwili sasa NSSF imekuwa ikishindwa kuwalipa kwa wakati wastaafu, inachofanya kwanza ni kukusanya michango ya walio kazini (hand to mouth) ili iweze kuwalipa wastaafu. Katika miaka hii miwili NSSF imekuwa ikitumia kisingizio cha uhakiki, kabla ya hapo ilikuwa ikitumia kisingizio cha shirika la POSTA kuchelewesha malipo, hata hivyo sasa ni NSSF ndio wenye jukumu la kutoa malipo lakini wanashindwa.
Haitakuwa jambo jema Bunge kusubiri mpaka lione NSSF imekufa, wakati ni huu kabla mamia ya wastaafu hawajaathirika.
Nikisikia haya, nikalinganisha na sifa alizokuwa anamwagiwa bw. Dau! Hakika binadamu wa Afrika hii hatujafikia ubinadamu unaosemekana tunao. Bado tunateteana kwa dini, makabila, vyama vya siasa, n.k. Waliokuwa wanamtetea wote ni kwa sababu ya dini. Alipoondolewa ikawa eti anaonewa na wengine kuona ni dini yao inaonewa. Alisifiwa kwa elimu ya kutosha sana, leo hii ndo hiyo NSSF inavyokwenda. Huwezi ukasema ni kwa sababu ameondoka, ni kwa sababu alikuwepo na kufanya ufilauni huo.

Yaani kweli aliyestaafu akose mafao kwa sababu li-mtu limoja lilijiamini na kutapanya pesa za mfuko? KIla mradi wa nssf ulikuwa ni bei za ajabu.
 
Hii ni kazi ya SSRA. Nafikiri hawa jamaa wa SSRA wanatakiwa kuendesha ukaguzi maalum wa jinsi NSSF wanavyolipa mafao hasa kwenye mikoa ya Dsm, Mwanza, Kagera, Morogoro, Tanga na Dodoma. Watagundua madudu mengi sana aisee. NSSF imeoza mikoani.

Sent using Jamii Forums mobile app
Iko juu ya SSRA kwani waliochota hawawezi kuhojiwa na SSRA wako juu zaidi, ni bunge tu linaloweza.
Hata hivyo hakuna sababu kuwa na SSRA, ni kuongeza gharama za kiuendeshaji tukichukulia kuwa NSSF ina fedha za wanachama tu sasa badala ya wanachama kufaidika na pesa hizo zinapelekwa kuiendesha SSRA! Huku wanachama wakiishia kulipa mafao kidogo sana na ni aibu kulipa mtu chini ya laki moja!
 
Leo ni tarehe 27 January 2019 NSSF haijaweza kuwalipa wastaafu pensheni zao na kulingana na ujumbe iliyowatumia wastaafu haina uhakika wa tarehe ya kuwalipa! Kwa hali hii ni wazi hawana pesa.
 
Kwenye report mojawapo ya CAG aliyepita, ilionyesha kwamba mkataba kati ya Serikali na NSSF za mkopo wa kuijenga UDOM ni bilioni tano. Lakini zilizotoka ni bilioni 40. Hakuna aliyewahi kuhoji kwa nini zlitoka kinyume na mkataba. Ina maana hapo kuna fungu lilienda kwa watu, yaani walichota kupitia kisingizio cha ujenzi wa chuo.
Halafu Zito pamoja na ushujaa wake wa kuibua na kusambaza uozo wa serikali, ila kwenye mfuko wa NSSF hajawahi ibua wala kukemea lolote
 
Tarehe 27 January 2019 NSSF imetuma ujumbe kwa wastaafu wakajihakiki badala ya kuwafahamisha kuhusu malipo yao! Miaka miwili ya uhakiki wakidhani wazee hawana kumbukumbu.
Ninajiuliza kwanini wabunge wanaliogopa swala la NSSF ukizingatia pesa husika ni za wafanyakazi na waajiri wao, serikali haina pesa zake huko.
 
Hilo Ni kweli,mfano Ni machinga complex.Hatua inabidi zichukuliwe lakini pia serikali katika kuyafirisi haya mashirika haikwepi

Makonda kama kawaida yake anaanzisha mambo kwa kukurupuka, aliunda tume ya kuchunguza ule Mradi wa MACHINGA COMPLEX sijui matokeo yake aliyaficha wapi? Au ndio kama kawaida yake hiyo tume haikumaliza kazi?
 
Halafu Zito pamoja na ushujaa wake wa kuibua na kusambaza uozo wa serikali, ila kwenye mfuko wa NSSF hajawahi ibua wala kukemea lolote

Inawezekana kwasababu alipokuwa mwenyekiti wa PAC alikuwa anawekwa sawa na Ramadhani Dau!
 
Bunge lipi liingilie NSSF wakati ni Wabunge hao hao ndo wanaliua shirika kwa kukopeshana na kutokulipa madeni? Shirika linakufa pia kwa uzembe wa aliyekuwa anajiita Mkurugenzi wa SSRA, alichokuwa anakijua ni kuwabana wanachama wa mifuko wasifaidike na siyo kuangalia madudu yanayofanywa na mifuko

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom