Tetesi: Bunge kutengua azimio lake kesho na Jumatano kupokea ripoti ya CAG(?)

CWR2016

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2017
Posts
2,773
Reaction score
6,349
Aisee mambo yamepamba moto.
Ni hivi, vitisho mfulululizo vimekuwa vingi lakini mpaka sasa havijafua dafu. Heko CAG Prof. Assad kasimamia taaluma na kiapo cha katiba na msahafu.
Vyanzo vya kuaminika kabisa vinasema Rais ameshauriwa aipeleke ripoti bungeni ndani ya muda maana wamesema asipofanya hivo CAG Prof. Assad mwenyewe ataipeleka na hapo watu wataamini azimio ni lake.

Kibaya ni kwamba bwana mkubwa sasa kaagiza ripoti irekebishwe na kuondolewa kasoro kubwa zote alizobaini CAG ndo apeleke bungeni ripoti iliyohaririwa.
Kazi ya kuhariri inaendelea kwa kasi huko.

Ununuzi wa ndege, ujenzi wa Dodoma, utaratibu wa tender, matumizi nje ya bajeti na matibabu ya viongozi nje ya nchi ni pasua moyo.

Tuendelee kusubiri.

Mwana JF kuwa wa kwanza kujua
 
Duuuh.... Nimekuta habari kama hii Twitter..... Hivi wakihariri si CAG ata upload the original report kwenye website yake muda ukifika?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizo kasoro kwanini ziondolewe wakati si yeye aliyeandika hiyo ripoti? Huko ni kuingilia mamlaka ya CAG kama ni kweli na ni uvunjaji wa katiba ambao unaweza kumpandisha kizimbani.

Huyo nduli si CAG hivyo hana mamlaka ya kufuta au kuongeza chochote kile.

 
Kwani hata wakifanya editing itawasaidia nini?
In God we trust
 
Sizani kama umeongea ukweli maana umeongea kisiasa report ya CAG ikiisha sainiwa haiwezi kubadilishwa sasa wanabadilisha wakina nani unamanisha CAG anachezea report yake ? Sio kweli
 
CAG kamkabidhi report Rais, Then Rais ndo awapatie Bunge.

Sasa bunge likigoma kupokea report linakua linamgomea nani??
 
Sizani kama umeongea ukweli maana umeongea kisiasa report ya CAG ikiisha sainiwa haiwezi kubadilishwa sasa wanabadilisha wakina nani unamanisha CAG anachezea report yake ? Sio kweli
Kama ulikua hujaelewa mpaka unauliza maswali, kwa nini tena umehitimisha kua "sio Kweli?"....
 
Mkuu, kwani leo si ndio siku ya 7? muda wa kupeleka ripoti huyu jamaa si umeshapita?
 
Audit report is a legal document no one has authority to temper with anything in that report.
Ndio namshangaa anawalisha watu matango pori sizani kama CAG anaweza kukubali uo ujinga atajizulu maana ndiye atakayeenda kuisoma bungeni yaani aende kusoma takataka sizani!
 
Reactions: BAK
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…