Bunge Kutumia zaidi ya MILIONI 500 kutengeneza FIMBO..

Bunge Kutumia zaidi ya MILIONI 500 kutengeneza FIMBO..

Eng. Y. Bihagaze

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2011
Posts
1,487
Reaction score
910
Nazidi kuamini zaidi Kwamba kuna Mtu/Watu wamesaidia kutengeneza Shimo la Fedha ambazo Ni Nyingi mno zinazosaidia Bunge la KATIBA Kufanya kila inalojisikia kufanya hususani Matumizi ya Fedha pasipo Kujali mustakabali wa maisha ya Leo ya Mtanzania.

Kama Bunge (bila Aibu) Leo wanajadili kutengeneza FIMBO Kama Kinyago flan wanachokiita SIWA, Yenye uzito wa kilo Nne Na Nusu ya Dhahabu (4,500gram Kama gram moja Ni 97,000/= hapo tuna (97,000 x 4,500 = 436,500,000) hapo ukitia ufundi (Artist ambayo Ni 1/3 ya gharama hiyo nadhani Hii Ni Fedha ya Kutisha mno.. Naskia PATAKUWA NA SIWA MBILI hapo Ni zaidi ya Bilioni Moja..

Nadhani Kama wanaamini FIMBO Ni muhimu watengeneze FIMBO ya Mbao hasa mpingo Yenye thamani ya Chini ya Laki Nane ambayo in mbao ya Tanzania. Na endapo wanataka Alama Za historia ujengwe mnara Kama alivyoshauri Professa Tibaijuka ambao hauta gharimu zaidi ya Milioni 20.

Kama wakiitengeneza hiyo SIWA YA dhahabu ya zaidi ya Milioni 500 wakaandika hayo majina yako ...najiuliza nani atalinda dhahabu hiyo Baada ya Bunge hili. Je itahifadhiwa Ndani ya CHUMBA imara (STRONG ROOM) nani Atasoma majina hayo. Sidhani Kama wabunge wanawaza Ni Nini wanakijadili Unless watufafanulie huyo aliyewatengenezea shimo la Fedha ndiye anayewalazimisha Kufanya matumizi hayo kufuru..!!!!!

---------

Chanzo Ni kikao Cha Bunge la KATIBA kinachoendelea Leo wakati asubuhi Mwenyekiti wa Kamati ya Muda ya kutunga kanuni Za Bunge Prop Mahalu aliwakilisha KaZi Yao ya siku Sita kupitia, kuchambua Na kutoa mapendekezo ya kanuni Za Bunge.. Na Mwisho ndipo uundaji wa SIWA (FIMBO) ya Bunge.
 
Whaaaat!Si bora wangewaongezea wajumbe hizo pesa wakasomeshe watoto wao?

Sasa nimeanza kuamini kuwa Tanzania si nchi maskini kama viongozi wanavyotuaminisha!Yaani za kulipa malimbikizo ya waalimu hakuna ila za kutengenezea fimbo zipo za kutosha!

HIVI TUMELAANIWA?
 
Mkuu chanzo cha habari hyo plz!

Chanzo Ni kikao Cha Bunge la KATIBA kinachoendelea Leo wakati asubuhi Mwenyekiti wa Kamati ya Muda ya kutunga kanuni Za Bunge Prop Mahalu aliwakilisha KaZi Yao ya siku Sita kupitia, kuchambua Na kutoa mapendekezo ya kanuni Za Bunge.. Na Mwisho ndipo uundaji wa SIWA (FIMBO) ya Bunge.
 
hii nchi bado haijapata viongozi madhubuti ina viongozi wanaowaza kwa kifupi sana.
 
Na ukisema wote waliohusika kufikiria jambo hilo la kutngeneza fimbo (siwa) kwa pesa yote hiyo wachalazwe viboko .....lazima utaonekana mmwenda wazimu.
 
Siwa hiyo itatengenezwa saa ngapi wakati Bunge limeshaanza? Kwa nini wasiazime la Bunge la JMT?
 
Tumepeleka mizigo Bungeni lakini Mungu atahukumu kwa haki
 
hili bunge ni la muda tu, maximum ni siku 90

fimbo ya nini??

au wameshajisahau?
 
Sikujua kama kwenye hili bunge tumepeleka mijitu mipumba.vu kiasi hicho?

Mijitu haina huruma na fedha ya walala hoi? Tumbaff kabisa! Bunge lenyewe ni siku 90 tu halafu hatutaliona tena sasa hiyo fimbo itakuwa na umuhimu gani? Yanaacha kujadili mambo ya maana yanabaki kujadili fimbo?? Na humo tuna miprofessa imejazana kumbe upuuzi mtupu?
 
Ulaji mwingine huo
Humo bungeni Mhe Kashilila anajua pana wajanja wachache wanakula hela sana. Wakati mjadala wa SIWA ukiendelea spika akatoa taarifa SIWA YENYEWE ISHATENGENEZWA.. Jamaa wakastuka kisha wajanja hao faster faster wakamwambia Tena Chair imetengenezwa Sampo.

Huo mchakato (procurement) ya kumpata mzabuni wa Kufanya KaZi Hii ulifanyika wapi Na saa Ngapi, procurement ya Namna Hii lazima ianze Na call of Interest . Sijui mambo haya yalifanyika wapi Kwa utaratibu upi.. Nani anahoji haya?!???!!!
 
Hawa ni mafano wa ule msemo "Ni mora unyimwe pesa kuliko akili".
 
kumbe pesa tunayo eh,sijui hadi hili bunge liishe tutakuwa tumeteketeza pesa kiasi gani
 
Nchi hii ni ngumu sana kuiondoa kwenye umaskini ikiwa chini ya ccm, %95 ya wana ccm ni wapiga dili!
 
Potelea bali naomba inchi hii vita ikuje tuheshimiane hata kama kukufa kupo,
 
Nazidi kuamini zaidi Kwamba kuna Mtu/Watu wamesaidia kutengeneza Shimo la Fedha ambazo Ni Nyingi mno zinazosaidia Bunge la KATIBA Kufanya kila inalojisikia kufanya hususani Matumizi ya Fedha pasipo Kujali mustakabali wa maisha ya Leo ya Mtanzania.

Kama Bunge (bila Aibu) Leo wanajadili kutengeneza FIMBO Kama Kinyago flan wanachokiita SIWA, Yenye uzito wa kilo Nne Na Nusu ya Dhahabu (4,500gram Kama gram moja Ni 97,000/= hapo tuna (97,000 x 4,500 = 436,500,000) hapo ukitia ufundi (Artist ambayo Ni 1/3 ya gharama hiyo nadhani Hii Ni Fedha ya Kutisha mno.. Naskia PATAKUWA NA SIWA MBILI hapo Ni zaidi ya Bilioni Moja..

Nadhani Kama wanaamini FIMBO Ni muhimu watengeneze FIMBO ya Mbao hasa mpingo Yenye thamani ya Chini ya Laki Nane ambayo in mbao ya Tanzania. Na endapo wanataka Alama Za historia ujengwe mnara Kama alivyoshauri Professa Tibaijuka ambao hauta gharimu zaidi ya Milioni 20.

Kama wakiitengeneza hiyo SIWA YA dhahabu ya zaidi ya Milioni 500 wakaandika hayo majina yako ...najiuliza nani atalinda dhahabu hiyo Baada ya Bunge hili. Je itahifadhiwa Ndani ya CHUMBA imara (STRONG ROOM) nani Atasoma majina hayo. Sidhani Kama wabunge wanawaza Ni Nini wanakijadili Unless watufafanulie huyo aliyewatengenezea shimo la Fedha ndiye anayewalazimisha Kufanya matumizi hayo kufuru..!!!!!

kama haya ni kweli basi fedha hizo ni zaidi ya mshahara wa Waziri mkuu wa Uingereza kwa mwaka.
Mshahara kwa Mwaka: TZS 368.450.118,00
Kwa Mwezi: TZS 30.704.176,00
Kwa Wiki: TZS 7.369.002,00
Kwa Siku: TZS 1.473.800,00
David Cameron - Waziri Mkuu wa Uingereza -
Kuzaliwa: 1966 Uingereza.
 
Back
Top Bottom