Nazidi kuamini zaidi Kwamba kuna Mtu/Watu wamesaidia kutengeneza Shimo la Fedha ambazo Ni Nyingi mno zinazosaidia Bunge la KATIBA Kufanya kila inalojisikia kufanya hususani Matumizi ya Fedha pasipo Kujali mustakabali wa maisha ya Leo ya Mtanzania.
Kama Bunge (bila Aibu) Leo wanajadili kutengeneza FIMBO Kama Kinyago flan wanachokiita SIWA, Yenye uzito wa kilo Nne Na Nusu ya Dhahabu (4,500gram Kama gram moja Ni 97,000/= hapo tuna (97,000 x 4,500 = 436,500,000) hapo ukitia ufundi (Artist ambayo Ni 1/3 ya gharama hiyo nadhani Hii Ni Fedha ya Kutisha mno.. Naskia PATAKUWA NA SIWA MBILI hapo Ni zaidi ya Bilioni Moja..
Nadhani Kama wanaamini FIMBO Ni muhimu watengeneze FIMBO ya Mbao hasa mpingo Yenye thamani ya Chini ya Laki Nane ambayo in mbao ya Tanzania. Na endapo wanataka Alama Za historia ujengwe mnara Kama alivyoshauri Professa Tibaijuka ambao hauta gharimu zaidi ya Milioni 20.
Kama wakiitengeneza hiyo SIWA YA dhahabu ya zaidi ya Milioni 500 wakaandika hayo majina yako ...najiuliza nani atalinda dhahabu hiyo Baada ya Bunge hili. Je itahifadhiwa Ndani ya CHUMBA imara (STRONG ROOM) nani Atasoma majina hayo. Sidhani Kama wabunge wanawaza Ni Nini wanakijadili Unless watufafanulie huyo aliyewatengenezea shimo la Fedha ndiye anayewalazimisha Kufanya matumizi hayo kufuru..!!!!!
Acha utani?! Najua unatania tu au watakua wanatania tu, unajua mle ndani kuna watu wa kila aina mabubu, wanasiasa, waekti muvi, wakulima sijui wametoka kijiji gani, wafugaji lakini wenyewe hawa hami hami ndo mana wako pale, viongozi wa dini naomba waongoze ibada kuwaombea viongozi na serikali. Kwani sisi tunataka fimbo au katiba?'?'!!! kwani katiba yenyewe si kumbukumbu tosha, hili la kutengeneza fimbo ni wazo la wajumbe wa bunge la katiba au ni serikali?!? Tayari kuna mnuko wa ufisadi, jamaa wana mbinu sana. Hiyo fimbo ndo nini sasa, au ndo maishara ya kishetani!