Bunge la bajeti 2011/2012 na yatokanayo

Bunge la bajeti 2011/2012 na yatokanayo

Askari wa barabarani ambaye atashindwa kujenga jumba la kifahari lazima atakuwa na mtindio wa ubongo.Trafiki polisi Mungu awape nini tena?
 
Mkulo ni Raia wa Malawi ndo maana hajaili kitu kwa Watanzania
 
Mkuu umenena vizuri sana. Hili suala la kuongeza notification fine nadhani ni kutaka kuwafurahisha traffic. Hivi serikali haina watu wa kufikiri kiasi hicho? Kila siku PCCB na watu wengine wanatuambia kuwa Traffic Police ndio wanaongoza kwa rushwa hapa nchini, leo unasema unaongeza fine ya papo kwa papo hao hao ndio wakusanye hiyo fine. Nadhani sasa trafic imekuwa deal. Huko CCP Moshi itabidi watu wafanye michakato ili wakimaliza tu wapangiwe traffic na wengine ambao wako general duty kwa sasa itabidi waende bagamoyo ili wapangiwe traffic manake kuna neema huko.


RED ALERT:
Mbona imeenza siku nyingi mkuu.
Hata hivyo ngoma droooooo=UBUNGE + TRAFFIC POLICE = 1
 
Na hii itawafanya mabosi wao wawapandishie hesabu ya kila siku accordingly....
wa tiGo.............. toka kiasi cha sasa hadi kipya
Barabarani................... toka kiasi cha sasa hadi kipya
Kigofu...................... toka kiasi cha sasa hadi kipya
Difenda...................... toka kiasi cha sasa hadi kipya ............ NA BEI YA TEKSI DIFENDA KWA SISI WA KURUDI HOME USIKU LAZIMA IPANDE
 
Safari hii natafuta Mume Traffc maana najua kwa siku 2 tuna kamilioni ketu mfukoni hapo ni mambo yakiwa hayako sawa but mambo yakiwa poa aah hata 1.5m kwa siku, akiamka asubui hadi jioni anavyotoka atakuwa amekamata mangapi ikiwa tu kipindi cha 20000/ kwa siku alikuwa anakusanya hadi 350laki sembuse hii ya elfu 50.

Jamani mwenye ndugu Traffic aniambia niko veri siriazi! :brushteeth::brushteeth:
 
Na hii itawafanya mabosi wao wawapandishie hesabu ya kila siku accordingly....
wa tiGo............ toka kiasi cha sasa hadi kipya
Barabarani................... toka kiasi cha sasa hadi kipya
Kigofu...................... toka kiasi cha sasa hadi kipya
Difenda...................... toka kiasi cha sasa hadi kipya ............ NA BEI YA TEKSI DIFENDA KWA SISI WA KURUDI HOME USIKU LAZIMA IPANDE

mkuu hapo watataka 40 hadi 50 badala ya 15-20
 
SERIKALI imeahidi kuendelea kuboresha maslahi ya watumishi wa umma wake, huku ikitangaza juhudi za kudhibiti matumizi yake kwa kusitisha ununuzi wa magari, kupunguza posho mbalimbali na ununuzi wa samani za ofisi hususan zile zinazoagizwa nje ya nchi.

Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo alisema hayo jana wakati akiwasilisha bungeni mjini Dodoma Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka 2011/2012.
06_11_8hchbf.jpg


Kuhusu maslahi ya watumishi, Mkulo alisema Serikali itaendelea kuboresha maslahi hayo
kulingana na uwezo wa mapato yake kwa lengo la kuwawezesha kumudu gharama za maisha.

Lakini Waziri Mkulo alisema Waziri mwenye dhamana ya Utumishi, atatoa maelezo zaidi kuhusu suala hilo wakati atakapowasilisha makadirio ya Wizara yake.

“Maeneo ambayo yatatiliwa mkazo ni pamoja na malipo ya mshahara na likizo kwa wakati, kuhakikisha watumishi wanalipwa mafao yao mara baada ya kustaafu, pamoja na pensheni zao za kila mwezi.

“Sambamba na hayo, Serikali itatoa mafunzo kwa maofisa wa Hazina ndogo wa Mahakama zote zinazoshughulikia mirathi, na kuweka mikakati ya pamoja kuwaondolea kero wasimamizi na warithi wa mali ya marehemu,” alieleza Waziri Mkulo.

Katika kudhibiti matumizi yake, Mkulo alisema Serikali katika mwaka wa fedha 2011/12, itasitisha ununuzi wa magari ya aina zote isipokuwa kwa sababu maalumu na kwa kibali cha Ofisi ya Waziri Mkuu.

Vile vile, Serikali itasitisha ununuzi wa samani za ofisi hususan zile zinazoagizwa nje ya nchi; kupunguza malipo ya posho mbalimbali yasiyokuwa na tija; kupunguza matumizi ya mafuta kwa magari ya Serikali na kupunguza safari za ndani na nje ya nchi ikiwa ni pamoja na ukubwa wa misafara.

“Na pia kuendelea kupunguza uendeshaji wa semina na warsha isipokuwa pale inapobidi na kwa kibali cha Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na kupunguza gharama za maonesho na sherehe mbalimbali,” alifafanua Mkulo juhudi hizo za kudhibiti matumizi ya Serikali.

Katika kudhibiti matumizi, Mkulo alifafanua zaidi kuwa Serikali imepanga kufanya sensa ya watumishi wote wa Serikali na taasisi zake kwa kuandaa siku maalumu ya malipo ya mshahara dirishani.

Alisema Serikali itasimamia utekelezaji wa Waraka Namba 2 wa Hazina wa mwaka 2010 kuhusu uwajibikaji na udhibiti katika usimamizi wa malipo ya mishahara pamoja
na ukamilishaji wa maboresho ya mfumo wa kuandaa mishahara utakaoimarisha udhibiti
wa malipo ya mshahara.

Mkulo alisema Bajeti hiyo ya Serikali itazingatia vipaumbele vya umeme, maji, miundombinu ya usafiri na usafirishaji (reli, bandari, barabara, viwanja vya ndege
na Mkongo wa Taifa), kilimo na umwagiliaji na kupanua ajira kwa sekta binafsi na ya
umma.

Akizungumzia maeneo ya kipaumbele katika mchanganuo wa bajeti, alisema miundombinu
ya barabara, reli, bandari na Mkongo wa Taifa zimetengewa Sh trilioni 2.78 ikilinganishwa na Sh trilioni 1.5 mwaka 2010/11 sawa na ongezeko la asilimia 85.

Mkulo alisema kipaumbele cha pili ni elimu iliyotengewa Sh trilioni 2.28 ikilinganishwa na Sh trilioni 2.04 mwaka 2010/2011, sawa na ongezeko la asilimia 12.

Afya imetengewa Sh trilioni 1.209 ikilinganishwa na Sh trilioni 1.205 kwa mwaka 2010/11, sawa na ongezeko la asilimia 0.3 na kilimo na umwagiliaji kimetengewa Sh bilioni 926.2 ikilinganishwa na Sh bilioni 903.8 mwaka 2010/2011 sawa na ongezeko la asilimia 2.5.

Kipaumbele cha tano ni maji na kimetengewa Sh bilioni 621.6 ikilinganishwa na Sh bilioni 397.6 mwaka 2010/11 sawa na ongezeko la asilimia 56.

Nishati na Madini inakamilisha kipaumbele cha sita kwa kutengewa fedha nyingi ikiwa imetengewa Sh bilioni 539.3 ikilinganishwa na Sh. bilioni 327.2 mwaka 2010 sawa na ongezeko la asilimia 65.

Aidha, Mkulo alieleza kuwa Serikali imefanya mabadiliko katika muundo wa Wizara ya Fedha kwa kuifanya Ofisi ya Msajili wa Hazina kuwa wakala anayejitegemea, kwa lengo la kuzisimamia kwa karibu, wakala, taasisi na mashirika ya umma na hivyo kuongeza ufanisi, tija, mapato na kupunguza utegemezi wa ruzuku kutoka Serikali Kuu.

Mkulo akizungumzia ongezeko la bei ya mafuta ya petroli, alisema Serikali imeamua kufanya mapitio ya kukokotoa tozo zinazotozwa na mamlaka mbalimbali kwa lengo la kuzipunguza na zoezi hili litakamilika katika mwaka wa fedha 2011/2012.

Alisema Serikali pia inakamilisha utaratibu wa ununuzi wa mafuta kwa wingi kwa lengo la kuziuzia kampuni za usambazaji kwa bei ya jumla.

Alisema kanuni zitakazotoa mwongozo katika uagizaji wa mafuta kwa pamoja, zimekamilika na utaratibu huu unategemewa kuanza katika mwaka huu wa fedha wa 2011/2012.

Alisema nia ni kupunguza bei na gharama za usafirishaji wa mafuta hayo. Kwa kutambua umuhimu wa vitambulisho vya Taifa, Serikali imekamilisha taratibu za kumpata mzabuni na tayari mkataba umekwishasainiwa.

Mkulo alisema mradi huo utagharimu Sh bilioni 355 mpaka utakapokamilika; na kwamba kwa mwaka 2011/12, Sh bilioni 70 zitatumika kama ilivyopangwa.

“Awamu ya kwanza ya uzalishaji wa vitambulisho hivyo itakamilika mwishoni mwa 2011,” alisema Mkulo na kuongeza: “Mradi huu ukikamilika utawezesha wananchi kuwa na vitambulisho na hivyo kusaidia, pamoja na mambo mengine, kuongeza wigo wa ulipaji kodi, kurahisisha upatikanaji wa huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na huduma za kifedha na
kuwatambua maharamia haramu.”

Mkulo alisema Serikali itatekeleza majukumu mengi ikiwamo kulipa kiasi cha Sh bilioni 10.5 kwa ajili ya madeni ya watumishi wa Serikali za Mitaa wasio walimu kulingana na uhakiki uliofanywa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

Mengine ni ujenzi wa hospitali tatu za mikoa ya Manyara, Singida na Mbeya pamoja na ukarabati wa hospitali 10 za mikoa na 17 za wilaya; ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma, nyumba tatu za wakuu wa mikoa, ofisi 22 za halmashauri na nyumba 210 katika halmashauri.

Chanzo: Habari Leo
 
nina miaka 40 ccp watanikubali kweli?
maana nimejaribu kuufikiria ubunge nikaona ni maji marefu.
mwenye namba ya mwema anitumie sasa hivi nijaribu kete ya mwisho kwani umri ndio unaenda hivyo.
kazi tz zipo mbili tu ubunge na sasa trafic
 
Hii ni kuleta uonevu katika jamii. Polisi watatunyanyasa sana sasa! Inaonyesha jinsi ccm wasivyojua ukweli wa nchi!
 
Askari wa barabarani ambaye atashindwa kujenga jumba la kifahari lazima atakuwa na mtindio wa ubongo.Trafiki polisi Mungu awape nini tena?

Ijapokuwa sipendi such thinking, lakini hii comment imetoa summation nzuri!!
 
Kamakabuzi, uchambuzi wako ni mzuri sana, nimeupenda nami ningependa kuongezea kitu kidogo serikali inaposema "Serikali itaendelea kuboresha maslahi ya watumishi kulingana na uwezo wa mapato yake kwa lengo la kuwawezesha kumudu gharama za maisha". "Itaendelea" Hilo neno maanake kitendo kinaanza na kinaendelea bila ukomo, ni kwa kasi gani tendo linaanza is still undefined, ni kwanini Serikali isiseme "Tunaboresha" ikamaanisha sasa. Inaposema kuwa itaendelea kuboresha na haijaboresha na haijaweka ukomo, huko ni kutuhadaa, huku wafanyakazi wakiendelea kubanwa na msamiati wa kuendelea. Tunataka Serikali ituambia tunaboresha na itupe timeframe.

 
Jamani wanajamii naomba tuangalie kurasa 104 kwangu naiona ni mbaya mno kwani wamebadilisha sheria ya faini kwa makosa ya barabarani (traffic notification) ambayo kwa sasa kwa kosa inatozwa TSZ 20,000 na kua TZS 300,000.
Hii maana yake serikali ime adopt faini likyoleta kero kubwa hasa dar es salaam iliyokua iatolewa na majembe wakikamata gari, Faini hii haitasaidia serikali kwani itawanufaisha Trafik wataongeza kudai hongo za hata TZS 100,000 ili wasikupe faini.
Pia kipato cha wenye magari wengi hawawezi kuilipa hasa wenye TAxi, Daladala ambao wanapata kwa siku TZS 10,000/30,000. Itakua ni usumbufu mkubwa wabunge naomba mkiiona hii ikalipie ishindwe kupita, Pia wenye namba za simu za waheshimiwa washitueni italeta machafuko.
tuendelee kuipitia bajeti na kutoa michango yetu wanaJF
 
kwakweli hii inauma sana toka 20,000 mpaka 300,000 ni ongezeko la asilimia ngapi mbona serikali hawatumii akili, wameiga toka majembe faini zilizoleta kelele mno sasa wenye taxi, bodaboda na daladala watafanyia kazi traffic. Nina Hiace yangu ikipita hii bajeti nauza sitaki tena biashara hamna kitu na hapa arusha kila siku traffic wanasumbua
 
Polisi na hasa trafiki i sababu ya umaskini wa watanzania.
 
there are systems coming to ensure that the money goes to the right channel...stay tuned!
 
Ni vigumu kuamini kuwa serikali inataka kupambana na madereva wazembe kwa sababu wengi wa wanasiasa wamewekeza kwenye mabasi hasa haya ya mikoani. Hivi Abood imepata ajali mara ngapi in the last 12 months? Na hizi daladal zinamilikiwa na nani? si hao hao matraffic police?

Kwa nini kwa mfano kama mabasi ya kampuni fulani yanapata ajali mara kwa mara yasifungiwe leseni kabisa maana muhimu ni roho za watu na wala sio faini. Ushauri wangu ni kwamba pamoja na faini ya fedha kuwepo na 'track record ya usalama barabarani kwa kila gari/kampuni hasa mabasi na kama wanaonekana kupata ajali mara kwa mara kama haya ya Abood, basi waondelewe kwenye soko.
 
cjui ni namna gani na ni lini serikali itaangalia uhalisi wa maisha ya watanzania walio wengi katika bajeti suala la utendaji pia halimo hatsa kwa hico kiduchu bad kikubwa kinaishia mikononi mwa wachache,kuongeza faini za barabarani sio suluhisho la ajali zitokeazo au njia ya kuongeza pato la taifa bali ni kuwaenzi mtrafki pia waongeze viwango vya rushwa ,cjui cjui cjuti kuwa mtanzania bali najuta sana kuzaliwa tanzania.:majani7:
Tulia baba hapa ni kwenu, unataka kuhamia mwezini???????????? Muda muafaka utafika watu wenye huruma na wananchi wa nchi hii wazalendo wataleta ukombozi halisi wewe mwenyewe ukishiriki!!!!!!!! Aluta Continua!!!!!!!!!!
 
Jana bwana Mustafa Mkulo akisoma bajeti ya mwaka 2011 -2012 wananchi wengi bado kwao wameiona inafurahisha sana na kuwapa matumaini lakini hiki ni kitendawili na ni kiini macho kwa taifa hili tunalotegemea kuiona ilie nnchi tuliyoahidiwa ya maziwa na asali.

Hivi kweli serikali haina njia nyingine mbadala ya kuuongezea mapato zaidi ya bia/sigara pamoja na mvinyo? inamaanisha watanzania ni watu wa anasa sana jamani?

Kwa mfano tuna viwanja vya ndege ambavyo landing fees yake kwa nchi kama Tanzania ni ghali mno kupita hata Kenya/Uganda ukilinganisha na ubora wa viwanja vya majirani zetu hawa lakini kwao gharama ya landing fees ni ndogo ukilinganisha na kwetu!

Hii ingesaidia kwa upande wetu wa Tanzania kupunguza ushuru wa ndege kutua viwanjani mwetu na kutuongezea watalii wengi kuja Tanzania na kuongeza pato la taifa na wananchi kuondokana na dimbwi la umasikini!

lakini wageni wengi wanakata ticketi zao za ndege halafu wanashukia Kenya na nchi nyingine ili kuepuka gharama ya kuja kwetu directly! tunavyanzo vingi vyakuongeza mapato ili tuepukanae na umasikini uliokidhiri hata kufikia raisi wa nchi kujibu maraisi wenzake kua hajui kwanini wanachi wake ni masikini!

Kwangu mimi binafsi bado haitaingia akilini kwa Tanzania kwenye kila bajeti zake cha kwanza kabisa wanachokipa kipaumbele ni kuongeza ushuru kwenye bia/sigara pamoja na mvinyo! Kidogo nimeona CCM wamejaribu kukubali sera za wapinzani kwatuambia kua watapunguza misafara ya viongozi na ziara za kwenda nnje ya nnchi lakini kwangu mimi naona utekelezaji wake ni kitendawili tu kwakua kauli ya kujivua gamba kila mtu kwenye chama hicho ni mwizi. Tanzania bado tutaendelea kua masikini tu Unlesss uongozi mpya uingie madarakani. Godbless Tanzania!:confused3:
 
Waziri wa Fedha na Uchumi Mustafa Mkulo akinadi mkoba wa Bajeti

Bajeti ya Serikali 2011/2012 hii hapa
bilachoo.jpg

mpaka leo watu wanakunya kwenye
vichaka na ni 2011 bajeti munagawa nyinyi
na kuwawacha wanyonge wakiendeleya kutabika
join-toilet-cistern.jpg

serekali ya tanganyika huyu jamaa anahitaji
choo kama hichi wacheni kuiba pesa wapeni
wananchi na wao wawe na maisha mazuri
kama mulivyo nyinyi
72207_1630755205240_1127403497_31793227_2798227_n.jpg

watu wana picha zake badala ya faida yake
Nyumba_ya_masikini.jpg

watu wana picha yake badala ya faida zake

new+004.jpg

DSC02746.JPG

Kenya-kibera-maisha-ap-%5B1%5D.jpg

watu kama sisi ndio wenye haki ya bajeti hiyo

two_liter_shoes.jpg

iwafikiye watu kama hawa maana unaonyesha kuwa umefurahi
mpaka jino la mwisho maana ushajuwa chako ni ngapi ila
watu kama sisi hivi ndio viatu sasa na nyinyi habari hamuna
2354254_orig.jpg

hili ndio daraja pesa zote munazo gawana ktk bajeti mumeshindwa
kuwajengeya madaraja ktk nchi
IMG_0314.jpg

hichi ndio choo na bafu pia watu wanaoga humu humu bajeti
itafika lini kwa watu kama hawa nyinyi munaendeleya tu kugawana
high-level-toilet.jpeg

wananchi pia wanataka kuwa na vyoo na bafu la kuogea kama haya
ambayo yamo ndani ya nyumba zenu mulizo jenga kwa jasho la
walipa kodi masikini

Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo akiwaonesha wapigapicha na waandishi wa habari mkoba uliona nyaraka za Bajeti ya Fedha ya Serikali kwa mwaka 2011/2012 baada ya kuwasili katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma leo ikiwa ni muda mfupi kabla ya kuingia Bungeni kusoma Bajeti hiyo.
SAFARI+MOJA.JPG

kikwete.JPG

umesahau ulipokuja kutuomba kura ukasema
utatujengea na tutakuwa na maisha mazuri vipi
mbona unatukana na bajeti haitufiki au ndio umepata
kura na sisi ndio tumeruka patupu maana hii ni miaka
mitano ya mwisho na sisi bado tunaishi kwenye vibanda
ulivyokuja kutuomba kura mpaka leo bado tumo humu humu
Does-George-Soros-Make-Money-On-Third-World-Countries.jpg

mpaka tunakuomba na bado unawambiya nchi za ulaya
tunaishi maisha mazuri na unashaga kama hujuwi kama tunalal na njaa
Mr.Simango-and-his-wife-outside-their-house-in-chamwino-crop21.jpg

usiwaonyeshe wapiga picha waonyeshe wananchi wa tanganyika
ndio wanao uhitaji sio wapiga picha



Mkoaba wa Bajeti ya Serikali 2011/2012.
TATIZO+LA+MAJI+NKOME+GEITA+%281%29.JPG

tumechoka kunywa maji machafu bajeti naije huku mara hii
NDIZI+PIX+NO+2.JPG

bajeti..? bajeti..? bajeti..?
madafu.jpg

ndio ukubwa huwo mwanangu sukuma sukuma bajeti
sisi haitufiki wanakula wenye kwa wanyewe tu sukuma sukuma
g.jpg

labda mwaka huu bajeti ikija na mimi sitouza tena machungwa
nita nunuwa nyumba na dala dala
332.jpg

nyinyi pigeni picha mimi nasubiri bajeti ili na mimi
nipate pesa za kununuwa nguwo sina kitu msela
7636976_orig.jpg

mei+mosi.jpg

hatuna hata gari ya kutu bebeya matofali tunayotaka kujenge nyumba
DSC00206.jpg

mustafa mkulo bajeti ilete huku tuchibiwe misingi ya
kupitiya maji machafu na mataka taka​
 
Back
Top Bottom