Bunge la Cameroon laanzisha nafasi ya Makamu wa Rais. Upinzani Wapiga Yowe

Bunge la Cameroon laanzisha nafasi ya Makamu wa Rais. Upinzani Wapiga Yowe

McLaren

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2025
Posts
1,170
Reaction score
3,743
Wakuu.

Katika kile kinachoonekana kama maandalizi ya mapema ya kurithishana madaraka, nchi ya Cameroon inajiandaa kuanzisha nafasi ya Makamu wa Rais kwa mara ya kwanza baada ya zaidi ya miongo mitano.

Hatua hii inakuja huku kukiwa na maswali mengi juu ya hatma ya kisiasa ya nchi hiyo inayongozwa na Rais Paul Biya, ambaye sasa ana umri wa miaka 93, akiwa ndiye kiongozi mwenye umri mkubwa zaidi duniani madarakani.

biya.png


Mabadiliko ya Sheria: Nini Kimebadilika?​

Chini ya mabadiliko ya katiba yaliyopitishwa na Bunge, Makamu wa Rais sasa atakuwa ndiye mtu wa kwanza kuchukua mikoba ya uongozi endapo Rais atafariki, kujiuzulu, au kushindwa kutekeleza majukumu yake.

Tofauti na mfumo wa awali ambapo Spika wa Seneti alitakiwa kuongoza nchi kwa muda mfupi (ndani ya siku 120) kisha kuitisha uchaguzi mkuu, sheria hii mpya inampa Makamu wa Rais mamlaka ya kumalizia muhula mzima wa Rais aliyekuwepo.

Kwanini Upinzani Unachemka?​

Viongozi wa upinzani na wanaharakati wa demokrasia nchini humo wamepokea mabadiliko hayo kwa hasira na shaka, wakitoa hoja zifuatazo:

  • Uteuzi Badala ya Kura: Hofu kubwa inatokana na ukweli kwamba Makamu wa Rais hatachaguliwa na wananchi, bali atateuliwa na Rais Biya mwenyewe. Wakosoaji wanasema hii ni mbinu ya kumpachika mtu anayependwa na Rais (ikiwemo tetesi za mwanawe, Franck Biya) ili ashike nchi bila ridhaa ya umma.

==============================

Cameroon is set to introduce a vice-president for the first time in over 50 years, following constitutional changes approved by parliament. The move comes during the long rule of President Paul Biya, currently the world’s oldest serving head of state at 93.

The amendment means that if anything happens to the president, the vice-president will automatically take over and complete the remaining term. Earlier, this responsibility fell to the Senate leader, who would serve only temporarily until fresh elections were held.

The bill was passed during a joint sitting of both houses of parliament, with an overwhelming majority backing it. It now awaits the president’s formal approval to become law.

Supporters argue the change will make governance smoother by ensuring continuity and reducing institutional uncertainty during transitions, whereas the opposition said that the amendments were hastily drafted and aimed at consolidating power.

Source: BBC, First Post, Reuters
 
Waafrika ni manyani yaliyochangamka isipokuwa wewe unayesoma hii comment na mimi.
 
Back
Top Bottom