Bunge la Dkt. Tulia lenye Paul Makonda na David Kafulila ndani yake litawaka moto na kuteka mioyo ya watanzania hapo mwakani

ephen ana masihara sana anasema eti wewe una Bachelor's Degree in Mechanical Engineering wakati wewe ni chawa mwandamizi wa mama,ana utani sana huyu Binti.
Akisemecho ephen juu yangu ni sahihi kabisa na kinakuwa cha ukweli kabisa. Hata akikuambia nawaza nini ujuwe anakuwa sahihi maana yeye ndiye nimemkabidhi moyo wangu.
 
Hizo ni ndoto za mchana unazoota wewe. Hao watatangazwa mapema sana kuwa wameshinda. Na kuna uwezekano wasiwe na washindani majimbo mwao.
Huna habari kuwa sheria zimebadilishwa,ule upuuzi wa kuteka wapinzani ili mpite bila kupingwa siku hizi hakuna.
 
Mbona yeye haandiki utopolo kama wewe.?
Kwani mimi wapi naandika kama unavyosema au ndio njia ya kummendea? Sasa ole wako nikute unaleta mazoea kwa ephen utaona nitakacho kufanya. Nitakutegua Mwili na sitakuwa na kesi polisi wala mahakamani maana nitakuwa najilinda na kulinda mali yangu jambo ambalo linaruhusiwa.
 
Huna habari kuwa sheria zimebadilishwa,ule upuuzi wa kuteka wapinzani ili mpite bila kupingwa siku hizi hakuna.
Watapigiwa kura ya ndio au hapana.ambapo naamini kura za ndio zitamiminwa kwa kishindo kwa miamba hii.
 
Kwani mimi wapi naandika kama unavyosema au ndio njia ya kummendee? Sasa ole wako nikute unaleta mazoea kwa ephen utaona nitakacho kufanya. Nitakutegua Mwili na sitakuwa na kesi polisi wala mahakamani maana nitakuwa najilinda na kulinda mali yangu jambo ambalo linaruhusiwa.
Huyo mbona mimi ndiye nilianza naye kitambo tu,wewe umekuja macho juu nakuangalia tu,hiyo pisi yangu kabisa. Ngoja akuchune kwanza halafu anazileta tunazitia kiberiti.
 
Yule Binti ni akili kubwa na hawezi kuwa na vichwa panzi aina yako.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Kuna wakati nilishuhudia kwa macho yangu Mwenyewe watu wakiacha na kusimamisha kazi ili wafuatilie mijadala ya Bunge, nilishuhudia watu wakiwa vikundi vikundi vibanda umiza wakiwa wanafuatilia kwa ukaribu sana bunge na kujuwa kabisa akitoka fulani kuchangia anafuata fulani. Nilishuhudia watu wakiwa na hamasa na kiu ya kusikia Mbunge Fulani Zamu yake ifike ili wasikie mawazo yake.

Nilishuhudia Hata magazeti yenyewe yalikuwa yakipambwa kwa picha na matukio ya kutoka Bungeni.Wabunge wenyewe walikuwa na morali na kujisomea sana ili asiachwe nyuma ya mijadala inayoendelea Bungeni,kwa kuwa ndani ya Bunge zilikuwa zinashushwa hoja nzito nzito kwelikweli zinazoambatana na vifungu vya kisheria,nyaraka na matamko,ambapo kama hujasoma utaishia kuburuzwa na kupewa taarifa muda wote.Hii ndio sababu Bunge lilikuwa na mvuto wa kipekee kabisa.

Mimi mwenyewe nilikuwa nikitoka shuleni nilikuwa nakwenda maeneo ya Mwanjelwa au Kabwe pale Mbeya mjini kununua magazeti hata mawili kwa hela ambayo ilikuwa ni ya mboga.nilikuwa najibana hela nayopewa kwa matumizi shuleni ili ninunue magazeti.na kwa kweli nilikuwa nafahamika sana shuleni kuwa ni Nguli wa Siasa shule nzima.

Unajuwa kwanini Bunge liliteka hisia za watu? Jibu ni kuwa lilikuwa na wabunge machachali sanaa ,wengine walikuwa wakizungumza unaweza ukafikiri ni kutoka Upinzani kumbe ni wabunge wa CCM. Mawaziri walikuwa wanapata joto na kazi kwelikweli katika kuomba na kushawishi bajeti zao zipitishwe, maana wabunge walikuwa wanajenga hoja Nzito sana.wabunge walikuwa wanapambana kwa kujuwa kuwa ukizembee tu kidogo basi unapigwa mueleka jimboni katika sanduku la kura.

Sasa basi naamini hapo Mwakani pamoja na uzuri wa wabunge wetu waliopo Bungeni kwa sasa,pamoja na ujenzi wao mzuri wa hoja,pamoja na utetezi wao wa hoja zinazogusa maslahi ya watanzania,pamoja na uchungu wao wanapojadili hoja .

Naamini kwa dhati ya Moyo wangu kuwa kuingia Bungeni kwa Miamba hii miwili hapo Mwakani kutateka hisia na mioyo ya watu, kutafanya bunge liwe kivutio cha watu, kutafanya watu washinde kutwa nzima wakifuatilia uwasilishaji wa Bajeti za wizara mbalimbali Bungeni .

Embu fikiria Upande mmoja yupo Mwamba Mwenyewe Paul Christian Makonda kijana jasiri kusini mwa jangwa la sahara na upande Mwingine kipo Chuma David Kafulila Msomi wa BBA , halafu mbele yao Yupo Dada wa Taifa na Nguli wa sheria kuwahi kutokea nyanda za juu kusini Mheshimiwa Dkt Tulia Rais wa IPU. Mnafikiri hali itakuwaje huko Bungeni? Mnafikiri nani atapanga kukosa kufuatilia Bunge hilo?

Ikumbukwe kuwa hata mashabiki wa mpira huenda kwa wingi uwanjani kutokana na Nyota waliopo katika vikosi vya timu zote. Unafikiri kwanini wakati fulani El classico ilikuwa na mvuto sana Duniani? Jibu ni kwa kuwa upande mmoja wa Madrid alikuwepo Mwamba Christiano Ronaldo na upande Mwingine wa Barcelona alikuwepo Mwamba Lionel Messi.

Mnafikiri kwanini uchaguzi wa 2015 ulikuwa na mvuto sana? Jibu ni kwa kuwa kulikuwa na Miamba miwili kutoka vyama viwili shindani. Yaani huku Hayati Daktari Mwalimu John Pombe Magufuli na upande wa pili kulikuwepo na Mwamba wa kasikazini Hayati Edward Ngoyai Lowassa. Huku Helkopta inapita juu halafu upande wa pili magari yanapita chini na Helikopta inapaa angani ikiwa na Rangi ya kijana kuashiria chama Tawala kikitawala anga la siasa . Ilikuwa ni raha juu ya rahaaa. Utamu juu ya utamuu.

Mwisho niseme kuwa sijamaanisha na wala nisinukuliwe vibaya kuwa nimesema kuwa bunge la Awamu hii kuwa halifuatiliwi au haina mvuto,bali namaanisha kuongezeka kwa Miamba hiyo kutaongeza chachu namvuto wa kipekee kabisa.

Ni kama ambavyo Yanga ilivyobeba Ubingwa na Mayelle, msimu uliokujaa ikaongeza usajili mkali kwa kuwaleta watu kama Pacome Zouzou , yao yao, Zengeli, Guede na wengine ambao wameleta uhondo wa kipekee ambapo kama siyo hujuma ya Refa ,basi Yanga ilikuwa inakwenda Nusu fainali klabu Bingwa Afrika katika Historia ya soka letu kwa kuiondosha Mamelodsundown ya Afrika kusini.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa.Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Makonda mpaka 2026 atakua jera Kwa mashitaka ya mauaji ikiwa ni pamoja namakoaa ya kumshambulia LISSU Kwa RISASI za kivita vuta muda
 
Bunge liliwaka moto kwa kuwa na wabunge wanaoweza kusoma na kuchambua nyaraka kwa umakini. Ninaowakumbuka ni kuanzia kwa akina Tundu Lisu, Zito Kabwe, Msigwa, Mnyika, Mbatia etc. Kafulila alikuwa mzuri, ila baada ya kuingia Serikalini anakuwa sehemu ya utetezi ila sio mashambulizi. Makonda mtoe kwenye kundi la watu wanaotumia akili, mpeleke kwenye mikutano ya kutukanana na vijembe.
 
Hao niliyowataja ni miamba kwelikweli.angalia namna Chuma Mheshimiwa Kafulila alivyokuwa akilitikisa bunge kwa hoja Nzito nzito.Muangalie pia Mwamba Mwenyewe Paul Christian Makonda katika Bunge maalumu la katiba.
 
Sasa bunge la chama kimoja cha wezi kinakuwaje na mvuto? Hata wakiongezeka na wengine 3000 hali itakuwa mbaya zaidi tu, kumbuka mwaka ule bunge lilipokuwa la moto kwa hoja za maana kutoka kwa wabunge wa upinzani serikali ya ccm(ambayo nayo ilikuwa na wabunge humo ndani) iliamuru bunge liendeshwe kimya kimya,wakazuia redio na Tv station wasionyeshe ili raia wasisikie madudu yaliyokuwa yakiibuliwa na wapinzani,bure kabisa nyie
 
Kinachofanya Bunge likawa na mvuto ni Uzito wa hoja na mijadala mizito inayoendeshwa na wabunge ndani ya Bunge. ambapo hiyo Miamba niliyoitaja Ni miamba kwelikweli katika suala la kujenga hoja zenye ushawishi.
 
Back
Top Bottom