POTOSHI Bunge la Iran limetangaza kuongeza mishahara April 2026, kwa wafanyakazi baada ya vita

POTOSHI Bunge la Iran limetangaza kuongeza mishahara April 2026, kwa wafanyakazi baada ya vita

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1
kumekuwepo na chapisho ambalo limechapishwa na baadhi ya watumiaji wa mitandao ya facebookk wakiwa na ujumbe unao nukuu kuwa bunge la iran limetangaza kuongeza mishahara baada ya vita
katika chapisho hilo ambalo lina nukuu inayosomeka "Baada ya Bunge kuidhinisha sheria mpya ya Malipo kada ya afya nchini Iran Serikali imetangaza Mishahara mipya kwa Wahudumu sekta ya afya kuanzia Madaktari, Manesi na wengine wote kada hiyo watapata ongezeko la mshahara kuanzia mwezi huu wa April sambamba na posho huku wale Waajiriwa wapya zaidi ya 500,000 pia wata faidika na ongezeko hili"
je nu upi uhalisia wa chapisho hili?
669603649_122107451073068294_2243235740570484893_n.jpg
 
Tunachokijua
Baadhi ya watumiaji ikiwemo wa mtandao wa Facebook wwalichapisha Taarifa mwezi Aprili, 2026 ikieleza kuwa Bunge la Iran limepandisha mshahara kwa watumishi hasa wa kada ya Afya.

Mtumiaji mmoja aliandika;

"Baada ya Bunge kuidhinisha sheria mpya ya Malipo kada ya afya nchini Iran Serikali imetangaza Mishahara mipya kwa Wahudumu sekta ya afya kuanzia Madaktari, Manesi na wengine wote kada hiyo watapata ongezeko la mshahara kuanzia mwezi huu wa April sambamba na posho huku wale Waajiriwa wapya zaidi ya 500,000 pia wata faidika na ongezeko hili.

Kweli hapa marekani aligusa sehemu mbaya aisee.


Hii Ina maana gani?"

Uhalisia wa Taarifa hiyo

Baada ya ufuatiliaji kwa njia ya mtandao JamiiCheck imejirirdhisha kuwa Taarifa hiyo ni Potoshi.

Uhalisia ni kuwa Iran kupitia bunge lake haijatangaza ongezeko la mishahara kwa watumishi wake kwa mezi wa nne kama vyanzo hivyo vilivyripoti.

Taarifa ya ongezeko la mishara ya kima cha chini kwa watumishi nchini Iran kufuatia mfumuko wa bei uliosababishwa na vita inayoendelea kati yao na Marekani pamoja na Israel. Vyanzo viliripoti Machi 16, 2026 kuhusu ogezeko hilo lilioanza kutumika mwezi huo huo.

Mathalani Euro News walichapisha taarifa Machi 17, 2026 kupitia tovuti yao yenye kichwa Iran imeongeza kima cha chini cha mshahara kwa asilimia 60 huku vita vinavyoendelea na vikwazo vya kiuchumi vikiharibu uwezo wa kaya kumudu gharama za maisha. Tazama hapa, hapa na hapa

Utawala wa Iran umetangaza ongezeko la asilimia 60 ya kima cha chini cha mshahara huku nchi ikikabiliwa na vita vinavyoendelea na mfumuko mkubwa wa bei.

Waziri wa Kazi wa Iran, Ahmad Meydari, alithibitisha kuwa mshahara wa chini wa kila mwezi umeongezwa kutoka rial milioni 103 (takriban euro 67.5) hadi rial milioni 166 (takriban euro 109). Euro News


Hivyo hakuna uthibitisho kuwa Iran imetengaza ongezeko lingine la mshahara kwa watumishi wake haswa wa kaa ya afya kwa mwezi Aprili, 2026.
Back
Top Bottom