Bunge la Katiba: Kutokuonyeshwa kwenye TV Live ni hujuma kwa watanzania

Bunge la Katiba: Kutokuonyeshwa kwenye TV Live ni hujuma kwa watanzania

Acuity

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2013
Posts
391
Reaction score
118
Ndugu wana Jamvi,

Nimetafakari kwanini Uongozi wa Bunge umeamua kutokuonesha Bunge LIVE sijapata jibu. Katika sheria zetu, ni haki kwa kila mtanzania kupata taarifa, kama hii ya mchakato wa Katiba, Bungeni. Tuishawishi Serikali kupitia Jukwaa hili kuhakikisha Kipndi cha Bunge kinarushwa Live ili tuweze kuona moja kwa moja majadiliano ya wawakilishi wetu Bungeni. Tafakari, paza sauti yako kupitia Jukwaa hili, nafahamu watasikia!

Karibuni
 
Hii kitu kuna agenda ya Siri Hapo! Tusitegemee katiba muzuri Hapo Zaidi ya uozo tu!

Wantumia fedha zetu za kodi hovyo Alafu wanatuletea katiba mbovu!
 
Hii kitu kuna agenda ya Siri Hapo! Tusitegemee katiba muzuri Hapo Zaidi ya uozo tu!

Wantumia fedha zetu za kodi hovyo Alafu wanatuletea katiba mbovu!

Just imagine, ni sawa na wewe ni Mwenyekiti wa Kijiji, upo mkutanoni kujadili ajenda walizowasilisha wananchi kuwa ni kero zao, halafu wewe unajadili agenda wananchi bila kushirikishwa ili wasikie majadiliano. Kigezo kwamba wananchi wamewakilishwa, siyo kigezo cha kutokuonesha Live Majadiliano ya mambo yanayotuhusu. Ni dhihaka na dharau kwa watanzania. Ni njama yao tusijue wanachojadili....ikija huku tuikatae maana tungesaidia kushauri baadhi ya mambo laiti tungepata fursa ya kusikia moja kwa moja bila kuambiwa na media!
 
Ni Moja ya nchi za kipumbavu Kuwahi kutokea..

Wanajua Fika hakuna anayeweza kuhoji..

Ni haki yetu lazima tuone nini wanajadili..

CCM inaongoza nchi kipumbavu sana..Ni wajinga wajinga ndio wanaweza kushabikia Upumbavu wao..

Na ole wao watuletee katiba isiyo na maslahi na Taifa...Manina zao..
 
Hii ndio tz zaidi ya tunavyoifahamu....usijeshangaa pia wanakataza waandishi wa habari wa magazeti!!!
 
mi nawaomba tu tena kwa unyenyekevu wa hali ya juu sana kwamba Mh RAISI naomba uwaruhusu vijana wa serkali yako sikivu watuoneshe Bunge la katiba kupitia tv
Naamini kwa kufanya hizo walau na sie ambao hatukupata fulsa hii ya kuingia humo ndani tutakuwa tunafuatilia kwa karibu mijadala yote inayoendelea humo
Narudia tena kwako mkuu wa kaya tafadhali nakuomba tamka neno tu nayatatimia maana najua wazi kwamba kauli yako yatosha kufanya viongozi wote walioko chini yako wakatiii
 
Sasa hapo baadae wanapotuletea mikaratasi yao ili tupige kura ya maoni ili iweje? Tunataka kusikia mijadala ili halafu tuwe kwenye nafasi nzuri ya kupiga kura ya maoni kwa vitu tunavyovijua sio mambo ya gizani kisha kutuletea.
Hivi kwa nini nchi hii tunaendekeza ujinga?
 
Ndugu wana Jamvi,

Nimetafakari kwanini Uongozi wa Bunge umeamua kutokuonesha Bunge LIVE sijapata jibu. Katika sheria zetu, ni haki kwa kila mtanzania kupata taarifa, kama hii ya mchakato wa Katiba, Bungeni. Tuishawishi Serikali kupitia Jukwaa hili kuhakikisha Kipndi cha Bunge kinarushwa Live ili tuweze kuona moja kwa moja majadiliano ya wawakilishi wetu Bungeni. Tafakari, paza sauti yako kupitia Jukwaa hili, nafahamu watasikia!

Karibuni
Kwa michezo wanayofanya hawa jamaa zetu wa CCM na serikali ingekuwa ni busara kwa wao kuepuka gharama za kuitisha bunge la katiba . Wangeitisha kamati kuu ama Halmashauri kuu ya CCM waandae katiba mpya na mapema ianze kutumika mwezi ujao.
 
hii katiba hiii nawasi wasi nayo sana kama kweli itamsaidia mwananchi wa kawaida...
 
Wakionesha watatoa wapi uzushi wa kuwadanganya wananchi?

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Ndio mana kumbe nakodoa macho kwa tv sipati updates zozote... du huu ni uhuni sana jaman...
 
Ni Moja ya nchi za kipumbavu Kuwahi kutokea..

Wanajua Fika hakuna anayeweza kuhoji..

Ni haki yetu lazima tuone nini wanajadili..

CCM inaongoza nchi kipumbavu sana..Ni wajinga wajinga ndio wanaweza kushabikia Upumbavu wao..

Na ole wao watuletee katiba isiyo na maslahi na Taifa...Manina zao..

Hakika huu ndo mchezo mchafu wa CCM. Tunanyimwa haki yetu ya kikatiba kupata habari za moja kwa moja??

Nani kaagiza tusioneshwe????
 
Ndio mana kumbe nakodoa macho kwa tv sipati updates zozote... du huu ni uhuni sana jaman...

Habari ndo hiyo, wahuni wameamua kutunyima haki yetu mkuu, unashauri tuwafanyeje??
 
Sasa hapo baadae wanapotuletea mikaratasi yao ili tupige kura ya maoni ili iweje? Tunataka kusikia mijadala ili halafu tuwe kwenye nafasi nzuri ya kupiga kura ya maoni kwa vitu tunavyovijua sio mambo ya gizani kisha kutuletea.
Hivi kwa nini nchi hii tunaendekeza ujinga?

This is absolutely true. Kwamba kila siku tunaona na kusikia walichokijadili, then siku ya mwisho tunafahamu kabisa Katiba inayoletwa iko hivi. Nahisi ni mkakati wa kuwahadaa wananchi ili wasielewe kilichomo ili mwisho wa siku isipingwe. Ni hatari sana, tunahitaji kukemea kitu hiki.
 
Miss Chagga, habari ndo hiyo, wameamua kufunika kombe ili mwanaharamu apite. Mtambumburuka mwishoni Katiba ilishapitishwa

napitisha idea za waume na wake zao .... ngoja niondoke mimi naweza tukana bure hapa
 
This is absolutely true. Kwamba kila siku tunaona na kusikia walichokijadili, then siku ya mwisho tunafahamu kabisa Katiba inayoletwa iko hivi. Nahisi ni mkakati wa kuwahadaa wananchi ili wasielewe kilichomo ili mwisho wa siku isipingwe. Ni hatari sana, tunahitaji kukemea kitu hiki.

You are right. Nadhani hao wabunge wa bunge hilo wawe wa kwanza kupiga kelele kuhitaji ushirika wa wananchi katika kuona na kusikia rasimu hiyo kifungu kwa kifungu ili baadae kama wamechakachuliwa sie wananchi tuweze kuwatetea kuwa walichokuwa wanasema sicho hicho tunacholetewa kukipigia kura.
Bila kufanya hivyo hata wao wakiwa na malalamiko yao sio rahisi kuwaamini kuwa wanacho lalamika kina ukweli, wasizungumze kwa nguvu kuhusu posho tuu kwani pamoja na kuwa posho kubwa zinatuumiza sisi lakini KATIBA YA KIJINGA NDIO ITATUUMIZA ZAIDI NA KWA VIZAZI VINGI VIJAVYO.
 
Sasa hapo baadae wanapotuletea mikaratasi yao ili tupige kura ya maoni ili iweje? Tunataka kusikia mijadala ili halafu tuwe kwenye nafasi nzuri ya kupiga kura ya maoni kwa vitu tunavyovijua sio mambo ya gizani kisha kutuletea.
Hivi kwa nini nchi hii tunaendekeza ujinga?

Tunaendekeza ujinga kwa sababu hatuna elimu ya uraia kwa hiyo hatujitambui, mnaojitambua ni wachache ndo maana shule za kata hazina walimu ili wengi msijitambue, msitusumbue ili tuendelee kuwaongoza ninyi wachache mliojitambua kwa mgongo wa wengi wasiojitambua.
 
Hii nchi inaongozwa kipumbavu sana, Television ya Taifa inaona bora kuonesha vipindi vya rusha roho na bongo fleva kuliko sisi walipa kodi kuona na kusikia kinachoendelea Bunge la katiba.
 
Back
Top Bottom