BUNGE LA KATIBA: Yanayojiri leo tarehe 27/02/2014

BUNGE LA KATIBA: Yanayojiri leo tarehe 27/02/2014

Samahani Mkuu hapo kwenye rangi nyekundu pasomeke 'wachangiaji'. Yalikuwa makosa ya uchapaji. Sasa unaweza kunijibu. Asante kwa kusoma mchango wangu.
"Wacangiaji wengi tu ameliona". Kwa wataalamu wa lugha adhimu ya kiswahili wanisaidie mnyumbuliko wa hiyo quoted sentens kabla sijamjibu.
 
Steven Wassira awataka wajumbe watumie nguvu ya hoja kuleta ushawishi kwa wajumbe na siyo vijembe,na kama huna hoja ni vyema ukanyamaza kimya na kuhamasisha kuwa kura ni uamuzi wa mwisho baada ya mazungumzo.
Pia anazungumzia maadili ya bunge na taratibu za nchi zifuatwe mathalani wako DOM kwa lengo mahususi la KATIBA.
KUHUSU KURA:Yeye amependekeza kura ya wazi na kuhamasisha watu waache uwoga wa kuongea kweupeeee kwa kutolea U.S.A kama mfano wa kupiga kura ya wazi!

Wasira Kichwa sana.
 
Mzee Rungwe kweli kaongea mpaka hapa nimesisimkwa pamoja na Mh Esther Bulaya....real patriotic na Kapuya pia....!!
 
Yaaa ameongea vizuri sana, kura ya siri ni must!!! SSM wanataka kumalizana baada ya pale!!! Wakafanyiane vikao na kuondoana katik auongozi ifikapo 2015. Ndiyo maana Anna Kilango amelikoroga, anaogopa atawekwa tena kiti cha moto. Mnafiki sana huyu.
 
kwenye maslai ya chama mnafananisha Tanzani na U.S.A, ila kwenye maslahi ya wananchi mnasema haya ni mambo ya ndani.

Wassira acha kuwatisha wanaccm huru.!
 
Mheshimiwa Stephen Wasira anasema wanaosema CCM imekwenda na msimamo wa serikali mbili ni wanafiki kwa vile hakuna kundi ambalo halina msimamo wake na ndiyo maana CUF kupitia Kwa Habib Mnyaa walikwenda kwa Maandamano, CHADEMA wana msimamo wao ndiyo maana walizunguka kwa HELIKOPTA nchni nzima kuinadi serikali tatu. Makundi mengine kama ya wakulima, wavuvi, akina mama n.k nao wamekwenda na misimamo yao.

Huyu mzee ni kichwa sana. Bunge zima tulii, mzee anamwaga sera.

Kichwa sana, kichwa cha nazi!
 
kwani katiba ina kipengere kimoja tu cha muungano wa serikali na muundo wake?
 
Licha kulilia posho Shibuda amehoji akiitwa Askofu na kuulizwa na Mkiti akasema hapana halafu Sheikh akaitwa kwa hoja hiyohiyo na Mkiti na kusema ndio nini hatima ya nchi yetu. Hataki kura ya WAZI
 
Kama kuna mtu ameongea kwa manufaa ya Taifa hili Mh Hashim Runge ni Mtanzania kamimili asiye mwoga aliye mzalendo wa kweli ,
Ikiwa kutokuwa Mwoga ni uzalendo, basi majambazi ni wazalendo namba 1. Haujatuambia kaongea kitu gani, unaleta porojo za kukamilisha posts ulizopangiwa kwa siku na wakuu wako tu.

Achane kukurupa, leteni issue kamili na za maana. Wewe unasema kaongea kwa maufaa ya Taifa, unataka sisi tuote huyu ndugu Rungwe kaongea kitu gani. Na unaposema manufaa ya Taifa unamaanisha kitu gani, maana mvuta BANGI akisikia mtu anaongelea kuharalisha Bangi atasema MANUFAA YA TAIFA, au shoga akisikia mbunge anatetea ushoga atasema ameongelea manufaa ya Taifa
 
Na huyu Selina anaongea nini jamani???

Aunt amenihuzunisha sana....kanifanya niwe down sana leo.....ni kweli alipinga ujio wa Katiba akiwa pale Sheria 2011 lakini sikutaraji kumuona anashindwa kuwa na msimamo huru. Nway....nitamuandikia private maoni yetu wana Ulanga
 
Mzee Rungwe kweli kaongea mpaka hapa nimesisimkwa pamoja na Mh Esther Bulaya....real patriotic na Kapuya pia....!!

Sasa ndugu, umepost ili kututaarifu jinsi ulivyosisimka. Maana hamleti walichoongea ili nasi tusisimke ama tusinyae.
 
Aache kuwarubuni wananchi, wakati yeye ndiye mshirika mkubwa wa kuipnga rasimu ya walioba.
 
Back
Top Bottom