Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,895
- 20,392
Kesho , alhamisi tarehe 5/09/2013 BUNGE LA KENYA litakutana kwa dharura kujadili uwezekano wa nchi hiyo kujitoa kuwa mwanachama wa mahakama ya kimataifa, INTERNATIONAL CRIMINAL COURT(ICC) .
Hatua hiyo ya kwenye Kenya inakuja wakati Wiki ijayo, Makamu wa Rais William Ruto anatakiwa kwenda the Hague kwenye kesi yake kutokna na vurugu zilizopeleka watu kufa katika uchaguzi wa mwaka 2007 huku Rais Uhuru Kenyatta akitakiwa kwenda kwenye kesi hiyo mwezi novemba mwaka huu.
Endapo Kenya itafanikiwa kujitoa kwenye mahakama hiyo , itakuwa ni nchi ya kwanza kufanya hivyo.
Hata hivyo wakuu wa Icc wamesema wakuu hao wa KENYA wataendelea na kesi hata kama nchi yao itajitoa kwenye mahakama hiyo iliyoanzishwa mnamo mwaka 2002.
Mwezi may mwaka huu, umoja wa Afrika(AU) uliishutumu ICC kuisakama Afrika kutokana na rangi yao madai ambayo yalikanushwa vikali na viongozi wa ICC na kudai kuwa wanapigania haki za wahanga wa Kiafrika.
Mahakama ya ICC inaundwa na nchi 121 zikiwemo 34 kutoka Afrika.
SOURCE:BBC