Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ni kweli hutasikia kiongozi mkubwa wa nchi hizo kushtakiwa. Utakachosikia na kukiona ni haki kutendeka kwa kushtakiwa kwa wahusika wa kashfa hiyo. Kiongozi aliyepanga huo uhalifu hatapandishwa cheo kama Kamuhanda ila sheria itamuandama barabara.Nimetizama Aljazeera hivi punde documentary ya uhalifu uliokuwa ukifanywa na Makomandoo wa Marekani kwa Mateka wa Kivita wa iraq. Inaonekana Walikuwa wakiwalenga wa-Shia na kuwakamata kama mateka halafu baadae huwauwa wakiwa njiani kupelekwa kwenye kambi na kisha kuwatupa katika viunga vya Baghdada kuenyesha kama watu waliokufa katika majibishano ya silaha. Ni vitu vya aibu, lakini kamwe hatutasikia kiongozi yeyote yule wa mataifa haya makubwa akatiwa hatiani kwani wao bila shaka ndio wafadhili wakubwa wa Mahakama hii na wanaitumia vema kuwaadhibu viongozi ambao walikinzana na mipango yao ya siri ya kupora rasilimali ya nchi zinazoendelea.
Hebu tizameni hapa: Al Jazeera's War in Iraq - BBC Control Room Documentary - YouTube
Bado idadi kubwa ya wahalifu ni viongozi wa nchi zinazoendelea.
Source:BBC SWAHILI
Baadhi ya wabunge wa upinzani nchini Kenya wameondoka bungeni wakati mjadala mkali ukiendelea kuhusu kuunga mkono au kupinga nchi hiyo kujiondoa kutoka katika mahakama ya kimataifa ya ICC.
Wabunge hao wameondoka bungeni baada ya kusema kuwa kamwe hawataungana na upande wa serikali kuunga mkono hoja hii ya kujiondoa kutoka katika mahakama ya ICC.Ni kutokana na kuwa kwamba upinzani una idadi ndogo zaidi ya wabunge bungeni.
Mjadala huu unatokana na hatua ya Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto kukabiliwa na kesi za uhalifu dhidi ya binadamu katika mahakama hiyo wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi mkuu mwaka 2007-2008Naibu kiranja wa wabunge walio wachache bungeni Jakoyo Midiwo, alisema kuwa wabunge wa upande wa serikali wanaotetea hoja hii ya kujondoa Hague watakuja kujuta.
Hatua hii ya wabunge inakuja zaidi ya wiki moja kabla ya kuanza kwa kesi dhidi ya naibu Rais wa Kenya Williiam Ruto kuhusiana na ghasia za baada ya uchaguzi mwaka 2008.
Ruto anakabiliwa na mashtaka ya uhalifu dhidi ya binadamu.
Rais Uhuru Kenyatta pia anatarajiwa kufika katika mahakama hiyo mwezi Novemba kwa kesi dhidi yake.
Wawili hao wanashtakiwa kwa kuhusika na ghasia za baada ya uchaguzi mwishoni mwa mwaka 2007.
Msemaji wa ICC ameambia BBC kuwa kesi hiyo itaendelea hata ikiwa Kenya itajiondoa kwenye mkataba wa Roma uliopelekea kuanzishwa kwa mahakama hiyo.
Bwana Fadi El Abdallah, alisema kuwa itachukua karibu mwaka mmoja kwa mchakato wa nchi yoyote ile kujiondoa kutoka katika mahakama ya ICC na hii bila shaka inaathiri tu kesi zilizokuwa mbele ya mahakama hiyo kwa wakati huo.
Hii ni hatua ya dharura inayochukua serikali kujitoa katika Mkataba wa Roma wa mahakama hiyo ulioidhinishwa na Umoja wa mataifa mnamo tarehe 17 July, mwaka1998.
Kenya inataka kutoa mfano wa kuwa nchi ya kwanza Afrika kuchukua hatua hiyo licha ya kwamba uamuzi huu hautoathiri kwa namna yoyote kesi zinazoendelea sasa katika mahakama ya ICC.
Mahakama hiyo ya kimataifa imesema kwamba kesi hizo zitaendelea hata iwapo Kenya itajitoa.
Imesema itaichukua Kenya kiasi ya mwaka mmoja kabla ya kukubaliwa ombi hilo la kutaka kujiondoa katika mkataba wa Roma na hilo litaathiri tu kesi zitakazozuka baada ya muda huo.
Haya yanajiri wakati makamu wa rais William Ruto anatarajiwa kuondoka Kenya kueleka Hague Uholanzi wiki ijayo kukabiliwa na mashtaka ya uhalifu dhidi ya binadaamu katika mahakama hiyo ya ICC, kesi inayoanza tarehe 10 mwezi huu.
Wote wameshtakiwa kwa kuhusika katika ghasia zilizojiri baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007.Kesi dhidi ya rais Uhuru Kenyatta inatarajiwa kuanza tarehe 12 mwezi Novemba.
My take:
Sijui itazuia nini Kenya kujiondoa maana kesi zitaendelea na pia ombi lao la kujitoa inaweza kukubaliwa au kukataliwa baada ya mwaka mmoja.
Naona kama wamerahisisha kazi ya ICC maana sasa watakuwa wanaangaliwa zaidi kwa jicho pevu.
Civil war in the making in Kenya. The bad guys should not assume that good guys will just sit back and watch their country get f****d. Also Kenya leaving ICC means that now the cases can not be transfered to East Africa and the only option left is that the suspected gangsters, thugs, murderers and rapists will simply skip the Hague trials. Since the good guys will demand for them to go for the trials and even try to arrest the suspects when the warrants are issued by ICC Kenya will be split into two and civil war will begin. Then I will get rich somewhere in the mix of civil war. Ha! ha! then I will run for help to the country that helps its African brothers to gain freedom (we all know it)