Mwana wa Mungu
JF-Expert Member
- Aug 14, 2008
- 1,003
- 85
nilishangaa kuona jana kenya wanapeleka mswada bungeni kuamua kama wajitoe kwenye mkataba wa Roma wa ICC au la. nilishindwa kuelewa hasa pale wengi wao wakiwa wabunge walivyokuwa wanaongea kwa comfidence kabisa kuwa, kama watafanikiwa kujiondoa, watakuwa huru kama ilivyo kwa israel, china, marekani, sudan etc.
kitu cha ajabu ambacho nilishangaa ni kwamba, ni kama vile kenya hakuna wanasheria wa sheria za jinai za kimataifa, na hawana washauri kuhusiana na sheria hizo. hii ni kwasababu, jambo hili wamepotea kabisa.
UKWELI NI KWAMBA: hata kama kenya wakipitisha kujitoa ICC, wakawa sio member, bado uhuru kenyatta na wenzake wataendelea kujibu shitaka kwasababu uchunguzi wa makosa yao na kesi yao ulianzishwa wakati wao wakiwa member wa ICC, hivyo jambo hili halitafunika yale ya zamani. isipokuwa kuanzia siku hiyo watakapo jitoa ndipo prosecutor na state parties watakuwa hawana nguvu kupeleka jambo icc.
cha ajabu ni kwamba, nchi hata kama sio member wa ICC, haina immunity kwa watu wake kutoshitakiwa ICC. hii inakuwaje? ni kwamba, ili ICC ianze uchunguzi au kuendesha kesi thidi ya mtu, lazima jambo liwe limepelekwa ICC na state party, au prosecutor mwenyewe awe ameamua kuanzisha mwenyewe after approval by judges. njia nyingine ambayo ni ya tatu na ya mwisho kwa jambo kufika ICC ni kwa kupitia security council resolution. HAPA NDIPO KWENYE KIKOMO, kama suala litapelekwa ICC na security council, haijalishi nchi/kenya ni member wa ICC au la, security council inaweza kurefer matter ya nchi yeyote iwe member au sio member hakuna limitation hiyo, na once prosecutor akipokea toka UN security council basi anaanza uchunguzi au/na kuomba arrest warrant itolewe.
hivyo basi, dawa pekee kuwakamata viongozi wa nchi ambazo sio member wa mkataba wa roma na kwa kupitia security council resolution. na hii ndio iliyotokea kwa omar al bashir wa sudan ambayo ni nchi isiyo member wa ICC lakini rais wao anapata shida mno, hata kusafiri anashindwa, ni utumwa na ufungwa.
KITAKACHOTOKEA KENYA: ni kwamba, wakijitoa wawe sio member, basi, kama kosa litafanyika, nchi wanachama hawatakuwa na nguvu ya kisheria kupeleka jambo hilo icc, lakini security council itakuwa na nguvu hiyo. na kama security council ikipeleka jambo na arrest warrant ikatokea, ina maana kuwa mtuhumiwa huyo asije hata siku moja akatembelea nchi mwanachama, kwasababu akitembelea nchi mwanachama tu atakamatwa kule (pamoja na kwamba nchi mwanachama nyingine zinakuwa marafiki hivyo hawamkamati kama al bashir alivyotembelea tz etc). kwa mfano kama uhuru kenyatta ndio angekuwa amefanya hivyo na kenya sio member, basi asitembelee nchi yeyote ile iliyosaidi, atakamatwa kwasababu nchi zilizosaini zilikubaliana kuwa mtuhumiwa akiwa nchini kwako lazima ushirikiane na icc kumkamata kwani icc haina polisi, inategemea state parties. hii ingemfanya kenyatta kuwa mfungwa wa kuishi kenya tu, ni sawa na al bashir, huwezi kumwambia aende ulaya leo, hawezi hata siku moja. sasa najiuliza, kwanini kenya wanakuwa hawalijui hili?
to be continued....................