Makonda bado ni kijana mdogo ana familia inakua changa nadhani yeye mwenyewe ataangalia haya yanakuaje kwasababu inavyoonekana hawa wanaoitwa mabeberu wamemkalia vibaya..
Ni vizuri tukipata nafasi za uongozi tujue kuna kesho na tuna watoto wanakua.. na kwamba matendo yetu yaweza kuwasumbua hata kama hawajahusika nayo moja kwa moja..hili ni jambo zito sana.
Kitendo cha kutajwa kwa mke wake kimenitisha kumbe ukifanya mambo usisahau inawagharimu hata ndg zako wa karibu..Kwa nchi kama US kutajwa namna ile tena na Waziri wa mambo ya nje na Jasusi kama huyo Pompi ujue kweli kuna mahala sio sawa.
Ile barua inasema credible sources ina maana wamefuatilia na wana jambo pengine..
Tukiangalia hili tatizo kishabiki tutakosea , kwasasa ni kuchukua muda tujitafakari kwamba je kuna shida kama ipo sisi wenyewe kama Wtz tunaimalizaje kwanza..Kenya saiv wao wakiwa na shida wanakaa wenyewe wanamaliza. Na sisi tumalize yetu kwasababu Dunia leo hii imetuangalia vibaya hasa hawa tunaowaita mabeberu.