Wabunge wa Bunge la Ulaya (MEPs) wamepitisha azimio la kuitaka Tume ya Ulaya kufuta rasimu ya mpango wa ufadhili wa kiasi cha Euro milioni 156 uliotengwa kwa ajili ya Tanzania kwa mwaka 2026. Uamuzi huu umefikiwa kufuatia kile bunge hilo linachokieleza kama ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na misingi ya kidemokrasia baada ya uchaguzi mkuu wenye utata wa Oktoba 2025, ambapo serikali ilitumia nguvu kuzima maandamano na kusababisha vifo vya mamia ya watu na wengine wengi kukamatwa kwa tuhuma za uhaini.
Sababu za Bunge la Ulaya: Wabunge hao wameishutumu Tume ya Ulaya kwa kupuuza wasiwasi wao na kuandaa rasimu inayoenda kinyume na sheria za Umoja wa Ulaya. Vilevile, wameikosoa Serikali ya Tanzania kwa kuendelea kukwamisha ziara ya ujumbe wa Kamati ya Haki za Binadamu ya bunge hilo iliyolenga kufuatilia utawala wa sheria. Kutokana na dosari hizo, wameagiza kuandaliwa kwa rasimu mpya itakayohakikisha kuwa fedha za msaada zinaelekezwa moja kwa moja kwenye kutoa huduma za msingi kwa wananchi, kulinda demokrasia, na kusaidia asasi za kiraia pekee.
Matukio Yaliyochochea Mvutano: Chimbuko la msimamo huu mkali ni mwendelezo wa matukio ya ukandamizaji wa kisiasa nchini humo. Hii inajumuisha ripoti ya tume ya uchunguzi iliyokiri kuwa zaidi ya watu 518 waliuawa kwenye vurugu za uchaguzi bila wahusika kuwajibishwa, na hivyo kukwamisha upatikanaji wa haki. Zaidi ya hayo, bunge hilo limekumbushia kulaani kwake kukamatwa kwa Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, kwa mashtaka yanayochochewa kisiasa yanayoweza kusababisha adhabu ya kifo, likisisitiza ulazima wa kumuachia huru na kumlinda.
Soma, Pia

- Bunge la Ulaya (EU) lapinga Msaada wa Euro Milioni 156 (Tsh. Bilioni 440+) kwa Tanzania. Wataja Haki za Binadamu na Uchaguzi wa 2025
- Ufafanuzi wa Serikali Kuhusu Kura ya Kamati za Bunge la Ulaya (EU) Dhidi ya Tanzania