Hawa jamaa wanaotuongoza ni muda wa kujitathmini sasa.
Huku serikali za maghaibi zinatulima barua za maonyo,kisha vikwazo,
Raia kupiga kelele kuhusu mifumo ya usalama inavyowakandamiza,
Gen Z wanawasha moto Kila kukicha. Sasa hivi Dar imekuwa kama Sudan Kila barabara na roundabout askari wamejaa Huku wamejikoki na silaha nzito na mabomu ya machozi vifuani,
Bandari road wamewatoa bodaboda wote kwenye vijiwe vyao walivyokuwa wanajitafutia riziki. Wenye Private cars wanaoishi kigamboni wanapitakwa ugumu hadi wakuscan utadhani tupo mpakani wa mexico na U.S. kumbe tupo Tz. Hatukuwahi kuona hii hali.
Ni kama jamaa wapo katika panic mode.
Kila kukicha viongozi wanapiga mikwara kuhusu wanaotukana viongozi wa serikali,
Msigwa kila kukicha yeye ni kuwatisha waandishi wa habari kuwa siyo wazalendo na wanaovujisga siri za serikali "wataokotwa"
Kafa Mbunge bwege Kila mmoja ametoa pole hakuna matusi Wala kashfa ila akifa kiongozi wa sisiem hata awe mjumbe wa nyumba kumi,taarifa ikifika mtandaoni sisiem wote wanaoga matusi ya nguoni hukunwatu wakishukuru Mungu kwa "kidogo" huku wanaombea wafe viongozi wazito kule juu
Ila ajabu wanasema Hawa ni watu wachache wanaopiga kelele wakiwa nje ya nchi.
Sijui lini waamtaacha kujidanganya na kuamua kubadilisha mwelekeo wa hii nchi!
Au mpaka vikwazo vituchakaze? Ile kenge hasikii hadi atoke damu kwa msikio?