Waafrika tuna matatizo lakini Watanzania tuna matatizo makubwa sana
Nchi zinazotuletea misaada husikii mambo ya kipuuzi namna hii.
Katika nchi hizo, Waziri anapewa 'credit card' ya kampuni kutumia kwa ticket na accommodation
Majuzi viongozi wa Bunge hili wamepitisha sheria ya kulipa 'watu wanaopendana' kwa kisingizio cha Wenza.
Kwamba hata wakiacha utumishi 'Wenza ' wanaendelea kulipwa. Wakifariki tayari wana 'insurance' ya familia zao
Wakati hayo yakiendelea kuna Walimu, Wauguzi, madktari, wahasibu, Wahandisi wastaafu hawajapata hata kikotoo cha kuanzia maisha. Kuna Polisi anasema miaka 30 ya utumishi amepewa milioni 18 yaani mshahara wa mwezi mmoja wa hao Wabunge wanaotunga sheria.
Tunaomba Bunge lipitishe haya
Bunge la JMT lipiisha sheria ya kuhakikisha kila mzazi anapewa kitanda na godoro kabla ya kujifungua
Bunge Lipitishe sheria ya kununua magari yatakayopeleka mishahara kwa Walimu vijijini
Bunge linunue 'Coaster' za kuharakisha mabwana shamba kufika mashambani haraka
Bunge lipitishe sheria Wahasibu wote wapewe magari maalumu kwa kusafirisha pesa na 'cheki'
Bunge lihakikishe kila Mwalimu ana Noah ili kuwahi darasani.
Bunge lipitishe sheria ya kila jimbo kuwa na Helicopter ya Wagonjwa
Mwisho, Wananchi wajilaumu kwasababu Katiba hii ndiyo inawapa uwezo wa kufanya upuuzi tunaouona
Kama wewe ni mwananchi na unasema siasa haikuhusu, Katiba mpya haikuhusu ni vema lakini gharama za hizo ndege zinakuhusu 100%
Afrika ina umasikini wa Viongozi si rasilimali.
JokaKuu Pascal Mayalla