Bunge laazimia Serikali inunue ndege nyingine kwa ajili ya kuhudumia viongozi

Punguza Hasira dunia ya Africa ndivyo ilivyo.
 
Yaani hawa WATAWALA wetu hawashabiani na sisi kabisa,..wana dunia yao tofauti kabisa na sisi!!

Wakati sisi tunawaza UMEME wa uhakika,wao wanawaza maV8

Wakati sisi tunawaza na kuomba kuboreshewa usafiri wa barabarani na majinii kama DART na Kivuko ferry,wao wanawaza kuongeza NDEGE..dah
 
Serikali ina ndege tatu za viongozi kama tulivyoarifiwa; ndege ya Rais na ndege zingine mbili kwa ajili ya Makamu wa Rais na Waziri Mkuu.

Katika hali mbaya ya kiuchumi ambayo tunakabiliana nayo ikiwemo madeni ya Taifa, maisha magumu kwa wananchi,
Kama mtu anasema watoe pesa kwenye Vituo vya Afya Ili wanunue ndege unadhani kuna mwanasiasa ana maana kumtetea mtu wa chini? 👇
 

Haikande Hichilema aliuza hata hIyo moja iliyokuwa imenunuliwa na watangulizi wake.

Kwetu, kazi iendelee; vipaumbele hamna!

Tutakapo wafurusha madarakani tutapiga mnada majumba hadi magari wanayopeana.
 
Piga kura ya kuwaondoa wahuni. Pigania kipatikane chama kipya cha kuwatetea Wananchi.


Huoni kwamba wakati umefika kwa wananchi kujitetea mwenyewe? Huyu Mwananchi amekua akitetewa enzi na enzi, hakuna matokeo chanya.


“Aliebebwa mgongoni haujui urefu wa safari.
 
Hapa inabidi tuwapongeze wawakilishi wetu,tabu waliokuwa wanapata Viongozi wetu kwa kuwa na ndege chache siyo jambo zuri.Zinunuliwe hata tatu za Kuanzia alafu zingine mwakani ili Viongozi waweze kutuhudimia vizuri.


Nakuunga mkono.

Ikiwezekana kila jimbo nchi nzima lipate ndege yake na kila Wizara nao wapate za kwao.
 


Huwezi kuwalaumu viongozi kana kwamba wameshushwa kutoka mawinguni.

Viongozi wetu wanaakisi uhalisia wa sisi wananchi na aina ya maisha tuliyoyachagua.
 
Yaani unashindwa hata kuendana na mada
Hii inaonyesha wewe kweli ni mhenga aliyepitwa na wakati
Yaani unakuja kuliomba bunge ndani JF 😳
Hebu tufatilie wa kileo tunavyoipelemba mada, na inaenda kwa mtiririko unaotakiwa
Sio kutoa nasaha za kizeezee kama malenga
At least hujatumbikizia kuhusu Muungano, ambao unakusosesha usingizi.
 
Huoni kwamba wakati umefika kwa wananchi kujitetea mwenyewe? Huyu Mwananchi amekua akitetewa enzi na enzi, hakuna matokeo chanya.


“Aliebebwa mgongoni haujui urefu wa safari.

Mwananchi mwenyewe bado hajapewa elimu ya kutosha hajui tatizo lake kubwa ni nini, hana biashara, kazi, mlo mmoja kwa siku, ana watoto saba.

Inabidi kumsaidia asimame. Baada ya hapo atajitetea mwenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…