Bunge lajadili juu ya adhabu ya Mbunge Luhaga Mpina. Laamua kumfungia vikao 15

Stuxnet

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2011
Posts
13,417
Reaction score
23,310
Kwa mujibu wa Kanuni ya Bunge #84 (3) (a) ya mwaka 2023 amekutwa na hatia na Kamati ya Hadhi na Madaraka ya Bunge.

Tuendelee kufuatilia bunge
≈=====================

"Mheshimiwa Luhaga Mpina (Mbunge wa Kisesa) alimtuhumu Mheshimiwa Waziri (Hussein Bashe, Waziri wa Kilimo) kuwa amelidanganya Bunge kwa kusema wamebadili kanuni za Nation Food Reserve Agency (NFRA) kuruhusu NFRA kuwa na mandate ya kuingiza sukari wakati hakuna tangazo la serikali lililotangazwa kuipa NFRA mandate ya kuingiza sukari, Waziri (Hussein Bashe, Waziri wa Kilimo) aliieleza kamati kuwa walitumia sheria ya usalama wa chakula sura ya 249 kukabiliana na uhaba wakati wa dharura kupitia NFRA ambapo alisema kuwa wameanza mchakato wa kubadilisha sheria ili NFRA waruhusiwe kuagiza, kuhifadhi na kusambaza sukari hata kwa kipindi kisicho cha dharura na mchakato huo ulianza kwa kutoa tangazo serikalini namba 225 (b) la tarehe 01 Aprili 2024" -Makoa

"Kamati ilipitia kifungu cha 14 cha sheria ya tasnia ya sukari kuhusu wanaoruhusiwa kuingiza sukari na kupitia kifungu cha 15 cha sheria ya usalama wa chakula ya mwaka 1991 na kubaini kuwa wakati wa dharura kama ilivyojitokeza sheria ya usalama wa chakula inakuwa na nguvu zaidi kuliko sheria ya tasnia ya sukari" -Makoa

"Kamati ilipata nafasi ya kujiridhisha kuhusu GN namba 25 (b) ya tarehe 01 Aprili 2024 na kupitia muswada wa sheria ya fedha iliona mapendekezo ya marekebisho yaliyoelezwa na Waziri kupitia kumbukumbu za Bunge na maelezo ya Waziri kamati ilikuwa na maoni kuwa hakuna uwongo uliozungumzwa na kwamba hakuna ukiukwaji wowote wa sheria uliofanywa" -Makoa

Ni sehemu ya maelezo ya Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Haki, maadili na madaraka ya Bunge Ally Makoa akiwasilisha Bungeni kuhusu tuhuma zilizotolewa na Mbunge wa Kisesa (CCM) Luhaga Mpina dhidi ya Waziri wa Kilimo Hussein Bashe

-----
Kamati Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge imewasilisha bungeni taarifa ya kamati hiyo kuhusu tuhuma za Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina, jijini Dodoma leo Juni 24, 2024

Mbunge wa Mtera, Livingstone Joseph Lusinde amesema kutokana na tuhuma zinazomkabili Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina kuhusu kumtuhumu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe kuwa alilidanganya Bunge kuhusu sakata la Uagizaji wa Sukari, anatakiwa kufungiwa kuhudhuria vikao 15 vya Bunge

Ameyasema hayo Bungeni baada ya Mwenyekiti wa Kamati Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge, Ally Makoa kuwasilisha Bungeni Taarifa ya Kamati kuhusu tuhuma hizo, leo Juni 24, 2024
---
"Mheshimiwa Luhaga Mpina (Mbunge wa Kisesa) alimtuhumu Mheshimiwa Waziri (Hussein Bashe, Waziri wa Kilimo) kuwa amelidanganya Bunge kwa kusema wamebadili kanuni za Nation Food Reserve Agency (NFRA) kuruhusu NFRA kuwa na mandate ya kuingiza sukari wakati hakuna tangazo la serikali lililotangazwa kuipa NFRA mandate ya kuingiza sukari, Waziri (Hussein Bashe, Waziri wa Kilimo) aliieleza kamati kuwa walitumia sheria ya usalama wa chakula sura ya 249 kukabiliana na uhaba wakati wa dharura kupitia NFRA ambapo alisema kuwa wameanza mchakato wa kubadilisha sheria ili NFRA waruhusiwe kuagiza, kuhifadhi na kusambaza sukari hata kwa kipindi kisicho cha dharura na mchakato huo ulianza kwa kutoa tangazo serikalini namba 225 (b) la tarehe 01 Aprili 2024" -Makoa

"Kamati ilipitia kifungu cha 14 cha sheria ya tasnia ya sukari kuhusu wanaoruhusiwa kuingiza sukari na kupitia kifungu cha 15 cha sheria ya usalama wa chakula ya mwaka 1991 na kubaini kuwa wakati wa dharura kama ilivyojitokeza sheria ya usalama wa chakula inakuwa na nguvu zaidi kuliko sheria ya tasnia ya sukari" -Makoa

"Kamati ilipata nafasi ya kujiridhisha kuhusu GN namba 25 (b) ya tarehe 01 Aprili 2024 na kupitia muswada wa sheria ya fedha iliona mapendekezo ya marekebisho yaliyoelezwa na Waziri kupitia kumbukumbu za Bunge na maelezo ya Waziri kamati ilikuwa na maoni kuwa hakuna uwongo uliozungumzwa na kwamba hakuna ukiukwaji wowote wa sheria uliofanywa" -Makoa

Ni sehemu ya maelezo ya Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Haki, maadili na madaraka ya Bunge Ally Makoa akiwasilisha Bungeni kuhusu tuhuma zilizotolewa na Mbunge wa Kisesa (CCM) Luhaga Mpina dhidi ya Waziri wa Kilimo Hussein Bashe.

WABUNGE WAKUBALIANA KUMFUNGIA MPINA VIKAO 15 VYA BUNGE
Luhaga Mpina, Mbunge wa Kisesa amefungiwa kuhudhuria vikao 15 vya Bunge kuanzia Juni 24, 2024 kwa kosa la kukiuka Kanuni za Bunge, kudharau Mamlaka ya Spika na mwenendo wa shughuli za Bunge, atarejea Bungeni katika kikao cha pili cha Novemba, 2024

Mpina ametiwa hatiani baada ya kuzungumza na Wanahabari kuhusu ushahidi aliouwasilisha kwa Spika kabla ushahidi huo haujawasilishwa mezani au kupewa idhini na Bunge kufanya hivyo

Awali, Mpina alidai Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe alilidanganya Bunge kuhusu Uagizaji wa sukari Nchini

Spika wa Bunge, Tulia Ackson amesema Mpina hatakiwi kufika eneo la Bunge wala kujihusisha na shughuli zozote za Bunge wakati wa adhabu yake

PIA SOMA
- Spika Tulia amburuza Luhaga Mpina Kamati ya Maadili

- Luhanga Mpina apewa siku 10 na Spika kuleta ushahidi wa Bashe kulidanganya Bunge

- Luhaga Mpina: Usambazaji wa sukari haukuwa ukifanywa na mfanyabiashara mmoja wa Mwanza pekee, Waziri Bashe alidanganya

- Luhaga Mpina amshukia Waziri Bashe, adai amelidanganya Bunge, awataja Magufuli, Rais Samia
 
Mpina ni jasiri ana heshima yake mbele ya jamii ya watanganyika. Kamati inasema tu ilijiridhisha na GN bila kutuwekea hicho kithibitisho ili nasi tuone, wajinga sana.

Hiyo adhabu anayopewa na wajinga haina maana kwa watanganyika kwasabau wanajielewa, wao sio wajinga.

Haiwezekani wale waliompiga vita Mpina wakiongozwa na Spika Tulia, wakishirikiana na mama Abdul leo wamtendee haki, hiyo mahakama ni batili haina fairness.

• Hii kamati inataka kutudanganya watanganyika kwamba, wakati wa dharura, serikali inaweza kuagiza sukari hata kwa kutumia kampuni zisizo na ujuzi kwenye hiyo issue ilimradi sheria iwaruhusu? na isiyo na mtaji wa kutosha kama ile stationery ya mtaji wa 1 million kuagiza sukari ya bilion 6.6?!

Kamati ya wapuuzi wanajibu hoja za Mpina kama watoto.

Spika Tulia na hiyo kamati yake wasitufanye wajinga, wao wote hawana mamlaka ya kumhoji Mpina kwa kitendo chake cha kuongea na wapiga kura wake nje ya bunge, wasitake kulifanya bunge liwe juu ya mamlaka na uhuru wa watanganyika kutoa maoni yao kikatiba.

Bunge ni lile jengo tu pale Dodoma ambapo wakiwa ndani yake ndio hutakiwa kusema chochote wasishtakiwe, lakini wakitoka nje ya lile jengo wao ni wabunge wa kawaida na raia kama tulivyo wengine, wasijikuze.

Simply Mpina ameonewa, hastahili kuadhibiwa kwani hajavunja sheria yoyote ya nchi, standing orders za bunge haziwezi kuwa juu ya katiba yetu, mafisadi walaaniwe, shame on them.

Hoja za Mpina zijibiwe, mmeshindwa kuzijibu kutuonesha nyie ni mafisadi wa vitendo na ushahidi upo, adhabu yoyote kwa Mpina haitafuta dhambi ya ufisadi wenu, aibu iwe kwenu.
 
Hayo ni Maigizo ya CCM wakikaribia uchaguzi. Kumtoa mtu wao kafara ili awe mgombea wa urais wa upinzani halafu baada ya uchaguzi anarudi ccm.

Chadema, Act msiingie kwenye huo mtego. 2025 Tundu lissu achukue fomu ya urais.

Ohoo!Msiingie mtego, mtapigwa za uso 🤣
 
Kamati Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge imewasilisha bungeni taarifa ya kamati hiyo kuhusu tuhuma za Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina, jijini Dodoma leo Juni 24, 2024

Mbunge wa Mtera, Livingstone Joseph Lusinde amesema kutokana na tuhuma zinazomkabili Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina kuhusu kumtuhumu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe kuwa alilidanganya Bunge kuhusu sakata la Uagizaji wa Sukari, anatakiwa kufungiwa kuhudhuria vikao 15 vya Bunge

Ameyasema hayo Bungeni baada ya Mwenyekiti wa Kamati Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge, Ally Makoa kuwasilisha Bungeni Taarifa ya Kamati kuhusu tuhuma hizo, leo Juni 24, 2024
---
"Mheshimiwa Luhaga Mpina (Mbunge wa Kisesa) alimtuhumu Mheshimiwa Waziri (Hussein Bashe, Waziri wa Kilimo) kuwa amelidanganya Bunge kwa kusema wamebadili kanuni za Nation Food Reserve Agency (NFRA) kuruhusu NFRA kuwa na mandate ya kuingiza sukari wakati hakuna tangazo la serikali lililotangazwa kuipa NFRA mandate ya kuingiza sukari, Waziri (Hussein Bashe, Waziri wa Kilimo) aliieleza kamati kuwa walitumia sheria ya usalama wa chakula sura ya 249 kukabiliana na uhaba wakati wa dharura kupitia NFRA ambapo alisema kuwa wameanza mchakato wa kubadilisha sheria ili NFRA waruhusiwe kuagiza, kuhifadhi na kusambaza sukari hata kwa kipindi kisicho cha dharura na mchakato huo ulianza kwa kutoa tangazo serikalini namba 225 (b) la tarehe 01 Aprili 2024" -Makoa

"Kamati ilipitia kifungu cha 14 cha sheria ya tasnia ya sukari kuhusu wanaoruhusiwa kuingiza sukari na kupitia kifungu cha 15 cha sheria ya usalama wa chakula ya mwaka 1991 na kubaini kuwa wakati wa dharura kama ilivyojitokeza sheria ya usalama wa chakula inakuwa na nguvu zaidi kuliko sheria ya tasnia ya sukari" -Makoa

"Kamati ilipata nafasi ya kujiridhisha kuhusu GN namba 25 (b) ya tarehe 01 Aprili 2024 na kupitia muswada wa sheria ya fedha iliona mapendekezo ya marekebisho yaliyoelezwa na Waziri kupitia kumbukumbu za Bunge na maelezo ya Waziri kamati ilikuwa na maoni kuwa hakuna uwongo uliozungumzwa na kwamba hakuna ukiukwaji wowote wa sheria uliofanywa" -Makoa

Ni sehemu ya maelezo ya Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Haki, maadili na madaraka ya Bunge Ally Makoa akiwasilisha Bungeni kuhusu tuhuma zilizotolewa na Mbunge wa Kisesa (CCM) Luhaga Mpina dhidi ya Waziri wa Kilimo Hussein Bashe.

WABUNGE WAKUBALIANA KUMFUNGIA MPINA VIKAO 15 VYA BUNGE
Luhaga Mpina, Mbunge wa Kisesa amefungiwa kuhudhuria vikao 15 vya Bunge kuanzia Juni 24, 2024 kwa kosa la kukiuka Kanuni za Bunge, kudharau Mamlaka ya Spika na mwenendo wa shughuli za Bunge, atarejea Bungeni katika kikao cha pili cha Novemba, 2024

Mpina ametiwa hatiani baada ya kuzungumza na Wanahabari kuhusu ushahidi aliouwasilisha kwa Spika kabla ushahidi huo haujawasilishwa mezani au kupewa idhini na Bunge kufanya hivyo

Awali, Mpina alidai Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe alilidanganya Bunge kuhusu Uagizaji wa sukari Nchini

Spika wa Bunge, Tulia Ackson amesema Mpina hatakiwi kufika eneo la Bunge wala kujihusisha na shughuli zozote za Bunge wakati wa adhabu yake

PIA SOMA
- Spika Tulia amburuza Luhaga Mpina Kamati ya Maadili

- Luhanga Mpina apewa siku 10 na Spika kuleta ushahidi wa Bashe kulidanganya Bunge

- Luhaga Mpina: Usambazaji wa sukari haukuwa ukifanywa na mfanyabiashara mmoja wa Mwanza pekee, Waziri Bashe alidanganya

- Luhaga Mpina amshukia Waziri Bashe, adai amelidanganya Bunge, awataja Magufuli, Rais Samia
 
Hawezi kugombea Urais , MPINA anafaa kua Waziri Mkuu
Hayo ni Maigizo ya CCM wakikaribia uchaguzi. Kumtoa mtu wao kafara ili awe mgombea wa urais wa upinzani halafu baada ya uchaguzi anarudi ccm.

Chadema, Act msiingie kwenye huo mtego. 2025 Tundu lissu achukue fomu ya urais.

Ohoo!Msiingie mtego, mtapigwa za usoMPINA
 
Hayo ni Maigizo ya CCM wakikaribia uchaguzi. Kumtoa mtu wao kafara ili awe mgombea wa urais wa upinzani halafu baada ya uchaguzi anarudi ccm.

Chadema, Act msiingie kwenye huo mtego. 2025 Tundu lissu achukue fomu ya urais.

Ohoo!Msiingie mtego, mtapigwa za uso 🤣
Zitto Kabwe ameshatangaza kugombea uRais wa JMT kwa niaba ya Kambi ya upinzani
 
Back
Top Bottom