Bunge Lakatizwa Ghafla!

Bunge Lakatizwa Ghafla!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,
Nimekuwa nikifuatilia kikao cha Bunge asubuhi hii live kupitia TBC, mara ghafla matangazo yakakatishwa ghafla, TBC kwanza wakaweka promos na baadaye documentary ya underwater.

Kwanza nilidhani ni technical problem ya TBC, nikahamia Star TV ili niendelee na Bunge maana na wao huwa wanarusha live, nikakuta nil.

Ndipo nilipododosa toka source fulani Bungeni akaniambia Bunge limeahirishwa ghafla for technical problem.

Vyombo vyetu vya habari lazima viwatendee haki wateja wake kwa kuwanotify something, the usual one ni ile excuse ya kawaida

" Tunawaomba radhi watazamaji wetu, hatutaweza kuendelea na matangazo haya kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu, asanteni"

Hii ingetosha, hili la kukatisha tuu matangazo, no excuse ni a bit rude!

KWA MSAADA WA BLOG YA MROKI
======================

PM.JPG

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mbunge wa Karatu, Dr. Wilbroad Slaa kwenye ukumbi wa zamani wa Bunge wa Pius Msekwa mjini Dodoma jana. Bunge lilihamia katika ukumbi huo baada ya mfumo wa sauti katika ukumbi mpya wa Bunge kupata hitilafu.

Joho.JPG

Askari akihamisha joho la Spika kutoka kwenye ukumbi mpya wa Bunge kwenda kwenye ukumbi wa zamani wa Msekwa baada ya mfumo wa sauti katika ukumbi mpya leo.

Siwa.JPG

Askari wakihamisha siwa kutoka kwenye ukumbi mpya wa Bunge kwenda kwenye ukumbi wa zamani wa Msekwa baada ya mfumo wa sauti katika ukumbi mpya leo.

Bunge.JPG

Spika wa Bunge Samwel Sitta akiingia kwenye ukumbi wa zamani wa Bunge wa Msekwa baada ya mfumo wa sauti wa ukumbi mpya wa Bunge kupata hitilafu jana.
 
Au wanahofia tutaona uozo wao? mjadala wa TICTS leo ndani ya nyumba. Hii Bongo bana hakuna aliye msafi wizi mtupuuuuuuuuuuuuuuu
 
bunge ndo wamekatiza mjadala au vyombo vya habari vimekatisha matangazo? whats the problem? au wameona unga ukimwagwa tena!!
 
bunge ndo wamekatiza mjadala au vyombo vya habari vimekatisha matangazo? whats the problem? au wameona unga ukimwagwa tena!!
Bigirita, jina lako linanichanganya na Birigita,
Ni bunge ndio wamesitisha mjadala ghafla na sio vyombo vya habari. Technical problem huweza kutokea popote, naamini hivyo vyombo vya habari, walielezwa bungeni sababu za kuahirishwa ghafla, walichotakiwa kufanya ni wao kutujulisha sisi watazamaji wao, na sio kukatiza ghafla na hawakusema chochote hadi sasa, program zingine zinaendelea as if nothing happened.
 
Si taarifa atatupa Mzee wetu au kuna kifungu kinachozuia wabunge kutoa taarifa ya yatokanayo bungeni? kwani hawa wazushi wasituzingue Bunge ni la nani?
 
Tupe feed back mkuu! kama umejua nini kinaendelea.
Dreamliner, hata mimi nilikuwa nafuatilia toka kwenye TV tuu, siko Dodoma, feedback ya ukweli lazima itoke Dodoma, huyo source wangu wa hapo Bungeni ameniambia kwa sentensi moja tuu, technical problem, nikashindwa kumuulizia zaidi asijejihisi kama namhoji.
 
mitambo ya kurekodia yaani hansard imeleta shida kidogo na bunge haliwezi kufanya kazi bila mitambo hiyo ndio maana kikao kimeharishwa kwa muda.
 
Si taarifa atatupa Mzee wetu au kuna kifungu kinachozuia wabunge kutoa taarifa ya yatokanayo bungeni? kwani hawa wazushi wasituzingue Bunge ni la nani?
N-handsome, hakuna kifungu kinachozuia wabunge kutoa taarifa ya yatokanayo, taarifa rasmi itatolewa na Spika watakapokutana leo saa 10 jioni kwa kikao cha mchana.
 
Wanabodi,
Nimekuwa nikifuatilia kikao cha Bunge asubuhi hii live kupitia TBC, mara ghafla matangazo yakakatishwa ghafla, TBC kwanza wakaweka promos na baadaye documentary ya underwater.

Kwanza nilidhani ni technical problem ya TBC, nikahamia Star TV ili niendelee na Bunge maana na wao huwa wanarusha live, nikakuta nil.

Ndipo nilipododosa toka source fulani Bungeni akaniambia Bunge limeahirishwa ghafla for technical problem.

Vyombo vyetu vya habari lazima viwatendee haki wateja wake kwa kuwanotify something, the usual one ni ile excuse ya kawaida

" Tunawaomba radhi watazamaji wetu, hatutaweza kuendelea na matangazo haya kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu, asanteni"

Hii ingetosha, hili la kukatisha tuu matangazo, no excuse ni a bit rude!

Hatuweji kujifunza kitu hata kama tumesoma. Tuna 'tendency' ya kufanya yaleyale yanayoendana na hulka zetu. Ndiyo maana hata twende nchi gani yenye maendeleao kujifunza tukirudi nyumbani tunasahau as if hatujafika kabisa. Mfano, mzuri ni viongozi wetu. Kwani wametembelea nchi ngapi zenye maendeleo na ni kitu gani wameiga ili kifanyike hapa Tz? Pole Pasco, that's the real Mtz.
 
mitambo ya kurekodia yaani hansard imeleta shida kidogo na bunge haliwezi kufanya kazi bila mitambo hiyo ndio maana kikao kimeharishwa kwa muda.
Asante PhD, kumbe ni mitambo ya kurekodia sauti. Haya mambo ya mitambo yametufikisha mahali kila kitu sasa tunategemea mashine, nijuavyo mimi, ma hansard reporters ni yale majitu ambayo yako very fast kwa kuandika tena wanatumia hatimkato/shorthand. Bunge lilikuwa likiendeshwa hivyo siko zote.

Sababu hiyo ni lack of innovation, kama kweli ni mitambo ya hansard tuu, pale bungeni wana digital camera zinarekodi kila kitu, hivyo bado kikao kingerekodiwa kwa hiyo video camera na baadae watu wa hansard waka reap sound track toka digita video.

TBC1,wako hapobungeni, wanarekodi kila kitu kwa camera zao, Ofisi ya Bunge si ingeomba sound track yao na kuwapatia hao hansard reporters!.

TBC-Taifa wamefunga mitambo yao ya sauti humo mjengoni, wanarekodi kila kitu, ofisi ya Bunge imeshindwa nini kuomba msaada?!. Hapo sijawataja Star TV, hawa wasingeomba kwa vile ni chombo binafsi kingehisiwa kuweza kuhujumu.

Tanzania bana!. all and all, ni baadhi ya 'kasi na viwango' !.
 
Hatuweji kujifunza kitu hata kama tumesoma. Tuna 'tendency' ya kufanya yaleyale yanayoendana na hulka zetu. Ndiyo maana hata twende nchi gani yenye maendeleao kujifunza tukirudi nyumbani tunasahau as if hatujafika kabisa. Mfano, mzuri ni viongozi wetu. Kwani wametembelea nchi ngapi zenye maendeleo na ni kitu gani wameiga ili kifanyike hapa Tz? Pole Pasco, that's the real Mtz.

Magobe T, hii ndio bongo yetu..Bongo tambarare..!.
 
Nimeonana na mtazamaji wetu wa Tv wa familia ameniambia kuwa TBC walitangaza kuwa kumetokea matatizo ya kiufundi ndiyo maana wanakatisha matangazo.
 
Mitambo ya kurekodia sauti ndio isababishe kikao kiahirishwe!
 
Kutakuwa na umeme wa mgao Dom mpaka jenereta litoke USA bunge lijalo.
 
Kweli kikao cha Bunge kilipoanza kwa wimbo wa Taifa pamoja na Dua picha
ilikuwa haina sauti kwa Star TV na TBC, nilitegemea wangewaeleza watazamaji matatizo
ya pale Bungeni lakini wameendelea kwa kuonyesha vipindi vyengine bila ya taarifa ya
kuomba radhi ili watazamaji waweze kuelewa kama Bunge linaendelea na kikao chake
au nalo limeahirishwa.
 
Jamani msiwe na wasiwasi, mfumo wa mawasiliano pale Mjengoni umebuma ila nimesikia wanahamia kwenye Mjengo wa zamani yaani leo hadi kieleweke kwa kweli..
 
wanafanyakazi kazi kwa mazoea, kwanini hawakuajiandaa kwani bunge la mwisho lilikuwa lini.
wanaficha uchafu wao tu wote wako ovyo.

Back
Top Bottom