Bunge Lampa Tano Rais Samia kwa Kujenga Vituo Maalum vya Kudhibiti Wanyama Wakali Nchini

Bunge Lampa Tano Rais Samia kwa Kujenga Vituo Maalum vya Kudhibiti Wanyama Wakali Nchini

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii, imempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kusikiliza kilio cha wananchi kuhusu wanyama wakali na waharibifu na kuwajengea vituo na kutoa vifaa vya kukabiliana na changamoto hiyo katika maeneo mbalimbali nchini.
Gj_hSoAXsAAQZhO.jpg

Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Mhe. Timotheo Mnzava (Mb) ametoa shukrani na pongezi hizo wakati kamati hiyo Februari 17, 2024 ilipokuwa ikitamatisha ziara yake ya siku 3 katika Mkoa wa Tanga kukagua mradi mbalimbali ambapo leo imekagua ujenzi wa kituo maalum cha kukabiliana na tembo kilichokamilika kwa asilimia 100 katika kijiji cha Goha kata ya Mkumbara, wilayani Korogwe.

"Tumeridhishwa na kazi kubwa na nzuri inayofanywa na Mheshimiwa Rais wetu kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii katika kukabiliana changamoto hii katika kipindi kifupi, kwa niaba ya kamati naomba nimshukuru na kumpongeza sana" amesisitiza Mhe. Mnzava

Kituo hicho ambacho kimetumia milioni 48 kukamilika pia Serikali imetoa vifaa yote muhimu ikiwa ni pamoja na samani, ndege nyuki 1, gari 1 na askari sita ambao watakuwa kituoni hapo wakati wote.
Gj_hSn-XwAAX4EA.jpg

Kituo hicho ambacho kina vyumba vikubwa 3, Ofisi moja, jiko, bafu na choo kitasaidia kukabiliana na changamoto hiyo katika vijiji zaidi ya kumi vinavyovunguka eneo hilo.

Baadhi ya vijiji vitakavyofaidika moja kwa moja na kituo hiki ni pamoja na Manga, Mtitiro, Masira, Kwenangu, Mkomazi na Mikochen imeeleza taarifa ya Hifadhi ya Ngorongoro, taasisi ambayo imepewa jukumu la kujenga na kusimamia.
Gj_hSn7XcAAXuZo.jpg

Aidha, Mnzava ameitaka Wizara kuhakikisha mara baada ya kukamilisha vituo hivyo kuleta vifaa yote muhimu na watumishi wanaohitajika na wawepo muda wote.

Kamati hiyo iliambatana na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dunstan Kitandula, Katibu Mkuu, Dkt. Hassan Abbasi, Naibu Katibu Mkuu, Kamishina wa Polisi, Benedict Wakulyamba na watendaji kutoka wizarani na kwenye taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo.
Gj_hSoEW0AABzGL.jpg
 
Akumbuke pia kulipa madeni ya watu wa bonde la mto msimbazi. Tuliambiwa mradi unaanza mwezi wa pili 2025 lakini hakuna dalili na mkataba na world bank ulishasainiwa kwa mujibu wa maneno ya wazirihusika kupitia vyombo vya habari
 
Back
Top Bottom