Bunge lapitisha muswada wa marekebisho ya sheria za hifadhi ya jamii

Suala la kikotoo limekaaje hapa? Watu kulipwa theluthi ya michango yao wanapostaafu? 🤔
 
Nakeleka sana na hii tabia ya ccm jiwe aliharbu sana kipondi chake kuuletea huu mfuko siasa. Na kuuwekea sheria ili aweze kuchota pesa zaid.
Hakuna kiongozi aliyeharibu mifuko kama Kikwete,sema watanzania wengi ni wasahaurifu..aliyepitisha SSRA,sijui kufuta fao la kujitoa ni Kikwete...mimi ni mdau mkubwa sana na nimehudhuria sana vikao wakati huo Jenister Mhagama akiwa mwenyekiti kamati ya mambo ya jamii bungeni,Kikwete alikuwa anawatumia sana Zitto na Msigwa kufanikisha hizi sheria kupata sapoti ya upinzani,nakumbuka mwaka 2010-2015 watu wa migodini walipokuja juu,Zitto akiwa naibu wa kambi ya upinzani bungeni akachezesha karata kuomba kamati ya uongozi wa bunge wakutane kujadili ili kuzuia Mswada uliokuwa umepelekwa na Jaffo (Jafo akiwa Mbunge) usijadiliwe kuhusu kupitia sheria waliokuwa wameipitisha kwenye bunge lilopita wakati huo...
Baada ya kamati ya uongozi wa bunge kukutana wakaja na pendekezo kwamba sheria isitekelezwe kwanza...sio kwamba ifutwe...hapana isimamishwe mpaka pale kanuni zitakapo tungwa...wakampa jukumu Waziri husika kuhakikisha kanuni zinatungwa...hizi sheria zote za kishenzi na za dharura kuhusu Mifuko ya Jamii zimetungwa kipindi cha Kikwete.
Magufuli alipoingia viongozi wa TUCTA na mifuko ya hifadhi wakamfuata kumuomba utekelezaji wa sheria zilizokuwa zimesitishwa tu kutumika,TUCTA na wawakilishi wengi wa serekali wakiaminishwa kuwa kufanya hivyo kutaboredha zaidi mafao yao kufikia kiwango walichokuwa wanapata wastaafu wa mashirika ya Uma...Kalakabao wakawa wamepigwa kekundu,kushtuka wakaanza kulalamika kwa Magu tena,kama unakumbuka mkutano mmoja Magu akazuia sheria kutumika na akawa anashangaa kwa nini mifuko hawataki kuwapa wastaafu pesa zao zote...akaamuru sheria itumike kuanzia 2025...
 

Sijaona hapo kama lengo ni kumsaidia mfanyakazi ,serikali ikileta muswada bungeni lengo ni kujinufaisha yeye kama yeye na si mlaji(mwananchi)...Wenye mifuko(wafanyakazi) wenyewe wanataka kikotoo kiondolewe ,wafanyakazi wanataka akishmaliza kazi kuwe na option ya kuchukua mzigo wake na si kumlazimisha mpaka miaka 55..
 
Mtoa mada amekurupuka. Alicholeta ni news headline. Alipaswa a dig deep ili kutaja kipengele husika kilichobadilika
Kwa namna nikivyomsikiliza Waziri Ridhiwani Kikwete, ni kuwa mabadiliko makubwa ya mifuko hiyo, ni pale mwanachama anapofikia umri wa kustaafu, lakini Mwajiri wake hajapeleka michango yake, ambayo alikuwa akikatwa toka Kwenye mishahara yake.............

Hivi sasa mifuko hiyo itamlipa mwanachama huyo mafao yake, halafu mifuko hiyo ndiyo itskayo-deal na waajiri hao wakorofi😁
 
Wakati wakikwete mtu akiachishwa kazi alikua anapewa mafao yake yote, au mkataba ukiisha alilipwa stahiki zote Tena kwa mkupuo. Magufuli ndio alibadili Sheria akaja na mambo ya kikokotoo, baadae alivyoona watu wanalalamika sana akasimamisha kisitumike Bali kifanyiwe maboresho. Acha kumtetea kwenye hili.
 
Unadili na matokeo hudili na mchakato. Mtaalamu Ikizu Bukama kadadavua mchakato uliokoanzia na chanzo cha tatizo halisi kakupa timeframe na key events zilivokuwa zinatokea. Wewe unadili na matoke tu rubbish kabisa
Soma hapo tayari watu walikuwa wanagomea hilo fao la kujitoa kufutwa hiyo ni 2012 na SSRA akiwa culprit sawia na mtaalamu alivotuelezea hapo juu
 
Sheria ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma, Sura ya 371, na Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi, Sura ya 263.
Swali la uelewa! Eti ni kwa watumishi wa umma tu!?? vipi sekta binafsi?
Vipi kikokotoo kwa sekta binafsi?
 
Ndo maana nakwambia haya mambo huyafahamu vizuri,Kikwete ndo alitunga hiyo sheria na baada ya watu kuwa wakali,ikabidi sheria ihairishwe,sina haja ya kumtetea yoyote kwenye hili,fuatilia hiyo sheria ni ya mwaka gani....yani pamoja na maelezo niliyotoa hujaelewa chochote
 
Wote hao ni wale wale kila mmoja kwenye awamu Yake anatengeneza namna ya kupiga haswaa,, Nchi yenyewe yenye Katiba ya kiduwanzi inayotengeneza viongozi waduwanzi,, waliozaliwa na kutoka kwenye jamii za kiduwanzi.
 
Na ndicho unachoulizwa kama Kikwete alisema ihairishwe kwa nini Mwendazake aliitekeleza licha ya aliyeisaini kuona ametoa boko?.
 
Mtu alipwe fedha zake zote pindi ukomo wa ajira unapofika au ukifanyika

Kinyume cha hapo ni MAHOKA TUU
Hili ndio la msingi watu wapewe Fedha zao tu nasihivyo tu, pia fao lakujitoa lirudishwe Ili watu wastaafu kazi za kuajiriwa mapema wakajiajiri.
 
Na ndicho unachoulizwa kama Kikwete alisema ihairishwe kwa nini Mwendazake aliitekeleza licha ya aliyeisaini kuona ametoa boko?.
Sheria ikishapitishwa is either ifutwe au itekelezwe,kumbuka Kikwete kwa kiasi kikubwa alikuwa hawakilishi michango ya wafanyakazi,kwa hiyo liquidity ya mifuko ilikuwa hoi,na pesa iliyokuwa imechangwa toka private sector ndo ikawa imewekezwa kwenye majengo yasiokuwa na wapangaji
 
moyoni huwa ninahisi kuwa Tz hatuna Bunge. Hivi tuna Bunge kweli?!

YESU NI BWANA&MWOKOZI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…