Bunge lapitisha Muswada wa Marekebisho ya Sheria za Ulinzi wa Mtoto

BUNGE LAPITISHA MUSWADA, MAREKEBISHO YA SHERIA ZA ULINZI WA MTOTO.

Na WMJJWM, Dodoma

Bunge la Tanzania limepitisha muswada wa marekebisho ya sheria zinazohusu ulinzi wa mtoto wa mwaka 2024 leo Agosti 30, 2024 jijini Dodoma.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima, akiwasilisha Muswada huo amesema madhumuni yake yanalenga kuondoa upungufu uliojitokeza wakati wa utekelezaji wa baadhi ya masharti ya sheria hizo ili kuimarisha ulinzi na maslahi bora ya mtoto.

Amebainisha kuwa, muswada huo umetoa mapendekezo katika sheria tatu ambazo ni Sheria ya Makosa ya Kimtandao Sura ya 443, Sheria ya Mtoto, Sura ya 13 na Sheria ya Msaada wa Kisheria, Sura ya 21.

Waziri Dkt. Gwajima amesema kazi ya kuboresha sheria na miongozo mbalimbali inayohusu ulinzi wa mtoto itaendelea kufanyika kama kazi endelevu kwani, kwa sasa kasi ya mabadiliko kwenye jamii ni hasa katika mazingira ya maendeleo ya ulimwengu wa kidigitali.

"Kila mwaka hatutasita kuja na marekebisho ya Sheria kutokana na Kasi ya mabadiliko ya kijamii kwenye ulimwengu wa maendeleo ya kidigitali kwani, kasi hiyo pia inagusa maendeleo na ustawi wa maisha ya watoto wetu katika rika mbalimbali" amesema Waziri Dkt. Gwajima.

Akiwasilisha maoni ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii Mhe. Michael Kembaki ameishauri Serikali kuhakikisha sheria zote zinazohusu ulinzi wa mtoto zipitiwe upya ili kuendana na mazingira ya sasa, kutenga bajeti ya kuendesha mabaraza ya watoto pamoja na kuongeza kasi ya kuajiri Maafisa Ustawi wa Jamii.

Soma Pia:
Nao baadhi ya wabunge wakichangia kuhusu Muswada huo wameipongeza Serikali kwa kuona umuhimu wa kufanya marekebisho ya Sheria zinazuhusu ulinzi wa mtoto ili kumlinda mtoto na mabadiliko ya sayansi na teknolojia na vitendo vya ukatili na udhalilishaji.

MWISHO
Ivi watoto wanawezaje kufanyiwa ukatili wa kingono mtandaoni pindi wanapotumia simu janja?
Mtu ambaye hamjuani Wala hamjawai kuonana unawezaje kumkatili kingono mtandaoni au ni Mimi sijalewa?
Na huwo muswada WA kuwalinda watoto kimtandao utajuaje anayetumia mitandao ya kijamii kwa wakati huo kwamba ni mtoto au mtu mzima Ili ludhibiti maudhui yake?
Mimi naona jukumu kubwa liko kwenye kutoa elimu zaidi kwa wazazi pengine ingesaidia zaidi.
Ili tuweze kujilinda na kuwalinda walengwa wa huu ukatili
 
Ivi watoto wanawezaje kufanyiwa ukatili wa kingono mtandaoni pindi wanapotumia simu janja?
POP-up ads unazijua hauzijui? Jibu alafu tuendelee kuna POP-up ads na POP-under ads sasa POP-up ads unazijua?

Mfano: Ime POP-up pornographers ads yupo kwenye browser eeh akibinya si unajua watoto wanavyopenda kubinyabinya akiona hiki anataka akione zaidi na zaidi na zaidi eeh sasa akibinya hapo kahama ndio ukatili unaanzia hapo

Wewe unajua mwanao kakodolea Simu anaangalia katuni YouTube kumbe kuna Wahuni wachache wasioelewa km hio Simu janja muda na wakati huo inatumiwa na mtoto mdogo washamwamisha anaangalia mambo mengine ya kingono ambayo hakupaswa kuangalia kwa umri alionao kwa hio anafanyiwa ukatili wa kingono

Hio ni 1 ukihitaji 2 useme nitakwambia wanafanyiwaje ukatili wa kingono mtandaoni na hio IPO wazi

Mfano: tiktok tiktok na mtandao X X X .com zamani twitter takataka za ajabu utazikuta huko sasa mtoto akibinyabinya akatumbukia huko atakayokumbana nayo ni ukatili wa kingono kwa umri wake

Hio ni 2 ukitaka na 3 useme nitakwambia tu bila shida yoyote
 
Hongera sana Mheshimiwa waziri, una heshima yetu hapa jukwaani maana unapambana na unajibu hoja Kwa wakati, tungepata mawaziri 7 wa aina yako maendeleo ingekua chap,
 
Malezi ya mtoto yanaanza na wwe mzazi, ukitegemea hizi sheria ndiyo zikulindiea mwanao utakuja kuula wa chuya ,wazazi tuwe serious sana na malezi bora ya watoto wetu kama sisi tulivyolelewa zamani na wazazi wetu!!
 
Simu janja weka mbali na mtoto atakutana na mambo ya wakubwa huo ni Ukatiri kwa mtoto
 
POP-up ads unazijua hauzijui? Jibu alafu tuendelee kuna POP-up ads na POP-under ads sasa POP-up ads unazijua?

Mfano: Ime POP-up pornographers ads yupo kwenye browser eeh akibinya si unajua watoto wanavyopenda kubinyabinya akiona hiki anataka akione zaidi na zaidi na zaidi eeh sasa akibinya hapo kahama ndio ukatili unaanzia hapo

Wewe unajua mwanao kakodolea Simu anaangalia katuni YouTube kumbe kuna Wahuni wachache wasioelewa km hio Simu janja muda na wakati huo inatumiwa na mtoto mdogo washamwamisha anaangalia mambo mengine ya kingono ambayo hakupaswa kuangalia kwa umri alionao kwa hio anafanyiwa ukatili wa kingono

Hio ni 1 ukihitaji 2 useme nitakwambia wanafanyiwaje ukatili wa kingono mtandaoni na hio IPO wazi

Mfano: tiktok tiktok na mtandao X X X .com zamani twitter takataka za ajabu utazikuta huko sasa mtoto akibinyabinya akatumbukia huko atakayokumbana nayo ni ukatili wa kingono kwa umri wake

Hio ni 2 ukitaka na 3 useme nitakwambia tu bila shida yoyote

Kwa nini umpe Mtoto mdogo smartphone?
 
Hongera sana Mheshimiwa waziri, una heshima yetu hapa jukwaani maana unapambana na unajibu hoja Kwa wakati, tungepata mawaziri 7 wa aina yako maendeleo ingekua chap,
Hakika...

Kongole kwake [emoji7]
 
POP-up ads unazijua hauzijui? Jibu alafu tuendelee kuna POP-up ads na POP-under ads sasa POP-up ads unazijua?

Mfano: Ime POP-up pornographers ads yupo kwenye browser eeh akibinya si unajua watoto wanavyopenda kubinyabinya akiona hiki anataka akione zaidi na zaidi na zaidi eeh sasa akibinya hapo kahama ndio ukatili unaanzia hapo

Wewe unajua mwanao kakodolea Simu anaangalia katuni YouTube kumbe kuna Wahuni wachache wasioelewa km hio Simu janja muda na wakati huo inatumiwa na mtoto mdogo washamwamisha anaangalia mambo mengine ya kingono ambayo hakupaswa kuangalia kwa umri alionao kwa hio anafanyiwa ukatili wa kingono

Hio ni 1 ukihitaji 2 useme nitakwambia wanafanyiwaje ukatili wa kingono mtandaoni na hio IPO wazi

Mfano: tiktok tiktok na mtandao X X X .com zamani twitter takataka za ajabu utazikuta huko sasa mtoto akibinyabinya akatumbukia huko atakayokumbana nayo ni ukatili wa kingono kwa umri wake

Hio ni 2 ukitaka na 3 useme nitakwambia tu bila shida yoyote
Kweli apo nakubali Kuna siku mama moja alinipa nimsetie simu yake anadai watoto wake wanachezeaga,,, notification nilizokutananazo ase awo watoto lazima wapagawe
 
Eenh ilikuaje kuaje hapo Watoto kupagawa kutokana na ukatili wa kingono mtandaoni au kupagawa na nini? Au na Wewe ulikua unakutana nazo unabinyabinya tu?
 
Izo notification Zina picha zenye maudhui ya kingono inaonyesha waliziaccept bila kujua wanachofanya mimi nilichofanya ni kuziblock na nikamwambia mwenye simu asiruhusu watoto wake wasihezee simu hasa kwenye mitandao ya kijamii maana inaonyesha ni tabia yao kudowload game mtandaoni na kuangalia video
 
Back
Top Bottom