Bunge likutane haraka kuondoa ukomo wa mgombea Urais Tanzania

Bunge likutane haraka kuondoa ukomo wa mgombea Urais Tanzania

toa upumbavu wako hapa
Tatizo la wengi wamemshambulia mleta mada badala ya kujadili mada yenyewe.

Tumpe nafasi afunguke zaidi ili tupate kiini cha hii hoja.

Shocker , ni nini kiini cha hii hoja yako..utawala uliopo umefanya nini cha kufanya kufikiri kuondoa ukomo wa kutawala!?
 
Ndipo pale inaposemwa wenye wivu wajinyonge,mnatoka povu aafu povu lenyewe la kangara,sasa maneno yasio na heshima ya nini ? Nyie watu wa ajabu yaani aondoke yeye mbaki nyie mnaojua kutunga matusi mitandaoni.

Mi nakumbuka tuliomba sana tupate kiongozi mchapa kazi asieogopa na anaeweza kupambana asiemuonea haya mtu ,anampa mtu makavu mbele ya kadamnasi,umeona yule waziri aliekuwa hajui kuunganisha herufi , kilio kimesikika mbinguni na tumeletewa kiongozi anaeongoza watu na kuwasimamia ,nchi sasa inasimamiwa vizuri mno kuliko tulivyozoea.

Bunge la serikali kwa vile lipo na asilimia kubwa ni wachama cha Magufuli na hawatashindwa wacha kuondoa ukomo hata wakiamua sasa hivi nchi iwe na Mfalme ,linapita kwa asilimia miamoja.

Mbona Lesotho wana Mfalme na hatusikii haya makelele ya upinzani pinzani,hili nalo neno tulifikirie ,Sasa Mheshimiwa Magufuli ni Mfalme mtarajiwa,hivi la ajabu litakuwa lipi ? Lesotho haipo mbali ni mfano hai,haya ya kuwa na vyama vya wapinzani wengine wanapika pilau,wengine wanachemsha bata wengine wanapandisha tanga wengine wanavaa makoti kama madaktari wa wanyama pori. Ni balaa tu.

Na nchi yetu ilivyo tajiri chini ya Mfalme Magufuli tutaondoka hapa tulipo na kupiga hatua za mwendo kasi kuelekea maendeleo kamili kwa kila mwananchi,mpaka asie na kazi atalipwa.
 
Ndipo pale inaposemwa wenye wivu wajinyonge,mnatoka povu aafu povu lenyewe la kangara,sasa maneno yasio na heshima ya nini ? Nyie watu wa ajabu yaani aondoke yeye mbaki nyie mnaojua kutunga matusi mitandaoni...
Reference yako iwe miaka mitano iliyo pita na hii ijayo
 
Ni wakati mwafaka Bunge letu tukufu likutane ili lipitishe uondoaji wa kikomo kugombea urais, ile miaka kumi sasa isiwepo. Kama mtu anafaa na hali inamruhusu aendelee milele hadi kifo kitakapomuondoa.

Lakini hapa pia litayarishe Tume huru japo kutakuwa na jamaa wenye mkono mkono, ila ikubalike na wapinzani wote.
Pia watumishi wote wasiwe wanasitaafu ,waendelee kuwa kazini hadi kifo.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Mheshimiwa Kessy Hili Jambo Lako Kaa Nalo Moyoni
Bunge Lijalo Tukirudi Salama Uanze Nalo Mwenyewe!!!
Atake Asitake Mpaka Afie Kwenye Kiti Ndiyo Ukweli Wenyewe


Mheshimiwa Job Ndugai
Ova.
 
Ni wakati mwafaka Bunge letu tukufu likutane ili lipitishe uondoaji wa kikomo kugombea urais, ile miaka kumi sasa isiwepo. Kama mtu anafaa na hali inamruhusu aendelee milele hadi kifo kitakapomuondoa.

Lakini hapa pia litayarishe Tume huru japo kutakuwa na jamaa wenye mkono mkono, ila ikubalike na wapinzani wote.
Piga Gwajima awe waziri .

Na pia wamteue jokate kuwa mkuu wa mkoa
 
Mheshimiwa Kessy Hili Jambo Lako Kaa Nalo Moyoni
Bunge Lijalo Tukirudi Salama Uanze Nalo Mwenyewe!!!
Atake Asitake Mpaka Afie Kwenye Kiti Ndiyo Ukweli Wenyewe


Mheshimiwa Job Ndugai
😁😁😁😁😁😁,chali cha mende!
 
Ni wakati mwafaka Bunge letu tukufu likutane ili lipitishe uondoaji wa kikomo kugombea urais, ile miaka kumi sasa isiwepo. Kama mtu anafaa na hali inamruhusu aendelee milele hadi kifo kitakapomuondoa.

Lakini hapa pia litayarishe Tume huru japo kutakuwa na jamaa wenye mkono mkono, ila ikubalike na wapinzani wote.

Mkiwa wanufaika sababu mlipita bila kupingwa mnajiangalia nyie bila kujali Jamii inayoteseka. Je akitokea mwingine asiyefaa nae akae milele. Pili unatumia vigezo gani kupima kufaa kwa mtu
 
Kha! Binadamu mna nongwa kweli
Angekubali yangekua maneno..... Sasa amekataa ndio kubali yake🙄🙄
Umewaona eeih !
sasa kuna wau wanauliza vipimo vya Mfalme mtarajiwa ,eti miaka mitano iliyopita,nionavyo kama ni kutengeneza barabara unahitaji mikakati na utafiti bila kuwacha upimaji ,itakuwa huelewi nazungumza nini,miaka mitano na mitano mingine ni kusafisha maeneo ambapo barabara itapita,miaka mitano iliyopita tumeona ni kwa jinsi gani ameweza kusimamia viongozi au viranja ambao anawahitaji katika kusafisha barabara ,ameweza kuweka sawa kukata milima kuchonga mabonde ni pilikapilika za kuinyoosha njia na bado anajipanga.

Usiwe na tamaa ya maendeleo ndani ya miaka mitano,usiniambie CCM ipo miaka 54 kuna mitume na manabii walivutana na wafuasi na wapinga Mungu kwa miaka zaidi ya mia+ ,kwa hio tulieni.

jambo lingine usiifananishe serikali iliyopita ya huyu huyu Mheshimiwa Magufuli na hii aliyoiunda sasa hii imekuwa upgraded more powerful kuliko iliopita ,na upgraded sio kwa kubadili watu,hapana kiujumla imekuwa inawajibika na imezidi kuwa karibu na wananchi.

Kila kiongozi sasa anaona umuhimu wa yeye kuwa na kuitwa kiongozi na kusimamia waliochini yake kwa uleule ujumbe wa mwalimu Nyerere ,tusimuonee haya mtu.
wazungu wameendelea kwa kuwa wameondoa mambo ya kuoneana haya,tunasikia Husein nae amesema hatamuonea haya mtu,huyu mtoto wa fulani huyu rafiki,huyu nilisoma nae hapana. Huko ndio kutmia miaka kuchonga njia,njia ya Tanzania tunayoitaka.

Nikirudi kwenye mada Bunge letu lisidharau wala kuogopa vipaza sauti vya upinzani ,ni haki yao ila mwisho wa siku wataelewa na kukaa kimya kama Maalim Seif na wengine sasa wapo kimya wakijadiliana namna ya kusema Tanzania kwanza upinzani unapokaribia uchaguzi.

Kwa maoni yangu hata wakiamua kuweka Mfalme Tanzania basi sio shida ukoo wa Magu umeonyesha kuthubutu kuiongoza Tanzania,ni kuamua japo maamuzi mengine magumu.ila huko tunakoelekea tutaona tumechelewa sana.

sasa hivi kila raia anaelalamika kwenye vyombo utamsikia Mheshimiwa Magufuli kama unanisikia au unatusikia hapa mtaani kuna hiki na kile, GEAR HABIB TV inarusha malalamiko ya raia wasioogopa kmshitakia raisi moja kwa moja,iwe wanaemshitaki ni raia au kiongozi wa serikali,wanamwaga kila kitu ,sasa jiulize kwa nini wananchi wamefikia kueleza hayo, mjue Magu ni mfalme alieletwa Tanzania na wananchi masikini ndio wanamuelewa,ila wale walanguzi wa upinzani wanaona gere mirija yao sasa imezibwa.
 
Back
Top Bottom