Hivi unaamini Viongozi wa CCM Zanzibar na wenyewe wanataka muungano uvunjike kirahisi rahisi tu?! Hivi hushangai hata zile Kura za Maoni (for Katiba Mpya), ni Pemba ndiko walipendekeza zaidi Suala la Serikali 3 ukilinganisha na Unguja?!
Zanzibar waliotaka muungano ni wale walio madarakani tu ambao mara zote wanatishwa kutoka huko tanganyika wasijaribu kuvunja muungano na zaidi ni kwa maslahi yao binafsi., Sasa kama pemba tu sehemu ndogo ndio iliyotaka serikali 3 kwanini Warioba alikuja na referendum ya Watanzania wanataka serikali 3?
WHY? Pemba ilikuwa ni ngome ya CUF wakati Unguja ni ngome ya CCM!! Kwahiyo hao akina Lukuvi wanasimamia kiapo chao cha "imma fahima, lazima muungano uendelee"
Kama Unguja ni ngome ya CCM kwanini jecha alifuta uchaguzi 2015?? use your head
Ni sawa na kusema Msukuma asinunue ardhi Dar es salaam kwa sababu Usukumani ardhi ni kubwa ukilinganisha na Dar es salaam!!
Lengo la mtanganyika kutaka ardhi Zanzibar ni kujenga makanisa na kueneza ukiristo hamtafanikiwa
Jiulize wewe kwanini Karume akakukbali kulazimishwa?!
Karume alipokuja kudai mamlaka ya zanzibar
aliuwawa baada ya mchongameno kwishafanikiwa alilokuwa anataka hakuna asiyejua
Kiroja hiki!! Hivi unafahamu kwamba mfumo unaotumika hivi sasa ni kwamba, SMZ wanakusanya kodi zao kupitia ZRB na JMT inakusanya kodi kupitia TRA? Lakini linapokuja suala la matumizi, pesa za ZRB ni Zanzibar peke yake lakini zinazokusanywa na TRA zinatumika pande zote mbili!!
Hakuna hela ya TRA inatumika kwa maendeleo ya Zanzibar., zile 4% wanazodai kuzipeleka zanzibar tokea uhuru zimeanza kupelekwa zanzibar baada samia kuwa rais., na kwanini Zanzibar wapewe 4% wakati mulikubali kuunganisha nchi 2 huru?? ni vile munaneemeka kupitia jasho la wazanzibari ndio mana mnagoma kuachia, TRA ndio inawatia umasikini zaidi Zanzibar
Na nyie chanzo chenu cha mapato kinachowawezesha kulipana mishahara ni nini?! Hivi kwa akili yako unadhani Wazanzibar wenzako wote waliopo ZNZ wanalipwa kwa pesa za ZRB?
Sasa Kama zanzbar hawana vyanzo vya mapato TRA na Ofisi zao wanafanya nini kule Zanzibar, Hiyo mishahara yenu na maposho mungetoa wapi tanganyika?
Yaani Tanganyika ifaidike kupitia mgongo wa Zanzibar?! Ikiwa kodi yote inayokusanya na ZRB inatumika Zanzibar, sasa hiyo Tanganyika inanufaika nini kutoka Zanzibar?! Tanganyika ina-import nini kutoka Zanzibar?
Narudia kusema Tanganyika wanachukua mapato yote ya bandari pale Zanzibar, TRA kila leo wanakusanya hela nyingi kutoka Zanzibar ndizo munazolipana mishahara yenu, chakula chenu na maposho mbali mbali, mnajenga hizo barabara, flyover, sjuwi sgr nk
Kimataifa Tanganyika ikipata misaada au helza maendeleo kutoka World bank na mashirika mengine Zanzibar hamupeleki maendeleo munajinufaisha Tanganyika tu.
Lete mfano wowote Serikali ya Muungano ilijenga au onyesha mradi wowote Tanganyika iliwafanyia wazanzibari lakini mkienda kutandaza bakuli mnaitaja Serikali ya Muungano, mlisema maalim seif ni mwarabu ataleta waarabu lakini Anna Makinda alivaa baibui la kamba na ninja akaenda kupiga magoti Omani, watu gani nyie bora mupotelee mbali tu vunja muungano huu wa kidhalimu
Kwani wakati wa JPM hapakuwa na kelele?! Wakati wa JK hapakuwa na kelele?! Au na wenyewe ni Wazanzibari?
Nani alisubutu kuinua mdomo wake wakati wa JMP? Unaambiwa JPM miaka yake 5 alikopa trilioni 29 Ndugai alikuwepo hakusema chochote, alijenga airpot kule kwao hakuna yoyote aliyeiunua mdomo wake zaidi ya wapinzani.,
Fikiria saivi Mama ajenge uwanja wa ndege kule kwao makunduchi unguja si itakuwa balaa kubwa zaidi., Samia amekaa miezi 9 tu sasa nongwa hazishi., yaani mumeongoza Jamuhuri ya Muungano miaka 60 bado mnataka muendelee na madaraka tu njaa tupu., wakati umefika sasa Zanzibar kuishika JMT mpaka baada ya miaka 60 ndio irudi huko Tanganyikani kama hamtaki tuvunje muungano.