Bunge linalokuja mwezi Februari lijadili kwa hati ya dharura Mkopo wa tril 1.3. kwa maslahi ya Taifa. Namna ulivyopatikana na matumizi yake

Bunge linalokuja mwezi Februari lijadili kwa hati ya dharura Mkopo wa tril 1.3. kwa maslahi ya Taifa. Namna ulivyopatikana na matumizi yake

Sawa!
JamiiForums344346608.jpg
 
Hivi unaamini Viongozi wa CCM Zanzibar na wenyewe wanataka muungano uvunjike kirahisi rahisi tu?! Hivi hushangai hata zile Kura za Maoni (for Katiba Mpya), ni Pemba ndiko walipendekeza zaidi Suala la Serikali 3 ukilinganisha na Unguja?!
Zanzibar waliotaka muungano ni wale walio madarakani tu ambao mara zote wanatishwa kutoka huko tanganyika wasijaribu kuvunja muungano na zaidi ni kwa maslahi yao binafsi., Sasa kama pemba tu sehemu ndogo ndio iliyotaka serikali 3 kwanini Warioba alikuja na referendum ya Watanzania wanataka serikali 3?
WHY? Pemba ilikuwa ni ngome ya CUF wakati Unguja ni ngome ya CCM!! Kwahiyo hao akina Lukuvi wanasimamia kiapo chao cha "imma fahima, lazima muungano uendelee"
Kama Unguja ni ngome ya CCM kwanini jecha alifuta uchaguzi 2015?? use your head
Ni sawa na kusema Msukuma asinunue ardhi Dar es salaam kwa sababu Usukumani ardhi ni kubwa ukilinganisha na Dar es salaam!!
Lengo la mtanganyika kutaka ardhi Zanzibar ni kujenga makanisa na kueneza ukiristo hamtafanikiwa
Jiulize wewe kwanini Karume akakukbali kulazimishwa?!
Karume alipokuja kudai mamlaka ya zanzibar aliuwawa baada ya mchongameno kwishafanikiwa alilokuwa anataka hakuna asiyejua
Kiroja hiki!! Hivi unafahamu kwamba mfumo unaotumika hivi sasa ni kwamba, SMZ wanakusanya kodi zao kupitia ZRB na JMT inakusanya kodi kupitia TRA? Lakini linapokuja suala la matumizi, pesa za ZRB ni Zanzibar peke yake lakini zinazokusanywa na TRA zinatumika pande zote mbili!!
Hakuna hela ya TRA inatumika kwa maendeleo ya Zanzibar., zile 4% wanazodai kuzipeleka zanzibar tokea uhuru zimeanza kupelekwa zanzibar baada samia kuwa rais., na kwanini Zanzibar wapewe 4% wakati mulikubali kuunganisha nchi 2 huru?? ni vile munaneemeka kupitia jasho la wazanzibari ndio mana mnagoma kuachia, TRA ndio inawatia umasikini zaidi Zanzibar
Na nyie chanzo chenu cha mapato kinachowawezesha kulipana mishahara ni nini?! Hivi kwa akili yako unadhani Wazanzibar wenzako wote waliopo ZNZ wanalipwa kwa pesa za ZRB?
Sasa Kama zanzbar hawana vyanzo vya mapato TRA na Ofisi zao wanafanya nini kule Zanzibar, Hiyo mishahara yenu na maposho mungetoa wapi tanganyika?
Yaani Tanganyika ifaidike kupitia mgongo wa Zanzibar?! Ikiwa kodi yote inayokusanya na ZRB inatumika Zanzibar, sasa hiyo Tanganyika inanufaika nini kutoka Zanzibar?! Tanganyika ina-import nini kutoka Zanzibar?
Narudia kusema Tanganyika wanachukua mapato yote ya bandari pale Zanzibar, TRA kila leo wanakusanya hela nyingi kutoka Zanzibar ndizo munazolipana mishahara yenu, chakula chenu na maposho mbali mbali, mnajenga hizo barabara, flyover, sjuwi sgr nk

Kimataifa Tanganyika ikipata misaada au helza maendeleo kutoka World bank na mashirika mengine Zanzibar hamupeleki maendeleo munajinufaisha Tanganyika tu.

Lete mfano wowote Serikali ya Muungano ilijenga au onyesha mradi wowote Tanganyika iliwafanyia wazanzibari lakini mkienda kutandaza bakuli mnaitaja Serikali ya Muungano, mlisema maalim seif ni mwarabu ataleta waarabu lakini Anna Makinda alivaa baibui la kamba na ninja akaenda kupiga magoti Omani, watu gani nyie bora mupotelee mbali tu vunja muungano huu wa kidhalimu
Kwani wakati wa JPM hapakuwa na kelele?! Wakati wa JK hapakuwa na kelele?! Au na wenyewe ni Wazanzibari?
Nani alisubutu kuinua mdomo wake wakati wa JMP? Unaambiwa JPM miaka yake 5 alikopa trilioni 29 Ndugai alikuwepo hakusema chochote, alijenga airpot kule kwao hakuna yoyote aliyeiunua mdomo wake zaidi ya wapinzani.,

Fikiria saivi Mama ajenge uwanja wa ndege kule kwao makunduchi unguja si itakuwa balaa kubwa zaidi., Samia amekaa miezi 9 tu sasa nongwa hazishi., yaani mumeongoza Jamuhuri ya Muungano miaka 60 bado mnataka muendelee na madaraka tu njaa tupu., wakati umefika sasa Zanzibar kuishika JMT mpaka baada ya miaka 60 ndio irudi huko Tanganyikani kama hamtaki tuvunje muungano.
 
Naunga mkono hoja, kwani Kuna tetesi nimesikia kuwa zenji wamepata mgawo wa Bil. 200. Hii haikubaliki kulingana na uwiano wa watu na eneo Kati ya bara na zenji
wakipata bilioni mia mbili na ushee ni sawa kwa kuzingatia uwiano wa idadi ya watu wa 1.7 : 60. Ili mradi kiasi hicho na riba yake pia kije kirudishwe na wazanzibari. Isije kuwa wale wazanzibari halafu walipe watanganyika!!
 
Zanzibar ni nchi huru, mchongameno aliungana na zanzibar kwa hiyari yake chochote kinachopatikana ni nusu kwa nusu na sio izo bil200 asilimia 4 sijui., mama ana kazi bado ya kupeleka hizi fedha zanzibar miaka mingi tanganyika wanazitumia hizi hela peke yao, wamejenga madaraja sijui wamenunua ndege, flyover na ma sgr kule zanzibar hakuna kitu., lakini on top of that zanzibar wanalipa kodi zinaenda tanganyika kupitia TRA., ni unyama mkubwa hawa wanyamawezi wanaowafanyia wazanzibari
Zanzinzibar wana ZRA , wana BOZ.
 
Zanzibar wanapewa asilimia za mkopo kisheria, kama tunaona wanapewa zaidi ni kubadili sheria na kupunguza kiasi kulingana na hali halisi.
Hatuwezi kulalamika kwenye jambo tulilojitungia sheria wenyewe.
Hizi siyo zama za kutawaliwa na mzamzibar tubadili Sheria
 
W
Umeongea vyema, na Bado wazanzibar awaoni faida ya Muungano wengi wanaitaji kujitoa kwa kisingizio Cha kutokua na tija kwao
Wakijitoa tunafukuza wapemba wote waliojaa kila kona Tz bara. Halafu tunawarudisha Wanyamwezi (Wazanzibara) huku Tanganyika na kila mmoja tunamkabidhi shamba heka 5!! Tanganyika ina mapori hayana wa kuyalima.
 
Kila siku Tanzania matahira wanaongezeka.Ni tahira peke yake ndiye anaweza kuamini kuwa Tanzania kuna Bunge.

Hili Bunge hewa litatoa wapi uthubutu wa kuhoji Serikali ambayo ndiyo iliwapa hawa wabunge hewa ubunge?
 
Taahira baba yako,je ikitokea wakahoji na ukweli ukajulikana kama ilivyokuwa kwenye Escrow na Richmond?
Escrow na richmond lilikuwa ni Bunge la wananchi.Lilikuwa ni Bunge ambalo wabunge wake walitokana na wananchi.

Bunge hili halijatokana na wananchi.Bunge hili wabunge wake wametokana na uchafuzi wa serikali ya CCM katika ule uchaguzi mkuu.

Bunge hili lina wabunge wa CCM ambao hata wana CCM wenyewe wanawakana kuwa siyo wabunge wao kwa sababu kwenye kura za maoni walipitishwa kibabe watu ambao hawakuwa ni chaguo la wana CCM.Ni Bunge la maajabu.
 
Bongo vilaza Ni wengi Sana na ndio maana wanasiasa wanazidi kuzalisha vilaza wa kutosha.
Return ya huo mkopo Ni Nini au faida ya kujenga madarasa mengi bila kuwa na Walimu wa kutosha faida yake Ni Nini?
Karne hii unachukua mkopo unajenga madarasa et hayo ndio maendeleo.
Je unajua Elimu inakoelekea Karne hii.
Je unajua kipato Cha Mwalimu ambae ndie mtoa hiyo Elimu?
Je kipi Bora uwe na walimu wa kutosha alafu madarasa machache au uwe na madarasa mengi huku walimu wa kuunga unga
Waliochukua mkopo huohuo na kununulia barakoa nao unawaweka kundi gani?.
 
Acheni kumchanganya mama!mbona mikopo ya Magufuli haikujadiliwa Wala kupitishwa na BUNGE?!au mnamdharau MAMA kwa kuwa ni mwanamke?!kwa taarifa yenu uraisi ni TAASIS,Nyuma ya Mama TUPO wanaume kibao tunaomuunga mkono


#kaziIendeLee
 
Taahira baba yako,je ikitokea wakahoji na ukweli ukajulikana kama ilivyokuwa kwenye Escrow na Richmond?
kwanini tulalamikie bilioni 200 hatangalii bilioni 1,100 tuliyobaki nayo Bara mleta mada angeanza na Spika ni nani atakayechaguliwa je atapita chini ya Mkiti wa CCM aweze kuhoji mkopo huo?
 
Hivi tangu muungano mpaka leo tumewapiga ngapi znz?

Tuache ubishi na u Tz tuongee ukweli
Miaka ya nyuma nilienda pemba na unguja kwa kweli ni dhiki sana yaani kwa sasa hela nyingi zikipelekwa huko ni haki yao

Sisi yakijengwa madaraja tunapinga
Barabara tunapinga sasa wao wakipata mgao kwanini tulie lie wakati hatutaki maendeleo?
 
Kila kitu kiwekwe sawa na ukweli ujulikane. Hata kama ni mkopo wa WB kupitia janga la Uviko lakini kuna giza nene.

Bunge linalofuata mwezi Februari liisimamie serikali iweke wazi namna pesa zilivyotumika na kugawanywa kati ya Zanzibar na Bara.

Bara ni sh ngapi kwa ajili ya nini? Na Zenj sh ngapi kwa ajili ya nini? Matumizi yawekwe wazi kuna siri kubwa.
Naongezea.. Lijadidili pia zile more than 1.5trl manunuzi ya mwewe bila idhini ya bunge.....
 
Mikopo kuwa siri haijaanza leo wala jana wakati mwingine ni sehemu ya masharti ya wanaotukopesha.

Hizi siasa za chuki dhidi ya nani anayeiongoza awamu ya sita, haziwezi kubadilisha tamaduni na taratibu za mikopo tunayopewa na taasisi za dunia ya kwanza.
Kwani watu kutaka kujua ni tatizo!? Kama watu wanakopa wanaenda kutumia kwa mipango tofauti na waliyoombea mkopo, ndio itashindwa serikali!? Kwa kuwa mikopo kuwa siri haijaanza leo, kwa hiyo huo ndio utaratibu sahihi!?
 
Kila kitu kiwekwe sawa na ukweli ujulikane. Hata kama ni mkopo wa WB kupitia janga la Uviko lakini kuna giza nene.

Bunge linalofuata mwezi Februari liisimamie serikali iweke wazi namna pesa zilivyotumika na kugawanywa kati ya Zanzibar na Bara.

Bara ni sh ngapi kwa ajili ya nini? Na Zenj sh ngapi kwa ajili ya nini? Matumizi yawekwe wazi kuna siri kubwa.
kwanini mnatuzuga? kwanini ufafanuzi niwamkopo wa 1.3 tl pekee? Kama mikopo ndani ya miezi9 ni tl10 na zaidi kwanini hoja isijikite hapa? Nakama niukuaji wa deni nimkubwa kuliko kawaida kwanini tusifuate ushauri napendekezo la Nape?
 
Kwani watu kutaka kujua ni tatizo!? Kama watu wanakopa wanaenda kutumia kwa mipango tofauti na waliyoombea mkopo, ndio itashindwa serikali!? Kwa kuwa mikopo kuwa siri haijaanza leo, kwa hiyo huo ndio utaratibu sahihi!?
Hatawakiweka taratibu zote wazi pengine haitaweza kuzuia kama nchi tusiendelee kukopa.
 
Kuna haja ya kuendelea kubana uhuru wa kujieleza, wewe ni nani hadi uhoji mamlaka? Wasiojulikana waongezewe bajeti kwa sababu wasaliti wanaongezeka.
 
Back
Top Bottom