Bunge lisitishe kusafirisha abiria usiku, hali sio shwari

Bunge lisitishe kusafirisha abiria usiku, hali sio shwari

Njia za udhibiti vyombo vya moto ziongezwe, trafiki wawe wengi sana ,vifaa vya kisasa vifungwe, abiria waelimishwe wajibu wao, namba za simu ziwekwe wazi ili abiria akiona vitendo visivyafaa vya madereva iwe rahisi kupiga simu, kuwepo na vituo vingi vya ukaguzi, abiria wakitoa malalamiko kwa madereva safari isiendelee mpaka dereva abadilishwe mara nyingine dereva anaposhtakiwa anakuwa katika msongo wa mawazo na makosa ya dereva mmiliki pia awajibike moja kwa moja hii itawafanya wamiliki kutafuta madereva bora.
 
Si ndio nyie mlishangilia wakati mama yenu kupitia kinana anapunguza matrafic barabarani, mkisema anafuta legacy?
 
Mbona East Africa wote wanasafiri usku na ajali sio nyingi Kama kwetu tatizo huku ni mwendo amini nakwambia Mara nyingi nimekua nikisafiri Kenya na uganda kwakweli utaboreka mwendo mdogo lakini ni salama gari ni usiku kucha hakuna haraka
 
Nimesema tu, wenye mabasi waendelee kuchangia
Vinginevyo abiria wanao safari usiku wawe na Bima kubwa
Ajali zipo muda wowote, yule mama aliyekatika mkono alikuwa akiendesha basi mchana jua linawaka, wale polisi maharusi walipata ajali Iringa huku jua likiwa linawaka na ajali nyingi za malori zinazotokea Mbeya hutokea huku jua likiwaka.
 
Hujapatwa na Shida Wewe.. Usiogope kufa,, Usiku tusafiri pia Kwa umakini.
 
Si ndio nyie mlishangilia wakati mama yenu kupitia kinana anapunguza matrafic barabarani, mkisema anafuta legacy?

Kinana alisema traffic wa mjini sio huko high way

Sasa kariakoo traffic anakwambia washataa saa Saba mchana what if gari yako haitembei usiku?
 
Safari salama ya usiku ni ile ya treni tu
 
Pamoja na uzembe wa madereve lakini barabara zetu zinachangia, ni mbovu, nyembamba - hadi hapo tutakapokuwa na uwezo wa kuweka double road ndipo tutapona na hizi ajali
Umenena vyema mkuu. Kama hakuna barabara bora hizo ajali haziwezi kukoma haiwezekani barabara ndogo kiasi hicho iudumie nchi zote za majirani na ujumlishe na population yetu sisi Watz halafu ufikirie kuwa ajali zitaisha. Tutabaki kuongoza vibao vya 50 visivyo na tija na kuongeza ulaji kwa matrafiki
 
Nimesema tu, wenye mabasi waendelee kuchangia
Vinginevyo abiria wanao safari usiku wawe na Bima kubwa
Tatizo ni askari wa usalama barabarani, wao kutwa kucha ni kuchukua hela kwa madereva, swala la usalama halina msimamizi tena
 
Uzembe wa maderava...
Muundo wa barabara kutokuwa dual carriage au zaidi...
Mabasi na malori kutofaniwa ukaguzi wa mara nyingi iwezekanavyo...
.
.
.
.
Mwisho kabisa tusisahau mambo yetu yale ya mauzauza...
 
Wakodiwe madereva toka Kenya au Somalia wasiosinzia hovyo kutokana na kubugia mirungi toka utotoni watuendeshee basi zetu
 
Back
Top Bottom