Bunge litunge Sheria ili mali ambazo hazikuandikiwa wosia zimilikiwe na Serikali inapotokea mmiliki amefariki

Hii itasaidia kila mtu mwenye mali sehemu awe anatunza wosia na kuufanyia marekebisho mpaka siku anapofariki.

Wosia uandaliwe kwa kufuata matakwa ya kisheria na ikiwezekana kuwe na centralized electronic database ya kutunza wosia. Mahakama ndio itoe idhini ya kufungua akaunti ya marehemu kujua wosia unasemaje.

Itasaidia sana kuondoa migogoro inayofuatia baada ya mtu kuaga dunia. Itaboresha mahusiano baina ya ndugu.

Serikali itakuwa imeongeza chanzo cha mapato ikiwa watu hawataandika wosia. Kimsingi faida kubwa zaidi kwa serikali ni uwepo wa mahusiano mazuri katika jamii baada ya misiba.
Halafu sheria hiyo pia iweke bayana kuwa mali zote zilizopatikana au zinazopatikana kutokana na michango ya wananchi katika shughuli za kitaifa ni ya umma, siyo ya chama cha siasa.
 
H
🤣🤣 Mkuu unataka kuanzisha mpambano na sisi wa imani nyingine?
Hapana - ila Sikubaliani na wazo la mleta mada kwamba serikali ilazimishe wosia ziandikwe kabla ya kuaga dunia! Kwanza, je! Wosia uandike wakati mtu ana umri gani?
 
Kukiwa na ulazima wa kuandika wosia kuna tatizo gani? Mtu aandike wosia mara baada ya kuwa na mali yoyote kama umri wake umefikia miaka 18.
 
Utaratibu huo unafaa nchi zilizoendelea ambazo zinamchango mkubwa wa pato lako la kila siku, kwa huku Africa ambako toka uzaliwe unaangaika kama kuku wa kienyeji, serikali haijui kama unakula, unaumwa haijui lolote juu ya maisha yako ni wewe tu na Mungu wako, jamaa, watoto na marafiki ndio wanaangaika na wewe mpaka siku ya mwisho, serikali inaanzaje kuchukua mali za marehemu huoni kama hiyo dhuruma kubwa.
 
Hii itasaidia kila mtu mwenye mali sehemu awe anatunza wosia na kuufanyia marekebisho mpaka siku anapofariki.

Wosia uandaliwe kwa kufuata matakwa ya kisheria na ikiwezekana kuwe na centralized electronic database ya kutunza wosia. Mahakama ndio itoe idhini ya kufungua akaunti ya marehemu kujua wosia unasemaje.

Itasaidia sana kuondoa migogoro inayofuatia baada ya mtu kuaga dunia. Itaboresha mahusiano baina ya ndugu.

Serikali itakuwa imeongeza chanzo cha mapato ikiwa watu hawataandika wosia. Kimsingi faida kubwa zaidi kwa serikali ni uwepo wa mahusiano mazuri katika jamii baada ya misiba.
Hii Serikali haishindwi. Kama ilivyoamua kudhulumu Wazee wanaostaafu Mafao Yao kwa Kikokotooo.
 
Unajua wakati Mwingine Sheria za Mirathi ni upuuzi mtupu. Hivi inakujaje mama yangu kanisomesha Kwa tabu na Ndugu zangu Kwa maana kaka na dada zangu. Siku naoa mwanamke nikliyekutana naye Ukubwani baadaye nakufa ATI Mali zote zinakuwa za mke na watoto. Halafu mama na Ndugu walionitoa Nkololo Bariadi huko ambao waliokuwa wananitegemea wasipatee kitu atii!

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
Sheria ina assume wazazi watakufa kabla yako.🤣 Ndugu wengine wanatakiwa kujitafutia vyao. Mke anapewa nguvu kwasababu mnachuma pamoja.

Ndio maana mimi ninaamini zaidi kwenye kumwachia mtu aandike wosia kuamua matumizi ya mali anazoacha.
 
Haujui tu yanayoendelea mtu akifa ghafla , hoja ya mtoa mada ipo Sawa kabisa , taratibu za kimila Kwa sasa hazina nguvu, Mkono wa serikali ndo utakaotiisha , watu Wanauana Sana .... Wosia unatakiwa uwe updated kila mwaka
Nadhani serikali ibaki kuwa first Custodian wa mali za marehemu ambao hawajaandika mirathi na familia zinagombania mali
 
Huko teknolojia yenu ya asili haijaweza kuwasaidia?

Inasaidia kwenye mishemishe nyingine, lakini haitasaidia kwenye idea hii uliyoileta...

Si watu wote wenye kufikiwa na teknolojia ya mtandao, kiasi kwamba kukiwa na database ya serikali ni watu wawili watatu ndio wataweza kuwa na access nayo...
 
Ni kweli mkuu. Teknolojia inaweza kuwa moja ya changamoto za utekelezaji kwa baadhi ya maeneo. Kama anayeandika atafanya editing mara mbili kwa mwaka basi inawezekana hata kwa kuwa na access ya umma kwenye kila kata.

Kama wazo litakuwa la manufaa basi njia inaweza kufikiriwa.
 
Haki ya nani apate kiasi gani anayo mwenye mali mwenyewe. Anatakiwa tu afuate utaratibu wa sheria utakaowekwa.

Kukiwa na sheria ya kulazimisha kila mtu aandike wosia tutakuwa tumeruka kiunzi cha kwanza muhimu pindi mtu anapofariki.
A very strange take! Unafanya kama vile vifo vya wanadamu ni kitu kinachopangwa na mwanadamu yeyote. Umesahau kuwa matatizo yaliyoko katika mirathi ni pale mwenye mali kufa bila kuwepo na wosia. Mada ilikuwa ni serikali kuchukua mali za marehemu eti TU kwa kuwa hakukuwa na wosia. Do not pivot na kuleta mini topics. Sheria inayopendekezwa isaidie kwa kutambua madeni kwa watu na taasisi, madeni ya watu na taasisi kwa marehemu, haki ya wategemezi wake wa msingi (primary dependents) ili kumaliza matatizo. Hatuwezi kuwa na serikali inayomiliki mali za marehemu huku wanaostahili wako!
 
Sheria ikiwepo kila mtu ataandika wosia kwahiyo scenario unayoielezea haitakuwepo.
 
Hii itasaidia kila mtu mwenye mali sehemu awe anatunza wosia na kuufanyia marekebisho mpaka siku anapofariki.

Wosia uandaliwe kwa kufuata matakwa ya kisheria na ikiwezekana kuwe na centralized electronic database ya kutunza wosia. Mahakama ndio itoe idhini ya kufungua akaunti ya marehemu kujua wosia unasemaje.

Itasaidia sana kuondoa migogoro inayofuatia baada ya mtu kuaga dunia. Itaboresha mahusiano baina ya ndugu.

Serikali itakuwa imeongeza chanzo cha mapato ikiwa watu hawataandika wosia. Kimsingi faida kubwa zaidi kwa serikali ni uwepo wa mahusiano mazuri katika jamii baada ya misiba.
Utakufa masikini, blaza!
 
Back
Top Bottom