Bunge litunge sheria ya kuwalinda wazazi

Bunge litunge sheria ya kuwalinda wazazi

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Wazazi wanatumia rasilimali vitu, pesa, watu na pesa kumfikisha mtoto wao hadi kujitegemea. Rasilimali ambazo kama angeziwekeza zingemsaidia hata uzeeni kwake.

Wazazi wanaporwa haki na mali zao na vijitu na majitu kwa kisingizio Cha ndoa kwakuwa hakuna sheria inayosimamia haki zao. Ndoa zinapora haki zote za mtoto wake mwenyewe.

Hakuna sheria inayomshurutisha mtoto kumpa matumizi mzazi wake na wala mzazi kupata sehemu ya mali ya mtoto wake punde mtoto wake huyo atakapofariki. Hii ni dhuruma mbaya sana kuwahi kufanywa kwa watu ambao wamejitoa mhanga kuzaa, kulea, kutunza na kumsomesha mtoto wao kwa gharama kubwa sana.

Haiwezekani mume au mke awe mmiliki wa mali zote za mtoto wake na yeye kuachwa mikono mitupu na sheria. Yaani mke au mume afaidi mali ya mtoto wake wakati yeye anakufa njaa na kusubiri hisani TU ya mtoto wake ampe au asimpe chakula na matumizi.

Kuna wanawake na wanaume ambao sababu zao kubwa za kukubali kuokewa au kuoa ni za kupata maisha mazuri na kupata mali za mwenza TU, Hivyo atafanya kila mbinu kuithibiti hiyo mali ili Ndugu na wazazi wa mwenza wasipate hata tone. Ndugu na wazazi wanabakia kuwa watazamaji TU wakati mkwe wao akiogelea kwenye Raha.

Sheria ya wazazi itungwe ili watoto isiwe hiari kuwatunza wazazi wao na wazazi kupata sehemu ya mali ya mtoto wao kama mambo yataharibika.

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom