Bunge na ubinafsishaji wa Bandari ya Dar es Salaam, huu ni ufisadi mkubwa

Unalinganisha nchi ya wanaojielewa na Tanzania huku ambako wizo na ufisadi ukitokea adhavu yake ni kuitwa stupid? US wanafanya hayo kwa kuwa wapo vizuri kila eneo na sheria zao ni ngumu kwa mtu kuhujumu au kuiba
 
Utumbo wa uendeshaji? Mbona walisema sasa hivi kipindi Cha mama bandari Ina ufanisi wa Hali ya juu sana na mapato yameongezeka sana
 
Ikibinafsishwa ndio kila kitu kitakua poa? Mashirika mengi tuliyobinafsisha hakuna lililofanya vizuri zaidi yalianza kufa
 
Una wazimu sio bure.
 
Umeandika huku umepaniki, lakin pale bandarin kwakweli Mimi naona Bora wabinafishe tu maana tumekuwa tukisikia kila siku Kuna hujuma Mara makontena yamevushwa bila Kodi, Mara mifumo ya bandari na TRA haisomani, Mara mtu kapenyeza bomba la mafuta, na hayo Mambo kila kiongozi akienda bandarini lazima atoe/aone mapungufu, serikali inapoteza hela nyingi Sana kutokana na mismanagement ya watumishi wasio waminifu. Naona muwekazaji akiingia hata zile nafas za ajira zitatolewa kwa uwazi. Na mapato yataongezeka
 
Hakuna shirika la umma lilibinafsisgmhwa tukafanya vizuri, zaidi ndio hufa. Kwenye migodi tuliwaps watu kwa assumptions hizo lakini hadi leo hakuna nchi ilichopata zaidi
 
Hakuna shirika la umma lilibinafsisgmhwa tukafanya vizuri, zaidi ndio hufa. Kwenye migodi tuliwaps watu kwa assumptions hizo lakini hadi leo hakuna nchi ilichopata zaidi
Nitajie shirika moja wapo ambalo lilibinafishwa na wageni likafa....Kuna viwanda kibao vimekufa kwasabu ya uhujum, sahz ishu za ajira isingekuwa shida..hebu angalia operation za private sector zilivyo strong chukulia mfano wa mitandao ya simu ndo utajua
 
ATCL, TTCL et al
 
Umesema viwanda vilibinafsishwa vikafa, alafu hapo hapo unaniambia nikutajie shirika lililobinafsishwa likafa?

Tulibinafsisha trc, unajua kilichotokea?
Tulibinafsisha atcl unajua kilichotokea?
Tanesco tuliwapa wale wasouth Africa, nini kilitokea?
TTCL tuliwapa wale waholanzi, nadhani unakumbuka kilichotokea
UDA?
THB?
Hapo kweyewe TPA, tuliwapa ticts kuendesha hizo ghati je ufanisi uliongezeka? Mapato? Ikawaje tena tukaona bora hizo operations zirudi kuwa chini ya tpa?
 
Waarabu skills walizo nazo kuuza na kununua sasa hii ya kuendesha mitambo sidhani kama wanayo wao wenyewe kampuni zao zinaendeshwa na wataalamu wa kichina,wazungu.Hapo usikute ni TICS Huyo kwa mlango wa nyuma
 
Hayo mashirika sahz yapo chini yetu Nini kinaendelea....Yale matangazo ya posta na simu yalipotea baada ya kutoka muwekazaji
 
Huu mkataba utakuja vunjwa huko mbeleni na mmojwapo wa watawala.
 
Ni nani ameshauri jambo la ajabu kama hili?!
Twafa, masikini Tanzania.
 
Kwani watanzania hatuwezi kuendesha taasisi zetu hadi tumpe mwarabu, baada ya hapo tumpe na shirika la ndege halafu sisi tukae kijiweni kunywa gahawa na kashata, siyo?
Umasikini upo katika hali mbili, wa fikra na ule mali.
Mbaya zaidi ni ule wa fikra kwa kuwa unapoteza hata Ile mali ndogo iliyokuwepo.
Wahenga walisema, "Cha mlevi huliwa na mgema."
Kuna tatizo kubwa la tafsiri ya maendeleo katika nchi yetu. Kwa mfano tukiwapa wachina kandarasi ya kujenga barababa, tunaita maendeleo, ambapo ukweli tumeendeleza wachina sisi tukirudi nyuma.
 
Walianza na Ngorongoro na sasa ni Bandari yetu macho.
 
Mpaka mtakapotawaliwa na hao Waarabu ndipo mtapata akili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…