Bunge: Wabunge wanakatwa kodi zote stahiki ikiwemo 'PAYE''

Bunge: Wabunge wanakatwa kodi zote stahiki ikiwemo 'PAYE''

Yani izo milioni 12 zote zikatwe kodi mkuu! Mimi nimeona salary slip ya mtu wangu wa karibu yani basic inajumlishwa na posho nyingine ndo inakatwa kodi mkuu... Imagine na uyu ni mtumishi wa kawaida kabisa kwann wao basic tu ndo inakatwa kodi hii si sawa

Sent using Jamii Forums mobile app
Sentensi yako ya kwanza sijakupata vema. Kwamba nimesema zikatwe? Mimi ninamaanisha kwamba hawa jamaa kwa kawaida hawapo fair. Watalipa hiyo kodi,kisha watakachofanya watapaisha mshahara na marupurupu.

Hawaumii chochote kama vile wengi tunavyofikiria. Kwa mfano, kuna baadhi ya taasisi wanakatwa kodi kama kawa lakini mshiko wao ukitajiwa unaweza ukaachama mdomo kutwa nzima
 
Taxable income huwa ni kwenye basic kiongozi.. Gross ina allowances ambazo kwa wafanyakazi wa uma, huwa hawakatwi kodi kwenye allowancess..!!!

By the way, siyo unavyotaka wewe, bali inavyosema sheria..
Hivi hapa, kwanini kuna double standard? Wasiokuwa serikalini, paye inakatwa kwenye gross, walio serikalini paye inakatwa kwenye basic.

Serikalini, 10% ya PSSSF na zifananazo inakatwa kwenye basic, private wakatwa kwenye gross.

Kama kisingizio ni ukubwa wa mishahara kule private, sioni logic, posho za serikalini ni kunwa mno ambazo hazikatwi.

Kuna jamaa yuko taasisi ya serikali, basic ni 1.2mil, ila meal allowance yake kwa mwezi ni sh 750,000 achana na allowances nyingine nyingine
 
Taxable income huwa ni kwenye basic kiongozi.. Gross ina allowances ambazo kwa wafanyakazi wa uma, huwa hawakatwi kodi kwenye allowancess..!!!

By the way, siyo unavyotaka wewe, bali inavyosema sheria..
Wanakatwa mkuu niamini! Huku huku serikalimi mimi mtu wangu wa karibu sana naona pay slip zake jamaa wanapita na kodi yani mshahara unajumlishwa na allowances alafu ndo wanatoa Paye,nhif,pspf... Kamshahara kenyewe kadogo na bado wanapita na pesa ndefu sana i wish ningekuwa na uwezo nikuwekee iyo salary slip hapa ungelia walahi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Taarifa kuhusu Waheshimiwa Wabunge kukatwa Kodi .

Ofisi ya Bunge la Tanzania imesema kama ilivyo kwa Watumishi wengine wa Umma pamoja na Viongozi wa Kisiasa, Wabunge wanakatwa Kodi ikiwemo ya Mapato (PAYE) inayokatwa kwenye Mishahara yao kwa mujibu wa Sheria.

Kauli hiyo imekuja baada ya taarifa zinazodai Wabunge hawalipi Kodi kwenye Mishahara kusambaa Mitandaoni.

Zaidi, soma: Jerry Silaa: Wabunge tuanze kukatwa kodi kwenye Mishahara yetu
 
Attachments

  • 2854150_Slaa_kodi.mp4
    19.2 MB
Ushawai kufanya kazi kampuni binafsi? Kitu gani kinafanya Kampuni A ikate NSSF/PPF kwenye Gross na B kwenye Basic?
Mkuu
1. Tunaongelea kodi wewe unaleta mengine.
2. Per diem inakatwaje kodi
3. Kuna allowable allowances ambazo hazikatwi kodi kwa sababu ni mahsusi kwa ajili ya jambo fulani. Tuseme karo ya mwanao ni shs 1000- Mwajili anakupa 1000. Hiyo ikikatwa kodi inakaaje?
 
Kauli hiyo imekuja baada ya taarifa zinazodai Wabunge hawalipi Kodi kwenye Mishahara kusambaa Mitandaoni.
Aambatanishe Pay Slip ya mbunge mmoja afute tu jina la mbunge huyo kwenye barua hiyo. Na sisi raia tutaridhika.
 
Mshahara net wa Mbunge huo hapo milioni kumi na moja na zaidi

mbunge wa aanika wazi mbele ya wananchi.Kodi je inakatwa shi;lingi ngapi? Mbunge Lusinde alisema wanakatwa milioni moja na kitu la!!! Mamilioni yote hayo wanakatwa milioni moja na zaidi TU WAKATI WANACHUKUA MILIONI KUMI NA MOJA NA ZAIDI NET kwa mwezi

Cheki huyu mbunge akitaja mshahara wake kwenye mkutano wa hadhara

Si Mlete pay slip moja hapa Tuone?? Mbona haina shida Ndugai Leta Pay slip yako tuone...Nyie waongo hamuaminiki..Hamkatwi wala hamlipi kodi
 
Jerry slaa hajawahi kuangalia salary slip yake ndo maana hajui km anakatwa kodi au laah! Wabunge mtatapatapa sana huu mjadala ni non stop! Lipeni kodi washenzi nyie!!
 
Mkuu
1. Tunaongelea kodi wewe unaleta mengine.
2. Per diem inakatwaje kodi
3. Kuna allowable allowances ambazo hazikatwi kodi kwa sababu ni mahsusi kwa ajili ya jambo fulani. Tuseme karo ya mwanao ni shs 1000- Mwajili anakupa 1000. Hiyo ikikatwa kodi inakaaje?
Unatakiwa ujumlishe kila kitu kwenye mshahara, bonuses na marupurupu.

Allowable expenditure unatoa baada ya hapo based on receipt evidence.

Uwezi kupewa hela ya kulala laki mbili kwa siku halafu wewe ukalale kwa ndugu yako bure uachwe. Allowable expenditure yoyote inahitaji ushahidi.

Wabunge walipe kodi stahiki, halafu afadhali hao watumishi wa umma ndio salaleh kodi wanazoachiwa wabunge afadhali.
 
Mkuu
1. Tunaongelea kodi wewe unaleta mengine.
2. Per diem inakatwaje kodi
3. Kuna allowable allowances ambazo hazikatwi kodi kwa sababu ni mahsusi kwa ajili ya jambo fulani. Tuseme karo ya mwanao ni shs 1000- Mwajili anakupa 1000. Hiyo ikikatwa kodi inakaaje?

Ndio maana nimekuuliza ushawai kufanya kazi kwenye mkamapuni binafsi? Kampuni Binafsi allowance yeyote unayopata inalimwa kodi.
 
Kiinua mgongo chao kinatakiwa kukatwa kodi sababu wabunge hawachangii hata mia mifuko ya jamii kama NSSF au PSSF wanajizolea tu pesa za walipa kodi free.Wakatwe kodi wakilipwa

Ni unfair unamkabidhi mtu mamilioni ya mafao wakati hachangii mifuko ya jamii tax free

Wanapotaka wigo wa walipa kodi upanuliwe unatakiwa upanuke hadi kwao sio kwa wanyonge tu
 
Back
Top Bottom