Heri ya asubuhi wanajamvi wenzangu, ni matumaini yangu mu buheri wa afya na kwa wale wanaoumwa Mwenyezi Mungu awajalie nafuu ya haraka.
Bajeti Kuu ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mwaka wa fedha 2021/2022 kuwasilishwa leo Juni 10, 2021 Bungeni katika Bunge la Tanzania jijini Dodoma saa 10:00 jioni na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Nchemba ameeleza kuwa Bajeti ya mwaka huu ni Bajeti ya kimkakati na ikumbukwe kwamba uwasilishaji wa leo utakuwa ni wa kwanza kwa Serikali ya awamu ya sita ambayo inaongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Moja ya watu waliopewa mwaliko maaalum wa kushuhudia uwasilishaji huu Bungeni ni wajumbe wa Kamati Kuu (KK) ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi.
Matangazo ya moja kwa moja ya uwasilishaji wa Bajeti Kuu kwa mwaka wa fedha 2021 - 2022 yatarushwa na televisheni ya Taifa (TBC) na vyombo vingine vya habari vya nchini Tanzania.
#BajetiYaKimkakati
#BajetiYetuMaendeleoYetu
#BajetiRafikiNaShirikishi
#KaziInaendelea
View attachment 1813921
View attachment 1813920