Bungeni Dodoma: Hotuba Ya Waziri Mpango, Akiwasilisha Bajeti kuu Ya Mwaka 2020/2021 kiasi cha Tsh.Trilioni 34.88

Bungeni Dodoma: Hotuba Ya Waziri Mpango, Akiwasilisha Bajeti kuu Ya Mwaka 2020/2021 kiasi cha Tsh.Trilioni 34.88

Nimemnukuu Dr.Mpango akitaja Tanzania ina maadui wa nje na ndani.Hao maadui wa ndani ni wapi?Au ana maanisha wapinzani wa CCM?Kama ni wapinzani wa CCM basi hao sio maadui wa Tanzania bali ni maadui wa CCM .Tena uadui wao ni wa kuondoana kupitia sanduku la kura ambayo hiyo ipo kikatiba na kisheria.CCM wasitake kutuaminisha kwamba maadui zao ni maadui wa Tanzania!
 
Mzee yawezekana sijaelewa vizuri hiyo document lakini unapotoa matusi badala ya kunielekeza nisipoelewa wewe ndio unakuwa hujielewi
Mkuu ni hivi aliyenufaika ni anayepata below TZS 270,000/= kwa mwezi ndio hatakatwa kodi, Na wanaopata kuanzia TZS 271,000 hadi TZS 1000,000/= kwa mwezi ndio Kodi zao zimepungua sana. Wanaozidi TZS 1000,000/= kwa mwezi, ni kwamba kodi zimepungua kidogo sana.
 
kama sijalielewa hivi
Mfano mtu mwenye kipato cha 1m anadondokea wapi hapo, maana naona imeanzia 2m ambayo wamesema hakuna kodi
Angalia hapa chini mkuu;
1591897159345.png
 
Leo Taifa kupitia vyombo vya habari limeshuhudia usomwaji wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2020/2021 ambapo shilingi trilioni 34.88 zimependekezwa.

Pamoja na mengine mengi, uimara na umakini wa Waziri wa fedha Dkt. Mpango ni wakipekee sana ambapo ametumia saa 3 na dakika 20 akiwa amesimama bila kunywa maji wala kukunja goti akitekeleza jukumu hilo.

Kongole sana kwake.

Chanzo: Channel10

Waziri kaweka ushabiki wa kisiasa, matokeo yake hata watu hawana muda wa kuijadili hiyo bajeti. Pitia nyuzi zenye habari ya hiyo bajeti kama zina wachangiaji wa kuridhisha.
 
Kusomwa kwa bajeti bungeni kumegeuka kuwa sehemu ya kufanya kampeni na kupigiana debe kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka huu. Hivi kutokana na mila na desturi ya mabunge mengine ya nchi zilizopo ktk jumuiya ya madola haya mambo pia hufanyika!?

BTW, Mheshimiwa Mpango amenifurahisha sana alipoligusia goli la Morrison siku Yanga ilipowazamisha wazee wa utopolo kutoka Msimbazi. Naona bunge zima lilizizima kwa hoihoi, shangwe, nderemo na vifijo.

Bajeti imegeuzwa kuwa kampeni, matokeo yake hata humu mitandaoni hamna uchangiaji wowote wa maana. Ni kama vile bajeti imepuuzwa na watu wenye mitazamo huru.
 
Leo Taifa kupitia vyombo vya habari limeshuhudia usomwaji wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2020/2021 ambapo shilingi trilioni 34.88 zimependekezwa.

Pamoja na mengine mengi, uimara na umakini wa Waziri wa fedha Dkt. Mpango ni wakipekee sana ambapo ametumia saa 3 na dakika 20 akiwa amesimama bila kunywa maji wala kukunja goti akitekeleza jukumu hilo.

Kongole sana kwake.

Chanzo: Channel10
Kwa hiyo unampongeza kwa kusimama muda mrefu?

Sijui waafrika nani katuloga.
 
Back
Top Bottom