Mkuu nakudadavulia kama nilivyoelewa swali lako. Karibu.
Kumbuka kiasi cha fedha kilichotajwa ni kwa mapato kwa mwaka siyo kwa mwezi. Hivyo, kama hiyo 1m ni kwa mwezi basi unazidisha mara 12 kupata mapato kwa mwaka. Kwa hiyo, kwa 1m maana yake anapata 12m kwa mwaka. Unabeba hiyo tarakimu ya 12m na kwenda nayo kwenye jedwali.
Ukiangalia Jedwali Na. 1b." Viwango Vinavyopendekezwa ", Kwa mwenye kupokea 12m anaagukia kwenye mstari wa namba nne(4) wa jedwali tajwa hapo juu. Yaani yeye kipato hakizidi 12m, hivyo basi kodi yake kwa mwaka mzima itakuwa Shilingi ( 846,000/= + ((12,000,000 - 9,120,000) x 0.25))/=) = 1,566,000/= kwa mwaka mzima.
Hivyo kwa mwezi kodi atakuwa alipa (1,566,000 /12) = 130,500/= kulinga na kanuni zanazoongoza kukatwa kodi kwenye mshahara wake. Kuna baadhi, huwa wanakatwa kodi baada ya kuondoa malipo mengine yanayokatwa kwenye mshahara.
Hivi ndivyo nilielewa swali lako na majibu yangu ndiyo hayo. Karibu kwa maswali na ukosoaji kwa namna nilivyofanya ukokotozi huu.