Bungeni Dodoma: Hotuba Ya Waziri Mpango, Akiwasilisha Bajeti kuu Ya Mwaka 2020/2021 kiasi cha Tsh.Trilioni 34.88

Nimemnukuu Dr.Mpango akitaja Tanzania ina maadui wa nje na ndani.Hao maadui wa ndani ni wapi?Au ana maanisha wapinzani wa CCM?Kama ni wapinzani wa CCM basi hao sio maadui wa Tanzania bali ni maadui wa CCM .Tena uadui wao ni wa kuondoana kupitia sanduku la kura ambayo hiyo ipo kikatiba na kisheria.CCM wasitake kutuaminisha kwamba maadui zao ni maadui wa Tanzania!
 
Mzee yawezekana sijaelewa vizuri hiyo document lakini unapotoa matusi badala ya kunielekeza nisipoelewa wewe ndio unakuwa hujielewi
Mkuu ni hivi aliyenufaika ni anayepata below TZS 270,000/= kwa mwezi ndio hatakatwa kodi, Na wanaopata kuanzia TZS 271,000 hadi TZS 1000,000/= kwa mwezi ndio Kodi zao zimepungua sana. Wanaozidi TZS 1000,000/= kwa mwezi, ni kwamba kodi zimepungua kidogo sana.
 

Waziri kaweka ushabiki wa kisiasa, matokeo yake hata watu hawana muda wa kuijadili hiyo bajeti. Pitia nyuzi zenye habari ya hiyo bajeti kama zina wachangiaji wa kuridhisha.
 

Bajeti imegeuzwa kuwa kampeni, matokeo yake hata humu mitandaoni hamna uchangiaji wowote wa maana. Ni kama vile bajeti imepuuzwa na watu wenye mitazamo huru.
 
Kwa hiyo unampongeza kwa kusimama muda mrefu?

Sijui waafrika nani katuloga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…