Bungeni: Mbunge wa CHADEMA amtimua mpangaji wake ambaye ni Askari Polisi, adai haoni maana ya kushirikiana nae, Waziri Lugola amtisha

Bungeni: Mbunge wa CHADEMA amtimua mpangaji wake ambaye ni Askari Polisi, adai haoni maana ya kushirikiana nae, Waziri Lugola amtisha

Baada ya kauli ya Mbunge Sophia Mwakagenda (CHADEMA) aliyosema amemuondoa mpangaji ambaye ni Polisi kwenye nyumba yake kwa sababu haoni haja ya kushirikiana nae.

Waziri Kangi Lugola amemuagiza IGP Simon Sirro kumchukulia hatua Mbunge huyo na wengine wanaotoa kauli zenye viashiria vya uvunjifu wa amani.

Huyo mbunge ni mpumbavu na mjinga kupindukia. Mimi ningekuwa huyo askari ningeondoka kwa unyenyekevu mkubwa huku nikimsubiria aingie kwenye anga zangu!
 
Rais ana mamlaka ya ku revoke hati ya Nyumba ya mtu yeyote kwenye Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Nyumba ya huyo mbunge itaifishwe igeuzwe makazi ya Askari ‘Line police’ iwe fundisho kwake na wahuni wenzie huyo Mama

Kuna siku ataibuka kufukuza Waislam au Wakristo kwenye Nyumba anayopangisha au mwenye Basi pa abiria atawashusha Abiria kwa kuwa tu ni Wachaga au Wasukuma
Pumba tupu. Kasome hata Lawa of Contract kidogo upunguze ujinga.
 
Hahah eti mabilioni... kwa sheria gani?
Mawakili kesi ya bure hiyo hapo undeni jopo la mawakili nguli mumburuze huyo mwakagenda mahakamani mdai fidia mabilioni .Akilipa mtakata hela zenu za uwakili humo.Msaidieni huyo polisi bure bill hata kumdai shilingi ili huyo.mama ashikishwe adabu ajue kuwa na nyumba sio issue ya kumfanyia mpangaji utakacho
 
Mkataba Hana mamlaka nje ya mkataba wa kipanga.Mkataba una hayo yake? Nyumba yako mwenyewe yaweza kukupa matatizo ukafa kwa presha Kama hujali mikataba ya kupanga.

Lugora mtu wako huyo mbunge kajileta mwenyewe
Kwani wewe unajua mkataba wao ulikuwa unasemaje? mbna unarukia kufanya conclusion?
 
Rais ana mamlaka ya ku revoke hati ya Nyumba ya mtu yeyote kwenye Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Nyumba ya huyo mbunge itaifishwe igeuzwe makazi ya Askari ‘Line police’ iwe fundisho kwake na wahuni wenzie huyo Mama

Kuna siku ataibuka kufukuza Waislam au Wakristo kwenye Nyumba anayopangisha au mwenye Basi pa abiria atawashusha Abiria kwa kuwa tu ni Wachaga au Wasukuma
Hiyo haki hana,kuna utaratibu wa kisheria na lazima mmiliki wa hiyo mali atafidiwa kwa mujibu wa sheria ,katiba ya Tanzania inalinda haki ya kumiliki mali.
 
Nyumba yake alafu huyo IGP atamfanya nini?
Baada ya kauli ya Mbunge Sophia Mwakagenda (CHADEMA) aliyosema amemuondoa mpangaji ambaye ni Polisi kwenye nyumba yake kwa sababu haoni haja ya kushirikiana nae.

Waziri Kangi Lugola amemuagiza IGP Simon Sirro kumchukulia hatua Mbunge huyo na wengine wanaotoa kauli zenye viashiria vya uvunjifu wa amani.

Kwa issue hii serikali inabidi iwe makini sana vinginevyo ikikurupuka itawasha moto ambao utawaumiza sana askari wake wanao ishi mitaani kwa kupanga
Mwenyewe Mali hataki

Na mwenye Mali ndio anachaguwa nani ampangishe.

Kama Lugola anaona sio sawa serikali iwajengee watumishi wake
 
Baada ya kauli ya Mbunge Sophia Mwakagenda (CHADEMA) aliyosema amemuondoa mpangaji ambaye ni Polisi kwenye nyumba yake kwa sababu haoni haja ya kushirikiana nae.

Waziri Kangi Lugola amemuagiza IGP Simon Sirro kumchukulia hatua Mbunge huyo na wengine wanaotoa kauli zenye viashiria vya uvunjifu wa amani.

Maamuzi ni yake kama Polisi anashirikiana na majambazi ya jukwaani wanini sasa?
Kama kuna ukweli kwa hoja/tuhuma yako hiyo, mama mwenye, tena Mh Mbunge, kwa nini asichukue hatua stahiki kwenye vyombo vya Katiba? Isitoshe, kama mwanachama wa CHADEMA, mtetezi mkuu wa demokrasia, hatukutegemea kauli hiyo kutoka kwake Mh tena Bungeni.

Du!
 
Mpaka hivi sasa bado natafuta Mantiki ya Kumfukuza Askari Nyumbani Kwako ambako umempangisha kwa sababu tu za Kisiasa na Hasira. Askari Kufukuzwa kuna Uhusiano gani za matatizo ya Kiuchaguzi au ya Kisiasa? Hivi ukija kuwa Mzee na ukasikia nawe Mwanao ambaye labda amekuwa Askari nae akifanyiwa hivi kama Mama utajisikiaje?

Leo hii unaposema kuwa umemfukuza Askari Kwako kwakuwa huoni umuhimu wake hivi na Wao Askari ambao kwa bahati nzuri Sisi Wananchi tunawahitaji sana kwa Ulinzi na Usalama wa Mali zetu Siku ikitokea nawe ukapatwa na matatizo wakikususia na yakakukuta makubwa utamlaumu nani?

Kama unajinasibu kuwa Wewe ni mpenda Demokrasia na unapambania Haki za Watu unapomfukuza Askari Kwako ulikompangisha uliangalia pia na upande wake wa Pili wa Familia yake ambayo ni kama vile umeinyanyasa? Kwa Kitendo hiki unategemea Kweli upate hata Mwanachama Mmoja ndani ya hiyo Familia ambaye pengine Kura yake hiyo moja na nyinginezo zingeweza Kuitoa CCM Madarakani kama unavyotaka?

Ni kweli Askari wanaweza wakawa na Changamoto zao ila Kumfukuza Nyumbani Kwako halafu unakuja Kujisifia na Kuutangazia Umma wa Watanzania ni Uthibitisho wa aina ya Roho mbaya yenye Ukatili mwingi uliyonayo. CCM haitotolewa Madarakani kwa Kuwachukia Mapolisi bali itatolewa kwa Sera, Mipango na Mikakati thabiti.

Na kilichoniuma na kunisikitisha zaidi ni kwamba haya Maamuzi yamefanywa na Mwanamama ambaye nilikuwa naamini kuwa ndiyo Jinsia ambayo Kiasili imetawaliwa na Huruma kuliko hata Wanaume. Na hakuna Kitu kibaya kama Kutengeneza Bifu na Mapolisi na leo anaweza akafurahi ila natabiri mapema kuna Hatari naiona inaelekea kwa aliyemfukuza Askari Nyumbani Kwake.

Tujifunze Kutenganisha Hasira na Utu.
Sina ubaya na huyo askari kwa sababu simjui, lakini ni ndoto ya mchana kujidanganya kwamba unategemea kupata kura hata moja kutoka familia ya polisi, kwa sababu na makosa makubwa wanayofanya polisi ni kujifanya kuwa ccm, hawa polisi wangekuwa wanatenda haki sawa watu wote bila kubagua watu kwa misingi ya kisiasa haya yote yasingetokea, mienendo yao inasababisha wanachukiwa na watu wengi sana, wewe kama umesikitika sana ungeanza kulitatua hili tatizo kuanzia chini lilikoanzia na si kushughulika na matokeo, huyo Mama Mbunge amepatwa na hasira ndio maana akasema haoni sababu ya kushirikiana nao, na kumbuka, polisi kumhudumia huyo Mama ikitokea akawa na shida yeyote kwao ni jumkumu lao la msingi, usiseme kwamba eti wanaweza kukataa kumsaidia, btw ni mara nyingi tumekuwa tukioona polisi wanavyojitoa akili pale wanapotakiwa kutoa huduma kwa watu ambao sio wana ccm, huyo mama mbunge hajakosea, ukizingatia hiyo nyumba ni yake, hajasaidiwa na serikali kuijenga, ana maamuzi nayo kwa lolote, hata mimi nawachukia sana polisi, nimeshaona wakifanya mambo mengi ya kishenzi, lakini pia naamini unakumbuka kauli aliyotoa rais wenu hivi karibuni kwamba, "mtu yeyote atakae mpiga mwanaccm atakion cha moto, wakati huohuo kuna vijana wa ccm walimvamia kwa silaha (mchana kweupe) aliyekuwa M/kiti wa Chadema mkoa wa Geita (Marehemu Mawazo) mpaka akapoteza maisha, polisi hawajachukulia mtu yeyote hatua mpaka leo, unakumbuka kitendo walichokifanya polisi cha kupiga mabomu ya machozi waombolezaji nyumbani kwa Baba mdogo wa marehemu Mawzo ?!., ndio polisi unaowaonea huruma, huyo polisi aende akakae kwenye Kotazi za serikali kwasababu tulishaambiwa hawatakiwi kukaa uraiani
 
Back
Top Bottom