Bungeni: Mjadala wa dharura kuhusu kupanda kwa bei ya mafuta nchini. Mbunge asema tozo mbili zinaongeza 792 kwenye bei
Huo mjadala uwe kweli na immediate impact, sio wanajadili tu halafu mambo yanabaki vile vile huku bei ya mafuta ikizidi kupanda na kuwaumiza watumiaji.

Rais kuruhusu bei za vitu kupanda kwasababu ya vita ya Urusi na Ukraine haya ndio matokeo yake, tunaumizwa wananchi na mafisadi wajanja kwenye wizara ya nishati.

Watz tumezubaa sana.
Tuna rais hasiyejua impact ya matamko yake kwenye eneo zima la uchumi.
 
Badala ya kukopa fedha ili watoe ruzuku kwenye mafuta,ni heri matumizi ya zile fedha za tozo za miamala ya simu zisitishwe matumizi yaliyokusudiwa ( Kama bado zinatumika huko lakini) ndiyo ziende kutoa hiyo ruzuku ya mafuta.
Nasema hivyo kwa sababu tozo za miamala ya simu ni tozo zilizoletwa kufanya kazi ambazo Kodi zetu tulizokuwa tunatozwa za kawaida zilikuwa zinafanya..mfano walisema tozo ni kwa ajiri ya ujenzi wa barabara,madarasa nk, kazi ambazo zimekuwa zikifanywa na Kodi zetu za kawaida.

Basi fedha ya tozo ifanye kazi hizo za dharura Kama kuweka ruzuku kwenye mafuta badala ya kuchukua mikopo mingine..Hali ya Ukraine na urusi ikitulia Bei za mafuta zikirudi katika Hali ya kawaida,tozo zitarudi kufanya kazi yake iliyokusudiwa
 
Taifa linakosa kauli ya .mwisho yenye mamlaka.

Watu wanakaa wanajadili tu bila kufikia muafaka wa lolote.
 
Wanabodi,

Moja ya kazi za Bunge ni Kuisimamia serikali. Bunge la Mhe. Job Ndugai, lilituhumiwa kuwa ni Bunge dhaifu kuwahi kutokea, hivyo Spika Job Ndugai kuhesabika ni Spika dhaifu kabisa kuwahi kutokea, hivyo kupachikwa jina la "Bora Spika" Kwa kuanzia mimi niliisikia sauti hii Voices from within: Nimesikia sauti, Dr. Tulia Ackson ndiye Spika ajaye! Sauti hiyo imenieleza Ndugai, japo atatamani aendelee lakini...

Job Ndugai alipojiuzulu tukasema Kujiuzulu kwa Ndugai ni mpango wa Mungu kwa Tanzania ili tupate Spika Bora. CCM itateua Spika Bora au Bora Spika kama kawa?

Kwa vile Dr. Tulia alikuwa ni Naibu Spika wa Spika dhaifu, alipochaguliwa kuwa Spika, kuna watu walidhani Bunge la Tulia litakuwa ni Bunge Dhaifu kama Bunge la Ndugai.

Nilitoa ushauri huu Je, Wajua, Naibu Spika, Chini ya "Bora Spika", Anaweza Kuwa "Spika Bora?". Dr. Tulia, "Ukitulia, Una Fursa ya Kuwa Spika Bora Sana!" Hongera Sana!

Sasa hiki ndio kinatokea Leo,

Bunge la Dr. Tulia, sasa limeanza kuisimamia Serikali kiukweli ukweli!, leo limesimamisha shughuli zake zote kujadili hoja ya dharura ya Mhe. Omari Kigua, kujadili kupanda kwa bei ya mafuta ya petrol na dizeli.​


Hongera Sana Spika Tulia, Bunge sasa linaisimamia serikali

Keep Watching Bunge Live

na Kazi iendelee!

Paskali.
jamiiforuma tuwekeeni dislikes pia kusiwe na likes and quotes only
 
Wameongea weeee lakini mwisho wa siku Serikali ndio itakuja na jibu maana hakuna cha azimio la Bunge wala nini ila ni maelekezo ya serikali kukaa na kutafakari..

Ukimsikiliza Simbachawene alitoa msimamo wa serikali Kwa hiyo don't expect too much..

Mwisho mimi natoa ushauri,unapotaka haki kuwe na uwajibikaji.. Serikali ikiondoa hizo tozo lazima wabane watu wanaponunua bidhaa wawe na risiti Ili kufidia pengo vinginevyo itakuwa ni serikali ya Zima moto na Hawa Hawa wanaolalamika leo watakuja tena kulalamika Kuhusu barabara ,maji,afya nk na hawatajua kwamba Serikali ilitoa vyanzo vya mapato yake vya kwenye mafuta.
Hizo tozo haziondolewi moja kwa moja...Zinaondolewa kwa muda tu mpaka hali itakapokaa sawa sawa.
 
Tumelalamikia vifurushi siku mbili tumesahau. Hata hili nalo litapita
 
Keep Watching Bunge Live

na Kazi iendelee!

Braza Pascal Mayalla tunakutofautishaje na u-sisiemu wako...

Tunatenganisha vipi mabandiko yako na ukada wa chama cha mapinduzi,, Je tutumie historia yako ya nyuma au tuzingatie lipi hasa kujua hili andiko halina ukada ndani yake na hili lina ukada ndani yake....!! Ni wakati gani unafanya kazi za kichama na wakati gani unakuwa kitaifa...

Nauliza kwa vile 93% ya wana sisiemu wao huwa wanasifia almost everything cha mwenyekiti...Mna njaa NDIO, Mmekula NDIO, tunafuta tozo NDIO, tunarudisha tozo NDIO, tunafuta Bunge Live NDIO, tunarudisha Live NDIO...

Hii ni nje ya mada kidogo....
 
Niache kuitetea Idara yenyewe
inayonilipa, kula, kunywa na kulala, ndio nimtetee usalama mwenzagu Zitto kama utetezi huu

P

Kuitetea idara ni misimamo yako kama hii kuhakikisha CCM, hata ikifanya makosa unaitetea.
 
Braza Pascal Mayalla tunakutofautishaje na u-sisiemu wako...

Tunatenganisha vipi mabandiko yako na ukada wa chama cha mapinduzi,, Je tutumie historia yako ya nyuma au tuzingatie lipi hasa kujua hili andiko halina ukada ndani yake na hili lina ukada ndani yake....!! Ni wakati gani unafanya kazi za kichama na wakati gani unakuwa kitaifa...

Nauliza kwa vile 93% ya wana sisiemu wao huwa wanasifia almost everything cha mwenyekiti...Mna njaa NDIO, Mmekula NDIO, tunafuta tozo NDIO, tunarudisha tozo NDIO, tunafuta Bunge Live NDIO, tunarudisha Live NDIO...

Hii ni nje ya mada kidogo....
Mkuu Nas Jr , kwanza nakiri, the dividing line btn Pasco Kada wa Chama cha Mapinduzi, CCM, na Pasco Mzalendo wa kweli wa taifa hili, is very thin.
Tumia tuu kipimo cha objectivity kupima kama utetezi wangu ni wa kikada au kizalendo.
P
 
Mbunge wa Geita vijijini Msukuma asema mafuta yaliyopanda yalinunuliwa mwezi wa February 2022 kwa bei ya chini na yamepanda yakiwa ndani ya meli.

Hii ni harufu ya ufisadi ambayo inahitaji kuchunguzwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nilichojifunza hapa kuna watu wana elimu ya kawaida sana lakini michango yao ktk taifa ni zaidi ya maprofesa. Msukuma yuko vizuri ktk michango isiyohusisha ushindani wa siasa.
 
Japo huku Unguja tunapeta nilitaka kujua huko bara tozo 22 zilizopo kila unaponunua Lita 1 ya mafuta (petrol, diesel, kerosene) Tanzania bara ni zipi? Binafsi najua Ile "Road fund" tu. Karibuni Zanzibar.
 
Back
Top Bottom