Yaliyotokea ni haya hapa:
Kutoka ndani ya uvungu wao...
Walikaa Chadema na CUF ili waone wataingiaje Bungeni. Kabla ya Uchaguzi wa Spika, Hamad Rashid alitaka kugombea Uspika, Chadema wakamwambia hapana wacha Agombee huyu Mwanasheria, wewe utarudi katika kambi ya upinzani kwa cheo chako kile cha awali, na kwa kufanya hivyo tutagawana madaraka. Hamad akawakubalia na kuondoa azma yake ya kugombea U-Spika alipofanya hivyo, Zito akaibuka na kusema Wataunda kambi Chadema peke yake bila kushirikisha vyama vingine. hilo nalo. Hapo ndipo Marando alipozikosa kura ambazo zingemvusha kwenye Uspika. Na hii imefanyika kutokana na ufinyu wa fikra (kama sio viongozi waandamizi wa Chadema kupewa chochote toka CCM) wakidhani kwamba umaarufu unatokana na kuongoza kambi ya upinzani bungeni bila kuwa na ushirikiano kutoka vyama vingine. Walichokisahau Chadema ni kuwa CUF walijaribu kutoshirikisha vyama vingine awali na kisha wakajirekebisha, na hapo wasiomjua Slaa ndipo walipomtambua. Ila kwa kwa hili la ubinafsi wa CHADEMA wameumaliza UPINZANI Tanzania. Tutafute kaburi tuuzike...
Tusubiri kuundwa kwa chama kipya kisicho na damu ya U-CCM-CCM.:sad:
Nawasilisha.