Elections 2010 BUNGENI: Upinzani upo ndani ya kambi ya upinzani?

Elections 2010 BUNGENI: Upinzani upo ndani ya kambi ya upinzani?

Kaka Chadema magugu mengi, na magugu huwa yakiota mimea mizuri inakuwa hatarini. Zitto, wenje, .........

Hakuna shamba linalokosa magugu, wakati mwingine magugu yanafaida, wakati wa kiangazi Magugu hutunza unyevunyevu ardhini na kuzuia mchwa wasitafune mazao. Magugu mengine ni chakula cha mifugo tunayofuga, pia yakiozea shambani hurutubisha ardhi.
 
Ni kweli maneno yako maana ndio maana hawakuwashirikisha wenzao kuunda kambi ya upinzani bungeni kwa kujiona wao ndio wapinzani peke yao, hawakuwashirikisha kwa kuwapa japo umakamu.
Kwani walitaka ushirikiano CHADEMA wakakataa? We vipi!!??
 
Hakuna shamba linalokosa magugu, wakati mwingine magugu yanafaida, wakati wa kiangazi Magugu hutunza unyevunyevu ardhini na kuzuia mchwa wasitafune mazao. Magugu mengine ni chakula cha mifugo tunayofuga, pia yakiozea shambani hurutubisha ardhi.
chadema ndio wapinzani pekee na kweli wawe waangalifu na MaCCM B wasiwaaribie.
 
vaa miwani tazama vizuri kama huku bara wapo na sisi huko kwao tupo MATARAJIO YAO WALIJUA WATAKUA WAO NDIO KAMBI YA UPINZANI KUMBE LA WABARA WAMEAMUKA SASA WEWE ULEULE SONGA MBELLEE WEWE JF AMUSHA WALIOLALAAA
 
Kwa upande wangu unaonekana mtu mzima uliyekosa akili, unafikiri kura 30 za CUF zingeweza kushindana na kura 250 za CCM.
CUF ni chama Tawala, taka usitake. NCCR, TLP,UDP hawana impact. kwahiyo chama cha upinzani ni CHADEMA, Chama tawala ni CCM+CUF

Umenisaidia kumuelimisha huyo mzee mimi nilidhani ataongea mambo ya maana kumbe utumbo mtupu bila kuwaza ukweli ulivyo, ama kweli huyu ni mwanamageuko na mawazo yake pia yamegeuka kama jina lake.
 
sijue kupingana pingana ndio nini maana upizania ndani ya upinzani, CUF v/s Chadema kunani au kimojawapo CCM-B, kwanini wasielewane ndio maana hat wakati wa kampeini vijembe vyote vya kafu vilielekezwa kwa chadema hii sio shwali kabisa kuleta ukombozi wa walala hoi, sitawashaangaa kuwa chama kimojawapo kinakamilsha matakwa ya CCM

Tayari CUF inakamilisha Ilani ya CCM Zanzibar
 
usitufanye watu hatujui mahesabu kama CCM......CUF wako wangapi? na Marando kapitwa kwa kura ngapi?
 
Yaliyotokea ni haya hapa:

Kutoka ndani ya uvungu wao...
Walikaa Chadema na CUF ili waone wataingiaje Bungeni. Kabla ya Uchaguzi wa Spika, Hamad Rashid alitaka kugombea Uspika, Chadema wakamwambia hapana wacha Agombee huyu Mwanasheria, wewe utarudi katika kambi ya upinzani kwa cheo chako kile cha awali, na kwa kufanya hivyo tutagawana madaraka. Hamad akawakubalia na kuondoa azma yake ya kugombea U-Spika alipofanya hivyo, Zito akaibuka na kusema Wataunda kambi Chadema peke yake bila kushirikisha vyama vingine. hilo nalo. Hapo ndipo Marando alipozikosa kura ambazo zingemvusha kwenye Uspika. Na hii imefanyika kutokana na ufinyu wa fikra (kama sio viongozi waandamizi wa Chadema kupewa chochote toka CCM) wakidhani kwamba umaarufu unatokana na kuongoza kambi ya upinzani bungeni bila kuwa na ushirikiano kutoka vyama vingine. Walichokisahau Chadema ni kuwa CUF walijaribu kutoshirikisha vyama vingine awali na kisha wakajirekebisha, na hapo wasiomjua Slaa ndipo walipomtambua. Ila kwa kwa hili la ubinafsi wa CHADEMA wameumaliza UPINZANI Tanzania. Tutafute kaburi tuuzike...

Tusubiri kuundwa kwa chama kipya kisicho na damu ya U-CCM-CCM.:sad:

Nawasilisha.
usitake kudanganya wana JF bwana, Cuf walishafunga ndoa na CCM, TLP ndo kabisaa,(Rejea misimamo ya Mrema kwa JK). Chadema ndo mpinzani wa kweli kwa sasa, mengineo majungu. Hatudanganyiki.
 
Hakuna alieharibu kura yake kwa makusudi. Hao ni wabunge mbumbumbu ambao hawajui hata kupiga kura sijui watawawakikilisha vipi wananchi. Kazi ipo
 
Kwani chadema wao si wamesema wapo 12% na wanatosha? nadhani bunge sio sehemu ya majaribio wapinzani wengine wanaona mbali ndio maana wamempa mtu mwenye uwezo tatizo la chadema wameshalewa ukubwa mapema!!!!
 
chadema ndio wapinzani pekee na kweli wawe waangalifu na MaCCM B wasiwaaribie.

Bwana Sokomoko huna information lkn unakuwa mwepesi kuchangia. Nilitegemea ungekuwa unajua kwamba walialikaribishwa kuunda kambi wakatoa visingizio eti wao wanashirikiana kivyao. Nadhani wana malengo mengine zaidi ya yale tunayofikiri.

Yawezekana pia wanaona donge kwa mafanikio ya Chadema na tafsiri ya hilo ni ubinafsi.
Bravo! Chadema.!!!!!!!!!!!!
 
Huo sasa ni umbea taslimu.

CHADEMA 45 + CUF 34 + NCCR 4 + TLP, UDP 2 = 85

CCM = 251

Hapo uspika wa Marando uko wapi Mwanamageuko? au na wewe unataka kuchakachua JF?

I was of the same opinion. Maana kama nilisikia Hamad Rashid alikuwa asimame kwa ajili ya Uspika. Ila from no where nikasikia mzee wa Usalama wa Taifa naye anataka agombee. Na from there Hamad Rashid sikumsikia tena kugombea. Ila nilidhani kama this was a milestone opportunity na kuikosa kwake ni pigo mno kwa upinzania bungeni.

Unajuwa CHADEMA walishindwa kula na kipofu... automotically nafasi ya Hamad Rashid kushinda haikuwa kubwa mno ila lolote lingeweza kutokea. Binafsi yangu nadhani angeweza hata kupata kura za kutosha kutoka kwa CCM, Wazanzibari wenzake, wanawake wenzake wenye wivu, kambi ya Sita na wanaoamini kama Mwanamke hawezi kuwa speaker na yes hata kuna ambao wangepiga kidini dini tu.

All in all Marando hakuwa na mvuto mzuri..anaonekana ni hardliner sana na kwa wasiopendezwa na ku rise kwa CHADEMA ghafla wangeona kama hii ingewapa chati CHADEMA kwa kumchagua Marando anayetoka CHADEMA kuwa speaker.!

CHADEMA ku wa label CUF kama ni CCM-B haikuanza baada ya Maridhiano ya SMZ yalianza kabla na sidhani kama ni busara. Ungemuona Lipumba alivyo bitter ile siku ya kufunga mkutano pale Jangwani akiziponda sera za CCM na Kikwete ungeamini kama huyu jamaa ni mpinzani hasa.

Ila hakujaharibika kitu. Nadhani watu wenye busara kama Dr. Slaa bado wanaweza kukaa chini na wenzao wa CHADEMA kuona jinsi gani wanaweza kutibu majeraha haya kwa mustakbali na afya ya upinzani Tanzania.
Mungu ibariki Tanzania.
 
hakukuwa na sababu ya chadema kuungana na CUF, wao wanamuungano na CCM tayari
 
CCM hata wawe wengi watakuwa sawa na chadema tu kwani wengi wao wavivu wa kusoma na hawana point za kuchangia siku zote.

We angalia mimi huwa naangalia bunge mara nyingi na wabunge wengi wa ccm hawachangii kwenye mada nyingi wanasubiri kupiga kura ya kusema ndiyo siku zote bila kujali wananchi wako upande gani.
 
Kwani chadema wao si wamesema wapo 12% na wanatosha? nadhani bunge sio sehemu ya majaribio wapinzani wengine wanaona mbali ndio maana wamempa mtu mwenye uwezo tatizo la chadema wameshalewa ukubwa mapema!!!!

sheria ni kuwa unaweza kuunda kambi ya upinzani ikiwa idadi ya wabunge inafikia 12.5% hawakumanisha kuwa 12% is enough kama dhihaka yako ilivyo.
 
Halima mdee=viti maalum wote wa CCM na CUF + kumi wa kuchaguliwa wa CCM+Ana makinda
Tundu Lisu=jk+sitta+pinda+EL+RA+ wengine sitini
Mnyika=wa kuchaguliwa wote wa CUF+NCCR+UDP+TLP +majimbo waliyoiba kura ya segerea, temeke,kinondoni,ilala na kigamboni

Zitto=jaza mwenyewe
Vicent Nyerere=endelea
Mbowe=acha kabisa

utakuwa ujinga kwa ccm kuwapa watu wanaotoka a small area as pemba kuunda serikali ya upinzani il hali wapo wanaotoka almost all corners of the country. mwaka 2015 hiyo move itatumika kuwaadhibu sana.
 
Back
Top Bottom