Bure Series

Bure Series

NJIA PANDA ZA KUZIMU - 3

Siku ninayopata taarifa hiyo ndipo ikawa pia siku yangu ya mwisho kuwa katika nyumba ile nikarejea kule kambini.
Sikujua nini kilikuwa kinaendelea huku lakini kumbe kuna jambo moja baya sana lilikuwa linaendelea chinichini.
Kwanza nilimkuta yule msanii kule akiwa anateseka sana, niliogopa kumtazama machoni kwa sababu nilishiriki kumfikisha hapo.
Ukiachana na hili, jambo ambalo lilinishangaza na kisha kuniweka katika wakati mgumu zaidi katika maisha ya huko. Ni suala la Malkia na Adella kugombana, kisa kikuu ni baada ya malikia kusikia kuwa Adella ameshika mimba.
Vilikuwa ni vita baridi ambavyo vilikuwa vinanisubiri nifike ili viwake rasmi.
Wote walikuwa wamejipanga, wanasema kuwa wapiganapo mafahari ziumiazo nyika.
Niligeuka nyika katika hili.
Wa kwanza kuzungumza na mimi alikuwa ni Adella punde tu baada ya kurejea, alinieleza kuwa kuna vita inaibuka hivyo nijiandae lengo lake ni kunitorosha ilimradi tu nitoweke wakose wote.
‘’mkose wote, unamaanisha nini’’ nilimuuliza.
‘’malikia anakuhitaji na mimi nakupenda martin, malikia anataka kukupeleka njia panda ya kuzimu na mimi sihitaji uende huko..’’
‘’Mamaa weee njia panda ya kuzimu ni wapi kwani, Adella nisaidie nisaidie sitaki kwenda huko…’’ nilimsihi wakati hata sijapajua njia panda ya kuzimu.
Alipotaka kunieleza mara upepo ulivuma akanyamaza kimya.
Upepo ulipopita akanieleza kuwa malikia amejipitisha pale ili aweze kusikia ni kitu gani walikuwa wanazungumza.
Ile adella anataka kuendelea kuzungumza tena, mara wakafika watu watatu na kunieleza kuwa nilikuwa ninaitwa na malikia, hawakuwa na subira wakanivuta na kunipeleka nilipohitaji. Wakanisukuma ndani nikajikuta mbele yangu nikitrazamana na yule mwanamke anayeitwa malikia.
‘’acha kuwa mpumbavu kijana, yule binti anataka akupeleke njia panda ya kuzimu, epuka tamaa za muda mfupi ukiingia huko hautoki. Lengo langu nataka uishi vizuri hapa.. maana huko njia panda ya kuzimu, utakatwa ulimi nab ado utalazimishwa kuongea, utatobolewa macho yako na utalazimishwa kutambua rangi, hautapewa chakula nab ado utalazimishwa kufanya kazi. Ikiwa upo tayari muendekeze yule binti na hapatakuwa na muda wa kujuta’’ alimaliza kisha akanisukuma nikajikuta nipo nje.
Nilikuwa nimechanganyikiwa vibaya sana jamani, hasahasa maneno ya malkia yalinifanya nipagawe maradufu.
Kutobolewa macho, kukatwa ulimi…. Ama kweli hapo ndo palikuwa njia panda ya kuzimu…..
Sikujua ni kitu gani nifanye kwa wakati ule…..
Nikiwa bado palepale chini nilianza kuusikia mwili wangu ukiwa mzito na giza likaanza kutanda, wakati nazidiwa na usingizi ule niliwaona watu wawili wakiwa na ghadhabu kuu wakinikaribia, upandfe mmoja alikuwa ni malikia na upande mwingine akiwa ni adella.
Waliponifikia nikamwona adella akimkaripia malikia, malikia naye akamjibu adella sikuweza kusikia walichokuwa wakisema lakini kila mmoja alikuwa akijiamini nkuwa yeye ni mbabe kuliko mwenzake.
Mara wakatimua mbio na kunifikia, hapa sasa nikayasikia maneno yao machache.
‘’kama ni hivyo basi kila mmoja achukue nusu’’
Malikia akanishika miguu yote miwili na adella akanishika mikono, kila mmoja akaanza kuvuta kuelekea upande wake, walinivuta nikawa napiga makelele, lakini wao hawakujali waliendelea kunivuta, na baada ya muda kila upande ukaongeza wavutaji, hapa sasa niliipata joto ya jiwe.
Sauti haikutoka tena tumbo likawa linaniuma sana na upande wa uti wa mgongo pia.
Nikaanza kuhisi ngozi yangu ikianza kuachana, hapa sasa sauti haikutoka tena na nilikuwa naumia sana, waliendelea kuvuta hadi nikaliona tumbo langu likifunguka.
Nilitamani kusema neno lakini sikuweza kusema.
Nilitambua kuwa muda wowote ule kuwa mwili wangu unatengana nusu kwa nusu na hapo historia ya maisha yangu inafika ukomo.
Nikajaribu kupambania uhai wake katika dakika ya mwisho…. Nikajigeuza kwa nguvu sana huku nikiwasihi wasiniue.
Mara wakaniachia, na hapo nikaweza kufumbua macho yangu. Nilikuwa nipo pale chini nikigalagala huku tumbo likiniuma vibaya sana. Jasho lilikuwa linanitoka, lakini tumbo halikuwa limechanika kama nilivyoona katika maluweluwe yale.
Nilijaribu kusimama nikaanguka chini.
Nikasikia sauti ya kicheko kikali, nikageuka na kukutanisha macho yangu na malikia, nilipogeuka upande mwingine nikakutanisha macho na adella.
Kisha wote wakapotea….
Huo haukuwa mwisho bali mwanzo wa kuteseka.
Usiku mnene ulinikuta katika mtihani mwingine.
Nimesema ni usiku japokuwa sina uhakika, awali niliwaeleza kuwa huku usiku ulikuwa wa kufikia tu, akiamua malkia kuleta giza analeta, akiamua iwe mwanga analeta pia.
Nilishtuka kutoka gizani nikataka kuuliza ni nani anayenitikisa lakinmi nilishtukia nikiwa nimezibwa mdomo.
‘’nifuate Martin’’ sauti tulivu ya kike ilinisihi. Nikaitambua kuwa ilikuwa sauti ya Adella, akanivuta na kunisogeza pembeni.
‘’Martin, unatakiwa kuchukua maamuzi magumu sana ama la sivyo kuna jambo baya sana linaenda kutokea. Nilidhani ni mimi na malkia pekee tunaokuwania lakini kuna watu duniani wanakupigania urudi huko. Hii sasa ni vita, sikuangalia kwa makini sana lakini kuna mwanamke nimemuona kama anafanana na wewe sijui iwapo ni dada mama ama mama mdogo’’ alisita, sasa niliweza kuiona sura yako kwa mbali macho yalikuwa yamelizoea giza.
Maneno aliyozungumza sikuwa nikiyaelewa bayana, akanivuta karibu yake akachukua vitu fulani nisivyovitambua akavitafuna na kisha akanipaka chini ya macho yangu na kisha akanizaba kibao kikali usoni, nilitaka kupiga kelele kwa maumivu niliyopata lakini aliwahi kuniziba mdomo na hapo sasa akaniwekea mkono wake, mkono wake ukaanza kutanuka na hapo nikaiona sura ya mama yangu nikamuona Nasra yule mwanadada ambaye naweza kusema alikuwa daraja la mimi kufikia pale nilipo na pia nikamuona mwanaume fulani ambaye sikuwa namtambua sura.
‘’wote hao wanatakiwa kuuwawa mara moja kuna ambao wanafanya maombi lakini ni dhaifu katika imani, wapo wanaojaribu kwenda kwa waganga lakini bado hawajatimiza masharti ya waganga. Hawa wote ni maadui wa ufalme huu, kanuni ya ufalme huu ni kwamba tunakuleta sisi na sisi tutaamua wewe kurudi huko… sasa Martin ikiwqa ningeamua kukaa kimya basi hawa watu watatu wote wangeuwawa na siku ungeletewa miili yao hapa ili uwale nyama wasije wakaonekana tena duniani, maana bila wewe kula nyama yao watakuwa wakionekanba mara kwa mara na kuzua utata….’’ Alinizungumza kwa sauti ya chini huku akiwa amenikazia macho yake.
‘’sasa Martin ni kitu gani wahitaji zaidi nifanye ujue kuwa ninakupenda. Nimeamua kufanya jambo la hatari kama hili kwa manufaa yako lakini bado hauamini kuwa nahitaji kuwa mke wako…’’ alizungumza Adella kwa masikitiko.
‘’Adella, naomba unisaidie sana wasimuue mama yangu… mimi nitawapa chochote wanachotaka ilimradi wamuache mama yangu…’’ nilimsihi Adella.
Akacheka kidogo kisha akaniambia, ‘’hakuna wanachohitaji kwako zaidi ya roho yako, na hii sio kwamba wewe ndo unaamua la, wakiamua wanaichukua tu….. jambo la kufanya sasa Martin simama kama mwanaume, simama upigane….’’ Alinisihi huku akionekana kunitia ujasiri.
‘’mimi nipigane na malkia…’’ nilimuhoji huku nikiwa katika mshangao.
‘’kama haupo tayari kupambana basi uwe tayari kumla mama yako nyama…’’ alinijibu kwa hasira.
Jibu lile likaniingiza katika mtihani mgumu sana.
‘’sikia Martin nimemua kusimama kwenye upoande wako moja kwa moja… na wewe uwe upande wangu hasa… nahitaji ufanye jambo moja tu ili tuweze kuingia katika hii vita na kuokoa watu wasiokuwa na makosa……’’
‘’niambie lolote na nitafanya Adella niambie…’’
‘’nahitaji unywele walau mmoja tu wa malkia… utajua jinsi ya kuupata najua roho itaniuma lakini nakuruhusu kama ni kulala naye fanya hivyo lakini uje na uywele wake walau mmoja …..’’ alinieleza na hakungoja jibu, akapotelea gizani akiniacha nimeketi bila msaada wowote.
Sijui yalipita masaa ama dakika ngapi mwanga ukachukua nafasi yake, wale misukule wakaingia mashamabani wakisaidiwa na wafanyakazi wapya ambao walikuwa wakipatikana kwa kunyweshwa yale maji ambayo kwa macho yao waliona ni maji lakini ilikuwa ni damu.
Mashamba yalilimwa na kwa bahati nzuri mimi nilikuwa napewa nafasi ya kusimamia hii ilikuwa ni kwa sababu ya ukaribu wangu na malkia kimahusiano.
Siku hii nilishtuka na kumuona malkia mwenyewe akiwa anasimamia yale mashamba, nikakumbuka kuwa Adella alinieleza kuwa ninatakiwa kuupata unywele wa malikia, nilimuona jinsi alivyokuwa amejitanda kichwa chake hakuonekana nywele zake hata kidogo.
Nikasimama kutoka pale nilipokuwa na kujongea hadi alipokuwa amesimama.
‘’shkamoo mama.. malkia..’’ nilimsalimia huku nikiwa natetemeka, mwanamama yule alinigeukia na kunitazama jicho kali sana, jicho lake ni kama lilikuwa lina miale fulani ya moto.
Nilitishika sana.
‘’hiyo shkamoo hapa si mahali pake…..’’ alinijibu kwa kiburi.
Nikataka kuondoka akaniita, safari hii jicho lake halikuwa kali kama mwanzo. Alikuwa akinitazama tu na kisha kana kwamba ana umri sawa na mimi akaanza kuniomba msamahga ikiwa amezungumza vibaya.
Nikatumia fursa ile kujaribu kumlalamikia malkia kuwa hanitendei haki hata kidogo.
Mtego ukaenda sawa, akaniambia ni kweli hanitendei haki kwa sababu mimi namtesa.
Nikaduwaa, yaani hapo na hapo ninamtesa mama huyu.
Lakini sikutaka iwe mshangao wa muda mrefu nikamwambia nahitaji kuzungumza naye.
Akaniambia kuwa ataniita nyumbani kwake tutaketi na kuzungumza.
Akaendelea kusimamia shamba lile ambalo sijui lilitarajiwa kupandwa zao gani.
Nikajiweka kando kidogo hadi pale kilipovuma kimbunga cha ajabu, kimbunga kile kilivuma kuja upande wangu, nikajaribu kukikwepa kikawa kinanifukuza kwa nguvu, na kisha kikanipiga gwala nikaanguka chini, kikaendelea kuvuma huku kikininyanyua.
Kilipokuja kutulia nilikuwa ndani ya nyumba ile ya kifahari nba nilikuwa nikitazama na mwanamke mrembo wa kiarabu.
‘’karibu sana laazizi wangu…’’ sauti nyororo kabisa ilisema nami.
‘’wewe ni nani..na hapa ni wapi’’ nilihoji huku natweta kwa hofu.
‘’umehitaji kufanya mazungumzo na mimi…. Nipo hapa Martin sema nami kipenzi changu…’’ alizungumza binti yule mrembo katika maana halisi ya urembo.
Nilijisahau kabisa kuwa pale sikuwa katika dunia ya kawaida, nikajikuta nazipata zile hisia za kimatamanio kabisa ya waziwazi.
Nikajisahau kabisa kuwa nilikuwa nimeagizwa unywele wa malkia. Binti yule akanisogelea akinyata hadi akanifikia katika kochi ambalo nilikuwa nimetulizwa pale na kile kimbunga, akanishika mkono na kunivuta kuelekea nisipopajua.
Aliniingiza katika chumba kikubwa kilichokuwa na godoro kubwa sana akanisihi nilale pale. Nikatii amri yake na kujilaza pale.
‘’nahitaji kukupeleka katika dunia yap eke yako, nahitaji ukitoka hapa usimguse mwanamke mwingine bali mimi tu malkia wako’’ alizungumza kwa sauti nyororo sana iliyojaa mahaba tamanishi.
Nilipolala yeye akasogea kando na kisha akapiga makofi mawili.
Mama yangu wee….. lile godoro likaanza kubonyea na kisha taratibu likaanza kupotea na sehemu ile pakawa maji.
Kama hiyo haitoshi nilipojaribu kupiga mbizi nikahisi mguso fulani mgumu katika mbavu zangu.
Nikageuka kutazama ni kitu gani kilikuwa kimeniguza ni hapo nikakutana na domo kubwa la mamba…..
Hakuwa mmoja bali huo ukawa mwanzo wa kuwaona mamba wengi katika godoro lile la kimauzauza lililogeuka kuwa majki tena maji yenye mamba.
Nilipiga mayowe jamani, nililia sana huku nikiomba msamaha.
Nikimkwepa mamba huyu ninakutana na mamba mwingine……
Mara nikasikia kitu laini kabisa kikipenya katika mapaja yangu nikaingiza mkono na kukitoa.
Lahaula alikuwa ni nyoka mrefu mweusi.
Kitendo cha kumshika akavimba vipasa kisha akarusha kichwa chake kunifuata mimi…
Kifo nikakiona kikiwa katika mdomo wangu…..
Nyoka yule akanigonga katika mikono yangu, na hapo kimya kikatanda na matone ya damu yakaanza kuvuja kutoka katika dari pale ndani, damu ile ikawa inanimwagikia mimi.
Mamba wakaanza kunilamba kwa fuko…
Mamba ana ulimi mgumu jamani.
Hivi ni sayansi inasema kuwa mamba hawezi kutoa ulimi nje, mbona hawa mamba walikuwa wanbanilamba kwa fujo vile sasa……
Nguvu zikawa zinaniishia kadiri walivyokuwa wakinishambulia…
Kicheko cha yule malkia kiliendelea kutawala…..
UTATA…….
Kitu cha kushangaza ni kwamba licha ya wale mamba kuwa na sura za kutisha lakini nilijikuta nikifurahia namna ndimi zao zilivyokuwa zikiulamba mwili wangu, hapo awali nilikuwa nahisi kuumia lakini sasa ilikuwa ni raha ya ajabu sana. Nilitamani waendelee kunilamba vilevile, kweli wakaendelea hadi nilipofumba macho yangu.
Nilipofumba macho yangu nikawa katika ulimwengu mwingine kabisa nikiwa na yule malkia ambaye alikuwa amejiweka katika umbile la binti mrembo wa kiarabu.
Nikisema mrembo namaanisha haikuwa rahisi kumtoa kasoro, hata kile kicheko chake kikubwa kilikuwa kinasisimua bado.
Nilikuwa naye kitandani na ni yeye aliyekuwa akinilamba huku na kule.
Baadaye akaanza kuchojoa nguo zake.
Hatimaye akabaki mtupu na hapo nikaziona nywele zake jinsi zilivyomwagika mgongoni, palepale ikanijia ile kumbukumbu kuwa adell alaikuwa ameniagiza unywel wa malkia yule.
Nikatii alichotaka nifanye binti yule nikiwa katika mahaba mazito nikazifikia nywle zake na kukata kiasi cha nywele kwa kutumia meno yangu, nikaziacha mdomoni huku nikijipa tahadhari kubwa sana nisije nikazimeza.
Kweli mahaba yakachukua nafasi yake huku akinipa ahadi nzuri nzuri ambazo kwa mwenye tamaa angeweza kuingia mkenge, lakini mimi nilitaka kurejea duniani tu huku nikiwahi lisije likamkuta baya lolote mama yangu.
Baadaye akapotea yule malkia, kisha nikajikuta nipo katika kukimbizana na mamba. Nilikimbia kwa kasi hadi nikawa mbali na upeo wa wale mamba, na hapo fahamu zikanikaa sawa tena.
Nilikuwa nje ya kile chumba, nikiwa hata sijavuta pumzi zangu vizuri nikamsikia adella, alikuwa pembeni yangu na aliniuliza iwapo nilifanikiwa.
Hapo ndipo nikakumbuka kuwa niliagizwa nywele, nikakumbuka nilifanikiwa kuzihifadhi mdomoni.
Ila katika kukimbia ile dhahama ya mamba nahisi kuna kitu kilitokea.
Nilizimeza zile nywele bila kufahamu kama nilikuwa nazimeza.
Nilimueleza adella, akanieleza mara mbilimbili niseme ukweli nisimdanganye akajihangaisha bure.
Nilimsisitiza kuwa hakuna hata chembe moja ya uongo katika maelezo yangu.
Sikujua ni kitu gani alichokuwa anamaanisha dada yule.
‘’haya nikija unikaribishe usifunge mlango wako sawa…….’’ Aliniambia kauli tatanishi nikabaki kujiuliza huyu dada ana matatizo gani.
Hata kabla sijahoji zaidi akaondoka na kilichotokea baada ya dakika chache kila nikikumbuka huwa nasisimka na kusema kuwa duniani kuna vimambo vidogovidogo tu ila huko nilipokuwa ndio kuna mambo katika maana halisi ya mambo.
Nikiwa nimesimama pale mara alikuja nje usoni kwangu, ilikuwa mara ya kwanza kukutana na nzi kule lakini sikujali nikatumia mkono wangu kumpunga ili akae mbali nami, yule nzi akaondoka na kurudi tena usoni kwangu, nikampunga tena akaenda akarudi. Alikuwa anaunguruma kwa sauti iliyokuwa inanikwaza sana.
Nilipompunga kwa mara ya tatu alinigeuzia kibao nzi yule sasa akahamia upande wa masikio. Alilazimisha kupenya katika masikio yangu, nikaendelea kumpunga huku sasa hofu ikiongezeka.
Nikipunga sikio hili mara anahamia sikio la huku, nikipunga huku anakuja upende aliotoka awali.
Baadaye akatoweka zake nikajua ndio mwisho wa karaha ile, nikamngoja adell arejee nimuulize alikuwa ana maana gani aliposema kuwa akija nisiache kufungua mlango.
Nikiwa katika kuwaza vile nikamsahau yule nzi.
Hilo likawa kosa, nikashtukia ghafla katika sikio langu yule nzikapenya.
Ebwana eeh akatambaa upesi hadi kweli ngoma ya sikio huku akiendelea kuunguruma, nilikimbia jamani, usiombe kutokea na jambo kama hili. Kuingiliwa na mdudu sikioni. Hata akiwa mdogo hisia zinakuja kuwa ni mkubwa sana… mimi nilikimbia lakini sasa nikamsikia kabisa akipenya shingoni akawa anashuka chini huku akiunguruma. Niligalagala huku napiga mayowe. Nzi anazidi tu kupenya.
Ninasisimka mpaka leo nikikumbuka tukio lile, hakuna aliyekuja kunipa msaada nilikuwa mimi mwenyewe kwa asilimia zote.
Nilitapataba, hatimaye nikamsikia akitawala tumboni nzi yule.
Na baadaye akanza kupanda juu tena. Nilihisi kufa….
Safari hii hakupita sikioni bali alitokea mdomoni, upesi nikaachia mdomo akatoka.
Nikabaki nahema juu juu nisijue hata ni kitu gani hiki kimenitokea.
Nikiwa katika hali ile mara adella akafika, nilianza kumwelezea mkasa ulionikuta.
Adella akatabasamu kisha akaniambia.
‘’wewe nilikueleza kuwa uache mlango wazi ukaziba, nikaona nipitie mlango wa dharula..’’ alisema huku anatabasamu.
‘’adella… una unamaanisha nini wewe…..’’ nilimuuliza.
‘’niliingia kuchukua nywele, nilidhani umenidanganya, dah ulichukua nyingi zitatufaa sana…..’’ aliniambia. Sikutilia maanani kauli ya mwisho, nilitilia maanani kauli kuwa ni yeye alikuwa katika tumbo langu na ni yeye aliyepita sikioni kwangu.
Ilitisha sana kuamini katika tukio lile, lakiniu lilitokea na mimi ndiye mtokewa mwenyewe na hapa nafanya kukusimulia tu.
Usiombe ukakutwa na tukio kama hili.
‘’kesho tunaanza safari ya kuondoka, unatakiwa kuwa jasiri sana martin, tena jasiri sio kidogo yaani…. Kuna mambo magumu ukilemaa tu unakuwa katika mwisho mbaya. Utaishi njia panda ya kuzimu kwa mateso sana hadi kufa kwako…’’ alinieleza adella huku kwa mara ya kwanza kabisa nikiona ametawaliwa na hofu kuu.
‘’najua unawaza kuhusu yule nzi…. Hizo njia tunazitumia mara nyingi sana huku katika ulimwengu wetu.. sema mara nyingi tunaingia mwanadamu akiwa amelala, lazima tu ataacha masikio wazi lakini wale wanaolala midomo wazi tunawapenda zaidi maana ni rahisi sana kupitia mdomoni kuliko sikioni. Huwa tunaingia kwa akina mama kwa ajili ya kuzinyofoa mimba zao na kuzipachika mimba zetu feki, tunaingia kwa akina baba na kuvunja vizazi vyao….. huwa tunaingia katika namna hii martin. Ni njia hatari sana mfano mimi nilipokuwa napita mdomoni, ungesema unitafune tu basi kwisha habari yangu, na wewe pia ungekufa…. Ndo maana huwa tunaingia usiku wakiwa wamelala midomo wazi…..’’
Adella alinisimulia jambo lile kana kwamba ni jambo la kawaida sana katika maisha.
Kwangu mimi lilikuwa jambo linalosisimua na kutetemesha sana.
‘’kwa hiyo huwa mnaingia kwa yeyote mnayemtaka…..’’ nilimuuliza.
‘’mh hapana sio popote kuna watu wanazo kinga kali sana, ukimsogelea umekwisha, kwenye kinga hapa wapo ambao wametibiwa na kuwekewa kinga na mchawi ambaye anao utaalamu kupita sisi, na kuna wale wanaolindwa na Mungu…..’’
‘’hata nyie mnamjua Mungu kwani…’’ nilimuuliza nikiwa nimestaajabu.
‘’ni nani asiyemjua Mungu martin wangu, natambua kuwa haya tunayofanya sio sahihi nataka mimi na wewe twende duniani tukaombe radhi dunia na kisha tumtegemee Mungu…. Sasa hawa wanaolindwa na Mungu wapo katika madaraja tofauti, wale dhaifu kiimani huwa tunaingia bila wasiwasi, wale moto hatugusi hata nyumba yake, wale vuguvugu wasioelewa wapi pa kuegemea yaani wanategemea Mungu pamoja na waganga hawa ndo wepesi kupita wote katika kuwaingia….. maana wanaowategemea kila mmoja anategea kwa sababu hawapi imani wanayotaka….. unamtegemea Mungu na umefungwa hirizi nne….. hauna kitu wewe…’’ aliendelea kusema nami adella.
Na baadaye akaachana na mada hiyo, akanieleza kama nipo tayari kwa safari. Nikamjibu kuwa nipo tayari sana na ninamtegemea yeye kwa asilimia zote.
‘’twende kwa kutegemeana martin, usinitegemee mimi tu maana itafikia hatua hata mimi nitakutegemea wewe…’’ adella alizungumza kwa sauti ya chini iliyokuwa katika kitetemeshi cha wasiwasi….
‘’nitakuja kukushtua tuanze safari….’’ Aliniambia kisha akaondoka huku akiniachia pale chakula ambacho alikitoa katika mizunguko yake alipoagizwa duniani.
Kilikuwa chakula kizuri japokuwa kilikuwa kimepoa sana.
MWISHO???
 
HOUSEGIRL







  • SIMULIZI FUPI : HOUSEGIRL.



    "Kwanini umenifanyia hivi mke wangu, pamoja na kukupenda kote kule lakini umenifanyia mambo ya ajabu sana...." Rajabu aliongea kwa sauti ndogo yenye kuonesha maumivu makuu ndani yake.

    "Stop! Ishia hapohapo mjaa laana wewe, kwanza nani mkeo, labda useme nilikuwa hawala yako, cheo ambacho kwa sasa sikipendi hata kukisikia. Eti unanipenda, hivi unavyoniangalia mimi nina hadhi ya kupendwa na wewe, achana na mimi mwanaume suruali wewe!" Hanifa alisema kwa jazba huku akiwa ameshika kiuno chake, misuli ya shingo ikiwa imemtoka, ama hakika alikuwa amedhamiria.

    "Hanifa, leo hii mimi nimekuwa mwanaume suruali, sawa sikatai kweli kwa sasa mimi ni mwanaume suruali, tena unaweza kuniita hata mwanaume boksa kabisa, sina kitu kwa sasa lakini ni wewe ndiye...." Rajabu hakumalizia alichotaka kusema.

    "We we we! Koma kabisa, tena koma kama ulivyolikoma ziwa la mama yako, mimi nimekufanya nini, ni ujinga wako ndio sababu, sio mimi, ujinga ambao wewe unaiita mapenzi, mapenzi? sijawahi kupenda mimi, sijawahi kupendwa mimi, sina moyo wa kumpenda mtu, hapa inapendwa pochi, mama yangu mzazi mwenyewe simpendi itakuwa wewe, kama huna pesa hapa sepaa!" Hanifa alisema kwa nguvu zaidi sasa.

    "Hanifa, inawezekana kweli kwamba huna uwezo wa kukumbuka, ila nakuomba ujaribu, jaribu kukumbuka Hanifa...ulivyokuja hapa siku ile, ukiwa mnyonge, dhaifu tena mchafu, unakumbuka ulipokelewa kwa mikono miwili tena kwa upendo mkubwa sana, na mke wangu mama Sharifa..."

    "Baba, hiyo ni mwaka jana, huu mwaka mwengine, nilikuja kuomba kazi kama mfanyakazi wa ndani, nakubali ulikuwa Bosi wangu, lakini sasahivi mimi ndiye Bosi kwako, nakubali nilikuja bila nyumba, nilikuja kwa miguu toka kijijini kwetu Chamwino, lakini sasa nina nyumba na gari ya kutembelea, acha kuongelea yaliyopita. Kwa sasa.....huu mwaka mwengine baba, umenielewa baba?"

    "Nimemfukuza mke wangu kwa ushauri wako mbaya Hanifa..."

    "Baba, Penzi langu tamu ndilo lilikufanya umfukuze mke wako sio mimi, ni ujinga wako ambao wewe unauita mapenzi, hakuna mapenzi ya dhati dunia hii baba, kama unaamini kuna mapenzi ya dhati utagawa hadi roho yako bwege wewe!"dhati

    "Nimewafukuza watoto wangu wapendwa kwa ajili yako Hanifa, kwakuwa uliniaminisha utakuwa na mimi siku zote, na tutazaaa......"

    "He he he! Kikaragosi wewe uzae na mimi, unataka kunibangishia wanangu bure, ujinga wako nd'o uliokufanya uwafukuze wanao, hivi mtu mwenye akili zake timamu anaweza kuwafukuza wanae wa kuwazaa, kumfukuza mkewe eti kwa penzi la housegirl? Jitu kama hilo ndo nizae nalo....."

    "Hanifa umebadilisha jina la hati ya nyumba yangu....."

    "Ishia hapohapo babu wewe...nilikushikia bunduki ili uende kwa mwanasheria kubadilisha jina la hati ya nyumba yako, si wewe mwenyewe nd'o ulisema tukabadili ili uandike jina langu...Ahsante sana baba kwa hilo" Hanifa alisema huku akifanya ishara ya kupiga magoti.

    "Kadi ya gari...." Rajabu hakumalizia kusema alilotaka kusema, Hanifa alidakia.

    "Ulienda kwa mwanasheria kubadili jina la kadi ya gari ili kunimilikisha mimi, mapenzi tu hayo ndio yalikuchanganya toka kwa mwanamke wa Kigogo.....kwanza unaniharibia siku tu hapa, sina muda mchafu kabisa wa kuongea na wewe, nakuomba toka nje!" Hanifa alisema huku akilionesha geti kwa kidole.

    "Hanifa nionee huruma nitaenda wapi mimi...sina pa kulala.." Rajabu alisema kwa sauti iliyojaa huruma.

    "Nenda hukohuko walikoenda wanao na mkeo hapa toka!"

    "Hanifa.."

    "Jina langu, na Swalehe baba yangu"

    Hanifa alisema kwa nyodo.

    "Naomba..."

    "We Mwituuuuu!"

    Mlinzi anaingia kwa kasi akiwa na kirungu cheusi mkononi.

    "Toa huyu mbwa nje!"

    Mwitu anashangaa kidogo.

    "We mwitu!' Mwitu anastuka na kutekeleza agizo. Anamshika Rajabu kiunoni, anamnyanyua kiasi kwamba Rajabu anatembelea ncha ya vidole, mnyanyuo namna ile unaitwa Tanganyika jeki.

    Rajabu anatolewa nje ya nyumba aliyoijenga kwa nguvu zake mwenyewe, tena kwa dharau kubwa sana, tena na mlinzi aliyemwajiri mwenyewe.

    Anatolewa hadi nje ya geti na kubwagwa chini mchangani.

    Chozi la uchungu linamdondoka mchangani, analitazama geti la nyumba yake, anapangusa kamasi kwa mkono wake wa kushoto.

    Mara majirani wanaanza kujaa, kusaka umbea. Rajabu anaona akiendelea kulala pale chini atajaza watu, anainuka taratibu, na kwenda kusikojulikana.....

    " He he he Kantangazeeeeee" kicheko kikali kinasikika ndani toka ndani ya nyumba...

    Kilichoendelea mi' sijui.



    MWISHO
 
NILISHINDWA KUMLINDA MKE WANGU









  • "Kijana mmoja alipata uhamisho kikazi kutoka mkoa mmoja kwenda mkoa mwingine baada ya boss wake kufungua tawi jipya, wakati huo alimuacha mke wake ambaye ndo kwanza walikuwa na mwezi mmoja tu tangu wameoana hivyo kienyeji, yaani bila wazazi wao kufaham,, kijana yule aliyekuwa anaitwa Juma alijitahidi kumshawishi boss wake kutengua uhamisho ule lakini ilikuwa ni ngumu sana japo Juma hakujua ni kwanini, boss wake na Juma alimuongeza hadi mshahara na kumvutia zaidi Juma kwani Elimu yake ilikuwa ndogo hivyo aliona hiyo ni bahati kubwa,

    "baada ya kushauriana na mkewe hatimae walikubaliana huku mkewe akimuahidi Juma angeomba uhamisho kazini kwake pia ili amfuate mume wake, Siku ya safari iliwadia huku Juma akimuaga mkewe Jacky na safari ya kwenda mkoani mwanza ikianza, Wakati akiwa ndani ya basi Juma alikuwa akimuwaza zaidi mkewe Jacky huku mara kwa mara akipoteza Furaha kabisa...

    ***********

    "Hatimae Juma alifika kazini kwake, mwanzoni haikuwa rahisi yeye kuishi peke yake kwani alikuwa ameshamzoea sana mke wake, muda mwingi alikuwa akimpigia simu mke wake na kumuulizia kuhusu kuomba uhamisho lakini Jacky alishindwa kumpa jibu la kueleweka, Hatimae miezi mitatu ilipita Juma akapata rikizo, hakutaka kumuambia mkewe kwani alipanga kumfanyia suprise ambayo yeye aliamini ingekuwa ni suprise kubwa sana, alimnunulia nguo na maua mengi mazuri, kisha akaenda kupima afya yake kama kawaida na kukuta akiwa safi kabisa,

    Kutokana na umbali wa safari wa mwanza to Dar, alijikuta akifika saa sita kasoro usiku, alichukua bodaboda na kuanza safari ya kwenda nyumbani kwake huku akijihisi mwenye furaha sana na muda wote alikuwa akitabasamu kila akikumbuka anaenda kuonana na mke wake kipenzi sana ambaye wameona miezi michache tu iliyopia, Bodaboda ilimshushia hadi nje ya nyumba yake,alishangaa baada ya kuona gari ikiwa imepaki nje ya nyumba waliyokuwa wamepanga,

    *******

    "Juma alikuwa akimuamini sana mke wake, kwahiyo hakuwazia chochote kuhusu gari ile, alilisogelea dirisha la chumba cha mke wake ili agonge,, ila kabla hajalifikia vizuri alisikia sauti za mahaba zikiwa zimekitawala chumba kile, hapo ndipo joto la mwili wake lilipopanda na kujikuta akilegea, begi alilokuwa amelibeba lilianguka, huku Juma nae presha ikipanda na kuanguka hapohapo, kishindo cha Juma kiliwashtua Jacky na mwanaume wake ambaye walikuwa mapumziko baada ya kufika safari yao ila hawakujali sana waliendelea na raha zao bila kujua kama Juma ndiye aliyekuwa ameanguka nje,,,

    "Baada ya baridi la nje, Juma alishtuka saa kumi na moja asubuhi na kujikuta chini, aliinuka na kujikung'uta vumbi huku akiyakumbuka maneno ya mama yake,

    "HATA SIKU MOJA USIKUBALI KUFA KIZEMBE MWANANGU, SIYO KWAMBA MUUWAJI HADI AKUWEKEE SUMU AU KUKUCHOMA KISU BALI HATA ASIYEJALI UTU WAKO NI MUUWAJI PIA, UKIMGUNDUA ADUI YAKO NI RAHISI KUMSHINDA"

    "Maneno yale yalimkaa vizuri sana akilini mwa Juma, wakati anawaza hayo ghafla mlango wa nyumba yake ulifunguliwa, roho ilimuuma alipomuona jacky akiwa ameshikwa kiuno na boss wake, cha kushangaza Jacky hakushtuka zaidi ya kumkumbatia boss wake kwa dharau huku wakifunga mlango na kuingia ndani ya gari lao, kabla hawajaondoka Juma alifungua begi lale lililokuwa na zawadi za Jacky kisha akasogea hadi karibu na gari na kuzirusha kupitia dirishani,

    "Unanichafulia gari langu bhana, nyie wanaume suluari sijui mpojeee alaaah"!

    Ni maneno aliyozungumza Jacky na kuzidi kumuumiza zaidi Juma ambaye aliamua kuondoka na kurudi stand kisha akapanda gari za kwenda kijijini kwao...

    ****

    "Haikuwa rahisi Juma kumsahau Jacky wake hadi jitihada kubwa za mama yake zilipofanyika na kuamua kumpeleka mwanae mjini kwa baba yake mdogo ili kumtafutia kazi nyingine, kutokana na Elimu ya Juma haikuwa rahisi kupata kazi na alikaa kwa muda kidogo kabla hajapata kazi kama ya mwanzo ya hotel, alifanya kazi ile kwa muda mrefu huku akimsahau kabisa Jacky na kujikuta akipata mwanamke mwingine ambaye alikuwa ni askari polisi,, mapenzi yao yalidumu kwa muda mrefu hadi wakapanga kwenda kutambulishana kwa wazazi wao., juma ndo alikuwa wa kwanza kumpeleka Binti yule nyumbani kwao na kumtambulisha kwa mama yake, Zamu ikafika kwa Juma kupelekwa nyumbani kwa mchumba wake huyo mpya ambaye alichukua nafasi ya Jacky, waliongozana huku Juma akivaa nguo za heshima sana hadi nyumbani kwa akina Jane, walifika nyumbani pale na kumkuta mama Jane akiwa anajiandaa kutoka, walipomuuliza aliwajibu anaenda kituo cha polisi kwani wamemkamata mtu anayesambaza virusi vya ukimwi kwa nguvu, na tayari hata mwanae ameshamuambukiza hivyo wamemshtakì, Jane aliposikia hivyo aliungana na mama yake, hivyohivyo hata Juma naye hakutaka kumuacha Jane wake muda huo, waliongozana hadi kutuo cha police ili kumuona huyo mtuhumiwa,, Moyo ulimwenda mbio Juma alipomuona boss wake akiwa ndo mtuhumiwa mkuu, aliangalia pembeni akamuona Jane akikumbatiana na Jacky huku akiita" Dadaaa" wakati huo machozi yakimtoka...

    "Hapo ndipo Juma alipogundua kuwa Jane na Jacky ni mtu na dada yake,,,

    "Moyo wa Juma ulienda mbio zaidi baada ya macho yake kukutana na macho ya Jacky yaliyokuwa yamevimba kwa kilio huku yakiwa yamejaa machozi, Juma alitumia muda huo kuitazama mikono ya Jacky hapo akafanikiwa kuona moja ya ua alilowahi kumchukulia kama zawadi,inaonekana ua lile Jacky alikuwa anatembea nalo kila sehemu kama kumbukumbu kwake, Baada ya Jacky kumuona Juma,alimuachia dada yake Jane na kipiga hatua akasogea hadi alipokuwa Juma,kisha akapiga magoti huku akilia kwa uchungu sana,,

    "Juma baba, najua nilikuumiza sana ila haya ndo malipo yangu ya usaliti,nilishi

    ndwa kuridhika na kidogo ulichokuwa unanipa na nilichokuwa nataka,ona sasa hali yangu ilivyobadilika, sina kazi,sina mali,nilipokuwa naishi nilifukuzwa baada ya kushindwa kulipa kodi,kibaya Zaidi nimepata maambukizo na nimekupoteza pia wewe mwanaume uliyekuwa na msimamo kwangu,mwisho wa yote nawatakia maisha mema ya ndoa wewe na dada yangu"

    maneno yale yaliwatoa machozi wote,sio mama,Juma wala Jane, wote walijikuta wakilia kwa nguvu na kimfanya Juma kugundua lengo la boss wake kumhamisha kikazi ikikuwa ni kumpata kiurahisi Jacky alijilaumu kwa kushindwa Kumlinda mke wake,, hakuwa na kinyongo zaidi ya kumsamehe ingawa tayari sasa alikuwa kama shemeji yake na siyo mke tena,,,,

    FUNZO_

    =>We kama mwanaume unamlindaje mchumba/mke wako dhidi ya hatari kama hizi?

    =>Tamaa siyo nzuri,ridhika na unachokipata kwa muda huo kwani hujui mungu kakupangia lini ridhiki yako

    =>Usikubali kuuza utu wako kwa kitu.


    MWISHO
 
UNGEFANYA NINI?







  • UNGEFANYA NINI?

    Mwanamke alimkimbia mumewe na akamuachia mtoto mwenye miaka mitatu.

    Sababu kubwa ya kumkimbia mumewe ni kwamba alipata boyfriend mwenye hela ambaye alikuwa akiishi Michigan huko Marekani.

    Huyo Boyfriend au mchepuko wake walijuana kupitia mitandao ya kijamii. Walizoeana sana na mwisho yule boyfriend wake akamuahidi kumtafutia viza ya kuishi Marekani.

    Na kweli baada ya miezi kadhaa yule mwanamke alimtoroka mumewe na kutokomea Marekani, huku akiacha taarifa kwamba asitafutwe tena, anaenda kuanza maisha mengine mapya. (mumewe alifirisiwa kutokana na kutuhumiwa ubadhirifu wa mali za kampuni alikokuwa akifanya kazi).

    Kutokana na msongo wa mawazo na upweke kwa kipindi kirefu tokea mkewe amtoroke, yule mwanaume akaamua kuoa mke mwingine.

    Kwa bahati mbaya yule mwanamke mwingine aliyeolewa hakuweza kushika mimba. Hata hivyo yule mwanamke mwingine alimtunza vema mtoto wake wa kambo kama mwanae vile.

    Miaka michache baadae, yule mume alifariki kwa ajali ya gari alilokuwa akisafiri nalo kwenda kijijini kufanya biashara ya mazao.

    Mke wake wa pili alifanya kila jitihada kwa uwezo wale wote kumsomesha yule mtoto, na Mungu hakunyimi vyote kwani yule mtoto alikuwa na uwezo mkubwa wa kiakili.

    Mwanamke aliuza nyanya sokoni, alitembeza ndizi, alichoma mahindi barabarani na kadharika ilimradi aweze kujitunza yeye na yule mtoto wake wa kufikia.

    Yule mtoto alijua kwamba yule ndiye mama yake halisi na ndiye aliyekuwa akimuita mama.

    Mama yake halisi aliyetorokea Michigani, Marekani, hakuwahi hata siku moja kutuma salamu au kuwasiliana na mtoto wake, ingawa alipata habari kwamba mumewe wa zamani alifariki kwa ajali.

    Miaka mingi ilisonga na kijana alikuwa kwa akili na kimo, alikuwa Chuo kikuu akisomea Uhandisi wa mafuta na gesi (Bachelor of science in petroleum Engineering).

    Mama yake halisi aliyeko Marekani hakuweza kupata mtoto tena na yule mwanaume mwingine aliyemuoa, na kwa hilo yule mume wake mpya aliamua kumtimulia mbali.

    Kwa kutambua kuwa alifanya kosa kumkimbia mwanae, aliamua kurudi nyumbani kumtafuta mwanae na kumkabidhi utajiri alioupata akiwa Marekani (gawiwo la nusu kwa nusu la mali baada ya kutalikiana na mumewe wa Marekani)

    Bahati mbaya alifika na kumkuta mwane akipigania kati ya uhai na kifo kutokana na kufeli kwa figo zake. Madaktari walikuwa wakihitaji pesa nyingi kwa ajili ya upasuaji, pesa ambazo mama yake wa kambo alishindwa kabisa kuzipata.

    Mama yake halisi kutoka Marekani aliingilia hilo suala na kulipa pesa zote za hospitali kwa ajili ya matibabu, pia akatoa figo yake moja na maisha ya kijana yakawa yameokolewa.

    Baada ya matokeo ya mwisho ya chuo kikuu kutoka, kijana alipata ufaulu wa hali ya juu (first class degree) na akapewa ufadhili wa kwenda kusomea shahada ya uzamili (master's degree) na baada ya hapo udaktari wa falsafa (phd) huko Burnley, Uingereza.

    Katika kupokea cheti chake siku ya mahafali chuoni kwao, makamu mkuu wa chuo alimpa kipaza sauti kijana na kumwambia amuite mama yake katika stage na kupokea cheti cha heshima.

    Baada ya makamu mkuu wa chuo kusema hayo, mama yake halisi aliyemkimbia alisimama na kujiweka sawa kusubiri kuitwa na mwanae, wakati mama yake wa kambo aliyemlea tokea mdogo akiwa bado amekaa huku machozi mengi yakimtoka huku akimuangalia mwanae wa kufikia kule mbele.

    Jibu naliacha hewani.........................

    Fikiria wewe ndio huyo mtoto, utamuita nani aje kule stejini kupokea hicho cheti?

    A) Mama wa kambo

    B) Mama mzazi

    Nahitaji majibu yenu, kama huna share kwa wengine waje na majibu.
 
USISAHAU ULIPOTOKA







  • SIMULIZI FUPI : USISAHAU ULIPOTOKA



    Binti mmoja ambaye alitokea katika familia masikini alifanikiwa kusoma kwa shida mpaka kufanikiwa kuwa mwanasheria. Alipata kazi nzuri, akiishi katika nyumba nzuri ya kifahari.



    Pamoja na maisha mazuri lakini binti aliwasahau kijijini kwao, alikua akituma pesa kidogo lakini hakutaka kwenda. Alitaka kuyasahau maisha yake yote ya mateso ya kijijini.



    Hata kwa marafiki zake alijitambulisha kama kazaliwa Dar huku akidanganya kuwa wazazi wake wamefariki nayeye alikua ndiyo mtoto pekee, hii ni kwasababu marafiki zake wote walikua wakitoka katika familia za kitajiri.



    Baada ya kukaa muda mrefu bila kufika kijijini kwao wazazi wake walipata wasiwasi, huku wakiwa na wasiwasi kuwa kuna kitu kimempata, walichangisha nauli na Mama yake ambaye alikua mzee sana alipanda gari na kwenda kumuona mjini.



    Alipelekwa na jirani yao mmoja ambaye alikua akifahamu alipokua akiishi yule binti. Mama alifika na kukuta binti akiwa na afya nzuri, hana tatizo lolote. Binti alikasirika sana kumuona Mama yake kwani alikuja bila taarifa.



    Hakumsalimia vizuri na kila saa alikua akimlaumu kwanini hakupiga simu kwanza na kama ni hela si angesema amtumie. Mama huku akitokwa na machozi ya furaha alisema shida yake haikuwa hela bali kumuona mtoto wake baada ya muda mrefu.



    Binti alimdanganya Mama yake kua ile nyumba ni nyumba ya kampuni hivyo haruhusiwi kuishi na mtu yoyote kutokana na kazi aliokuwa anaifanya hivyo yeye asingeweza kuishi pale.



    Mama hakuwa na maneno, alimuambia hamna shida yeye kwakua ashamuona mwanae roho yake imetulia kwani hakuenda kukaa pale alienda tu kumuona.



    Binti alimuacha Mama yake apumzike siku ile na kesho yake ili siku inayofuata apande gari kurudi kijijini. Siku iliyofuata baada ya kutoka kazini rafiki zake walikuja, kulikua na sehemu ambayo walishapanga kwenda.



    Walimkuta Mama yake akiwa nnje akipunga upepo. Walimsalimia vizuri na binti alipowaona aliwakimbilia kuwawahi ili Mama sijitambulishe, alifika na kuwaharakisha rafiki zake ili waondoke.



    Walipotaka kujua ni nani, alijikuta anadanganya “ Huyo Mama amepotea njia, alipita hapa alikua anamtafuta mtoto wake akakosea nyumba, sasa ndiyo namsaidia, aligonga kwangu kuomba simu, kwani alikua na namba ya mwanae kwenye kikaratasi.



    Nimeshampigia mwane atakuja kumchukua. Binti alionge akiamini kuwa kesho yake anamuondoa Mama yake mule ndani hivyo rafiki zake hawatamuona tena.



    Wakati akiongea yale maneno hakujua kuwa Mama yake anasikiliza, alistuka baadaye alipogeuka wakati anafungua mlango wa gari ili aingie. Mama yke alikua anatokwa na machozi, binti alijikaza kama vile hakumuona akaingia kwenye gari na kuondoka.



    *****

    Baada ya mizinguko yake binti alirudi nyumbani, hakumkuta Mama yake, alimuuliza mfanyakazi wa ndani akasema hajui, alijua wameondoka wote kwani alimuacha nnje wakati yeye anatoka na gari.



    Binti alianza kupaniki, alisubiria mpaka usiku wa mamnane lakini Mama yake hakurejea. Hapo alianza kuchanganyikiwa, kichwa kikikumbuka maisha ya shida waliyopitia, namna ambavyo Mama yake alivyoteseka kwaajili yake.



    Machozi yalinza kumtoka akijutia mambo aliyomfanyia Mama yake. Alimtafuta yule Kaka ambaye alimleta Mama yake pale lakini hakuwa akijua chochote. Usiku ulipita akiwa macho, asubuhi alilazimika kwenda kazini kwani alikua na kikao.



    Lakini mchana alishindwa kuvumilia, ilibidi kwenda Polisi na kuanza kumtafuta Mama yake lakini hakupatikana. Siku moja ilipita na hatimaye yapili ilipita bila kumuona Mama yake, alianza kuwa na wasiwasi.



    Akiwa ofisini hajui hili wala lile rafiki yake mmoja alikuja, walianza kuongea akiwa hana raha kabisa. Rafiki yake alimuuliza tatizo lilikua nini akaamua kumuambia, lakini kabla hajaanza kuonge arafiki yake alisema.



    “Halafu shogaa nilitaka kusahau, unamkumbuka yule Bibi ambaye tulimkuta kwao jana?”

    “Ndiyo namkumbuka! Amefanya nini? Umemuona wapi?” Alijikuta anadakia kwa haraka kutaka kujua.

    “Basi jana wakati natoka kazini nikapita sehemu, nimekuta watu wamezunguka, kumbe kagongwa na bondaboda kaumia kichwani, watu wakawa wanakimbia kukwepa ushahidi.



    Namimi nikapita, sasa baadaye narudi kumbe watu walimuacha pale Bibi wawatu mpaka Polisi wanakuja lisaa lizima baadaye basi Bibi wawatu kashafariki. Kusema kweli roho iliniuma sana kwa kumpita bila kumsaidia…”



    Rafiki yake aliongea kwa masikitiko, lakini kabla hajamalizia yule binti alidondoka na kupoteza fahamu. Alizinduka yuko hospitali kazungukwa na marafiki zake na mchumba wake.



    Walimuuliza sababu ndipo alipoamua kuwaelezea, kila mtu alimshangaa kwa kumficha Mama yake, walihangaika kumtafuta wakakuta maiti yake, wakamsaidia kusafirisha maiti mpaka Kijijini.



    Walizika salama lakini baada ya kurudi mchumba wake alimuacha, marafiki zake wote aliokuwa akiwaona wa maana walimtenga kutokana na tabia zake. Binti alishikwa na msongo wa mawazo.



    Kila siku ilikua kulia tu, alishindwa kufanya kazi vizuri, sasa hivi amefukuzwa kazi. Kahama nyumba ya kifahari aliyokua akiishi na sasa yuko mtaani akitafuta ajira huku akiona hata aibu kurudi nyumbani kuwaona ndugu zake.



    MWISHO KAMA kisa hiki kimekugusa na unampenda sana Mama yako, unakumbuka uliko toka hembu SHARE na marafiki.


 
UTENGANO







  • UTENGANO



    “Mimi sitakubali hilo lifanyike hata kidogo humu nyumbani. Heri nimwondokee kuliko kuwa na mke mwenza.” Nilisikia sauti ya mama ikija juu. Baba naye aliguruma kwa sauti akimwarifu mama kuwa ni wajibu wake kumrithi huyo mjane na kuwa hakuna kitakachomzuia. Majibizano hayo makali baina yao yalinifanya kuingiwa na wasiwasi. Nilikuwa sebuleni nikifanya marudio ya mwishomwisho kwa matayarisho ya mtihani wa kitaifa. Runinga nayo ilionyesha pasi na wa kuitazama.

    Nikasikia tena sauti ya mama ikija juu, mara hii akitaka kupewa talaka na baba. Sauti yenyewe ilinifanya kunyanyuka halahala kutoka nilikoketi. Nikapitia mlango wa kati na kuelekea ndani kulikokuwa chumba chao cha kulala. Nikaegeza sikio langu mlangoni ili kusikia vyema yaliyokuwa yakisemwa. Nilijua vizuri kuwa huo ulikuwautovu wa nidhamu lakini nililazimika kufanya hivyo kwani pasipobudi hubidi.





    Sauti ya baba ilisikika ikimwonya mama kuufyata mdomo wake au aongezwe nyingine. Nikawa bado nawazia lile baba alidhamiria kumwongeza mama niliposikia mlipuko wa ghafla, uliofuatiwa na usiahi mkali wa mama. Kishindo kikubwa kikasikika sakafuni pu! Sasa nilikuwa nimepata fununu kuhusu yaliyokuwa yakiendelea baina yao wawili tangu Muge, nduguye baba kuipa dunia mkono wa buriani mwezi mmoja uliopita.

    Nilisikia kwato za baba zikiukaribia mlango na harakaharaka nikarejea sebuleni na kuketi kwenye zulia sakafuni, mara hii karibu na runinga. Sio kwamba nilitazama filamu iliyokuwa ikiendelea bali nilikuwa nikiwazia yaliyokuwa yanatusibu usiku huo. Vita vilikuwa baina ya baba na mama lakini kama motto wao wa pekee, niliathirika pakubwa. Kweli mtego wa panya huingia waliomo na wasiokuwemo.

    Kwa nguvu, nilisikia miguu ikitembea kwenye ushoroba na kukaribia sebuleni. Mlango ukafunguka ghafla na baba akaingia nilikokuwa. Kwa mitazamo ya kuibia, niligundua kuwa macho yake yalikuwa mekundu ajabu. Uso wake ulifinga na tabasamu huioni tena.nilimtazama kwa uchukivu mwingi. Nilinyamaa kama maji kwa mtungi kwani nami ningepata kichapo cha mbwa usiku huo kwani ukiona cha mwenzako chanyolewa chako tia maji.

    Nilisimama kwa utaratibu na kuelekea mle chumbani alimokuwa mama. Nilikuwa nimeukaribia mlango tayari kuufungua sauti ya baba iliponguruma kunionya utoingia mle.mnyonge hana hiari. Nilitii maagizo shingo upande. Nikatamani kumjibu lakini nikameza mrututu kwani samba akinguruma mcheza ni nani? Kwa muda mrefu kimya kilijiri na kutawala baina yetu, isipokuwa mtima wangu uliosikika ukipabapaba kwa nguvu kama mtambo wa jenereta. Kimya kingi kina mshindo. Baba aliyakodoa macho yake kwenye runinga na kujitia hamnazoasjue kilichokuwa kikiendelea. nilitamani kubonyeza kitufe kilichokuwa mbele yangu ili kuizima lakini nikabaini yale ambayo yangenisibu usiku huo.





    Mlango ukafunguka na mama akaingia sebuleni. Nikatambua kuwa shavu lake lilikuwa limevimba ana macho kufura kama ishara ya dhiki aliyopata hata ingawa alijifanya mcheshi.nilimfuata kuelekea jikoni. Ghafla baba akaingia mle akitaka chakula cha jioni.

    “Kamwendee huyo Amira aje akupe…” hata kabla kukamilisha sentensi yake, baba alimfikia na kuanza kumzaba makofi. Mara hii, mama hakulimatia. Vita vikawa vimeanza tena, mara hii wapiganaji wakielekea sebuleni. Mama alipata msukumo uliomfanya kunifikia na hata sahani niliyobeba ilinitoka mkononi na tang! Kuanguka sakafuni ikapasuka vijipande. Nilijiingiza kati yao na kujaribu kuwatenganisha huku machozi yakinidondoka pia. Uchungu wa mwana kuwaona wavyele wake wakivurugana ukaniingia na kunidhurubu kwelikweli. Kwa kiasi kidogo, kuwepo kwangu kati yao iliwazuia kupigana. Baba alikuwa ameumwa shavuni na miwani yake kupasuliwa. Akawa anazungumzia kumdunga mama kisu afe. Akamsukuma mama kwa nguvu na kumfanya kuanguka kwa kishindo akanjigonga ukutani na mapua kuanza kuvujaa. Baba naye akajibwaga kochini akihema na kutweta kama aliyetoka mbioni.

    Machozi yalizidi kunitiririka na nikatamanikuwaita majirani lakini mlango ulikuwa umefunwa ndi! Na baba. Nilitazama saa ukutani. Akrabu ziliashiria saa nne unusu. Kumbemavutano hayo yalikuwa yameendelea kwa masaa mawili mtawalia. Kando yake niliona picha ya wazazi wakifunga akidi za maisha. Picha yenyewe ilimwashiria baba akimvisha mama pete. Mama naye alijaa tabasamu usoni na kuonekana mrembo kupindukia. Kasisi pia alionekana akishuhudia na waumini wakishangilia. Kumbe kweli mambo ni kangaja.

    Kilichounganishwa na Mungu kanisani mbele ya hadhira, sasa kilikuwa kikitenganishwa kisiri na vita vya wenyewe kwa wenyewe. Sababu ya swala nyeti la urithi wa mke, jambo ambalo nililiona kama tamaduni iliyopitwa na wakati. Nilijilaza sakafuni angalau kusali iwapo sala ingesaidia kuokoa jahazi lililokuwa likizama. Daktari mzima kama mama ambaye huwatibu wagonjwa sasa alikuwa akigaaga sakafuni kwa maumivu pasi na wa mbinu zozote zakujisaidia. Kumbe kweli mganga hajigangi. Nilimhurumia mama na kumchukia babangu. Kwa mara ya kwanza nikatamani kuwa muuguzi, nimpe mama usaidizi na huduma ya kwanza.





    Baba naye, mwanasheria muungwana alikuwa amevunja sheria kwa kuendeleza taasubi za kiume nyumbani na kumpiga mama. Ni kweli kwamba mvunja nchi ni mwananchi. Nikaapa kutoshiriki katika ndoa iwapo hayo ndio mazao ya mapenzi na ndoa. Tena nikatamani kuwa hakimu ili nimpe baba hukumu ya kumfa maishani na kumfunza adabu. Nikashindwa la kufanya na nikajilaza sakafuni huku macho yamevimba na kichwa kuniwanga kutokana na kulia kwa muda mrefu.

    Akanifikia mama na kuushika mkono wangu wa kulia na kuninyanyua.

    “Amka twende zetu. Mahala hapa si salama kwako mwanangu.” Alisema mama huku akinifuta machozi. Akaonyesha bayana kuwa uchungu wa mwana aujuao ni mama. Kusikia hayo, baba pia aliinuka na kunifikia. Akaushika mkono wangu wa kulia.



    “Popote huendi mwanangu kwani nyumbani ni nyumbani hata kama hapakaliki.” Alisema na kunipa busu hata penzi la baba kwa mwana likadhihirika waziwazi.

    Wote hawa niliwapenda sana. Ningemfuata nani? Mtihani wangu ningeufanyia wapi na tamaduni zilizopitwa na wakati madhara yake gani? Maswali yalinihujumu mno. Wote walikuwa wakinivuta upande wao. Walikumbuka usemi wa wahenga kuwa kila mwamba ngoma huvutia kwake. Nilimtazama mama. Nikamwangalia baba. ‘Fanya uamuzi wa haraka.’ Nilijiambia kwani sasa familia yetu ilikuwa inatengana milele
 
MDUDU ALINIUMA









  • MDUDU ALINIUMA



    Mbinguni, jua lilikuwa limemaliza kazi yake na sasa lilijikokota magharibi huku mionzi yake miekundu ikiwapungia walimwengu kwa ulegevu kana kwamba kuwashukuru wale wote walioipenda. Masikini nilibaki pale uani nimelitumbulia macho, huku machozi yakijikusanya tayari kumwagika. Heri ningekuwa jua. Nisingekuwa na wasiwasi wa swala lolote. Langu lingekuwa tu kuchomoza asubuhi na kutua jioni.



    Nilikuwa nimechoka kuwatazama wapita njia na magari ya kifahari. Yalikuwa mapya na yalikwenda kwa kasi tena bila kutoa sauti. Lakini kuna yale yaliyochakaa yenye breki zilizokwaruzana kila yaliposimama. Watu nao walipita wa aina tofautitofauti; si weusi, si weupe, warefu kwa wafupi na hata vijana kwa wazee. Kwa umbali,taa za umeme zilikuwa zimelimwaia jiji mchana bandia wa mwangaza. Ishara kuwa usiku ulikuwa unaingia na giza kuanza kutawazwa.

    Yote hayo sikuyaonea fahari tena. Mambo yalikuwa kangaja kumbe na sasa yalikuja. Niliketi nikiwazia matokeo ya daktari, ambayo niliyapokea takribani miezi miwili iliyopita. Awali, walinificha ukweli lakini niliposisitiza, nilipasuliwa mbarika. Laiti wasingelinijuza kwani tangu hapo maisha yangu yalichukua mkondo tofauti mno. Mwenyewe, ile hamu na tama ya kula vyakula iliniondokea. Nikawa sili lolote, sinywi chochote. Mashavu yangu yalizidi kushobwekea ajabu. Nguo zangu ningezivua, mbavu zingehesabika hadharani moja baada ya nyingine. Nyele zangu zilizokuwa ndefu na nyeusi ti sasa zilibadili rangi na kuanza kuchipuka ovyoovyo. Mdudu alikuwa ameniuma. Lakini yupi?





    Darubini yangu ilinikumbusha mambo yalivyoanza. Yote yaling’oa nanga baada ya kumaliza kidato cha nne. ‘Mrembo’ nilijidai kwenda jijini kutafuta kazi ya ukarani. Niliwahakikishia wazazi kuwa nilikuwa na rafiki wengi waliojitolea kunipa makao wakati nikitafuta kazi. Wavyele wakadinda kuniruhusu mwanzoni lakini baada ya kuzidi kusisitiza na kufanya kiburi nyumbani, waliafikiana na kuniacha kwenda zangu. Pengine walikumbuka kuwa mtoto akililia wembe mpe. Nilipokuwa nikiondoka, mama alikuwa na huzuni mno na kwa uchungu, alinionya kuwa mwenda tezi na omo marejeo ni ngamani. Potelea pote. Sikutaka kusikia ya yeyote kwani nilijitia hamnazo nisikie la mwadhini wala la mteka maji msikitini. Nikawa binti kiziwi asiyesikia anayoambiwa.

    Kazi baada ya kuikosa,nilijiunga na wenzangu na tukajiajiri wenyewe. Malipo yakawa ya kuvutia ajabu kwani wateja walivyoongezeka ndivyo malipo yalivyoongezeka. Alimradi ujue namna ya kuwaongelesha na kuwahudumia wateja sawasawa. Jambo ambalo nilijifunza kufanya hata nikabobea na kutopea katika nyanja hiyo. Waume niliwabadili kama nilivyobadili mavazi yangu kwa siku. Nikawa ndiye jogoo la shamba lililowika jijini. Nikazika katika kaburi la sahau kuwa jijini kuna papa na papaupanga, ambao ukiwapapia, hukosi kupapatika kwa majuto, dhiki na mateso kama hayo yaliyonikumba sasa. Lau kumbe mwiba wa kujidunga hauna kilio.





    Kutoka hapo uani nilikoketi, taa za umeme nilizoziona zilinikumbusha mengi. Kuhusu mienendo yangu ya awali nilipokuwa kipusa ajabu. Niliingia kwa vilabu hivyo vyote vya usiku huku mikono ya watu tofauti yamezinga kiuno changu chembamba kama cha nyigu. Daima kucha zangu zilizokuwa ndefu na zilinaksishwa rangi sawia na nguo zilizovalika. Mdomo wangu ukakolezwa rangi nyekundu kana kwamba nililamba damu mbichi. Lakini kumbe dunia mti makavu kiumbe usiuegemee.

    Watu hao niliowatazama waliniongezea uchungu mtupu. Moyo wangu mchanga ulijaa uchukivu na furaha ikawa imeyeyuka kama kipande barafu katika utupu wa mchanga wa jangwa la Sahara. Wale wasichana warembo waliovalia mavazi yaliyoacha sehemu za miiliyao kuonekana waliniudhi zaidi. Laiti wangelijua kuwa dunia itawararua na kuwaacha uchiuchi, wasingefika hata barabarani. Nilitamani kuwafikia niwaonye na kuwapa ukweli wa mambo kuhusu madhara ambayo yangewasibu lakini nilishindwa. Mimi pia nilikuwa hivyo na sasa nilikuwa naangamia. Nikakumbuka kuwa asiyefunzwa na mamake hufunzwa na ulimwengu.

    Waume nao niliwatazama kama wanyama mwitu waliovalia suruali ndefu na sharti tofauti. Wanyama wenye uwezo mkali wa kukuvamia wakakumaliza kabisa. Wao ndio walionipa maji machafu yaliyokuwa na mdudu ambaye aliniuma na kunifanya kuugua sasa. Niliwatazama kwa uchukivu mwingi.





    Raha nyingi ya ulimwengu ulitoweka na badala yake ikawa sasa ni huzuni tupu na majuto. Sasa niliishi kwa jumba hilo kubwa peke yangu. Ulimwengu ulinitenga kana kwamba mwenye ukoma. Wale wote waliokuwa wakiingia na kutoka siku nzima hata usingewaona. Dada yangu mdogo ndiye alijitolea kuniuguza pale kwani sikutaka kuishi na wazazi na kuwapa mzigo wa kunitunza. Ikanijia kuwa mla nawe hafi nawe ila mzaliwa nawe. Sikujua wa kumlaumu. Wazazi? La wao walinitakia mema na kunionya kusoma kwa bidii. Marafiki? Kwa kiasi kidogo lakini ndimi niliyekubali kudanganywa. Ulimwengu? Ndiyo lakini sehemu gani ya ulimwengu? Mimi ndiye wakulaumu na sasa mwiba wa kujidunga hauna kilio.





    Ndoto zangu zote zilitoeka kama ukungu na umande. Azimio langu la kutaka kuendeleza masomo katika chuo kikuu katika fani ya sheria, na kufuzu katika uzamifu na uzamili lilitoweka ghafla kama mwangaza wa mshumaa uliozimwa na upepo. Nilitoka uani na kuingia katika chumba changu cha kulala. Mezani, kulikuwa picha yangu ya awali.nilijiangalia tena na kujiona tofauti; mnene, mwenye sura ya maji ya kunde tena mcheshi ajabu. Lakini sasa nilikuwa kama shetani hata ingawa sijawahi kuonana naye ana kwa ana. Haina maana kuishi katika hali hiyo! Niliifikia kalamu na kuandika kitu kwa karatasi iliyokuwa hapo kando. Kasha nikavuta kijichupa kilichokuwa hapo juu na kupiga makopo kadhaa ya yaliyokuwemo. Maini ya kaanza kukeketeka na koo kuungua ndanindani. Heri nife niiondokee dunia. Safari yangu ya kuenda jongomeoni ikawa imeanza nilikolala sakafuni.

    Niligutuka usingizini nikihema na kutweta kwa nguvu mno hata nikashindwa kuendelea kulala. Ilikuwa ndoto ya ajabu.



    MWISHO
 
SIKU NAJA DUNIANI











  • SIMULIZI FUPI - SIKU NAJA DUNIANI



    NIKIKUMBUKA NAZIDI KUMPENDA



    Zilikuwa zimepita wiki mbili tangu mwanamke mmoja arudishwe kutoka hospitalini ambako licha ya vipimo na dawa mbalimbali za kunywa,sindano na hata za kuchua hakupata afuheni ya ugonjwa alikuwa nao.Wanawe pamoja na mumewe waliamua kumpeleka katika kitongoji cha KILIMUSI eneo ambalo yeye na mumewe waliamua kupafanya nyumbani kwao licha ya nyumba walizokuwa nazo katika vijiji vingine



    Wakati mwanamke huyo ambaye tabia ya kumwita kila aliyemwona MWANANGU bila ya kujali umri wake ilimfanya hata wajukuu zake na hata wakubwa wenzake kumwita mama akigalagala kwenye godoro kuukuu pale sebuleni, nje yake kulikuwepo na mwanamke mwingine ambaye naye alihangaika juu ya kipande cha mkeka akiota jua la asubuhi.Sauti yake ya upole uliochanganyika na uoga iliuliza swali moja kwa kila aliyemhisi kuwa alitokea pale sebuleni."kaka mama anaendeleaje?"aliuliza yule mwanamke wa pale nje ambaye haikuhitajika elimu ya uuguzi kujua kama alikuwa mjamzito labda kwa sisi wa enzi hizooo ambao bado tunaamini watoto hununuliwa."Hivi hivi tuombe tuu Mungu"Alijibu yule baba akionekana kukata kabisa tamaa. "Mhhh,,"aliguna yule mwanamke akimtazama usoni kaka yake mwingine ambaye alikuwa ametoka tu kufika kumwangalia mama yake lakini hali aliyokutana nayo ndani kama si kujilazimisha kujikaza kiume angeweza kulia kwa sauti. Kiukweli hali ya mgonjwa aliyekuwa akijaribu kupambana na mauti ilimkatisha tamaa kila aliyemwona.Hakuna hata mmoja kati ya wengi waliokuwa pale kuwaza kitu kimoja tuu MSIBA wa mama ,mama ambaye watoto wake wengi na wajukuu walikuwa wakimkimbiamara tu muda wa kusali rozali ukifika kutokana na tabia yake ya kumlaazimishakuu walikuwa wakimkimbiamara tu muda wa kusali rozali ukifika kutokana na tabia yake ya kumlazimisha kila aliyekuwa jirani yake kujumuika naye kusali.Sala ndicho kitu alichokipenda huenda kupita vitu vingine japo uvivu na utoto wa wanae ndivyo vilivyowafanya wamkimbie na kumwona kama msumbufu. ''Jamani mama ameongea! Anamwita dada Kalista"ilikuwa ni sauti ambayo kwa kila aliyeisikia hakuhitaji utambulisho wa mhusika wake,Mtoto wa mwisho wa yule mama ambaye wakati wote alikuwa pembeni ya mama yake akimtaka apone huku kilio chake kikiwafanya wengi waliomwona akihangaika kumlazimisha mama yake aongee washindwe kuvumilia na waishie kutoka nje huku macho yao yakishindwa kuficha kilichokuwa moyoni mwao.



    "Wanini na we Thelesia, dada yako si anaumwa halafu unampigia kelele?"Aliongea Lusida mtoto wa kwanza wa yule mama ambaye alisutwa na sauti ya mama yake ikimwita Kalista na kuwafanya wote walioisikia wakimbilie pale sebuleni wakimwangalia yule mama ambaye yeyote ambaye angefika muda ule asingeamini kama mgonjwa yule ndiye aluyesikia habari zake kuwa alisubiri tu Israel mtoa roho ampitie. "Si nimemwita kalista nyie mnafuata nini?"aliongea yule mama akimalizis na kicheko na kumfanya mumewe awaamuru wengine kutoka kwa ishara. "Na wewe mbona unaelekeza tuu wenzako?, basi we mume wangu ubaki" sauti yenye tumaini ilisikika kutoka kinywani mwa yule mama na kuwafanya wengine kucheka huku wakitoka pale nje. "Niambie na mimi nitoke pengine mna siri zenu"aliongea mumewe skitishia kutoka lakini aliishia mlangoni ambapo alifunga mlango na kuketi kwenye kigoda kilichokuwa pembeni. "Sawa mwanangu haa mume wangu"yule mama aliongea na kuziba mdomo kwa kiganja chake na kuwafanya waliokuwepo kucheka. "Sawa mama nimekuelewa"alijibu yule baba na kupafanya pahala pale palipokuwa na huzuni muda mchache uliopita pawe pa furaha. "Enhee mwezi wa ngapi mama?"aliuliza akimgeukia Kalista ambaye mwonekano wake ulionesha wazi alikuwa akiumia.



    "Wa mwisho''alijibu kwa unyonge akikaa vyema. "Huyo sasa ni wa kiume na utampa ng'ombe wangu mmoja, najua huamini hadi umuone maana nasikia mumeo amechachamaa anataka vidume kwani kama mahari za wale wawili zinatosha"baada kuongea maneno yale alianza kubadika na kupoteza nguvu zake alizokuwa nazo muda mchache uliopita. "Mwanangu usiogope mtu akaribiaye kufa hupona kuaga, naona malaika wale wanakuja ,zingatia sal sa, ,sala mwanao wa kiume"Aliongea na kutulia kimya wakati huo Kalista naye alikuwa akilalamika maumivu makali hadi walipimtoa pale sebuleni kwa kumbeba na kumuingiza kwenye chumba kilichokuwa karibu. Wakati mauti yakimshinda yule mama pale sebuleni mkunga wa jadi ambaye naye alikuwa mfiwa alikuwa akisaidia kuokoa maisha ya kiumbe ambacho leo hii kinatimiza miaka ishirini na mbili.******★****** MWISHO**--
 
MWANZO MWEMA SIO MWISHO MWEMA







  • MWANZO MWEMA SIO MWISHO MWEMA



    Magoma bi bi bi! ndiyo yalinigutusha kutoka usingizini. Mara nilisikia ile sauti nyororo kama kinanda ya ngoi ikiongoza wimbo, ambao kwa kawaida uliimbwa katika sherehe za arusi. Niligutuka kwa haraka, kuitupilia blanketi yangu mbali na kujisongeza dirishani na kupenyeza pazia. Kumbe kulikuwa kumekucha kwa kiasi hicho!

    Shamshi lenye uhai lilikuwa lishachomoza, ishara kuwa ilikuwa mwanzo wa siku njema kwani siku njema huonekana asubuhi. Ingekuwa siku ya kukata na shoka kwani sahibu wangu Yohana angeuasi ukapera kwa kufunga akidi za maisha na kidosho Rebeka, waliyekutana na kupendana tangu tulipokuwa chuoni. Niliharakisha kujitayarisha ili nielekee kule kwani chelewachelewa utamkuta mwana si wako.

    Takribani mwendo wa saa nne na nusu, mambo yalikuwa yametengenea. Kanisa lilikuwa limepambwa likapambika. Maputo ya kila aina na kila rangi yaliangikwa na kutundishwa ukutani. Tungu za mle kanisani zilimwayamwaya mwangaza na kufanya mle ndani kuwa mchana zaidi.Pengine kanisa lingekuwa likipambwa vile kila Jumapili, lingewavutia na kuwanata waumini chungu nzima. Mimbarini, mandishi makubwa ya rangi tofauti yalionekana na kusomeka eti: ‘REBEKA AOLEWA NA JOHANA ’





    Mara ghafla Yohana na kundi lake liliwasili. Waume na vijana waliovalia nadhifu walimfuata unyounyo. Yohana alionekana mtanashati ajabu. Nilimhusudu. Ungelimwona msomaji wangu siku hiyo, usingelijua kuwa ndiye kijana aliyekuwa akipata adhabu siku zote shuleni kwa kuvalia sare zilizochakaa na kujaa makunyanzi kana kwamba zimetafunwa na ng’ombe na kisha kutemwa. Nywele zake daima zilisokotana kama vidude vya vinyesi vya mbuzi. Lakini kumbe maisha humbadili mtu. Pengine ni mapenzi ndiyo humafanya mja kubadilika.

    Sasa Yohana alivalia suti nyeusi ti! na tai ndefu juu ya shati lake jeupe. Ndevu zake alizoziacha zilimwongezea haiba iliyofanya wengi kumtamani. Akapokelewa kwa shangwe kuu na kuingizwa kanisani.

    Muda mfupi baadaye liliwasili kundi la bi arusi, Rebeka Mapesa na wafuasi wake.

    Waliwashangaza mno waumini kwa namna walivyong’aa. Rebeka mwenyewe alivalia nguo ndefu iliyomfunika hadi miguuni na kumpwayapwaya. Uso wake usingeuona kwani alikuwa kafunikwa kotekote. Sijui alionaje alikokuwa akikanyaga kwa kuwa mwendo wake ulikuwa wa mzofafa tena wa polepole kama kobe. Alikaribishwa na nyimbo za kuongoaongoa na kufuatilia zulia nyekundu waliyotandikiwa kuingia kanisani.

    Kanisa lilijaa watu kutoka tabaka mbalimbali. Si wageni walioalikwa, si wazazi na watu wa jamii zote mbili na pia baadhi ya tuliosoma nao. Nyimbo ziliimbwa na masomo kutoka katika kitabu takatifu yakasomwa. Ikafika kilele. Wakati wa kuwaunganisha wawili hao. Kasisi aliyevalia mavazi meupe pe na nadhifu kana kwamba kukubaliana na ndoa yao alisonga mbele tayari kutenda kazi yake muhimu ya siku. Wawili wale wakawa wamesimama mbele yake. Kutoka nilikoketi, Rebeka alionekana malaika wa Mungu.

    Wengi tulimmezea mate ndanindani lakini macho yake Yohana yalionekana kutuonya kuwa bahati ya mwenzio usiulalie mlango wazi. Aidha, nilikumbuka amri ya Mungu iliyoonya dhidi ya kutamani mali ya mtu mwingine.





    “Kabla ya wawili hawa kuunganishwa na kufanywa kuwa kimoja, kuna yeyote aliye na pingamizi?” kimya kikuu kikaibia. Hakuna aliyejitokeza na swali likarudiwa mara mbili na kasisi. Kisha mwanaume mmoja aliyevalia nadhifu akanyanyuka kutoka kule alikoketi! Waumini nyoyo ziliwabapabapa na kuwaenda benibeni. Kila aliyeketi akawa ameachama, mdomo wazi kama pango la nyoka na kumtupia tazamo refu kama la mjusi. Mimi nilimjua kama Bohaz, kakake Yohana aliyesomea Ujerumani, akaishi na kufanya kazi huko. Alitaka tu kuhahikisha kuwa hakuna yeyote aliyepinga arusi ya nduguye. Ndio maana Yohana na mchumba wake hawakustushwa kamwe aliposimama. Lakini waumini hawakumjua ndio maana walishakata kauli mapema. Kumbe usilolijua ni kama usiku wa giza.

    Ni wakati huo ndipo ilimjia msimamizi akilini kuwa pete zao zilisahaulika kule walikokuwa wakivalia na kufanyia mapambo ya Bi. Arusi. Alimnong’onezea kasisi mawili matatu na kuondoka kasi kama umeme. Kwa umbali kidogo, Yohana alionekana kukereketwa na kusinywa naye. Akatamani kumparamia na kumzabazaba makofi. Lakini alisimama patakatifu. Tena hakutaka kuonyesha hasira zake kwa umati. Pengine alikumbuka kuwa hasira hasara.

    Wanakwaya wakaendelea kuwatumbuiza waumini na nyimbo za kikristo kwa furaha hata wakasahau kilichotokea. Wakadhihirisha bayana kuwa kuvunjika kwa mwiko sio mwisho wa mapishi. Waliendeleza nyimbo hadi msimamizi aliporejea muda si mrefu. Shughuli za awali zikaendelezwa. Maarusi wakakiri maneno baada ya kasisi na wakaanza kuvishana pete, huku kanisa zima limeja shangwe, vigelegele, hoihoi na nderemo pamoja na makofi ya furaha.







    Kelele na furaha zilikatizwa ghafla na unyende kutoka nje. Mwanamke aliyeonekana chakaramu alikuwa akitimua mbio akielekea mimbarini. Alivaa nguo zilizoraruka na isitoshe alikuwa miguu mitupu.Maneno yalimtoka kwa sauti na haraka yasisikike vizuri. Vijitoto viwili vichafu vilimfuata pia mbiombio. Vilikuwa uchi na vilivyoparara ajabu! Mama yao alitamka kwa sauti kuwa Yohana alikuwa mumewe, baba ya vile vijototo. Eti walipendana na kuzaa vitoto hivyo kitambo kidogo Yohana alipokuwa angali chuoni! Kumbe ukistaajabu ya musa utayaona ya firauni.

    Umati wa waumini uliduwaa na kuzuzuwaa. Kasisi bibilia ilimtoka mkononi na tang! Kuanguka sakafuni. Tayari vitoto vilianza kumpandiapandia Yohana na kumwitaita ‘baba.’ Yohana mwenyewe alipigwa na butwaa na akawa na mshtuko mkubwa. Parafujo za mwili wake ziliregea regerege na kukataa kumsimamisha imara. Rebeka alikuwa akifunzwa adabu na yule mwanamke chakaramu kwa kumwibia mume. Waumini wakajazana jukwani angalau kumwokoa. Nguo zake zilizokuwa nyeupe zilipata rangi mpya ya uwekundu. Mambo yalimwendea segemnenge na mvange, maji yakazidi unga na akazimia jukwani. Akawa amelala asijijue asijitambue. Jukwaa takatifu la Mungu likabadilishwa kuwa jukwaa la miereka na ndondi ya watu kupimana nguvu..



    Naam, kilichoanza kwa mbwembwe na hanjam, sasa kilikuwa kikimalizika kwa fujo, rabsha, ghasia na vurumahi. Muumini mmoja alinivuta mabegani kwa nguvu akitaka kupita kuenda mbele kujionea sinema ya bure pia. Nikahisi uchungu wa ajabu na hapo ndipo niligituka na kupata kuwa misa ilikuwa imekwisha. Wanakwaya walikuwa wakiimba nyimbo za mwisho huku waumini wakiondoka na hapo ndipo mmoja alinigusa mbegani kuniamsha! Nilijinyanyua halahala kwa aibu hata sikutaka kuwatazama waumini walioonekana kunicheka. Kumbe nilikuwa nimelala muda huo wote kanisani mahubiri yalipokuwa yakiendelea na kupotelea katika ndoto hiyo! Niliapa kutoketi nyuma tena kila niingiapo kanisani kwa kuhofia kulala tena nyumbani mwa Bwana
 
MAMA AMKA UIPOKEE ZAWADI YAKO







  • SIMULIZI FUPI : MAMA AMKA UIPOKEE ZAWADI YAKO



    Kulikuwapo na mama ambaye alikuwa na kijana mmojatu, kijana ambaye mama alitokea kumpenda sana harikadharika kijana naye kumpenda mama.



    Lakini kutokana na mihangaiko ya maisha iliwapelekea wawili hawa mtu na mamaye kuishi mbalimbali. Kwakuwa mama alijitahidi sana kumsomesha kijana kwa bahati nzuri kijana alipata kazi na kwenda kuishi mjini huku mama akiwa kijijini. Hata hivyo umbali wao wala haukuwafanya wajisikie wapweke sana kwakuwa kijana alijitahidi sana kuwasiliana naye . Faraja ya mama ilimtengenezea maisha yenye furafa kijana wake kwa kiasi kikubwa akiwa mjini.



    Baada ya muda Fulani kupita mama alianza kutengeneza dukuduku moyoni kwakuwa kila anapohitaji pesa za matumizi kwa mwanaye basi lazima aanze yeye kumueleza mwanaye kuwa anashida ya pesa. Utu uzima ni dawa, mama alikuwa katika misingi hiyo. Kabla ya kumueleza shida zake alikuwa anaanza kutumia utuuzima wake kwa kumuulizia hali ya maisha aliyonayo kijana wake mjini. Kila asikiapo kijana wake akilalamika kuwa mjini maisha ni ya ghari kwakuwa kila kitu kinanunuliwa hadi maji ya kupigia mswaki, mama hakuwa na nyongeza.



    Kitendo kile kilimfanya mama alifute dukuduku lile, huruma ilimjaa juu ya mwanaye alitamani hata baadhi ya nyakati yeye awe anamtumia pesa mwanaye ila tu hakuwa na uwezo huo. Mahitaji ya mama hayakuwa makubwa sana pale nyumbani ila alikuwa anayakosa. Hakuweza kumueleza mwanaye shida zake kutokana na huruma aliyonayo juu ya mwanaye(wakina mama wengi ni wazito sana kueleza shida za pesa kwa wanao tofauti na wakina baba). aliamini wazi ingawa anafanya kazi ila bado anaishi kwa shida kutokana bado anajijenga kimaisha pili maisha ya mjini yanagarama sana. Aliendelea kumuombea mwanaye mafanikio.



    Wakati mama akiwaza hayo juu ya kijanaye, kumbe mambo yalikuwa tofauti kidogo. Siyo kwamba kijana alikuwa hapati pesa kabisa za kumsaidia mama yake, rahashaa, bali pesa alikuwa anazipata ila hazikuwa nyingi kama alivyokuwa akihitaji. Kijana alikuwa mzito sana kumsaidia mama yake siyo kwa nia mbaya bali aliona siyo jambo zuri kumtumia mama pesa kidogo kidogo. mfano akimtumia mama yake Tsh.10,000/= ndani ya siku chache atatakiwa amtumie tena, kwake hakupendezewa na hilo.



    Kijana hakuwa na mawazo mabaya na mamaye,alichokifanya ni kuanza kuwekeza pesa kwa njia mbali mbali mfano kuweka kibubu na kutenga mshahara aliokuwa akiupata, lengo ni kwenda kumuridhisha mamaye kwa mpigo (surprise).



    Maisha yalisonga, kiajana anazidi kujiwekeza huku upande wa pili mama anazidi kuteseka.taarifa ilimfikia kijana kuwa mama yake anaumwa. Aliamua kufunga safari na kwenda kumuona. Ingawa alikuwa anaenda kumjulia khari lakini pia alichukua kiasi chote cha pesa alichojwekeza kwa muda mrefu na kufanya maandalizi ya nguvu kwaajili ya mamaye. Kiasi kingine cha pesa aliendanacho kwa lengo la kwenda kutatua shida ndogo ndogo.



    Alipokwisha kufika matarajio yake yalikuwa tofauti sana. Badala ya kumjulia khari mamaye ambaye alikuwa akiumwa bali alifikia kuuaga mwili wa mamaye . tayari alikuwa ameshaaga Dunia. Ilimuuma sana kijana, alilia kwa uchungu huku akijilaumu kwa mengi juu mamaye ambaye walipendana sana.siyo sili kina alimpenda sana mama yake na alikuwa anatamani sana amfurahishe mama yake, hivyo moja ya njia sahihi ya kumfurahisha mama yake aliona ni ile ya kujiwekeza na kumfanyia Surprise. Kila alipokuwa akilia aliweza kuzungumza maneno machache sana “MAMA AMKA UIPOKEE ZAWADI YAKO”.



    MWISHO.



    ********

    FUNDISHO.

    Vijana wengi wa sasa tunaishi maisha ya namna hiyo, maisha ya kudhani mama/mzazi anahitaji kikubwa ndipo aridhike. Tunaishi kwa mfumo wa mwisho wa mwezi ndipo nimuwezshe mzazi.



    Vijana, sawa maisha ya sasa ni magumu. Lakini ukichunguza kwa kina mama aliyeko kijijini hana mahitaji makubwa kiasi kwamba wewe ukashindwa kuyamudu hadi ukajiwekeza kwa muda mrefu. Usione aibu wala usione kazi kumtumia mama yako ulichonacho. Sikuzote kidogo ukiwanacho, kwa asiye nacho ni kikubwa. Wazazi hasa wa kijini wanajitahidi sana kubana matumizi, Tsh.5000 utakuta anatumia hata wiki mbili. Sasa wewe unataka ujiwekeze hadi ifike laki sita ili atumia miaka?. Wengine utakuta anapesa kidogo ya hakiba, anawaza kumpa mama haimtoshi ila kwenye starehe anaenda kwa pesa ile.



    Mfanye mama yako ni sehemu ya furaha yako,kama huna basi muombe sana Mungu upate, ila kama unacho usiseme hicho ni kidogo mama atakidharau. Mpe ulichonacho kisha jitume na kumuomba sana Mungu ili kesho upate kikubwa zaidi ya hicho na utamfanyia hiyo Surprise unayopanga kumfanyia mama yako.



    Nimemtumia sana mama kwakuwa ndiye mhangaikaji mkubwa ndani ya nyumba. Binafsi nimepitia maisha ya U- bachelor , nakiri kuwa hamna kazi ngumu katika kuhakikisha unakula na kushiba kama kutafuta mboga. Hivyo kidogo unachokiona wewe, mama kwake kitatatua lile tatizo gumu la kupata mboga hakika atakuwa na furaha sana.



    Ninaimani vijana wenye tabia hii ya kuwasahau wazazi wetu na kusubiri tupate pesa nyingi ndipo tuwakumbuke tupo, tukiendelea nayo tabia hii tutakuja kuwakumbuka Maiti. Siyo kwamba hatuwapendi wazazi wetu, tunawapenda sana ila kumfanya mama awe anatabia ya kukuomba kila mara kwako, wala siyo nzuri kwani huyo hajawa ombaomba. Alikusomesha au alikuwezesha sasa unajitambua unatakiwa utambue na wajibu wako kwake.TUBADILIKE



    MWISHO
 
NAKUPENDA MAMA









  • NAKUPENDA MAMA



    Huenda ulikuwa ukifuatwa bombani, kanisani na hata sokoni walikufauata sana kifupi ulikuwa si mpweke karibu kila mahali ulipokuwa.Upweke uliutaka, lakini hukuupata ,japo wengi huepuka upweke lakini kwa upande wako upweke ndicho kitu pekee ndicho ulichoona kuwa na thamani sana maana hukufanikiwa kuupata upweke hata ukiwa usingizini maana ndoto zako nyingi ziliakisi vurugu za wasindikizaji wako.


    Ulipojiona mpweke lakini hukuwa mpweke nalo ulilijua hilo, kwa nini usijue maana kila ulipogeuka ghafla basi haikuwa ajabu kukutana na macho si chininya matatu yakiwa yametumbuliwa kukuelekea.
    Walipokuja kujua ulipokaa basi wauza mboga , nazi samaki na hata walipokuja kuulizia vyumba vya kupanga waliongezeka japokuwa kwa nyumba ilivyokaa hapakuwa na dalili ya kuwa na chumba cha ziada cha kumweka mpangaji hadi pale baba alipoweka tangazo la kusema hapakuwa na chumba cha kupanga.
    Baba alipokupa simu kwa kigezo cha kukurahisishia mawasiliano na mama ulifurahi sana kwa kujina umeingia kwenye dunia ya kisasa na ulikuwa ukipata nafasi ya kuwasiliana na mama na baba huko kijini maana walitamani sana kusikia sauti yako kwani licha ya kuwa kabla ulitumia simu za wenyeji wako kuna muda walikuwa wakiona ukiwasumbua bure.
    Sasa ukawa umejiwekea utaratibu wa kupunguza idadi ya nyanya za kununua sokoni ili upate salio la kuongea na mama nyumbani, NANI KAMA MAMA?.
    Kwa kuwa ulikuwa msichana mwenye akili hakuna aliyegundua kuwa kulikuwa na upungufu wa nyanya kwani siku ukipunguza nyanya utazidisha Mchuzi Mix , siku nyingine huweki kitunguu maji ila nyanya zinakuwa za kuzidi nani atajua wenyewe wakija kula washajishibia mishikaki na supu za huko hotelini wanakoenda? Ukajinafasi kila siku unaongea na mama kupitia kwa simu ya jirani wa mama kule kijijini.
    Siku moja wakati unaongea na mama tena akikusimulia juu ya yule mchumba wako aliyeenda kwao kutaka kukuoa ghafla simu ikaita na kwa hamaki ya kuisaka ndoa na kuwa na nyumba yako ukataka kujua nini kilichofuata kwani ulikuwa umechoka kusindikizwa na wakora wa mjini ulikuwa na kitu ulichotegemea kwa hamaki ukakimbilia ndani na kupapasa jui ya kabati na kuchukua hela uliyoiona asubuhi wakati unadeki na kwenda kuchua vocha duka la jirani ili umuwahi mama si ulijua simu haikuwa yake na mawasiliano ya kijini kwenu uliyajua wanaweza wasipatikane wiki nzima , mtandao wenyewe wa kusimama pale kwenye kibao cha shule au kule kilimani kwenye kanisa la Romani.
    Kufika dukani yule kijana wa dukani alidai hakukuwa na vocha labda akurushie salio umlipe nawe kwa haraka ukamtajia namba na kupokea salio na kuwahi nyumbani maharage uliyoyaacha jikoni yasiungue.
    Kufika nyumbani ulimkuta baba akihangaika kuangalia chini ya makochi, na kabla hujamsalimia akakutupia swali.
    ''Kuna elfu kumi niliiacha hapa mezani umeiona?"
    Na wewe kwa kuwa ulijua ilikuwa chini ya kabati na si mezani ukakataa katakata hadi alipotaka kukukagua ukasema ulikuwa na hela uliyoikuta chini ya kabati ambalo ilipita miezi mitatu bila kunyanyuliwa na siku ile kwa kuwa mama alikuwa amesafiri na alikutaka ufanye usafi wa uhakika.
    Baba alikuja juu na kutaka kukupiga kwa kosa la wizi ukampigia magoti ukimwomba radhi kwa mia tano uliyoitumia na huku ukimpa elfu tisa mia tano zilizobaki lakini hakufanya kitu kingine zaidi ya kupiga simu ile mahali alipopaita polisi na kukufanya umkumbuke mchumba wako , mama yako baba yako na wengine wengi kwa kifupi jela uliiogopa na uliona itakutenganisha na watu uliowapenda.
    Si masikhara ulisikia sauti ya magurudumu ya gari yakilalamika nje ya nyuma yenu ishara ya kuwa yaliamrishwa kuacha kuzunguka kabla ya watu watatu waliovalia sare za polisi wakiingia sebuleni kwenu.
    Kilio kilisikika lakini , hakuna aliyekusikiliza zaidi ya virungu vilivyotua mwilini mwako kwa amri ya baba.
    Kwa mara ya kwanza ulikiona kile chumba kidogo japokuwa ulikaa masaa mawili tuu ulikiogopa kile chumba kwa kadri kilivyokaa kitesaji uchafu wake yalikuwa mateso tosha.
    Baba alikuja kuwaomba askari wakuachie wakati ambao yule muuza duka alikuwa ameshakuja na kukupa mia tano ili umlipe baba lakini askari wawili walikuwa hawabandui macho kwako na hata ulipokuwa ukiondoka na yule baba na kuingia garini kuna aliyekupa kikaratasi bila baba kujua.
    Ulipofika nyumbani ukajaribu kuomba msamaha huku ukimpa baba ile miatano uliyopewa na muuza duka lakini alikataa akikutuhumu kuiiba ile hela na kukutishia tena kukurudisha polisi.
    Ukafyata na kusubiri adhabu maana hukuwa na haki mbele ya baba , kwa kifupi alionesha ukali wake haswa na kila ulipokumbuka kituo cha polisi basi ukajikuta ukipoa tuu.
    Ghafla bila kutegemea ulitazamana na silaha ya moti huku sauti kutoka kwa baba ilikuamrisha kuvua nguo zako kabla ya kuingiliwa kimwili na uliyemwona baba mwema huku akikutishia kukuangamiza endapo ungeleta upinzani wowote na hata alipomaliza haja zake tena sebuleni alikufukuza na kukutishia kukuua endapo ungeropoka popote juu ya alichokufanyia.
    Masikini zawadi uliyomwahidi kumpa mumeo aliichua asiyestahili tena kwa mabavu huku ukifukuzwa.
    Hukuwa na ndugu na kitendo kile uliona aibu haswa ukatoak na kwenda kukaa kweny nyuma ya jirani ambayo haikuwa mbali na pale nyumbani ukisikilizia maumivu makali kwani alikuwa amekuharibu haswaa.
    Ulisikia sauti ya baba akiwasimulia majirani hata yule muuza duka kuwa umemwibia hela na kutoroka lakini pia alikutuhumu kuwa ulikuwa na wanaume na aliwahi kukuonya na baada ya kukufumania zaidi ya mara e kujitokeza ukambishie lakini kila ulipokumbuka ile silaha yake ukaishia kulia, uliwaza ungekuwa na simu basi ungempigia hata mama yako lakini simu nayo alikunyang'anya basi ukawa mtoto wa mtaani.
    Usiku wa manane huku tumbo lako la chakula likilalamika jaa na lile lingine bado likiuma kwa kitendo ulichofanyiwa ulisikia sauti za watu zilizokiwa zikisogelea nyumba uliokuwa umekaa kisha zikaishia jirani kabisa na ulipokaa na kuwasha kile ambacho hata bila kuelezwa ulijua kuwa ni bangi ambayo moshi wake ulikufanya utoe kikohozi ilichopelekea wale watu wamulike tochi pale ulipokaa na walipokuona kama waliambizana walikusogelea kisha kukufanyia kitendo alichokufanyia baba mchana na safari hii walikuingilia hata kinyume, hadi pale ulipopoteza fahamu.
    Ulikujankushtuka ukiwa kweny nyumba pembeni yako akiwa yule askari aliyekupa kikaratasi, na akakueleza kuwa wakiwa kwenye doria walisikia harufu ya bangi na walipotaka kuingia kwenye ile nyumba walikimbia na kukuacha na kama bahati ni yeye pekee ndiye aliyepata wazo la kukagua ile nyumba na alipokuona alikuacha kabla ya kurudi baada ya doria na kuja kukupa hifadhi kwake huku akitumia taaluma yake ya udaktari kukutibu.
    Ulimshukuru sana na kumwombea kwa Mungu abarikiwe na kumtaka akusaidie nauli uende kwenu, kwa upole akakutaka ubakinpale hadi ukapo pona huku ukiendelea kukaa ndani.Kwa unyonge ukakubali kukaa pale huku akitoka usiku kwenda kazini na kurudi asubuhi hadi ulipopona kabisa lakini ulipomwomba uondoke akakupa la moyoni mwake kuwa alikuwa na pendo la dhati kwako na alitaka muende kijijini kwao kisha kwenu mkambukishane na mpate sakramenti ya ndoa.
    Ulitamani kupingana na wazo hilo lakini alitumia zaidi ya wiki tatu akikubembeleza huku wema aliokufanyia ukikufanya utamani kumhurumia lakini mchumba wa kijijini akakufanya usite kukubaliana naye hadi alipoamua kwa kinyongo kulipa fadhila zake kwa kumpa pendo lako na haraka haraka haraka ukapelekea kwao na mlipoamua kwenda kwenu hapo ndipo ulipokelewa kwa dharau na hata ulipomwambia mama yako juu ya madhila uliyopitia alikupa hadithi na wizi huku ukiambiwa kuwa ulikuwa unegeukia ulimwengu wa wanaume na kitendo cha kwenda na huyo mwanaume basi hawakuwa na wakati wa kusikikiza hoja zako zaidi ya kukufukuza kama mbwa huku wakidai ulikuwa umewaaibisha.
    Hukuwa na jinsi zaidi ya kurudi na yule askari wako mjini ambako mliamua kuishi kwa baraka za upande mmoja hadi pale ulipogundua kuwa ulikuwa mjamzito.
    Miezi ikapita hadi ulipojifungua, na hapo ndipo matatizo yalipozidi kwani baada ya kujifungua ukapata ugonjwa wa kutokwa na haja zote bila kujijua hadi mume wako alipokutoroka na kudai kuwa ulijifungua mwezi mmoja kabla ya mwezi aliotarajia kwa mantiki hiyo alidai ulikuwa na ujauzito kabla ya kukutana na wale vijana kwani aliikuta mipira iliyotumika eneo la tukio na kwa maana hiyo mimba ilikuwa ya baba mwenye nyumba kama utani ulijikut ukifukuzwa kweny nyumba ile siku mbili baada ya kugundua kuwa alikuwa amehama kituo cha kazi na hata ulipojaribu kumpigia simu ilipokelewa na mwanamke ambaye alitishia kukuua kwa kumnyang'anya mume wake kisa hakuwa na uwezo wa kupata mtoto.
    Hapo ndipo ulipogundua ulitambulishwa wazazi feki na usiku mwingi alidai alikiwa kazini kumbe alikuwa kwa mkewe.
    Hukuwa na namna zaidi ya kurudi kijijini ambako ulifukuzwa na wazazi wako hadi ulipoamua kwenda kuishi kwa bibi yako amabye naye alitengwa na wazazi wako kwa madai ya uchawi.
    Nasikitika kusoma barua ya historia yako leo hii nipo darasa la tano, baada ya kuikuta kwenye mabegi ya bibi yako wakati nahangaika kumtafutia dawa ya kifua kwani anaumwa sana na hapa ameniekeza kuwa fistula ilikuua mama yangu.
    POLE SANA MAMA YANGU NAKUPENDA NA NITAKUPENDA DAIMA BIBI YAKO NAYE AMEKUFA LEO HII NASHINDWA NITAENDA WAPI UPENDO WENU MKUBWA SANA.
    Mwisho.
 
FURAHA YA FACEBOOK







  • SIMULIZI FUPI : FURAHA YA FACEBOOK





    Pembeni yangu alikuwepo mpambe wangu wa siku zote Fakih Juma au Kakyfee kama ambavyo alijiita suti yake iliyokuwa imeendana na umbo lake dogo ilimfanya awe kama muigzaji mahiri kutoka Nollywood Nigeria huku pembeni ya malikia wangu Farha au Happy kama ambavo nilipenda kumuita, Farha alikuwepo shoga yake aliyeitwa Sherry gauni lake refu lililoachia mgongo wazi lilikuwa limemfanya awe kama mrembo wa Tanzania aliyepata umaarufu kupitia tasnia ya maigizo Elizabeth Michael ama LULU, kifua chake kilichohifadhi hazina ya chuchu ndogo ndio kilimn’garisha zaidi.





    Sitaki kuzungumzia kuhusu mimi na Farha lakini jinsi tulivyokuwa tunavutia waulize walohudhuria sherehe hiyo sitaki kujisifia baada ya sherehe fupi iliyofanywa na ndugu yake Farha ikiwa ni kupiga picha ya pamoja ya familia na kuvikana pete katika ukumbi wa Novelty Cinema ya Wete - Pemba . “Mh! kaka utafaidi leo!” Fakih alinin’gata sikio nikamjibu kwa tabasamu hafifu lililounga mkono hoja yake.

    “Anakwambia nini huyo Fakih nyie wambea kweli” Farha alinambia huku ameangalia mbele ili asijulikane kama ananiambia kitu, sauti yake ilikuwa laini sana. MC au mkuu aliyekuwa akiongoza shughuli ile alikuwa akiitwa Massoud Ali wengi walimwita Masu kama ambavyo amezoeleka kwa jina hilo naye alikua tayari ameusoma mchezo

    “Naona bi harusi anamwambia mista wake jamani dear saa ngapi tunacheza mziki nina hamu ya kukuonyesha umahiri wangu” ukumbi wote ukaripuka kwa vicheko, hata Farha alicheka nikauona mwanya wake.





    “Mama yangu hivi ndo Farha wa fesibuku huyu mh!” nilishtuka sana maana huyu binti uhusiano ulianzia katika mtandao lakini leo alikuwa amependeza sana nilitamani nimrukie mdomoni lakini umati ulinipa uoga pia maadili ya nchi yetu na kisiwa bado hayakuwa yakiruhusu.

    Wakati wa kucheza mziki sikutaka mtu amguse japo nilikuwa nimechoka lakini sikupumzika, vazi refu alilovaa halikufanikiwa kuficha hipsi na umbile lake la nyuma dah? jamani kuna watu wameumbwa ndo nilijisemea huku nikinesa naye taratibu midundo ya Celline Dion na zile za wasanii wanaoima nyimbo za rhythm & blues au R&B ukumbi ulichangamka sana . Leo mimi Hamad nimeoa mh! siamini lakini asingekuwa amenibania mchezo ndoa angeisikilizia redioni huko au kwenye maigzo mambo ya kuoa mapema haya sio ishu kabisa!!! Nilijilaumu kwa uamuzi wa kuoa lakini sikuwa na namna yoyote ile Farha hakuwa tayari kwa penzi iwapo sijamuita mke.





    “Fakih kawaambie hao ma MC tunataka kwenda kulala tumechoka” nilimwagiza Fakih ambaye naye fasta akaenda kupeleka ujumbe, lengo langu hata yeye alilijua vizuri tu.

    Kale kamchezoooo!!! Ambao wapemba husema kuingia ndani

    Majira ya saa tatu na dakika takriban arubaini hivi usiku gari ilisimama mbele ya hoteli kubwa ya kisasa “Pemba Clove Inn”, tulisindikizwa hadi kwenye chumba chetu kilichoandaliwa mahususi kwa ajili yetu kwa siku tatu mfululizo, fungate la kizushi. Dada yake na Farha nilimwona kama mzinguaji alivyoanza tena kupiga stori na Farha, hakika alikuwa anazingua maana wamekaa wote miaka kibao leo hii ndio anajidai anajua kuhamasisha. Dah! Fakih kama ninja vile akautegua mtego akamtoa huyo dada, nikampa ishara ya dole gumba yaani MIA.





    “Tukaoge mpenzi” sauti tamu ya Farha ikapenya masikioni mwangu. Sikujibu kitu haraka haraka nikamwondoa lile gauni, taiti yake mh! kilichofuata bikini weweeee! juu kafungashia cheni mbili zenye rangi ya dhahabu kama bikini yake jamani huu uchokozi hivi waliompamba walijuaje napenda bikini na cheni za kiunoni, he!!! wazo la kuoga likapotea nilipoona “tatoo” kwenye chuchu zake kama zile za akina Irene Pancras Uwoya ama Oprah kama ambavyo wengi walikua wakimuita pindi waangaliapo filamu zake anazocheza. Mh! kwani mie khanithi? hapana mie nimekamilika kabisa, kama vile ugomvi nikambeba (Usiniulize nguvu nilitoa wapi na kiafya changu hichi mgogoro cha kukopa au cha vidonge mkononi mana pumu ilikua hainiachi) nikamrushia kitandani duh! akatua kwa tumbo sehemu za nyuma zikawa zinaangaliana na macho yangu wewe ile mitikisiko niliyoiona haisimuliki sijui alifanya maksudi yule?? nikaona “tatoo” nyingine juu ya makalio yake imeunda alama “H” sikuwa na muda wa kujiuliza alimaanisha HAPPY au HAMAD . Mgongo wake ulikuwa laini sana hata kabla ya kuugusa huku cheni zake za dhahabu zikikizunguka kiuno chake laini. Mahamu yakanizidi nikashindwa kujizuia, Nikafumba macho nikamshukuru aliyeuanzisha mtandao wa kijamii wa facebook kwa kuniunganisha na binti huyu, sasa nilikuwa naenda kufaidi. Kwa hapo nilimpa pole maana yeye ametupatia mambo matamu kama haya halafu kwenye kufaidi hatumkaribishi, nilijichekea kimoyo moyo.



    Nikajongea kitandani mikono yangu ikawahi kumwingilia Farha kiunoni na yeye akafanya hivyo, kisha ndimi zetu zikakutana mh!! Mtoto ana midomo laini yule, nikamwachia mdomo wake nikaangukia kifuani nikazibugia chuchu zake, wacha mtoto aanze kulia nikasema ewalaaa!! Hapa hapa ndo udhaifu wake ulipo, ghafla akanigeuzia kibao na yeye akaniweka chini makucha yake yakaanza kunifinya nikahisi napigwa shoti, ulimi wake ulizagaa mara huku mara kule nikajikaza nisipige kelele mtoto wa kiume lakini hali ikawa ngumu nikaanza kuhema juu juu kama ambavyo inanijia ile pumu yangu ya kawaida , Farha akiwa hana chochote zaidi ya cheni kiunoni alitambaa hadi chini akawa ameniacha hoi kitandani akatulia katika vigae au taizi kama mtu anayetaka kukata roho kisha akajiweka chali na kujitanua.mmnhhh Bila shaka alikuwa ananiita sasa , nikasjisemea kimoyo moyo!!! Na mimi kwa hofu ya kumaliza hamu zangu hewani nikatii amri ile!!





    Kama vile narukia dimbwi la maji kwa ajili ya kuogelea nikaruka juu juu kwenda pale alipokuwa Farha!!

    “Puuuuu” kikasikika kishindo nikaanza kuhisi maumivu, Hamad mimi nimeanguka kutoka kitandani kwangu tena kwa aibu dogo anasoma hapo mezani kanishuhudia mtu mzima “NILIKUWA NAOTA” ayaaaaa!! Huku chini palikuwa wima kabisa maana sina utaratibu wa kulala na nguo usiku. Dogo akawa amenikazia macho nikajidai simuoni nikarejea kitandani nikamlaani Farha na hiyo ndoto niliyoiota.

    Nikachukua kisimu changu Nikaingia fesibuku nakuta status ya Farha “Never had a dream come true” nikaona haya nikamchukia aliyeanzisha facebook, nikahisi kama alikuwa amejua kilichonitokea nika log out uupesi ndo sasa hivi naingia tena!!!

    “””NDOTO NYENGINE BALAA!!!!””””
 
MAMA YANGU ANAKULA NYAMA ZA WATU







  • SIMULIZI FUPI : MAMA YANGU ANAKULA NYAMA ZA WATU



    Kutoka katika kijiji kimoja kijulikanacho kwajinala mangara kilichopo moshi. Kulikuwapo nakijama mmoja aliyejulikana kwajinala Nasibu Ally. Aliishi kijijini hapo nawazazi wake wawili Mzee Ally Mtakuja na B.fatma Songambele. Ilikuwa ni familia yenye uwezo kiasi kijijini pale, kwanili walikuwa na mifugo yakutosha na mashashamba kazaa.

    Baada yamiaka kusogea.kijana Nasibu alibahatika kuowa akiwa na miaka 25, yeye namkewe Madsam waliishi pale nyumbani kwa wazaziwake. Ingawaje Nasibu alikuwa peke katika familia yao ilayeye aliba hatika kupata watoto watatu. Nao ni Juma mtoto wakwanza akifuatiwa na Asha pamoja na Amina.

    Sikumoja kijana Nasibu alipokuwa shambani, aliletewa taarifa zakushtua, yakwamba mwanaye Amina yupohoi amelazwa katika hospitali ya wilanya, hiyo anahitajika haraka iwezekanavyo. Nasibu kwaharaka akatupa jembe chini nakurukia baiskeli yake nakuelekea hospitalini.

    Kufika hospitalini akamkuta mkewe Madisam pembeni yakitanda. "eenhee kulikoni" kwahali ya jazba aliuliza Nasibu. "hatakuliza hali yamgonjwa mumewangu" Madsam alijibu huku akisimama. Kisha akamwambia anadaikichwa kinamuuma ikiambatana nahomakali mumewangu, ilaanaendelea vizuri sasa. "Kilimuanza muda gani?" Nasibu aliuliza huku akimsogelea nakumgusa wanaye. Kwasautiya upole na unyenyekevu Madsam alisema "nighaflatu mumewangu, arudikutoka kwenye michezo nawenzake nakunyambia mama kichwa kinauma, ilahali ilizidikubadilika kilamuda. Ndipo nikaomba majirani wanisaidie kumleta hospitali." Nasibu alimgeukia nakumuuliza "mama yukowapi?" hakuwepo kwamudaule alitoka ilahakuniaga Madsam alimjibu.Maradokta akaingia nakumkuta mgonjwa ananafu. Hivyo akawaruhusu kurudi nyumbani nakuwapa dawa zakutuliza maumivu maana mngonjwa hakuonekana naugonjwa wowote.

    Baadayakurudi nyumbani. Ulupoingia usiku, ndani yausingizi mzito Amina akiwa ndotoni mara alimuona bibi yake B.fatma akiwa ndaniya shuka jekundu na wanawake wengine wawili nyuma yake....





    Amina baadaya kuona bibi yake nawale wanawake wengine wana msogelea nakumzonga mithiliya yakutaka kumkamata, alishtuka toka usingizini nakupiga yowe kali"mamaaa..." ingawaje hakuna aliyemsikia kwakua nguvu za giza zilitanda eneo lanyumba yao, hivyo haikuwa rahisi kwawatu wengine kujua kinacho endelea pale, nahatayeye hakuona uwepo wamtu yeyote pale chumbani. Pundesipunde kulipiga mwanga mkali mithili yaradi, uliotokea upande wa dirishani mwachumba cha Amina, ambapo ulimpiga usoni nakupelekea kupoteza fahamu. Ndipo bibi yake na wenzake wakajitokeza kimazingara. Wakiwa hawana hofu yeyote wanawake wale walitwaa kivuli cha Amina nakuondoka nacho katika makutano yao yaliyopo chini ya mbuyu mkumbwa uliopo karibu nakisima chamaji chapale kijijini mangara. Kulikua nakundi kubwakiasi lawatu naviumbe wengine waajabu wenye kuwaka mtoo machoni mwaoo. Kiongozi wakundi hilola mashetani alimuamuru B.fatma kuchukua kivuli chamjukuu wake akisaidiana na wenzake wakitundike kwenye kamba zilizo shikizwa kenye mbuyu ule. Baada yakufanya hivyo walivyo agizwa, kiongoziwao alichukua kibuyu kilicho jaa damu nakukipakaza kivuli kile mwilili mzima, kisha akawageukia wenzake nakuwambia hii ni kinga tosha niliyo mpaka hakuna binadamu atakaye weza kumuona hapa, nengepende muwahikwenda mjumbani kwenu kwani karibuni kutakucha, ilatutakutana siku ya tatu(3) baada yamazishi ya huyu mtoo mnalitambua hilo". Wote kwapamoja walitikisa vichwa kuashiria kukubadili..., baada yahapoo waliuzunguka mbuyu huku wakiwa wameshikana mikono. kufumba na kufumbua wote walitoweka eneolile. Kilichobakia kilikua kivuli chake Amina kiki chirizika damu nzito hukukiki tetema.

    Asubuhi namapema mama Amina(Madsam) aliamka nakuelekea chumba chawanawe Asha na Amina, baada ya kugonga hodi maratatu, Asha aliamka akiwa na hali yauchovu, kisha akafungua mlango nakumkuta mama yao kasimama pepembeni yamlango namwenye shahuku yajambo fulani. Ingawaje Asha hana hili wala lile..





    Baada ya Asha kufungua mlango, alimkuta mama yao akiwa amesimama pembezoni mwamlango. Asha akiwahana hili wala lile kuhusu mambo yaliyotokea jana usiku, alimsalimu mama yake kisha kuelekea nje. Mama naye aliingia chumbani na kukaa kando ya kitanda cha Amina, ndipo akauliza kwasauti ya upole huku akitelezesha mkono wake katika kichwa cha Amina "unaendeleaje kiziwanda wangu". Kwasautikavu kama mtu aliye pingwa roba Amina alijibu "sijisiki vizuri mama, nahisi baridikali naomba uniongeze shuka nijifunike". Usijali mwanangu mama alimjibu "ngoja nikakuchemshie uji, ukinywa utakupatia nguvu na joto sawa...?" Amina alitikisa kichwa kuashiria kuelewa. Ndipo mama yake akachukua shuka nakumfunika huku akimfariji "utapona mwanangu, Mungu atakusaidia" Mama Amina alitoka nakuelekea jikoni. Kwawakati huo B.fatma alikuwa chumbani kwake ameketi kitako juu yakitanda. Akiwa katika wimbi la mawazo kutokana na shinikizo layeye kumtoa mjukuwake(Amina) kafara. Maana anajua vyovyote iwavyo lazima Amina apoteze maisha siku ya leo kwakuwa sehemu ya roho yake ipokatika mikono ya mashetani.

    Muda ulipo sogea, majira ya saa 4 asubuhi, Nasibu alimwambia mkewe amuandae mtoto waende hosipitali kwani haliyake haikuwa mzuri. Mama Amina akiwa chumbani kumuanda mwanae kwa kuelekea hospital, Amina alianza kulalama kwasauti ya unyonge "bibi... bibi... bibiii...!" usinipeleke huko mama. Mama yake hakutilia manani malalamiko yake chazaidi alimtia moyotu " utapona mwanangu usijali tunaenda hospitali..." wakiwa wanaelekea hospitali, Nasibu, mkewe na mtoto wao Amina. B.fatma akiwa na Juma na Asha waliwasindikiza kwa macho. Asha akiwani mwenye unyonge alijisogeza mbavuni mwabibi yake kwa ishara yakuhitaji faraja. Ilikuwa nitofauti kwajuma yeye alionekana nimwenye kushangaa jambo lililokosa ufumbuzi ndaniyake. Nibaada ya kuona upungufu wa kivuli kimoja katiya vivuli vita3. Yaani cha baba yake mama na Amina. Kwani alikiona kivuli cha baba na mama tu.







    Baada ya Juma kuduwaa kwamuda kwakile alichokiona. Hakutaka kuliweka bayana jambo lile. Akawa nimtu mwenye wasiwasi kama aliyeibakitu. Bibi yake akimuuliza "vipi juma unanini?". Juma alikata huku akitikisa kichwa mmmmhm..! hakuna kitu bibi. Nakisha akaele chumbanikwake. Ingawaje bibi hakutaka kumdadisi sana ilaisha gundua kuwa aliona mapungufu aliyo nayo Amina. Juma akiwa pekee chumbani alitafakari "inaweze kana vipi mtu kukosa kivuli?" kabla hajapata ufumbuzi wowote alisikia sauti ya bibi yake ikimuita. "jumaa... njo upeleke mbuzi machungani...". Nasibu na mkewe pamoja na Amina wakiwa wemesha ingia eneo la hospitali walipokelewa kwa ukarimu na wauguzi wa hospitali ile. Baada ya Amina kupata huduma ya kwanza, Daktari akawauliza mbona mume mchelewesha mgonjwa kiasi hicho. Mama alimjibu "nighaflatu hali ilikuwa mbaya baada yakudai anajisikia baridi, ndipo tulipoamua tumuwahishe hospitali". "Vizur" dactari aliwambia, ila kulingana navipimo inaonyesha mwanenu anaupungufu wa damu na maji. Akiwa anaendelea kufunua makaratasi yaliyo pale mezani dactari alisema "Mbwana Nasibu mgojwa anahitajika kutundikiwa drip za maji nadamu, hiyo munahitajika kuchangia damukiasi kwakuwa hatuna damu hapa hospitalini kwetu. Nasibu bila kutafakari alisema "doctar nipotayari kutoa damu kiasi chochote kitakacho hitajika". Hivya basi daktari alimtaka Nasibu aende mahabara kwaajili ya vipimo vya damu, wakati mkewe akielekeo whodi za wagonjwa. Akiwa katika whodi mama Amina, alikaa kitandani nakukiegemeza kichwa cha mwanae mapajani mwake. Kisha kumbembeleza mwanae. Ndipo Amina alifumbua macho na kutamka kwa sauti hafifu "bibi.." Kisha akamwangalia mama yake kwahuzuni mkubwa huku machozi yaki mtiririka, kisha akasema "mama nakupenda sana, nasikitika kuto kukuona tena, ningependa uwasali kaka na dada kwani sitoonana naotena. Mwambie baba asiangaike kwani misiwakupona tena." Mama yake aliihisi hali hii, hivyo alishinda kujizuia machozi yahuruma yali







    Baada ya Amina kufariki pale hospitali. Maiti ilichukuliwa na kurejeshwa nyumbani, ndani ya muda mfupi vilio vilitanda eneo lile lanyumbani kwakina Amina. Haikuchukua muda shughuli za mazishi zilianza, majira ya sasa kumi jioni marehemu Amina alikuwa teyari keshawekwa kwenye makazi yake ya milele. Ilikuwa gumzo kwa wengi wao maana kilikuwa kifo cha ghafla, hawakuhitaji kudadisi zaidi waliliacha swala hilo kama lilivyo kwakuamini nimipango ya Mungu. Baada ya mazishi watu wote walisambaratika nakuendelea na shughuli zao.

    Siku ya 3 baada ya mazishi, Ulipo ingiausiku mnene jiji lilikua limepoa kwapirika za watu. Ndipo B.fatma(mama yake Nasibu) alikurupuka toka usingizini kisha akaelekea kwenye pembe ya chumba, nibaada ya kuvuu nguo zote nakubakia mtupu kama alivyo zaliwa. Kisha kutoweka kimazingara nakutokea mbuyuni, ambapo aliwakuta wenzake wakiwa wana msubiri yeyetu. Bilakupoteza muda, wote walikusanyana nakuelekea makaburini. Walipo wasili maeneo yale ya makaburini, walili zunguka kaburi la Amina huku wanaimba nyimbo zao za kichawi, wakatihuo kiongozi wao akiendelea kuufufua mwili wa Amina. Haikuwa kazi rahisi japokua muda mfupi walifanikiwa kuutoa mwiliule wa marehemu Amina.

    Walirudi namwiliule hadi mbuyuni, kisha kuulaza chali juu ya ardhi baada ya kuufungua sanda yake.

    Kiongozi mkuu, alisimama kisha kuitanga ziahadhira yake."hii ni kafara ya b.fatma kwa mizimu. kulinganana ahadi aliyoiweka miaka 20 iliyopita baada ya kushindwa kumtota kafara mwanaye Nasibu nahivyo analazimika kutoa wajukuu zake wawili tukianza nahuyu." baada ya hapo alianza kuucharanga charanga mwiliule bilahuruma, kisha kugawana mapande ya nyama ambayo hanyakuwa na damu kutokana ilisha nyonywa na mizimu. Baada yakula yamazile mbichi B.fatma yeye alikabidhiwa kichwa akakifukie nyuma ya nyumba yake, akiwa nimwenye kutetemeka alikipokea kichwakile. Nandipo wote walisambaratika kuelekea makwao. Muda ulikuwa umeenda sana ndipo b.fatma aliamua





    Kulingana na muda ulikuwa umeenda sana B.fatma aliamua kukiweka kichwa kile chini ya uvungu wa kitanda chake.

    Asubuhi kumepambazuka, watu walielekea kwenye shughuli zao za kilasiku. Mkewe Nasibu(Madsam) alikuwa kitandani akiwaza hili na lile mara ikamjia taswira ya marehemu mwanaye Amina, ambapo aliyakumbuka maneno aliyosema mwanae enzi za uhaiwake hukuakinung'unika "bibi...bibi...bibi..ananimaliza" Madsam alishituka kamamtu aliye kurupushwa toka usingizini, mapigo ya moyo yalimuendambiyo akanzakuwa na wasiwasi na mkwewe b.fatma juu ya kifo cha mwanaye Amina. Akalipunza jambo hili kwamuda nakisha kuendelea na shughuli zingine.

    Jioni watu wanarejea toka kwenye mihangaiko yakimaisha. Nasibu na mkewe wakiwa chumbani wanabadilishana mawazo, Madsam alimgusia suala lile juu ya mashaka aliyonayo kwa mama yake, ilikuwa tofauti kwaupande wa Nasibu hivyo alimkemea na kumkaripia mkewe, ingawaje hakuna aliyepata kusikia malumbano hayo. Madsam hakuishia hapo, kesho yake alimuita mwanae Juma na kumueleza juu ya jambolile. Juma baada ya kupata taarifa hizo alisema"Mama mimwenyewe kunakitu kilinishangaza sana mpaka leo siwezi amini" "kitugani tena mwanangu?" mama alimuluza. Juma alimjibu"Sikuile muliyokuwa muna mpeleka Amina hospitalini, sikuweza amini machoyangu kuona mwili wa mtu kutokutoa kivuli haliyakuwa jua lina muangazia". Mama alidakia "nini..!? mbona hukunyambia mapema.?" "Nilipitiwa mama" Juma alimjibu huku akikuna kichwa. Kimya kilitanda kwa muda. Mara Juma akasema "mama unaonaje tukienda kwa wataalam?" "kufanya nini?" mama maye aliuza hukuakiwa kamkazia jicho. Juma akasema "watufafanulie juu ya jambo hili" "Nitangalia" mama alimjibu huku akiondoka zake.

    Nisiku ya pili B.fatma hajafukia kichwakile tangu akabidhiwe, hivyo kilianza kuharibika na kutoa harufu kiasi. Mzee Ally(mumewe B.fatma) Alijisemea "nahisi kunamnyama kafia humundani, sijui paka huyo..! ilamufanye hadi kesho uweumeshatoka mzoga wake"







    Siku ya pili yake. Madsam alikatashauri hivyo alimwambia mwanaye Juma waelekee hukokwa mganga kupata ufumbuzi waswalalao. Asubuhi majira ya saa5, baada yakumaliza shughuli za pale nyumbani, Madsam na mwanaye Juma waliekekea kwamganga katika kijiji chapili (kisangara) ingawaje hakuna aliyejua mtokoule kwani Nasibu hakuwaradhi na suala lawaganga.

    Walipowadia kwamganga wakakaribishwa kwenye mkeka. Mganga akawambia "semeni shidayenu iliyo waleta" Madsam alielezea mkasamzima uliomkuta mwanaye Amina kabla ya kufariki. Mganga alicheka kwa sauti ya mnato"ha ha ha ha.." akawa kama nimwenye kuwakejeli, kisha akawaeleza "kunamengi ambayo hamuyajui, nduguyenu hajafa kiroho.." wote walitahamaki "Nini..! Unasemaje?" mganga akawambia "tulizeni munkari leo mtapata kujua yote yaliyojificha, nihivi nduyenu amekufa mwilitu haliyakua rohoyake ingalihai, nahata hivyo mwiliwake ulishaliwa nyama naistoshe kunamabaki ya viungo vya mwiliwake nyumbani kwenu. "naulemwili tuouzika je?" Madsam akiuliza huku akiwa na wasiwasi. Kabla hajajibiwa Juma naye alidakia "vipi kuhusu hiyo roho uliyosema ingalihai hadisasa?" mganga aliwambia "musijali nitawaeleza. Mwili wa ndugu yenu ulifufuliwa pale mulipo uzika, hivyo kwenye kaburi lake hakuna kituchochote na hiyo rohoyake imetundikwa katika mbuyu uliopo pale kijijini kwenu hatahivyo haitakuwa rahisi kuiona roho yake.









    Baada ya maongezi marefu. Madsam alimuliza mganga "ninani anayefanya mambo haya?" mganga alimwambia "mutamjuatu mbaya wenu mukirudi nyumbani kwenu ilanitawapa dawa itakayowapa uwezo wa kugundua vilipo hifadhiwa viungomva mwili wa ndungu yenu, halikadhalika mbayawenu. Juma alimuliza mganga "tutamjuaje mbayawawetu?" "swalizuli kijana" mgana alijibu utamtambua kwakumtanzama usoni ataonekama nimwenyeaibu. Chukueni dawa hinzi mutazinyunyizia kuizunguka nyumba yenu sawa. Kwapamoja walitikia "ndiyo" mgana aliwapatia dawa nakisha wakarejea nyumbani kwao.

    Walipofika nyumbanikwao majira ya sasa 8 mchana, hawakutaka kupoteza muda. Madsam alichukuwa dawaile aliyopewa nakuanza kuinyunyiza kuzunguka nyumba yao, hakutaka maongezi na mtu japokuwa mumewe alikuwa akimuliza "wewe unafanyanini..? Kwanza umetoka wapi?" Madsam hakumjibu lolote chazaidi alimwangalia hukuakiwa amemkunjiauso nawenye hasira. Nasibu alibaki akimshanga mkewe hakujua kilichokuwa kinaendeleya.

    Pundesipunde B.fatma alitokandani nakusima mlangoni. Nibaada ya kuchefuliwa na harufu ya dawa iliyomwangwa pale nje, usokwau machoyake yaligongana na macho ya Juma







    Mzee Ally aliporejea nyumbani toka kwenye mgahawa, aliwakuta Juma na bibi yake wanaangaliana kamawatu wenyekisasi, akawauliza "nyiye vipi mbona mnashangaana?" hakutaka kusubiri kupewa jibu laswali alilouliza, alimgeukia Juma nakumueleza "hivi wewe jana sinilikwambia utoe huomzoga unaonuka humondani?" Juma alimjibu "ndiyo babu, naendakuutoa sasa hivi" "harakisha..!" babu alimwambia hukuakiwa anakachini kwenye kitichake. Wakati huohuo Nasibu na mkewe walitokea nyuma yanyumba hukuwakiwa wanajibizana. Juma akiwa anaelekea ndani kufanya alichoagizwa na babu yake. B.fatma akiwa bado kasimama pale mlangoni mara nguvu zikamwishia, mwiliulitweta, kijasho chembamba kikaanza kumtiririka mashavuni huku akitetemeka kama kamwagiwa maji ya baridi, macho yake aliyainamisha chini. Moyoni alianza kujilaumu "uvivu wangu umeniponza launingali kifukia kichakile mapema yasingenikuta yote haya, leo nisikuyangu ya kudhalika" Wenzake walimshanga kwa haliile. Juma alipo ukaribia mlango, B.fatma alimzuia kuingia ndani kwa kumuwekea mkono kifuani kwake. Mzee Ally na Nasibu hawakujua kichokuwa kinaendelea, Madsam na Juma waliangaliana kwaishara ya kuligundua jambo fulani. B.fatma kwaaibu alikimbilia ndani nakujifungia mlango. Mzee Ally alimshanga "haaaa..! amechanganyikiwa au vipi?" kisha akawauliza wenzake "kwani kunatatizo gani?" Madsam bilakusita alimsimulia mkasa mzima. Mzee Ally alibaki mdomo wazi hakuamini alichokisikia. Nasibu baada ya kusikia yotehayo alipanda na hasira. Akauvamia mlango nakuanza kuungonga kwanguvu. B.fatma kulendani alishindwa kuvumilia nakuangua kilio.







    Mayowe yalipoendelea kuzidi, majirani na wapitanjia walisogea enoelile. Wengiwao walidadisi "kwani kunanini hapa?" baadhi walipata fununu, wengine wakajizushia mambo wenye, eti hoo.! "ameuwamtu", wengine "anatakakujiuwa" wengine "mchawi" basi ikawa tafrani hakuna taarifa iliyoeleweka katiyao. B.fatma kulenda baada yakujua kunaumati mkubwa wa watu pole nje, aliacha kulia ilamapigo ya moyo yalienda mbiyo. Alipogeuza macho pombeni yake alikiona kisu... akakifuata nakukitwaa kisukile, hakuwa najinsi aliweka uwoga pembeni na kufumba macho huku akiwa anaielekeza ncha ya kisuki kwenye moyo wake, kwaharaka alikimbia na kujibamiza ukutani nakile kisu. Kisu kulingana kilichongoka sana, kilipenya katiya mbavu mbili hatimaye kuutoboa moyo, hapohapo moyo ukasimama kudunda. Kulenje watu waliokuwa karibu na mlango walikaa kimya baada ya kusikia sautikali iliyotoka ndani ikiambatana na kishindo kikubwa. Minong'ono ilififia hatimaye kimya kikatanda, marawaka msikia mtu anakorofuka mlendani.

    Majirani wawili walimsaidia Nasibu kuvunja mlango. Waliupiga vikumbo vitatu tu, hatimaye walifanikiwa kuuvunja, wakamkuta B.fatma kesha fariki dunia kutokana na kupoteza damu nyingi. Nje kilammoja alitaka kushuhudia kilichotokea ikawa ni vurugu patashika. Wengine walilia wengine walisikitika nakuhuzunika. Juma alingia ndani nakutafuta vileviungo alivyo ambiwa na mganga kuwavimo nyumbani kwao, hatimaye alikiona kichwa cha marehemu Amina uvunguni mwakitanda, kwa ujasiri alikichukua, bila ya kujielewa alitokanacho nje. Madsam alipokionatu akiazimia Nasibu alibaki akibubujika machozi. Watu wengine wenye mioyo dhaifu walizimia wengine kilammoja alitafuta njia yake, ikawa ni kukanyangana. Asha alilia mpaka naye akapoteza fahamu. Baadhi ya wanaume walio salia eneoile walichukuwa kichwa na mwiliule na kuvihifadhi pamoja.

    Kisha kuendelea na shughuli za mazishi.

    Kesho yake kilekichwa kikazikwa kwenye kaburi lilelile la Amina.
    .....MWISHO.....
 
KISASI CHA AJABU







  • SIMULIZI FUPI - KISASI CHA AJABU





    Akiwa katika siku yake ya pili kwenye mafunzo kazini Muuguzi Melina Joseph anakutana na jambo la ajabu ambalo linamfanya ajute kusomea uuguzi.Japokuwa aliwahi kuwaona watu wakipoteza maisha lakini si kwa idadi na namna ile aliyoiona.Wajawazito watano kati ya kumi walipoteza maisha ndani ya dakika kumi na tano wakipishana kwa dakika chache sana lakini jambo la ajabu ni kwamba wote walitokwa na povu mdomoni kabla ya kukata roho.



    Melina aliingia ofisini kwa wauguzi na kutoka bila sababu yoyote huku akijaribu kumpigia muuguzi mwenzake ambaye hadi muda huo alikuwa hajafika .Kila alipompigia simu haikupatikana hadi pale alipofika dakika ishirini baadaye ambapo naye alishtushwa na idadi ya wauguzi na madaktari ambao walikuwa wakihangailka kuihamishia miili ile Mochwari. Alimuita Melina pembeni na kuanza kuteta naye juu ya sababu ya hali ile lakini jibu alilopata na kuamua kuungana na wauguzi wengine kuwashughuliia wajawazito wengine ambao walikuwa wakiingizwa kwenye chumba cha wagonjwa waliohitaji uangalizi maalum ( ICU).



    Idadi ya wagonjwa waliopoteza maisha ilizidi kuongezeka ikiwashangaza madaktari wa hospitali ile ya serikali iliyopewa hadhi ya kuwa hospitali ya Rufaa.Daktari bingwa wa magonjwa ya akina mama aliwaita wauguzi waliokuwa zamu muda ule na kuwauliza juu ya tatizo lile katika harakati zake za kutaka kujua sababu iliyopelekea vifo vile ambavyo hadi kwa wakati ule ni mjamzito mmoja tuu ndiye alikuwa ambebaki tena akiwa chini ya uangalizi maalum wa jopo la madaktari waliokuwa wakijitahidi kwa hali na mali kuokoa maisha yake.



    Hata hivyo hawakuwa maelezo yoyote ambayo yaliyosadia kujua sababu ya vifo vile huku Melina akionekana kuwa na uoga kujibu maswali yale jambo lililogunduliwa na yule daktari ambaye aliamua kumruhusu yule mwenzake na kumtaka Melina abaki hali iliyompa uoga yule mwenzake kutokana na kuchelewa kwake kufika zamu jambo ambalo alilikuwa kawaida kwake japo alikuwa amepewa onyo zaidi ya mara tatu.



    Tabia ya utoro na uchelewaji kazini ilisababisha vifo vya wagonjwa wengi lakini muuguzi yule hakupewa adhabu nyingine zaidi ya kuonywa ,huku ikisemekana uhusiano wake wa kimapenzi na mganga mkuu ukiwa sababu ya kutofukuzwa kazi. Wakati hayo yakiendelea Daktari mmoja kijana ambaye alikuwa na miaka miwili tuu pale kazini alifikiria kitu kilichomfanya aende kwa baadhi ya wauguzi na kuwauliza juu ya mwanamke mmoja ambaye alikuwa na kawaida ya kufika pale hospitalini na kupitiliza hadi wodi ya kinamama wajawazito.



    Bwana Stivin Ngonyani kijana mwenye umri usiozidi miaka thelathini alikuwa akitafakari juu ya makazi halisi ya Mwanamke yule ambaye baada ya kuuliza aliambiwa kuwa alikuwa akiitwa mama Rose japo hakuwepo hata mmoja aliyefanikiwa kujua alikokuwa akiishi licha ya kuwa na urafiki na wauguzi wengi ambao walizoea kumwona akiwaletea chakula wajawazito waliokuwa hawana ndugu wa kuwasaidia.



    Mama Rose alikuwa mtu mwema , na hata Stivin alijikuta anajiuliza kitu kilichomfanya apate mashaka juu ya yule mama.Hakujua kitu kilichomfanya amhusishe yule mama na vile vifo lakini alijikuta akizidi kupata shauku ya kutaka kumfuatilia na kujua makazi yake na sababu iliyomfanya apende kuwapelekea chakula wagonjwa hasa wajawazito. Ilipotimu saa moja na nusu jioni bwana Ngonyani aliinuka na kuingia ofisini kwake akijiandaa kuondoka na kuanza uchunguzi usio rasmi juu ya yule mama ambaye nafsi yake ilimhusisha na vifo vile.



    Akiwa kwenye harakati ya kukusanya vitu alivyoona vya muhimu kutoka navyo ghafla mlango wa ofisi ile ulifungwa na mfungaji alionekana kuondoka na ufunguo licha ya kujua kuwa palikuwa na mtu mle ndani. Kitu cha ajabu katika ofisi ile hakukuwa na daktari mwingine ambaye alikuwa akiitumia zaidi yake na mwenzake ambaye alikuwa Masomoni , hivyo kitendo kile kilimfanya akose jibu huku maswali yakizidi kuongezeka kichwani mwake juu ya sababu ya vifo vya akina mama wale wajawazito.



    Kelele zake za kuomba msaada hazikumfanya yeyote aliyezisikia kwenda kumsaidia jambo ambalo halikuwa la kawaida pale ofisini.Aliamua kurudi kitini akitaka kuchukua simu yake ili awapigie watu waliokuwa nje ya ofisi ile ili wamsaidie ajabu kila aliyepigiwa simu hakuipokea. Mara taa za mle ndani zilizima na hazikuwaka tena japokuwa palikuwa na jenereta lililowaka mara tuu umeme ulipokata.Nje kulionekana kuna mwanga lakini ndani ya ofisi ile hapakuwa na mwanga wowote jambo lililomfanya Ngonyani asogelee swichi ya ukutani na kuhakikisha kama taa ziliwashwa, jambo lililomfanya apigwe na shoti ya umema kurushwa hadi palipokuwa na makabati kabla ya kutua sakafuni na kupoteza fahamu.



    Kishindo kilichotokana na kuanguka kwa Daktari Stivin Ngonyani kilimshtua Muuguzi Melina aliyekuwa akipita karibu na ofisi ile na kumfanya asimame na kusikiliza ilikotoka ile sauti. Ukimya uliofuatia kishindo kile ulimtisha Melina huku kumbukumbu za maiti za wale wajawazito zikijiridia kichwani na kuamua kuondoka eneo lile. Lakini kabla ya kuweka chini mguu wa kwanza kuunyanyua sauti ya kike inaita jina lake na kumfanya ageuke kumwangalia muitaji.



    "Ha! Mama Rose, shikamoo...."aliongea baada ya kugeuka.



    "Marhaba mwanangu, poleni na matatizo"alijibiwa na Mama Rose ambaye alikuwa ameshamkaribia.



    "Asante sana mama yaani hapa hadi naogopa"Melina aliongea akigeuka geuka kwa uoga. "Mipango ya Mungu mwanangu, hivi Ngonyani yupo?"mama Rose aliuliza akiangalia mlango wa ofisi iliyokuwa jirani.



    "Mbona pamefungwa, atakuwa ameshaondoka",alijibu.



    "Ina maana funguo kazisahau hapa?"mama Rose alitikisa funguo alizokuwa amezichukua kwenye dirisha la ofisi ile.



    "Mhh labda amezisahau ",Melina aliongea akipokea zile funguo na kuzichunguza kwa muda huku akiangalia ofisi ile. Alitamani kuifungua lakini ugeni wa uoga ulimfanya aamue kuzipeleka kwa daktari mwingine .



    "Haya mwanangu ngoja niende tutaonana kesho",mama Rose aliondoka na kumwacha Melina akiingia ofisini kwa daktari ambapo hakumkuta licha ya mlango kuwa wazi. Kwa uoga alitembea kwa haraka hadi palipokuwa na kundi la watu ambao baada ya kuwasalimia waliendelea na mazungumzo yao. Alifanya hivyo kwa vikundi kama vitatu lakini hali ilikuwa vile vile.Alianza kupata mashaka juu ya wale watu kwani uitikiaji wao wa salam ni kama ulifanana hivi. Akaamua kukisogelea kikundi kimoja na kuwaangalia wahusika bila kuwasemesha. Uchunguzi juu ya mwonekano wao uliishia kwenye miguu ambayo ilimfanya aishiwe nguvu na kuanguka kama mzigo na funguo zake mkononi



    Mwonekano ya miguu ya watu wa kundi lile ulimfanya Melina akose nguvu kabla ya kupoteza fahamu.



    Hakuwahi kuona zaidi ya kusimuliwa kwenye hekaya kuwa kulikuwa na viumbe-watu waliokuwa na miguu iliyofanana na ng'ombe.



    "Mtu awe na miguu kama kwato za ng'ombe?, unatudanganya Melina"aliongea mmoja ya madaktari baada ya Melina kurejewa na fahamu na kueleza kisa cha tatizo lake.



    "Kweli walikuwa kwenye vikundi kama vitatu Dokta" Melina alijaribu kumshawishi yule daktari huku kumbukumbu za kuwaona wale watu waliokuwa na kwato zikimfanya afumbe macho yake.



    "Enhee na kisa cha kumfungia Dokta Ngonyani na kuzunguka na funguo ni kipi?"yule daktari aliuliza swali lililomstua Melina na kung'aka.



    "Kumfungia?, haya mauza uza kabisa yaani mbele ya macho yangu mama Rose ameokota funguo na nilikuwa namtafuta Dokta nimpe funguo zake.



    "Tangu lini dokta ofisi zake zikawa mochwari, kweli ulikokuwa ukienda ndiko kuna ofisi yake?"yule daktari alihoji wakati huo bwana Stivin Ngonyani alikuwa ameshaingia mle ndani na kubaki kimya bila kuongea chochote.



    "Nilifika mochwari!, Mungu wangu mbona nilikuwa hapo nje ya ofisi yake tuu" Melina aliongea kwa mshangao.



    "Mhh haya mambo sasa magumu"aliongea yule daktari na kushusha pumzi kwa nguvu mara baada ya kumwona Ngonyani nyuma yake.



    "Pole sana dada Melina" aliongea Ngonyani akikisogelea kitanda.



    "Asante pole na wewe kwa kufungiwa ofisini"Melina aliongea na kumgeukia Ngonyani lakini alishtuka baada ya kuona weusi uliokuwa upande mmoja wa uso wake.



    "Jamani dokta nini tena hicho?" Melina aliuliza kwa uoga.



    "Ni ajali ndogo tuu hapa nimepaka dawa ya kukausha"Ngonyani alijibu akimwangalia Melina kwa macho ya upole zaidi na kusababisha Melina kuyakwepesha macho yake.



    "Dawa gani nyeusi hivyo?" Aliuliza Melina kwa upole.



    "Ni ya kienyeji nimepewa na mama Rose" Ngonyani alijibu.



    "Mama Rose!" Alishangaa Melina lakini baadaye alibaki kimya.



    "Ehee kwani ana tatizo gani?" Alihoji yule daktari mwingine aliyeonekana kuwa kimya kwa muda kidogo.



    "Hamna kitu nimejikuta tuu nimeropoka"alijibu Melina na kunyong'onyea.



    "Lakini nina mashaka na yule mama" Ngonyani aliongea akiangalia mlangoni kuhakikisha usalama wa alichokizungumza.



    "Ehee hata mimi hivi anakaa wapi?" Melina alidakia lakini swali lile ni kama lilimkera yule daktari.



    "Na wewe ushaanza habari za kwato zako, ngoja nikupe dawa upumzike"yule daktari mwingine aliongea kwa hasira na kufungua kipakti cha dawa kilichokuwa pale mezani.



    "Samahani dokta hizo dawa si nzuri kwa tatizo la huyu binti ''Ngonyani aliongea na kujaribu kupokonya zile dawa lakini yule daktari alimgeukia na kumwangalia kwa macho makali yaliyomfanya Ngonyani na Melina wapoteze fahamu.



    Asubuhi ya siku ya pili Melina aliamka kutoka kitandani na kujipapasa kama alikuwa na majeraha yoyote mwilini mwake lakini hakuona kitu chochote wala kusikia maumivu mwilini mwake.Alipomwangalia muuguzi mwenzake ambaye alikuwa zamu kuanzia saa mbili asubuhi ,dakika arobaini zilizofuata alimwona akiwa kwenye usingizi mzito lakini badala ya kumwamsha Melina alianza kuzunguka mle chumbani akishika hiki na kile kama akihakikisha kitu fulani.



    Hakutaka kuamini kama kweli alikuwa amelala kitandani pake,alifikaje nyumbani hakuelewa,ina maana aliyokuwa akiyaona yalikuwa ndoto? Alibaki anajiangalia huku wazo la kumwamsha mwenzake likimjia akilini.



    Lakini kabla hajamwamsha yule mwenzake aliamka na kumwangalia kwa macho makali kabla ya kuangalia chini.



    "Vipi mbona unaniangalia hivyo?"Melina aliuliza.



    "Yaani hata siamini kama ni wewe"yule mwenzake alimjibu safari hii akimtazama usoni.



    "Kwa nini", aliuliza.



    "Mara utake kukimbia ,mara watu wanakwato, mara Mama Rose yaani hadi tulimwita huyo dokta jirani atusaudie maana ulitushinda mi na dada Sarah"alieleza yule mwenzake kwa kirefu.



    "Inamana nilikuwa naota,enhee nilifikaje nyumbani''?Melina alihoji huku taarifa ya uwepo wa daktari jirani yao mle ndani ikimkera kwani tangu anafika pale alikuwa akimtaka kimapenzi licha ya kuwa na mke.



    "Si ulikuja na Mama Rose ukidai kichwa chakuuma ulilala saa moja yaani bila Mama Rose sijui ungelala njiani, ukipona ukamshukuru sana"alieleza yule mwenzake.



    "Mbona sikumbuki kabisa" aliongea Melina akijaribu kuvuta kumbukumbu.



    "Tuachane na hayo wajisikiaje?"



    "Mi mzima sikumbuki kama niliumwa"



    "Sawa ila jana umeumwa kweli,kama mzima wacha tupumzike kwani napumzika nikikuuguza " aliongea yule mwenzake akijiinua pale kitandani.



    "Wacha wee kwa hiyo leo mapumziko?" Aliropoka Melina.



    "Mhhh nawe siku mbili tuu umechoka unataka kupumzika" yule mwenzake alimsuta.



    "We yale yaliyotokea jana kazini yanavumilika kweli? Ingekuwa si umasikini ningekuwa nimeacha kazi"alilalama Melina



    "Ila tangu nianze kazi sijawahi kushuhudia hali kama ile"alieleza yule mwenzake.



    "Yaani hata sijui tumwombe tuu Mungu".



    Hodi ....hodi wenyewe mpo? Sauti kutoka nje iliwashtua.



    "Karibu ,karibu hadi ndani, tupo"alijibu yule mwenzake akielekea sebuleni.



    "Ha dokta Ngonyani karibu sana"alikaribisha Melina.



    "Umemwona Ngonyani tuu mi hujaniona?"yule daktari aliyekuwa akimtaka Melina aliuliza kabla ya kukaa.



    "Jamani we si mwenyeji, basi Karibu"Melina alijibu na kukaa.



    " Haya lakini unaendeleaje?" Aliuliza yule Daktari.



    "He dokta Ngonyani mbona hivyo?" Aliuliza Melina baada ya kuona weusi kwenye upande wa kushoto wa shavu lake.



    "Ajali ndogo tuu dada" alijibu Ngonyani akipapasa shavuni.



    "Pole sana kaka" waliongea Melina na yule mwenzake kwa pamoja.



    "Asante",Alijibu.



    "Ilikuwaje kaka?"yule mwenzake aliuliza.



    "Jana nikiwa ofisini nilipata hitilafu kidogo nikapigwa shoti, yaani ashukuriwe Mama Rose asingekuwa yeye ningeweza kufia mle ndani"alieleza Ngonyani.



    "Yaani huyu Mama Rose Mungu ampe maisha marefu ,amemwokoa Melina akaenda kumwokoa na Dokta"aliongea yule mwenzake na Melina.



    "Kweli yule mama sijui mwanaye alipata malezi gani yaani ule wema umepitiliza"Ngonyani alichangia.



    "Mwanaye tuu mumewe je?"aliongeza yule daktari mwingine akicheka.



    "Hata ana mume kweli?"alihoji yule muuguzi mwingine.



    "Afu kweli maana sijawahi kumwona" alieleza yule yule daktari.



    "Huenda akawa mjane,halafu huyo Rose amewahi kuonekana,hata anapoishi mnapafahamu?"Ngonyani aliuliza.



    "Mie mwanaye hata akaapo sipajui atakuwa anaishi huko chini anakoelekea"yule daktari alieleza akionesha kwa mkono upande aelekeako yule mama.



    Alikumbuka kuwa miongoni mwa wanawake aliowataka kimapenzi ni yule mwanamke ambaye jibu lake moja lilikuwa ni lilelile kuwa 'nimeolewa'.



    "Sasa mgonjwa ngoja tuwahi kazini, ugua pole ehee"aliaga Ngonyani akiinuka.



    "Asante kazi njema na pole kaka Ngonyani"Melina aliaga akimwangalia Ngonyani kwa macho ya kichokozi.



    "Haya mgonjwa ugua pole utapona eee"yule daktari mwingine aliongea akimkonyezea macho Melina aliyegeukia pembeni kwa dharau.



    "Huyu mbaba anaonekana mhuni"Melina alimwambia mwenzake baada ya kujipa uhakika kuwa walikuwa wawili tuu pale ndani kwa kuchungulia mlangoni.



    "Mhhh ehhe.. mi amenitaka kweli ananidanganya kuwa ana hospitali yake atanipeleka baada ya kunisomesha"alijieleza yule mwenzake akijua fika alidanganya kwani alikuwa kwenye penzi zito na yule daktari na kutaka kusababisha kuvunjika kwa ndoa yake.
 
KISASI CHA AJABU - 2





  • "Eboo! Huko shule si angempeleka mkewe anayeshinda kuuza maandazi au binti yake aliyemaliza sekondari mwaka juzi mbona yupo tuu nyumbani akibadilisha tuu wanaume kama siti ya daladala, wazee wengine nao sijui wana laana?" Melina alimaliza na swali na maneno yale yakamwingia yule mwenzake huku akijiona mjinga kwa kuwa kwenye mahusiano na mzee wa umri wa baba yake.



    "Hajiheshimu tuu wala si laana" yule mwenzake alijibu kwa kifupi huku moyoni akijilaumu kudokeza lile jambo kwa Melina.



    Baada ya tukio la vile vifo hali ikajerea kama kawaida huku kila mtu akichukulia lile jambo kwa ukawaida tofauti na awali.Watu walizidi kusahau huku kumbukumbu juu ya Mama Rose zikipotea baada ya kutoonekana hadi miaka saba baadaye siku ya kuagwa kwa yule dokta mpenda dogodogo baada ya kustaafu na bwana Stivin Ngonyani alipokuwa akipewa udaktari mkuu wa ile hospitali huku Melina akiwa mkewe.



    Uwepo wa Mama Rose ulimfurahisha kila aliyekuwepo kwenye ile sherehe na hata zawadi alizowapa wahusika zilipewa umuhimu sana na wahusika.



    ___________



    Jioni ya ile siku kama ilivyokuwa kwa Ngonyani yule daktari mwingine aliifungua boksi lililokuwa na kuanza kuanza kutoa vilivyokuwemo.



    Kadi nzuri ya pongezi yenye maneno yaliyomfurahisha kila aliyeisoma ilikuwa juu huku harufu nzuri ya marashi ghali ilifunika eneo lile hali iliyowavuta hata wake zao kusogea karibu ili kujua kilichokuwemo.



    Zawadi iliyokuwa chini yake haikumfurahisha kila mmoja kwani palikuwa na biblia mpya.



    Walifungua zile biblia na kukuta karatasi zilizokuwa na maelezo ya vifungu vya kusoma.



    Walifungua vifungu vilivyoelekezwa na kuanza kuvisoma huku wake zao wakiwa wanahangaika na zawadi nyingine.



    Saa nane na nusu usiku kama vile waliambizana yule daktari na Ngonyani waliamua kulala baada ya kuona wamezidiwa na usingizi licha ya mioyo yao kuwasukuma kuendelea kusoma.



    Asubuhi iliyofuata, siku ambayo bwana Stivin Ngonyani ilikuwa ni siku yake ya kwanza kama Mganga mkuu wa hospitali ile alifika mapema sana tofauti na siku nyingine huku kichwani akiwa na malengo makubwa katika kuongeza sifa hospitali aliyokuwa akiiongoza.



    Alienda moja kwa moja hadi kwenye ofisi aliyokuwa amekabidhiwa jana yake na kuanza kupitia pitia taarifa fulani.



    "Dokta Ngonyani kumbe upo humu tunakuomba wodini" sauti ya kike ilisikika kutoka nje ya ofisi yake dakika ishirini tangu alipoingia .



    Ngonyani alikurupuka kutoka alipokaa na kutoka nje alipokutana na kundi la wauguzi walioonekana kuchanganyikiwa.



    "Kuna nini?"aliuliza baada ya kutoka nje.



    "Twende wodini"aliongea muuguzi mmoja aliyeonekana mtu mzima kidogo.



    Alipofika wodini alishangaa kukutana mapazia ya kijani yaliyozunguka karibu robo tatu ya ile wodi.



    "Mungu wangu !"alijikuta akiropoka Ngonyani baada ya kuona maiti za wajawazito zaidi ya ishirini na tano huku zikiwa na povu mdomoni.



    Idadi ya wajawazito walipoteza maisha iliongezeka kila dakika hadi kufikia saa tatu na nusu jumla ya wajawazito waliopoteza maisha ilifikia arobaini na tatu hulu wengine wakiwa katika hali mbaya.



    "We huyu Mngoni si mchezo anataka kujisimika"aliongea mmoja wa wafanyakazi aliyeungwa mkono na wenzake waliokuwa wamekaa kwenye benchi.



    "We huyu kijana anaogopa kupinduliwa"aliongea mzee mmoja aliyesimama jirani na alipokuwa akipita Ngonyani.



    "Huyu mwoneni hivi hivi alivyo" alikazia yule mzee ambaye alionesha chuki zake wazi wazi bila kujali kama alichokiongea kilisikika hata kwa Ngonyani ambaye alionekana mwenye mawazo lukuki.



    Kila alipopita vidole vilinyoshwa kwake kuashiria kuwa tuhuma za sababu ya vile vifo kuwa ni yeye.Hakuwa na raha hata kidogo,alikaa ofisini kwake huku akiwa na wazo moja tuu ,'kuomba kuacha kazi' kwani tuhuma zilizokuwa zikielekezwa kwake zilikuwa zimemwelemea.



    Maiti ziliongezeka mochwari kila baada ya dakika, magari nayo yaliingia pale hospitalini na kulifanya eneo la wazi lililokuwa pale hospitalini lionekane dogo.



    Waziri wa afya aliyekuwa ziarani kwenye mikoa ya jirani alikatisha ziara yake na kufika hospitalini pale kuangalia hali iliyokuwepo pale.



    Kikao cha dharula kilifanyika pale ofisini ukiwahusisha madaktari na wauguzi kadhaa pamoja na waziri wa afya aliyeonekana kushtushwa na mwenendo wa ile hospitali.



    Wakiwa katikati ya kikao mama mmoja aliomba kuingia mle ndani baada ya kubembeleza sana na kutambuliwa kuwa alikuwa ni Mama Rose aliruhusiwa kuingia.Alipoingia mle ndani aliuliza kama palikuwa na yule Mganga mkuu aliyetoka kustaafu jana yake na alipooneshwa aliomba wasaa wa kuzungumza akidai kujua chanzo cha vile vifo.



    "Mama kama unajua inabidi ukaeleze polisi" aliongea waziri wa afya aliyeonekana kukerwa na madai ya yule mama aliyeonekana kama alikuwa na upungufu wa akili mbele yake.



    "Nikaeleze polisi kwani kuna mtu ameua?" Aliongea yule mama kwa ukali jambo lililowafanya wauguzi wenyeji kutaka kumtoa yule mama kwa nguvu lakini kabla hata ya kumfikia waliashiriwa na waziri kuwa wamwache.



    "Samahani mheshimiwa Waziri naamini wengi hapa wananifahamu kwa jina la Mama Rose lakini jina langu nililopewa na wazazi wangu ni Rose Daniel" aliongea yule mama huku akitoa kitambaa kilichokuwa hakibanduki kichwani kwake , na kuonesha sura yake yote ambayo ilionesha jinsi umri wake uliokuwa ukielekea machweo.



    " Waliofanya kazi hapa mwishoni mwa miaka ya themanini watakuwa wanaikumbuka hii sura hasa hili kovu" aliinama kuwaonesha kovu kubwa lililokuwa kichwani kwake.



    " Mnakumbuka eee au mmenisahau"aliongea yule mama akimsogelea Ngonyani akimshika mabegani.



    " Umesahau mimi wa mtoto aliyekufa" aliongea kwa hasira huku machozi yakimtoka na kurudisha kidogo kumbukumbu yuma lakini yule mama alisimulia kisa chote.



    _____________



    SEPTEMBA 1988



    Kundi la wanafunzi saba kutoka vyuo mbalimbali vya uuguzi nchini walifika kwenye hospitali kukiwa na wavulana watatu na wasichana wanne.Ujio wa wauguzi wale waliokuwa kwenye mafunzo kwa vitendo ulipokelewa kwa hisia tofauti na wauguzi wenyeji na wagonjwa.



    Wakati wagonjwa wakiamini ni muda wao wa kupata huduma bora kutokana na wingi wa watoa huduma ,upande wa wahudumu wenyeji waliona ni wakati wa kutegea kazi na kuwaachia wale wanafunzi.



    Tofauti na mawazo ya makundi yale daktari mmoja alifikiria jambo tofauti juu ya ujio wa wale watu.Kilichokuwa akilini mwake ni juu ya uwezekano.wa kuwapata wale wasichana kuwafanya wapenzi wake huku akiamini mbinu yake ya kuwadanganya kuwa alikuwa na hospitali yake binafsi ingekuwa chambo.



    Alitumia mbinu ile kwa wale wauguzi watatu na kufanikiwa kufanya nao mapenzi kwa nyakati tofauti ila ofisi yake ikiwa sehemu pekee ya matukio.



    Alipofika kwa Rose Daniel haikuwa rahisi kumpata kama ilivyokuwa kwa wengine,mbinu zake zote hazikuwa na matokeo chanya kwake.



    Rose alijiheshimu kama msichana wa kiafrika anavyofunzwa kubaki na usichana wake hadi atakapoolewa,marehemu wazazi wake kabla ya kufariki walikuwa hawaishi kumwonya juu ya hilo hata shangazi.yake aliyekuwa akiishi naye alimtaka ajitunze na kuzingatia masomo ili akawasaidie wadogo zake ambao nao walipoteza maisha kabla hata ya kumaliza masomo.



    Siku moja akiwa kazini kama ilivyokuwa kawaida yule daktari alimwita Rose na kumtaarifu kuwa alikuwa zamu muuguzi mmoja mzoefu usiku wa siku ile jambo ambalo alikubaliana nalo bila kuhisi chochote.



    Usiku akiwa kazini yule muuguzi mwenyeji alimtuma Rose maabara akimweleza kwenda kuchukua daftari alilokuwa amelisahau mchana.



    Baada ya kuingia mle maabara mara mlango ulifungwa na taa ilizimwa na kusababisha giza totoro.Rozali aliyokuwa ameivaa Rose ilimwonesha alipokuwepo kutokana na kung'aa gizani jambo lililorahisisha kazi ya adui yule kumkamata.Mikono iliyokomaa ya yule daktari ilimshika Rose kwa nguvu kabla ya kurarua nguo zake.Kitendo hicho kilichukua dakika chache sana huku sauti dhaifu ya Rose ikishindwa kufika popote.



    Baada ya kumfanyia unyama ule alimwinua kwa nguvu na kwenda kuwasha taa.



    "Mungu wangu! Dokta "alilalamika Rose baada ya kumwona aliyemfanyia kitendo kileAliinua chuma kilichokuwa kilichokuwa mezani na kumwangalia yule daktari kwa hasira.



    Tofauti na mawazo ya yule daktari.kuwa huenda angemdhuru, alichukua kile chuma na kutaka kujichoma kichwani kabla ya kuzuiwa na yule daktari lakini damu zilikuwa zimeshaanza kumtoka.Baadaye alipoteza fahamu na yule daktari alimpa huduma ya kwanza kabla ya kwenda kumwita yule muuguzi mwenzake ambaye walipanga ule mchezo.



    "He! Ulitaka kuua?" Aliuliza yule muuguzi baada ya kuliona lile jeraha.



    " Alitaka kujiua mwenyewe" alijibu yule daktari alitetemeka.



    "Sasa tutafanyaje?"alihoji yule muuguzi.



    "Akipata fahamu unibembelezee akaseme aliangukia sehemu yenye chupa" alishauri yule daktari.



    Kama walivyopanga baada ya Rose kurejewa na fahamu alipewa somo na kiasi kikubwa cha pesa ambazo alizikataa lakini alikubaliana nao juu ya kutunza ile siri.



    Siku moja akiwa njiani kuelekea nyumbani alikutana na kiumbe wa ajabu ambaye alimshangaa kwa kumsamehe yule daktari kwa kumtunzia siri, Rose alishtuka kusikia maneno yale kutoka kwa kiumbe yule wa ajabu ambaye baadaye alijitambulisha kuwa ni shetani.



    Hakuamini kabisa kama shetani kiumbe anayefahamika kama chanzo cha dhambi duniani kulaani kitendo alichofanyiwa na yule daktari.



    "Ni uongo tuu ulioenezwa na malaika wengine ili nionekane mbaya kwa wanadamu" aliongea yule kiumbe baada ya kusoma mawazo ya Rose.



    "Nasamehe" alisema na kuondoka huku moyoni akiwa na hofu kuu.



    Sura ya yule kiumbe ilimtokea kila mara hasa akiwa ndotoni hadi pale alipoamua kukubaliana naye kulipa kisasi.



    Ile sura haikujitokeza tena hadi siku aliyomaliza mafunzo kwa vitendo na kurudi chuoni aliposisitizwa kulipa kisasi.



    Wiki mbili baada ya kurudi chuoni Rose alikuwa miongoni mwa wasichana watano waliokutwa ni wajawazito baada ya kupimwa kama ilivyokuwa kawaida ya kile chuo.



    Japokuwa walikuwa katika mwaka wa mwisho walifukuzwa chuoni kwa upande wa Rose alifukuzwa pia nyumbani jambo lililomfanya amrudie yule daktari aliyekuwa mwanaume pekee aliyefanikisha kuujua usichana wake.Mwazo alionekana kukataa lakini baadaye alikubali kumsaidia akidai angempeleka shule baada ya kujifungua.



    Alimtafutia nyumba ya kukaa huku akimhudumia kwa mahitaji muhimu lakini kila usiku alitoa huduma ya penzi kwa yule daktari.Hali ile iliendelea hadi siku ya kujifungua ambapo alikutana na daktari Stivin Ngonyani aliyekuja pale hospitalini kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo.



    Kabla ya kumpa huduma Rose, Ngonyani aliitwa na yule daktari aliyemwelekeza kumuua mtoto atakayezaliwa na kumwonesha maiti ya kichanga kilichoandaliwa .Ngonyani alikubaliana naye na kuendelea na kazi ambapo kama alivyoelekezwa alionesha ile maiti lakini yule mtoto alimkabidhi mwanamke mwingine aliyejifungua maiti.



    Alikuwa kichanga mzuri wa kike ambaye alipokelewa vyema duniani.na watu alioamini kuwa ni ndugu zake.



    " Mwanamke gani unanizalia maiti tokaaa!" Ilikuwa sauti kali ya yule daktari ambaye alikuwa akimfukuza Rose usiku wa siku aliyojifungua.



    " Ni mipango ya Mungu mpenzi" alibembeleza Rose.



    "Mungu huleta maiti? Tokaaaa!" Alimsukumia nje yule mama ambaye alitakiwa awe chini ya uangalizi maalum baada ya kujifungua masaa machache yaliyopita.



    Baadaye yule mama kwa kutambaa alijisogeza mita kadhaa kutoka nyumba ile kwani alihofia kipigo kutoka kwa yule daktari ambacho kilikuwa njiani.



    Akiwa pale chini ile sura ya kutisha ilimjia tena na kumtaka alipe kisasi lakini alikataa kata kata na kumtia hasira yule kiumbe aliyejiita shetani aliyeamua kumtoa roho yake na kujiingiza kwenye ule mwili





    "Hapo ndipo KISASI CHA AJABU KILIPOANZA ya uongo haya?" Aliuliza Mama Rose aliyeonekana kubadilika mwonekano wake na kuwa wa kutisha.



    " Nilitaka kusahau yule mtoto uliyemwokoa ndiye mkeo bwana Ngonyani" aliongea alimnyoshea mkono Ngonyani kabla ya kumgeukia yule daktari aliyeanza kutapatapa kabla ya kutoa povu na kupoteza maisha.



    Yule muuguzi aliyesaidia kubakwa kwa Rose naye alikufa kwa namna ileile kabla ya kiumbe yule wa ajabu kutoweka.



    Ngonyani aliwekwa chini ya ulinzi na kupelekwa kituo cha polisi kabla ya kupelekwa mahakamani alikohukumiwa kifungo cha miaka mitano huku akipoteza kazi yake.





    MWISHO.
 
UTAMU MTUPU






SIMULIZI FUPI - UTAMU MTUPU





Nilitamani muda wa vipindi darasani umalizike ili iweze kutimiza ahadi niliyokuwa naisubiri kwa siku nyingi.



Mwalimu alikuwa akifundisha lakini ni kama nilikuwa sielewi wala sisikii alichokuwa anaelezea.



Mawazo yangu yote yalikuwa kwa Madam Jesca. Siku hiyo nilijisemea kuwa iwe isiwe lazima nimweleze ukweli na ikibidi siku hiyo hiyo yatimie ninayoyawaza kila kukicha.



Madam Jesca alikuwa ni mwalimu aliyekuwa akitufundisha kwa muda tu baada ya kuwa amemaliza kidato cha sita. Wakati huo sisi tulikuwa kidato cha nne.



Somo alilokuwa akitufundisha ni Kiswahili.



Hatimaye mwalimu akatoka na baada ya nusu saa nikaondoka kuelekea nyumbani kwa madam Jesca.



Niliingia baada ya kuwa nimegonga hodi.



“We Joshua mbona muda wa vipindi hivi we umekuja huku..” aliniuliza huku macho yake yakionyesha mshangao wa waziwazi.



Kanga yake aliyovaa ilikuwa imelowana na hivyo kusababisha niuone mstari wa chupi.



Na kama hiyo haitoshi madam Jesca alikuwa ana kitu kingine cha ziada. Awali nilidhani nimekifananisha lakini alipotembea nikahisi ni chenyewe.



Aidha alikuwa amevaa cheni ama la alikuwa ana shanga kadhaa kiunoni.



“Mwalimu nimekuja unifundishe aina za NOMINO”



“Joshua ni lini sasa utaacha vituko, aina za Nomino nyumbani kwangu eeh!!” alinikaripia lakini sikurudi nyuma niliamua kuwa iwe siku hiyo. Siku ya maamuzi yangu!!



“Madam, kwa hiyo unataka nifeli ama….” Nilimuuliza kwa uchungu. Nikauona uso wake ukipunguza makali ya hasira.



“Hebu ni kitu gani huelewi sasa hapa kwenye Nomino,…..” aliniuliza.



Nikatikisa kichwa na kuingiza mtego wangu. Madam mwenyewe hakuwa mkubwa ni basi tu ye alikuwa amenitangulia kieleimu na sasa ni mwalimu wangu.



“Madamu…nitafundishwa nikiwa nimesimama hivi kweli..” nilihoji huku nikitoa tabasamu hafifu sana.



Madam akatembea na kuingia ndani huku akinionyesha ishara ya kumfuata. Nikafanya kama alivyoniambia, nikiwa nyuma yake nikauona utamu halisi wa Madam ambao huwa unajificha katika mavazi yake ya kiualimu.



Alikuwa amegawanyika vizuri, kiuno kilijitenga kivyake na makalio yake yalikuwa katika mlingano sahihi hivyo hata kutikisika yalitikisika katika namna ya kuvutia.



Upesi nikaingiza mkono katika suruali yangu ya shule nikaishusha injini iliyoanza kunyanyuka juu nikaibana vyema katika mkanda ili isije kuniaibisha mbeleni.



Ubaya na uzuri wa chumba cha Madam Jesca ni kwamba kilikuwa kimoja tu, hivyo hakupata fursa ya kubadili nguo aliketi kitandani na kuniruhusu mimi nikae katika kiti.



“Iwe mara ya kwanza na ya mwisho kuingia katika nyumba hii. Shida zote tunamalizia shuleni sawa???” alijaribu kunikoromea. Na hapo nikauona utamu mwingine.



Jesca alikuwa na mwanya!! Mama weee!! Nilikuwa wapi siku zote bila kuuona huu mwanya.



“Nimekuelewa mwalimu!” nilijibu kwa nidhamu.



“Haya ni wapi hukuelewa…’



“Madam usiseme tu sikuelewa yaani siku hiyo sikuwa darasani kabisa…”



“Sasa utoro wako nd’o uje kunisumbua mimi ebo!!!” aling’aka.



“Sio utoro madam….. nilikumbwa na majanga sana…..”



“Yapi uongo tu!!!” alizidi kuwaka….katika namna ya kunisuta…



Na hapo ndipo nilipopataka zaidi.



“Madam nilipata misiba mfululizo we acha tu, kwanza mdogo wangu, sijakaa sawa kuna rafiki yangu wa tangu utoto naye akagongwa gari…mama ameugua muda mrefu pia madam,,, yaani aargh!! Mwaka huu ni wangu madam mi nitafeli tu na sijui nitakuwa mgeni wa nani, hesabu nimekosa topiki mbili, Chemistry nd’o sijagusa praktiko hata moja…..” na hapo nikasita kisha nikaanza kulia, nililia kiume machozi bila kelele.



Madam akajiingiza mkenge, akanishika na kuanza kunibembeleza. Huu si ndio utamu niliokuwa nautaka sasa….



Alinibembeleza mwisho nami nikajilaza kifuani mwaka.



Wacha wee!! Madam alikuwa na embe dodo kifuani ambazo zilikuwa na joto fulani linalokulazimisha kuendelea kuzilalia hata kama hutaki kulala. Mikono yangu ikazunguka katika kiuno cha madam na kukutana na ile cheni, nikaifyokonoa na kuizamisha katika kiuno chake.



Nikazisikia pumzi zake zikipishana kwa kasi, nikajua nimegusa penyewe.



“Usijali Joshu aaaaah!! Usijali utafaulu sawa eeeh!! Usijali Jo….ooooooH!!! aaaaaaH!!!” he!! Madame alikuwa anazungumza ama analalamika.



Nikatambua kuwa mambo tayari, nikamsukuma ghafla akatua kitandani kwake. Macho yake yalijaribu kunitazama lakini yalionyesha kusinzia kwa huba!!



Kanga ilikuwa imekaa hovyo tu, paja laini likinidxhihaki na kichupi cheupe nacho kikinichungulia na kuniambia karibu!!!



Sikutaka kuwa na papara, nikamrukia na kukutanisha ndimi zetu, akazipokea.



Ebwa ee!! Joto likaongezeka na suruali ikazidio kunibana….



Ni kama alijua vile kuwa jogoo anataka joto, nikaisikia mikono yake ikitafuta mkanda wangu huku ndimi zikiendelea kushambuliana kwa kasi. Akaupta mkanda, akaufungua nami nikajipandisha juu kidogo ili aweze kuitoa suruali vyema.



Akaishusha kidogo kwa mikono kisha akaisindikiza kwa miguu.



Mara mapaja yakagusana….doh!! nikajihisi nipo ulaya na wazungu wanataka kutoka katika jogoo wangu.



Aibu gani hii wazungu kutoka katika nchi kabla ya uhuru!!! Nikajibana huku na kule huku nikijaribu kukwepesha hisia zangu nisije kuaibika.



Ghafla mkono wa Jesca ukaikamata ikulu vyema, mikono laini kabisa ikaanza kupanda juu na kushuka chini kwa sababu maalumu kabisa.



Lakini kama nilidhani kuwa ile mikono ndo laini kupita kila kitu nilikuwa nimekosea.



Ni kama tulikuwa tunacheza kuwahiana, mimi nilikuwa nimemnyonya masikio, mara akanirukia na kujikunja huku akihema, akaimeza ikulu nzimanziama mama weee!! Nikajikuta napiga kelele kwa mshtuko. Jesca akanishambulia kwqa kasi sana hadi nikakiri kuwa nisipokuwa makini wazungu watatoka kabla sijapewa uhuru. Nikambandua kutoka pale kisha ikawa zamu yangu kutazama chumvi ya uvinza ina kiwango ama imeharibika tayari.



Nikazamisha ulimi na kuanza kufanya upelelezi. Nilipopiga kelele nilidhani nimejiaibisha lakini madam alikuwa zaidi. Sijui kilikuwa kichaga kile. Neno kuu alilorudia mara kwa mara ni ‘yerewiiii na jingine mbombo ngafu…’ kama sikosei ni hayo. Nadhani mchaga yule. Chumvi yake ilikuwa ina ubora, madam alikuwa msafi kupindukia.



Hakuwa akitoa harufu kabisa!!



Maana akina Mwajuma wa mtaani kwetu almanusura nitapike nilipozama siku ile!!



Huyu alikuwa smart haswa!!



Kama ni utamu ndipo huu.



Masikioni utamu, mdomoni utamu, hadi huku kwenye chumvi napo utamu.



Ulikuwa utamu mtupu!!!



Madam kuona mashambulizi yamezidi na yeye akajaribu kupambana…safari hii kidogo aniue huyu dada.



Ebwana!! Umewahi kupulizwa korodani wewe!! Zipulizwe halafu zimezwe kitaalamu…….



Unaweza kuzirai!!! Na usiombe upate mtaalamu wa kuzipuliza na kunyonya unaweza kujifia kitandani ukapatia watu kesi zisizowahusu.



Madam akaninyonya, sijui na mimi nilizungumza kinyakyusa?? Sikumbuki kwa kweli…..



Baada ya hapo hapakuwa na jingine ulikuwa wakati wa kuwarudisha wazungu ulaya ili nibaki huru!!



Kibaba na mama!!! Staili ya kuwarudisha wazungu wa kwanza wenye kiherehere!!!



Nikajikunja na kuushika mguu wake nikaunyanyua juu..nikaingia golini. Haya nafungaje sasa…..



Huyu nakuna kushoto sana ambapo wasichana wengi wamezoea kwa sababu mashine nyingi za wanaume huwa zimeegemea kushoto…..nikishamkuna kushoto alipozoea nahamia kulia ambapo najua hajawahi kukunwa vizuri.



Kweli nikaanzia kushoto, nikakwangua kama mara ishirini, nilipohamia kulia. Madame akapiga kelele za utamu kwa nguvu. Nikatamani kumziba mdomo lakini nikajua huo ni utamu umempagawisha!!! Na mimi lazima niwatoe wazungu ndo nitajua hayo mengine.



Nikamkunja zaidi huku nikizidi kukuna kulia……..nikawakontrol wazungu wasitoke ili aendelee kufaidi.



“Baby iam coming…..iam coming baby…..” nikamsikia akilalamika kimombo, haya huwa nayasoma gazetini huko nikajua kuwa amekaribia mshindo.



“Jamani ankoo!!” nikamsikia akizidi kulalamika



Nikazidi kupampu kwa juhudi ili asinisahau tena maishani mwake.



Ile wazungu wanataka kuja na yeye akajipandisha juu zaidi. Akanisukuma kwa nguvu.



He!! Mara nikajikuta hewani, nikataka kurudi chini ikawa ngumu.



Mara macho yakafumbuka, nilikuwa nimeanguka na kiti changu darasani, wanafunzi walikuwa wanapiga kelele.



Wengine wakinizomea, wengine wakinisikitikia,,,,,, ile kujitazama suruali yangu ilikuwa imevimba haswa na wasichana walikuwa wakinitazama.



“Joshua yaani unaota mchana kweupe hivi mdogo wangu?? Tena unakoroma kama kondoo looh!!” lilikuwa swali kutoka kwa madam Jesca. Ebwana eeeh!! Ilikuwa aibu, kichwa kikaanza kuuma nikatambua kuwa nilijibamiza vibaya nilipoanguka. Na mawalimu niliyemuota nd’o kilikuwa kipindi chake sasa!! KISWAHILI



Looh!! Yaani utamu wote ule kumbe nilikuwa naota Joshua mimi aaargh!!!



Japokuwa ilikuwa ndoto lakini ule ulikuwa UTAMU MTUPU…..



Sema ilikuwa noma sana maana nilitaniwa sana hadi shule nzima ikajua kuwa niliota nafanya mapenzi nikashtuka nishajimwagia tayari!!!



MWISHO!!
 
VUNJA UKIMYA









1st year



nikiwa nimekaa leacture room nikimuangalia msichana aliyekaribu yangu,niliyekuwa nikimuita "Bestfriend"nilikuwa nikimuangalia nywele zake nzuri na sura yake ya upole huku nikitamani awe wangu,lakini yeye hakuwa akitamani hilo na nilikuwa nikilitambua hilo.



Baada ya leacture,alikuja kwangu na kuniomba notes za siku ya nyuma kwa sababu hakuweza kuingia darasani hiyo siku iliyopita.baada ya kumpa akasema "asante" na kushikana mikono na mimi.I wanted to tell her,i want her to know that i don't want us to be just friends,i love her but i'm just to shy,and i don't know why







2nd year




Simu yangu iliita,kupokea alikuwa yeye alikuwa akilia akinielezea jinsi gani boyfriend wake broke her heart,she asked me to come over because she didn't want to be alone,kwa kuwa ni rafiki yangu kipenzi ilinibidi kwenda kumfariji,as i sat next to her on the sofa,nilikuwa nikimuangalia Machoni nikitamani awe wangu.Baada ya masaa mawili baada ya kuangalia nae movie mbili tatu na kula nae chakula pamoja akarudi katika hali yake ya kawaida,hivyo akaamua kwenda kulala,before akaniangalia na kuniambia "asante" na kunipa tabasamu tamu,i want to tell her to know that i don't us to be just friends,i love her but i'm just too shy,and i dont know why.





3rd year




Siku moja kabla ya Tamasha la muziki chuoni alikuja kwenye meza yangu leacture room na kuniambia "Boyfriend wangu amepata udhuru hivyo naomba unipe campan katika tamasha la muziki leo usiku" kwa kuwa tuliwekeana promice kwamba ikitokea kila mmoja wetu amekosa mtu wa ku-date nae basi tutaenda pamoja just as "bestfriends".hivyo tukaenda.



katika tamasha baada ya kila kitu kuisha na muziki kufungwa,nilikuwa nimekaa nje ya ukumbi nikimuangalia jinsi alivyokuwa akicheka na rafiki zake,she saw me looking to her she smiled at me,i want her to be mine lakini yeye alikuwa hafikirii hilo kabisa na nilikuwa nikilitambua hilo,then she said to me "nimekuwa na muda mzuri na wewe asante sana" and she gave me a sweet smile.I want to tell her to know that i don't us to be just friends,i love her but i'm just too shy,and i dont know why.





Graduation Day

siku,wiki kisha mwezi ukapita ilikuwa ni mahafali yetu tukimaliza masomo ya chuo,akiinuka kwenda kutunukiwa shahada yake ya uchumi nilikuwa nikimuangalia akiwa amependeza sana siku ile,i wanted her to be mine,but she didn't notice me like that,and i knew it.



kabla watu hawajatawanyika kwenda makwao,alikuja kwangu akiwa na vazi lake la mahafali,na kulia pale nilipomkumbatia akainua kichwa chake na kuniambia "you are my bestfriend asante sana" i want to tell her to know that i don't us to be just friends,i love her but i'm just too shy,and i dont know why.



Miaka michache baadae



Nikiwa kanisani Yule Msichana akiwa anaolewa sasa,nilimuangalia akisema "ndiyo nakubali " and drive off to new life,kaolewa na mwanaume mwingine,i wanted her to be mine,but she didn't see me like that,and i knew it.



but before she drove away,alikuja kwangu na kusema "asante sana" and kissed me on the cheek.I want to tell her to know that i dont us to be just friends,i love her but i'm just too shy,and i dont know why.





Kwenye Mazishi



Miaka ilipita i looked down katika jeneza lilokuwa na msichna ambaye alikuwa ni "bestfriend" wangu,Katika Service ya mazishi wakasoma diary ya Bestfriend ambayo alikuwa akiiandika enzi za maisha ya chuo'



Diary yake ilikuwa Ilikuwa ikisomeka hivi




I stare at him napenda awe wangu,but he doesn't notice me like that,and i know it,i want to tell him,i want him to know that i dont want us to be just friends,i love him but i'm just to shy,and i dont know why.I wish he would tell me he loved me!



Nilipiga magoti huku nikilia nikijisemea moyoni i wish ningemwambia tu ukweli,nimeshachelewa sipo nae tena katangulia mbele za haki i cried!!



Share it up if it's touched your heart
 
CHOZI LA MAMA









SIMULIZI FUPI - CHOZI LA MAMA





KILA mmoja alimpa jina alijualo yeye. Wengine wakimuita kichaa mgeni, wengine chizi freshi na mengineyo mengi kulingana na wakati. Hakuna aliyejua wapi anatoka, lakini alikuwa katika kundi la vichaa pale mjini. Aliokota makopo na kuzurura nayo, alikula majalalani akigombea chakula na mbwa koko, Mungu alimwepusha na magonjwa na kumfanya acheke peke yake kila mara. Alipokasirika aliponda watu mawe, lakini licha ya hasira hizo baada ya miezi kadhaa akagundulika kuwa ni mjamzito.



Ikawa skendo mjini kumfahamu ni nani muhusika wa dhambi ile kwa mtu asiyekuwa na akili timamu. Hakupatikana!! Maisha yakendelea. Ilingojewa miezi tisa ifike aweze kujifungua ili atafutwe mchawi nani. Lakini hata miezi tisa haikufika ile mimba ikatoka, huku dhahiri shahiri yule kichaa akionekana kupitia maumivu makali. Wananchi wakanong’ona kimya kimya kuwa aliyemjaza mimba, amemvizia na kumlisha madawa makali hatimaye ile

mimba imetoka.



Hilo nalo likasahaulika. Ikapita miezi mingine miwili, akapata mimba tena yule mwanamama ambaye nyumba yake ilikuwa popote pale pasipofaa kukaliwa na mwanadamu wa kawaida. Kama ilivyokuwa awali watu walilaani kitendo hicho alichofanyiwa kichaa mgeni. Mimba ikaanza kukua, lakini hata hii haikufikisha miezi tisa, ikatoka kama ile mimba ya awali. Lakini hii ilikuja katika mtindo wa aina yake. Kichaa mgeni alizungumza kitu kwa sauti isiyokuwa ya kwake. Alizungumza mambo ambayo kila mmojaalibaki na maswali lakini wengi wakipata majibu.



MWAKA MMOJA NA NUSU ULIOPITA. MARIA akiwa amejipumzisha na mume wake asiyekuwa wa ndoa wala wa kutambulika popote bali waliishi uhawara na hatimaye kuzoeana. Wakaitana mume na mke lakini wakiwa hawana mtoto. Ugeni ukawajia siku hiyo, mwanamke mnene mfupi mweusi mwenye macho mekundu alikuwa akingoja nje baada ya mlinzi kumwambia subiri hapo. Maria alitoka akiwa ameongozana na mume wake wakiwa wameshikana viuno katika mtindo wa mahaba. “Nikusaidie nini?” aliuliza Christian ambaye ni mume wa Maria. Yule mama mwenye macho mekundu alijaribu kutabasamu na mdomo wake kufunguka, alikuwa na mapengo, meno ya mbele yote hayakuwa kinywani. Maria alimtazama kwa makini huku akiizuia hali ya kutaharuki iliyotaka kumtwaa. Mama yule mzee alikuwa na mtoto mgongoni. Bila shaka hakuwa mtoto wake labda mjukuu tu. “Wankuru haujambo..” alizungumza yule mama huku akimtazama usoni. “Wankuru nd’o nani tena..” Chris aliuliza huku akimtazama Maria. “Hata mimi nashangaa, ama amekosea nyumba.” Alijibu Maria kwa hofu!! “Wankuru umependeza wee mwanangu, yaani nilijiuliza kama ningeweza kukupata. Tangu nipoteze namba yako basi nimeshindwa kabisa kukweleza lolote. Hivi ukimuona Gilbert utamkumbuka kweli Wankuru wangu.”



Alizungumza kwa furaha na hakuona haya kuyaonyesha mapengo yake, wakati huo uso wake ulikuwa unavuja jasho. Miguu iliyopauka na nguo zake hazikuwa safi. “Maria unamjua…” Chris aliuliza. Maria akakana kwa mara nyingine. Lakini mama yule aliendelea kuzungumza kwa furaha akisimulia mambo kadha wa kadha. “Mama samahani..kwani unamtaka nani?” aliuliza kwa ghadhabu kidogo Chris. Mama yule akamtazama kwa mshangao. “Mama nimekuuliza unataka tukusaidie nini?” alikazia sasa. “Nimekuja kwa mwanangu, nimemleta mjukuu wangu amwone mama yake. Kwani kuna ubaya…..” akamgeukia Maria, “Wankuru eeh kuna kosa nimefanya mwanangu eeh” aliuliza kwa kubembeleza huku akijitoa katika hatia. “Huyu ni nani Maria na huyo mtoto ni wa nani.” Alihoji Chriss. Maria akajitoa utimamu wake na sasa akawa mbogo. “Kwa hiyo Chris unadhani namjua huyu mwanamke ama. Hivi hujui unaweza kurogwa hivihivi, unamuona mtu wa kawaida huyu!! Chriss unamuona wa kawaida huyu, mtazame macho yake mekundu na hicho kitoto maskini sijui amekirogea wapi kakichukua…ametolewa kafara meno yake na bado watamtoa na huyu mtoto maskini weee!!” alifoka. Maneno yakamwingia Chriss.



Yule mama akapigwa na butwaa macho yakamtoka na akazidi kutisha kumtazama. Chriss akaingiwa na maneno ya Maria akamwamuru mlinzi amwondoe yule mama nje. Mlinzi akatii, Maria na Chriss wakakokotana kurejea ndani. Nafsi ya Maria haikuwa katika utulivu hata chembe, alimtambua yule mama ipasavyo, alikuwa ni mama yake mlezi baada ya mama yake mzazi kufariki, mama huyu alimfanyia mengi sana yasiyostahili malipo yale. Maria alitambua kuwa kwa kukiri kuwa yule alikuwa ni mtoto wake wa kumzaa basi ule ulikuwa mwisho wa mahusiano na mwanaume yule ambaye anatambua kuwa Maria hajawahi kuzaa na hana ndugu wa karibu sana baada ya wazazi wake kufariki na yeye kukimbilia jijini Mwanza kutafuta maisha. Wakati akiwaza hayo Maria kwa mbali kabisa akakisikia kilio cha yule mama aliyekuwa anaomboleza. “Wankuru…Wankur u, unanikana mimi mbele ya hadhara, unanikana Wankuru, yaani umesahau nilivyokulea mimi, macho yangu mekundu haya si ni kwa sababu yako Wankuru yaani nimepika pombe za kienyeji ili usome Wankuru, nimechochea kuni na kujiharibu ngozi, kifua na macho yangu leo hii unasema mimi mchawi nataka kukuroga Wankuru, uuuuwi!!!



Wankuru ukabeba mimba huko kila mtu akakukimbia nimekutunza kwa shida, mume wangu akanipiga hadi kunitoa meno Wankuru leo hii nimekuwa kituko, unasema nimetolewa meno yangu kafara kweli Wankuru. Wankuru ukazaa mtoto, ukanidanganya kuwa unaenda nje mara moja kumbe unamkimbia mwanao, nimekukuzia mtoto Wankuru, nimemtunza kwa mapenzi yote mimi. Si nilikwambia mama yako alitaka atoe mimba yako kutokana na shida, nikamwambia nitamuhudumia asikutoe na akuzae ukue, nimekulindia uhai wako tangu upo tumboni mwa mama yako, nikakupenda kuliko mama yako mzazi leo hii nimekuwa ombaomba, unanikana mimi na damu yako unaikana Wankuru. Wankuru uuuwi!! Chozi langu la mwisho nilidondosaha siku ile yule mwarabu aliyekupa mimba alipokupiga na kusema hakujui, nilitoa chozi hilo kwa sababu ya kukupenda Wankuru, nikalia na kumlaani yule mwarabu kama kweli anaikana damu yake Wankuru. Ulikuwa shahidi wankuru, tulipolala njaa ulinisikia nikikimbilia kwa Mganga, niliwahi kukufunga hirizi Wankuru!!



Watu waliponiita mchawi nilikwambia Mungu atatulinda na malipo ni hapahapa. Yule mwarabu yupo wapi sasa! Wankuru muogope Mungu we mtoto, Wankuru majibu ya Mungu ni ya kweli hayaongopi. Nimemtumikia tangu usichana wangu hadi leo haongopi, hajanipa mamilioni ya kung’ara ili unipokee katika nyumba yako nzuri lakini amenipa moyo wa huruma moyo wa mama. Wankuru sio kwamba nilikupenda kisa tu sijapata mtoto, nilikupenda kwa sababu ulikuwa umetengwa na kila mtu. Sasa umempata mtu wa kukupenda umesahau kila kitu na leo kwa mara nyingine nadondosha chozi. Namlilia Gilbert kwa uchungu kwa sababu atakutana na akina Wankuru wenye roho mbaya na akili nyepesi ya kusahau. Watamkana na kumnyanyasa, lakini hatakuwa kama wewe Wankuru, hatakuwa mwepesi wa kusahau. Atamtegemea Mungu na utakuja kumkumbuka.



Chozi hili halitatua chini na kumezwa na ardhi burebure, Mungu ninayemuamini si Mungu wa kisasi lakini atanisuuza moyo wangu na kunionyesha uwepo wake tena. Chozi hili na litue katika utosi wa kichwa chako!! Kichwa chenye nywele bandia zinazoogopa maji ya kijijini kwetu, maji ya chumvi. Chozi hili langu la mwisho hapa duniani liwe chozi lako kwa lolote utakalopitia. Yaani unamkana mwanao uliyemzaa, Wankuru yaani mimi nilivyolilia mtoto miaka arobaini yote na nisimpate wewe umempata huyu mtoto mtiifu wa kiume unamkana, unamkataa katakata mbele yangu. Wankuru usipomkumbuka Gilbert, Mungu wangu hayupo hai!!!! Naondoka na Gilbert, kama nilivyojikongoja hadi kufika huku, nikitukanwa na wakati huohuo nikikutana na wachache wa kunifariji, nikiitwa mchawi na wapumbavu kama wewe, lakini wapo wachache walioniita mkarimu.



Narejea nikiamini wale wanaoutambua ukarimu wangu watanipokea, sitaishi miaka mingi lakini walau nimeishi umri wa kukukuza na kumkuza mwanao. Naenda Wankuru naenda ..” kilio kilikomea pale, Maria alijiwekea tabasamu bandia lakini moyo ukiteketea. Alitambua kuwa ni yeye aliyeitwa wankuru, Maria ni jina lake la mjini tu ambalo Chriss alilitambua. Chris pasi na hili wala lile akamliwaza mkewe huku akimwomba msamaha kwa yote yaliyotokea. Maria akapitiwa na usingizi. Siku iliyofuata akafunga safari kuelekea kijijini kwao, alitegemea kumkuta mama huyo kule, amwombe msamaha na kujirudi. Lakini mwangu wa kilio chake ukamvuruga, akapanda basi asifahamu linakwenda wapi, alijitahidi kuiweka akili yake sawa lakini hakujielewa hadi akajikuta mjini Dodoma. Alishuka kama Maria, lakini baada ya masaa kadhaa akageuka kuwa KICHAA MGENI. Hakuna aliyemjua.



Akajazwa mimba ya kwanza na haikudumu kuzaa kiumbe chochote, akajazwa ya pili na mtu asiyefahamika. Ni katika mimba hii alizungumza mambo mengi sana yaliyomfanya hadi afike hapo. Labda alipewa akili ndogo ya mwisho ya kusema ili watakaojifunza na wajifunze. Wasamaria wakahitaji kumsaidia, wakajipanga kwa ajili ya siku iliyofuata wamchukue Maria. Lakini hakuwa Maria tena…..alikuwa hayati Maria. Alikuwa mfu!! Na hakupatikana ndugu wa kumzika. Maiti yake yakazikwa na manispaa!! Aliishi maisha magumu, akampata mwenye upendo akamtunza, watu wabaya wakamjaza mimba bado yule mtu mwenye upendo hakumtelekeza, akazaa na kutelekeza mtoto lakini mtu mwenye upendo akatunza kiumbe. Maria akageuka na kulikana jina lake alipokuwa mjini, akamkana hata yule mtu mwenye upendo akamkana na mtoto wake!!! CHOZI LA MAMA likaishi katika utosi wake, Mungu akamwadhibu Maria kadri ya kilio cha mama yule!!



Mama mkarimu hakufa mapema aliishi!! Akakitunza kiumbe kinachoitwa Gilbert kwa hekima zote, kikakua wasamaria wakasaidia kikasoma. Na hata kilipofikisha umri wa kujitambua, kikiwa darasa la tano. Mama mkarimu akatokwa na uhai huku akitabasamu!!!



UJUMBE:

1. MAMA ni kiumbe cha kipekee, hupaswi kumsaliti mama yako….

.itunze ahadi kama yeye aliyekutunza kwa miaka mingi bila kuvunjika moyo.



2. STAREHE ZA MUDA MFUPI zisikufanye uwasahau uliosota nao kwa miaka lukuki.



3. MUNGU hujibu!! Muamini yeye sasa.



MWISHO!!!!
 
Back
Top Bottom