TANZIA Buriani Abbas Kleist Sykes

LGF,
Nadhani umekusudia, ''belatedly.''
Nakuitikia, ''Minalfaizin.''

Kitabu changu unakikosea jina kila siku unapokitaja.

View attachment 1789746
Sheikh Mohamed Said: ukiambiwa MINALFAIZIN unajibuje? Nina kitabu kinaitwa Teach Yourself Arabic nilinunua duka la Foyles liko Tottenham Court Road lakini hakikunisaidia. Kuna cha Sheikh Muhsin nilinunua pale Hindu Mandal nacho pia hakikunisaidia. Can you help?

Back to your point, I know the actual name but it is such a mouthful!! It's like ulikuwa na harakaharaka, kwa lugha ya siku hizi fastafasta, ulitaka Msomaji apate message palepale, kitaalamu (academic publishing) huitwa fuzziness au wishywash. Iwapo ningepewa mie kufanya moderation ningekata title yabaki maneno mawili tu: ABDULWAHEED SYKES. He was a great man, kingeuzika tu.

I am of course not talking about the Kiswahili translation, hicho babangu ulikichakachua (sijui walikufunza nini IFM); ningekuwa mie ningekushitaki kwa copyright infringement.

Kazi iendelee, naona umekwaa kisiki cha mpingo sijui utajinasuaje. Hoja ya huyo Bob ni kujikweza kwako na eneo lako dogo kana kwamba uhuru wa Nji hii umeletwa na Manyema wa Tandamti. Ila, ole wake akirogwa aanze kukikosoa kitabu, hapo Nduguzo tupo tutakutetea.
 
LGF,
Ahsante ndugu yangu.
Hufurahi kukusikia.
 
Yamekwisha yapi?

Na kwa nini unafikiri umefikia kuwa na uwezo wa kuniudhi?

Kwa nini unageuza mjadala kutoka mambo ya hoja kwenda mambo ya hisia?
Kiranga,
Basi ndugu yangu.
Niwie radhi.
 
Mtoto wa upanga vs kariako hiyo
Tunawafatilia tu wote mko njema kutetea hoja

Ova
 
Mtoto wa upanga vs kariako hiyo
Tunawafatilia tu wote mko njema kutetea hoja

Ova
Mrangi,
Mimi sina cha kutetea wala siingii katika ugomvi.

Ninapoona mtu kahamaki hurudi nyuma.

Ndiyo unaona nimemtaka radhi ndugu yangu.

Nimeandika yamesomwa basi.

Umependa kuamini sawa hukupenda sawa kwangu.
 


Disrespect invites Disrespect,

You can dwell with it in whatever language Of your choice, but we are putting this in the shortest term known to us,...'You are an idiot',and you don't know that you are...

Infact Mohamed Said had HAPA amekuheshim Sana,lkn imekuwa ni mtu uliokosa kuelewa,mtu mwenye maneno ya reja reja na usiokuwa na hoja ya msingi,

Tulidhan kuwa ungekuja na hoja ya kupinga kuwa haya yaliyoandikwa kuhusu hawa wazee wote waliokawa hawajaandikwa kuwa ni uongo,uzush na usio na ushahid,sasa Cha AJabu wewe unatuambia kuwa tunalalamika kwa kuendelea kuishikiza history ya hawa wazee ubavun mwa nyerere,na kwamba tunazid kumpa coverage nyerere,sasa hiyo kweli ni hoja unayotakiwa kujibiwa?,who are you,who are you trying to tell Mohamed Said what to write,who are you trying to tell Mohamed Said what to edit,unatuandikia kiingereza kiingi ili ikibid eti tukuelewe kwa lugha hiyo unasema,Kwan sisi waingereza?,Ili tukuone labda ni intellectual and ofcourse you are but who the hell are you?., Astonishing...

Come and criticize kuwa hii history ni ya uongo kwa hoja ili hadhira ikuelewe,Ila kuja na kusema Mara ooh watu wanalalamika,ain't nobody is complaining, sijui why history ya Sykes nyerere anapewa coverage kubwa ni nonsense and stupidity,don't you be ridiculous,nyerere aliish na wale wazee,unawaseparate vip kwenye kuandika mapito yao??mnaumia si ndiyo?hampendi kuona au kuskia ni namna gan hawa wazee mliowafuta walivyokawa close na nyerere?you must be so so crazy not to Understand this...
 
Muddy,kubali makosa usonge mbele
 
Anochoamini Mohamed ni kuwa bila familia ya Sykes na watu wa Kariakoo Tanganyika isingepata uhuru hataki kujua;

Michango ya viongozi kutoka majimbo mengine ya Tanganyika,

Hatuwezi kubeza akina Sykes lakini Nyerere alikuwa na talanta ya uongozi na maarifa laa sivyo wazee wake wangefanya wenyewe.
 
Hujajibu hoja umekuja na viroja.

Hoja ni kwamba hamjui mnataka nini.

Mnalalamika wazee wenu wamefunikwa katika historia, anasifiwa Nyerere tu, wakati wazee wenu ndio waliomkaribisha kigoda Nyerere mjini, wakamlisha na kumvisha mpaka akachukua nchi.

Halafu siku anafariki mzee wenu, mnamuandika Nyerere kuliko mzee wenu.

Yani hata kama mtu anakubali Nyerere aliwafunika wazee wenu kwa makusudi, nyie wenyewe mnaendelea kuwafunika hao wazee wenu na kumpaisha Nyerere miaka 21 baada ya Nyerere kufariki.

Sasa hizi habari za tazia ya Abbas Sykes iliyoandikwa na Mohamed Said kuwa imejaa jina la Nyerere kuliko la Abbas Sykes miaka zaidi ya 21 baada ya Nyerere kufariki mtamlaumu Nyerere hapo?

Tazia hii imeandikwa na makuwadi wa Nyerere?

You are contradicting yourselves.
 
Nyerere alijaaliwa maarifa
Waku...
Historia ya TANU Nyerere alipopanda kwenye jukwaa na kuwaeleza Watanganyika kuwa tunadai nchi yetu hali ya siasa ilibadilika nchi nzima ila hakufanya haya peke yake.

Abdul Sykes alijenga idara madhubuti ya propaganda na uhamasishaji.

Ilikuwa siku kabla ya mkutano Mnazi Mmoja kinafanyika kikao nyumbani kwake Mtaa wa Stanley kupanga namna ya kuujaza uwanja.

Abdul ndiye aliyewaingiza akina mama TANU na nyimbo zao za lelemama.

Hali ilikuwa hivi kote mikoani kulikuwa na watu na mimi baadhi yao nilibahatika kuzungumzanao na nilichuma mengi - Yusuf Olotu, Mmaka Omari, Joseph Mhando, Bilali Waikela, Haruna Taratibu, Msham Awadh, Suleiman Masudi Mnonji, Salum Mpunga, Yusuf Chembera kwa kuwataja wachache.
 
Kijana,kejeli na matusi ya nini?just argue don't shout!Hoja kapewa Muddy povu utoe wewe.
 
Kwanini Sykes hakwenda yeye ili historia imtambue barabara?
Waku...
Unakusudia kwanini Abdul Sykes hakwenda yeye UNO.

Nitakueleza In Shaa Allah lakini nitaanza na hili la historia imtambue.

Abdul Sykes na ukoo mzima ulikuwa unatambulika sana.

Baba yao ndiye aliyeasisi African Association 1929 na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika 1933.

Vyama muhimu katika kuja kuunda TANU 1954.

Ali Mwinyi Tambwe wakati ule ndiye alikuwa Katibu wa AA na Abdul Sykes TAA Act. President na Secretary.

Abdul Sykes, Hamza Mwapachu na Ali Mwinyi Tambwe ndiyo kamati iliyoamua kuwa Nyerere aingizwe kwenye uongozi wa AA 1953 na 1954 TANU iundwe na Nyerere aongoze harakati za kudai uhuru.

Kuanzia mwaka wa 1952 juhudi zilianza kwa ushauri wa Earle Seaton kupeleka ujumbe UNO na michango kwa ajili ya safari hii ilianza kukusanywa na Kamati ya Saadan Abdu Kandoro, Japhet Kirilo na Abbas Sykes.

Hivi ndivyo ilivyokuwa mwaka wa 1955 Nyerere akiwa Rais wa TANU akaenda UNO.
 
Mambo ya et al kwenye research paper , au adili na nduguze, wapi Steve bico kwenye jukwaa la Nelson Mandela hii haishangazi
 
Ndugu zanguni nimeandika kitu kidogo:

"Hukaa mara nyingi sana nikajiuliza na si katika kujipigia tarumbeta bali ni katika kufikiri kuwa ingekuwaje kama Kleist Sykes asingeandika historia ya maisha yake kabla ya kufariki kwake mwaka wa 1949.

Mzee Kleist katika mswada wa kitabu alioacha kaeleza mambo mengi kuanzia jinsi baba yake na vijana wenzake wa Kizulu walivyochukuliwa na Hermann von Wissman kutoka kijiji cha Kwa Likunyi Mozambique hadi Pangani kama askari mamluki kuja kupigana na Abushiri bin Salim Al Harith na Mtwa Mkwawa.

Mzee Kleist akaeleza pia jinsi alivyokutana na Dr. Kweggiyr Aggrey mwaka wa 1924 na kumshawishi kuasisi African Association (AA).

Kutokana na mswada huu wa Mzee Kleist ndipo hii leo tukayajua majina yote ya waasisi wa AA.

Hii AA ndiyo ikawa TAA mwaka wa 1948 mwaka mmoja kabla ya kifo cha Kleist Sykes na mwaka wa 1954 ikageuzwa na kuwa TANU chama cha kupigania uhuru wa Tanganyika.

Katika kuundwa kwa TANU mwaka wa 1954 watoto wote watatu wa Mzee Kleist walihusika, wawili, Abdulwahid na Ally wakiwa wajumbe wa mkutano wa uasisi wa chama na Abbas wakati ule akiwa kijana mdogo akiwa nje ya chumba cha mkutano akisubiri kutumwa kufanya hili na lile katika shughuli za mkutano ule.

Lakini hadi TAA kufika pale ilipofika kuasisi TANU kupigania uhuru wa Tanganyika, mchango wa Abdul na Ally Sykes haumithiliki.

Hauna kifani si tu kwa kuwa walikuwa wafadhili wakuu bali Abdul Sykes ndiye aliyempokea Julius Nyerere na kumweka katika uongozi wa TAA mwaka wa 1953 na mwaka unaofuatia TANU ikaundwa.

TANU imeundwa ndani ya jengo ambalo lilijengwa kila siku ya Jumapili kati ya mwaka wa 1929 hadi 1933 kwa wanachama kujitolea nguvu zao.

Mipango yote ya kuendea kuunda TANU ilikuwa ikifanyika nyumbani kwa Abdul Sykes Mtaa wa Stanley na Sikukuu.

Hii ndiyo nyumba Julius Nyerere alikuja kuishi mwaka wa 1955 baada kuacha kazi ya ualimu.

Abdul Sykes anaeleza anasema kuwa yeye alipokuwa mtoto baba yake alikuwa akimchukua kwenda pale New Street ulipokuwa unafanyika ujenzi ule na ameona kwa macho yake lile jengo likijengwa.

TANU ilipoundwa kadi 1000 za mwanzo zilinunuliwa na Ally Sykes na kadi no. 1 ya TANU Ally Sykes alimwandikia TANU Territorial President Julius Kambarage Nyerere no. 2 akajiandikia mwenyewe na no. 3 akamwandikia kaka yake Abdulwahid, kadi no. 4 Dossa Aziz, kadi no. 5 Denis Phombeah, kadi no. 6 Dome Okochi Budohi na kadi no. 7 akamwandikia mdogo wake Abbas na kuendelea na wengineo.

Nini ikimetokea hadi historia ya TANU ikawa imeandikwa na haya yote yakawa yamefutwa kiasi kuwa hadi hivi ninavyoandika TANU yenyewe chini ya uongozi wa Julius Nyerere hadi kufikia CCM chini ya Nyerere ikawa haitambui historia hii?

Abdul Sykes amefariki mwaka wa 1968 maziko yake yalihudhuriwa na umma wa watu wa Dar es Salaam si kwa sababu ya TANU bali kwa umaarufu wake binafsi.

Magazeti ya TANU The Nationalist na Uhuru hayakuandika taazia wala kueleza kuwa marehemu alikuwa na mchango mkubwa katika kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.

Ally Sykes kafariki mwaka wa 2013 CCM haikushughulika kwa lolote kueleza mchango wake katika kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.

Mimi ndiye niliyesimamishwa pale nyumbani kwake Mbezi Beach kumzungumza Ally Sykes na mchango wake katika kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.

Hapakuwa na rambirambi kutoka CCM.

Maziko ya Abbas Sykes yamefuata mkondo ule ule wa kaka zake wawili.

Kazikwa na ndugu zake watu wa Dar es Salaam.

CCM haikuwakilishwa na yeyote ingawa Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete alihudhuria maziko na akawa amekaa pembeni na Balozi Abdul Faraj, rafiki ya Abbas Sykes toka utoto wao.

Inakuwaje CCM inaikataa historia yake yenyewe?

Hii nini maana yake?

Kipi kisichopendeza katika historia ya kina Sykes?

Ni kuwa baba yao kaasisi harakati au ni kwa kuwa Abdul Sykes kampokea Nyerere?

Kipi hasa kisichowapendeza?

Juu ya haya yote Rais Kikwete katika kusheherekea miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika aliwatunuku Abdul na Ally Sykes, ''Medali ya Mwenge wa Uhuru,'' kwa mchango wao katika kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika."
 
Unajua Ndugu, huyu Mzee ni Mtu wa kujikweza sana, Mdini na pia ni Mtu mwongo na nilishamuainishia uongo wake mara kadhaa hapa jamvini

Aliwahi kusema wakati wa Urais wa B.W Mkapa eti waislam waliokuwepo bungeni ni 2% tu. Mpaka pascal Mayala alipomuumbua

Sasa badala ya TANZIA anatuletea historia yake
 
Wewe unaelewa hata hoja yangu ni ipi?

Au unalalama tu bila hata kutaka kuelewa hoja yangu ni ipi?

Unaandika kwa kufuata mantiki ya kujibizana kwa kumsoma mtu na kumjibu hoja zake?

Au unajiandikia unachotaka wewe tu bila kujibu hoja unayoletewa?
 
Shukran zangu kwako Mudeer,

Endelea kutupa yasiyo julikana,wanaoendelea kukunja sura eti KWA kusema kwann history hii ni wazee wetu Ila anatajwa nyerere na wanataka majibu katika swali kama hilo ni wa kupuuzwa,hawajui wanataka kitu gan,sasa wewe utawajibu kitu gan?

Ilichukua takriban miez sita ndan ya jukwaa hili hili ukitupa maarifa ya juu ya masuala haya,hawa sijui walikuwa wapi??

Wanadhan wewe ni mtu wa mchezoo mchezoo,Allah kakujaalia haya,kwann ww uyafiche,kikaz hiki na kijacho kitafaham vipi haya?... Jazakallahu khair
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…