naona anachokifanya bagamoyo ni kuleta balance ya ambacho umekuwa ukiongea humu siku zote
Kusema Martin alikuwa kibaraka ni kitu cha kutegemewa maana familia yake hadi yeye mwenyewe walifaidika na ukoloni kama elites wa mwanzoni wa Tanganyika hivyo, isingekuwa rahisi kuaminika kama angekuwa na nia thabiti ya kuupinga ukoloni. Kwangu naona ni kawaida kwa watu wa tabaka jingine kuwa insecured
Pia naamini wewe ni picha halisi ya waliokulea katika kukipigania kile unachokiamini hivyo, sitegemei kwa njia yoyote ile kama waliokutangulia kumuongelea Martin katika mlengo chanya kwa kiasi kikubwa
Nadhani ungetusaidia sana kama ungeweka wazi kwamba huyu Martin hakuwa na mchango wowote katika kuanzisha vuguvugu za ukombozi wa Tanganyika au la
Kumuita kibaraka yaweza kuwa out of context kwa kinachojadiliwa maana hata katika awamu iliyopita kuna madaktari, wanasiasa na wafanyabiashara waliitwa majina hayo kwa kusimamia wanachokiamini.
suala kuu ni mchango wake
Maso...
Ukoloni una mambo yake.
Wajerumani waliwaweka askari wao katika kambi.
Watoto wa askari hawa wote wakizaliwa katika hospitali na hapo wanaandikishwa na kupewa majina.
Mjerumani alikuwa anawapa watoto wale majina ya Kijerumani.
Lakini baba akifika nyumbani anatoa jina la Kiislam.
Watoto wanakuwa na majina mawili.
Kleist jina hili kapewa na Wajerumani na nyaraka zake zote zina jina hilo.
Sasa alipofikishwa nyumbani aliadhiniwa na kupewa jina la Abdallah.
Halikadhalika Schneider jina lake Abdillah.
Kaburi la Mzee Kleist jina la Abdallah liko pale.
Kaburi la Abbas Sykes limewekwa ''initial A,'' yaani Abdallah.
View attachment 1789637
Sheikh Mohamed Said: ukiambiwa MINALFAIZIN unajibuje? Nina kitabu kinaitwa Teach Yourself Arabic nilinunua duka la Foyles liko Tottenham Court Road lakini hakikunisaidia. Kuna cha Sheikh Muhsin nilinunua pale Hindu Mandal nacho pia hakikunisaidia. Can you help?LGF,
Nadhani umekusudia, ''belatedly.''
Nakuitikia, ''Minalfaizin.''
Kitabu changu unakikosea jina kila siku unapokitaja.
View attachment 1789746
Back to your point, I know the actual name but it is such a mouthful!! It's like ulikuwa na harakaharaka, kwa lugha ya siku hizi fastafasta, ulitaka Msomaji apate message palepale, kitaalamu (academic publishing) huitwa fuzziness au wishywash. Iwapo ningepewa mie kufanya moderation ningekata title yabaki maneno mawili tu: ABDULWAHEED SYKES. He was a great man, kingeuzika tu.
I am of course not talking about the Kiswahili translation, hicho babangu ulikichakachua (sijui walikufunza nini IFM); ningekuwa mie ningekushitaki kwa copyright infringement.
Kazi iendelee, naona umekwaa kisiki cha mpingo sijui utajinasuaje. Hoja ya huyo Bob ni kujikweza kwako na eneo lako dogo kana kwamba uhuru wa Nji hii umeletwa na Manyema wa Tandamti. Ila, ole wake akirogwa aanze kukikosoa kitabu, hapo Nduguzo tupo tutakutetea.