TANZIA Buriani Abbas Kleist Sykes

Huyu Mohamed Said anajua sana kusimulia mambo. Hongera zake kutujulisha yaliyopita

Unamvika sifa isiyo yake,Shekh Said ni mtu wa kujisifu na kuwasifu watu wa deen yake.

Akikusimulia kuhusu Mwl Nyerere robo tatu ya simulizi zitahusu Wazee wake wa Kariakoo.Robo nyingine zitahusu mihadhara yake yeye halafu page mbili za mwisho atamtia Mwl Nyerere kiduchu.
 
Sijaona kosa lake.. Ndio aina ya uandishi wake.. Anakuchota, unajikuta unakubali stori unayopewa unapewa na mtu mwenye kujua mengi sio kubabia babia.

Hayo ni mambo ya kifasihi zaidi.
 
Umesoma literature?
 
inalilah wainailah rajiun

Allah ampe makazi mema peponi.
 

Wenzie hao kina nan??

Shida yako umekariri,kwamba anavyoandika fulan tanzia basi lazima na mwingine aandike hivyo hivyo,hiyo umeskia wapi?

Mohamed Said ni scholar,na anawafaham personally hao watu anaowazungumzia,ni lazima aweke kumbu kumbu za history sawa Ili kizaz baada ya kizaz ipate kujifunza,tulia watu wapate elimu ww
 

Husda,chuki,wivu na roho ya nyongo tuh imekujaa,huna lolote...

Kama ww unajua basi andika tanzia au eleza unayoyafam km anavyoelezea Mohamed Said Ili tuone uhalisia wa hicho unachokisema,dini yake ww inakuchoma choma kwanin?wewe pia si unayo dini yako?unaongea ujinga ujinga kama mwanamke unaetafuta ndoa kwa nguvu jamaa,
 
Hiyo ni style yake ya uandishi,ni nzuri sana anakuhamisha msomaji kifikra unajiona na wewe ulikuwa Dubai,ulikuwa kwenye ndege iliyobeba mwili wa mwalimu nk.

Unaweza kuona anajimwambafai lakini si kila mwandishi anaweza kuandika hivyo,hicho ni Kipaji Cha kipekee.

RIP Balozi Abbas Sykes,naona Sykes brothers washaisha.

Pole Dully Sykes na ndugu wengine.
 
R.I.P Amb. Sykes.

Mimi naona tatizo tazia ya Sykes inapomuandika Nyerere kuliko Sykes.

Na hata Sykes anapoandikwa anaandikwa kama mtu ambaye hakuwa na maisha yake nje ya uhusiano wake na Nyerere.

Yani imekuwa kama Balozi Sykes hajafanya chochote kikubwa nje ya uhusiano wake na Nyerere, na hajafanya lolote tangu Nyerere afariki mpaka leo.
 
Innalillah wainailaih rajiuun.

Mfumo kristo ni hatari sana. Huyu mzee ht kutajwa tu
 
Binafsi nilikuwa sijui km huyu mzee kafariki, nilikuwa naperuzi facebook ndio nikaona post ikisema mzee Sykes ataswaliwa masjid Maamur na kuzikwa kisutu..

Yaani vyombo vya habari vinaandika kwa urefu habari za Sabaya ambaye alikuwa anaongoza wilaya moja tu Tanzania lakini mtu na familia nzima walijitoa katika kuipigania nchi hii uhuru wake ht gazeti moja kumpa front page kuwa mpigania uhuru katutoka hii si sawa.

Sijasikia katika tv,redio japo kutoa taarifa ya wasifu wake katika pumzi yake ya mwisho kuelekea ahera.

Ama kweli Tanzania inaubaguzi mno kwa baadhi ya mambo.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu amsamehe madhambi yake na amweke mahali pema peponi.
 
Ndio uzuri wa Sheikh Mohamed Said. Kutujuza tusichojua. Nampongeza kwa vile hakuna mwandishi mwingine aliyejitoa kutujulisha marejeo ya kale tusiyoyafahamu.
 
Ndugu yangu Mohamed Said,umeweka simulizi nzuri lakini mara zote kama kawaida moyo wako haukubali kama Nyerere alikuwa Rais wa kwanza wa TANU, Tanganyika,Tanzania na CCM.Unaamini kuwa kuna watu wako walistahili,ulitamani leo Hamza (RIP) na Abdul (RIP) ndio wawe wenye kuelezea historia ya nchi hii,unaamini Julius hajui historia ya nchi hii.Ni dhahiri moyo wako unatoa machozi kwani historia haiko kama unavyotaka.Uongozi ni riziki itokayo kwa Mola!
 

Uongozi ni riziki itokayo kwa Mola!

Well said mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…