TANZIA Buriani Abbas Kleist Sykes

TANZIA Buriani Abbas Kleist Sykes

Ndugu zanguni nimeandika kitu kidogo:

"Hukaa mara nyingi sana nikajiuliza na si katika kujipigia tarumbeta bali ni katika kufikiri kuwa ingekuwaje kama Kleist Sykes asingeandika historia ya maisha yake kabla ya kufariki kwake mwaka wa 1949.

Mzee Kleist katika mswada wa kitabu alioacha kaeleza mambo mengi kuanzia jinsi baba yake na vijana wenzake wa Kizulu walivyochukuliwa na Hermann von Wissman kutoka kijiji cha Kwa Likunyi Mozambique hadi Pangani kama askari mamluki kuja kupigana na Abushiri bin Salim Al Harith na Mtwa Mkwawa.

Mzee Kleist akaeleza pia jinsi alivyokutana na Dr. Kweggiyr Aggrey mwaka wa 1924 na kumshawishi kuasisi African Association (AA).

Kutokana na mswada huu wa Mzee Kleist ndipo hii leo tukayajua majina yote ya waasisi wa AA.

Hii AA ndiyo ikawa TAA mwaka wa 1948 mwaka mmoja kabla ya kifo cha Kleist Sykes na mwaka wa 1954 ikageuzwa na kuwa TANU chama cha kupigania uhuru wa Tanganyika.

Katika kuundwa kwa TANU mwaka wa 1954 watoto wote watatu wa Mzee Kleist walihusika, wawili, Abdulwahid na Ally wakiwa wajumbe wa mkutano wa uasisi wa chama na Abbas wakati ule akiwa kijana mdogo akiwa nje ya chumba cha mkutano akisubiri kutumwa kufanya hili na lile katika shughuli za mkutano ule.

Lakini hadi TAA kufika pale ilipofika kuasisi TANU kupigania uhuru wa Tanganyika, mchango wa Abdul na Ally Sykes haumithiliki.

Hauna kifani si tu kwa kuwa walikuwa wafadhili wakuu bali Abdul Sykes ndiye aliyempokea Julius Nyerere na kumweka katika uongozi wa TAA mwaka wa 1953 na mwaka unaofuatia TANU ikaundwa.

TANU imeundwa ndani ya jengo ambalo lilijengwa kila siku ya Jumapili kati ya mwaka wa 1929 hadi 1933 kwa wanachama kujitolea nguvu zao.

Mipango yote ya kuendea kuunda TANU ilikuwa ikifanyika nyumbani kwa Abdul Sykes Mtaa wa Stanley na Sikukuu.

Hii ndiyo nyumba Julius Nyerere alikuja kuishi mwaka wa 1955 baada kuacha kazi ya ualimu.

Abdul Sykes anaeleza anasema kuwa yeye alipokuwa mtoto baba yake alikuwa akimchukua kwenda pale New Street ulipokuwa unafanyika ujenzi ule na ameona kwa macho yake lile jengo likijengwa.

TANU ilipoundwa kadi 1000 za mwanzo zilinunuliwa na Ally Sykes na kadi no. 1 ya TANU Ally Sykes alimwandikia TANU Territorial President Julius Kambarage Nyerere no. 2 akajiandikia mwenyewe na no. 3 akamwandikia kaka yake Abdulwahid, kadi no. 4 Dossa Aziz, kadi no. 5 Denis Phombeah, kadi no. 6 Dome Okochi Budohi na kadi no. 7 akamwandikia mdogo wake Abbas na kuendelea na wengineo.

Nini ikimetokea hadi historia ya TANU ikawa imeandikwa na haya yote yakawa yamefutwa kiasi kuwa hadi hivi ninavyoandika TANU yenyewe chini ya uongozi wa Julius Nyerere hadi kufikia CCM chini ya Nyerere ikawa haitambui historia hii?

Abdul Sykes amefariki mwaka wa 1968 maziko yake yalihudhuriwa na umma wa watu wa Dar es Salaam si kwa sababu ya TANU bali kwa umaarufu wake binafsi.

Magazeti ya TANU The Nationalist na Uhuru hayakuandika taazia wala kueleza kuwa marehemu alikuwa na mchango mkubwa katika kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.

Ally Sykes kafariki mwaka wa 2013 CCM haikushughulika kwa lolote kueleza mchango wake katika kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.

Mimi ndiye niliyesimamishwa pale nyumbani kwake Mbezi Beach kumzungumza Ally Sykes na mchango wake katika kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.

Hapakuwa na rambirambi kutoka CCM.

Maziko ya Abbas Sykes yamefuata mkondo ule ule wa kaka zake wawili.

Kazikwa na ndugu zake watu wa Dar es Salaam.

CCM haikuwakilishwa na yeyote ingawa Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete alihudhuria maziko na akawa amekaa pembeni na Balozi Abdul Faraj, rafiki ya Abbas Sykes toka utoto wao.

Inakuwaje CCM inaikataa historia yake yenyewe?

Hii nini maana yake?

Kipi kisichopendeza katika historia ya kina Sykes?

Ni kuwa baba yao kaasisi harakati au ni kwa kuwa Abdul Sykes kampokea Nyerere?

Kipi hasa kisichowapendeza?

Juu ya haya yote Rais Kikwete katika kusheherekea miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika aliwatunuku Abdul na Ally Sykes, ''Medali ya Mwenge wa Uhuru,'' kwa mchango wao katika kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika."

20210522_074200.jpg
 
Wewe unaelewa hata hoja yangu ni ipi?

Au unalalama tu bila hata kutaka kuelewa hoja yangu ni ipi?

Unaandika kwa kufuata mantiki ya kujibizana kwa kumsoma mtu na kumjibu hoja zake?

Au unajiandikia unachotaka wewe tu bila kujibu hoja unayoletewa?
Samahani mkuu nikutoe nje ya mada, hivi nani alikupa jina la kiranga?
 
Wewe unaelewa hata hoja yangu ni ipi?

Au unalalama tu bila hata kutaka kuelewa hoja yangu ni ipi?

Unaandika kwa kufuata mantiki ya kujibizana kwa kumsoma mtu na kumjibu hoja zake?

Au unajiandikia unachotaka wewe tu bila kujibu hoja unayoletewa?
Ndugu zangu,
Kwa kuwa historia ya kweli ya TANU ilifutwa nami nikaja kuiandika huwa naleta yale ambayo wengi hawayajui ili wasibaki ujingani.

Wala huwa siingii katika mjadala kutaka kubishana.
 
hapa kuna hoja mzee mohamed.
 
Unamvika sifa isiyo yake,Shekh Said ni mtu wa kujisifu na kuwasifu watu wa deen yake.

Akikusimulia kuhusu Mwl Nyerere robo tatu ya simulizi zitahusu Wazee wake wa Kariakoo.Robo nyingine zitahusu mihadhara yake yeye halafu page mbili za mwisho atamtia Mwl Nyerere kiduchu.
Huwa anafanya hivyo lakini kamwe hawezi kuuficha ukweli kuwa :-

JK Nyerere was :-

- A born-to be a LEADER

- A Talented LEADER

- An EDUCATOR

- ACADEMICIAN

- A TEACHER

- MWANAHARAKATI MZALENDO ZAIDI

- MKATOLIKI MZURI

Ndio alipokelewa na familia ya akina Mzee Sykes na Waswahili wengine, lakini hawakuwa na Elimu zaidi ya Ilmu Akhera, hawakujua kuzungumza kiingereza, hawakujua management yoyote.

Jiulize tu: kama walikuwa tayari wana uwezo wa Mali na akili kwanini hawakuanza kupigania Uhuru na kumpata Baba wa Taifa kabla ya Nyerere?

Nyerere alizaliwa kuwa kiongozi, alikuwa na kipawa cha uongozi.

Na kwa Bahati nzuri AFRICA na DUNIA inafahamu hivyo.

Wanaofahamu hii Habari ya Mohamed Said ni Wasoma madrasa wa magomeni na Kariakoo na wale wanaosikiliza Redio Imaan na Nur
 
Unajua Ndugu, huyu Mzee ni Mtu wa kujikweza sana, Mdini na pia ni Mtu mwongo na nilishamuainishia uongo wake mara kadhaa hapa jamvini

Aliwahi kusema wakati wa Urais wa B.W Mkapa eti waislam waliokuwepo bungeni ni 2% tu. Mpaka pascal Mayala alipomuumbua

Sasa badala ya TANZIA anatuletea historia yake

There you are,and this is what we are talking about,

Lakin wewe ni wa wapi?inashangaza kutuambia kuwa huyu mzee ni mdini kisa amesimama kuelezea maslahi ya waislam,unadhan kwa kusema hivyo tutajiskia aibu au kuingiwa na ubarid?,usitake kuanzisha mada mpya,tutakesha hapa, wengine sisi mada kama hizi zikija had blood veins zinasisimka, that's our professional...

We love our religion to the extent ya wengine nyinyi kuchukia kias kwamba tunaposimama kuyasema yanayotuhusu mje mchukie na kutupa majina ya kejeli??,nin shida sasa,mna dini yenu na sisi tuna ya kwetu,kwann tukiipenda ya kwetu na kujivunia nyinyi mchukie,si mnayo ya kwenu??

This history will be repeated to be taught untill it's completely learned,chukien au kataeni,lakin ukweli ushawekwa waz,Tena long time ago,kwa sasa kinachofanyika ni kusherehesha tuh,

Alhamdulillah....
 
Wewe unaelewa hata hoja yangu ni ipi?

Au unalalama tu bila hata kutaka kuelewa hoja yangu ni ipi?

Unaandika kwa kufuata mantiki ya kujibizana kwa kumsoma mtu na kumjibu hoja zake?

Au unajiandikia unachotaka wewe tu bila kujibu hoja unayoletewa?
hoja yako haiwezi kueleweka kwasababu hata wewe mwenyewe hueleweki.
 
Innalillah wainailaih rajiuun.

Mfumo kristo ni hatari sana. Huyu mzee ht kutajwa tu
Ulitaka atajwe kuwa anatawadha mara 5 kwa siku?

Ni nani aliyewanyima waislam kumtaja na kumwandika popote pale

Jilalamikieni kwa kukosa Elimu ya kumuandika vitabuni sio Mfumo Kristo

Mlimwandika halafu mfumo Kristo ukawashtaki?

Ninyi ni wa kulialia tu na kulalamika miaka yote

Maamuma.
 
Binafsi nilikuwa sijui km huyu mzee kafariki, nilikuwa naperuzi facebook ndio nikaona post ikisema mzee Sykes ataswaliwa masjid Maamur na kuzikwa kisutu..

Yaani vyombo vya habari vinaandika kwa urefu habari za Sabaya ambaye alikuwa anaongoza wilaya moja tu Tanzania lakini mtu na familia nzima walijitoa katika kuipigania nchi hii uhuru wake ht gazeti moja kumpa front page kuwa mpigania uhuru katutoka hii si sawa.

Sijasikia katika tv,redio japo kutoa taarifa ya wasifu wake katika pumzi yake ya mwisho kuelekea ahera.

Ama kweli Tanzania inaubaguzi mno kwa baadhi ya mambo.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu amsamehe madhambi yake na amweke mahali pema peponi.
Ni kwamba waandishi wa habari wa sasahivi HAWAMFAHAMU wala usiwalaumu waandishi wa habari wa vyombo vya umma

Mbona ninyi Waislam hamjamweka kwenye Front page ya magazeti yenu?

Ona mlivyo WANAFIKI. mbona Redio Nuur na Imaan haijamwelezea mnalaumu nchi kuwa na ubaguzi

MAAMUMA
 
Wewe unaelewa hata hoja yangu ni ipi?

Au unalalama tu bila hata kutaka kuelewa hoja yangu ni ipi?

Unaandika kwa kufuata mantiki ya kujibizana kwa kumsoma mtu na kumjibu hoja zake?

Au unajiandikia unachotaka wewe tu bila kujibu hoja unayoletewa?

Your profile is low,

Mohamed Said hayupo hapa kujibu mashitaka yako au hoja zako ambazo hata hivyo hazina mantiki,

Hoja yako unasema kwamba Mohamed analalamika kuwa wazee wamefutwa kwenye history na kwann yeye anarudia kuwafuta si ndiyo??

Jibu lako ni kwamba,Kwanza Mohamed Said hajalamika,kama kuandika history ya wale wazee na kuweka kumbu kumbu ziwe sawa ni kulalamika basi hiyo ni kwa tafsir ya kwako wewe,hatuna Cha kukusaidia,

Pili,unasema kwamba why anazid kumtukuza nyerere kwenye maandiko yake wakati anawaelezea wazee wake,that's very ridiculous question, nyerere aliish na wale wazee,wale wazee walimpokea nyerere,walimpa hifadh nyerere,walimfadhil nyerere,walifanya mengi na nyerere,walimpenda nyerere siyo kwa kuwa wao ni waislam na nyerere ni mkristo,la hasha Bali kwa kuwa nyerere ni mtanzania,Ambae fikra zake na zao zilikuwa zinafanana,nazo ni kupigania uhuru wa Taifa hili,sasa wanawezaje kuandikwa separately??hata mohamed Said akimtaja nyerere Mara nyingi kuliko wao kunaondoa kitu gan kama na hao wazee wameelezwa pia??

Nin unataka Mohamed Said akujibu,wewe ni wa kuweka malumbano ya hoja na Mohamed Said,huna adabu,wewe ni wa kukaa chini Tena kwa unyenyekevu na kuomba kwa heshima akurudishe darasani
 
Especially if the writer is notoriously known as being aggrieved due to the so called injustice done to his ilk (the Sykes and other Dar/ coastal patricians as well as prominent and seminal old timer do gooders) following some grotesque and deliberate omissions in history by Nyerere and his trapeze act troupe of mandarins, scribes and pharisees in the establishment's literati cabal of unmitigated shameless propaganda fueled by institutional obfuscation and opacity, allegedly especially levelled by the intelligentsia against Muslims.

You are making Nyerere as powerful as some supermassive black hole at the center of the Tanzanian galaxy, everything revolves around him. More than 21 years after his death, this Nyerere phenomenon seems to bend space and time.

Even Abbas Sykes' obituary, by an acclaimed proponent of redressing the shortcomings of orthodoxy history, starts with Nyerere's funeral, and does not progress an inch past this gargantuan Nyerere vortex that sucks everything around it.
kingereza kingi lakini ulichoandika ni pointless
 
Ndugu yangu Mohamed Said,umeweka simulizi nzuri lakini mara zote kama kawaida moyo wako haukubali kama Nyerere alikuwa Rais wa kwanza wa TANU, Tanganyika,Tanzania na CCM.Unaamini kuwa kuna watu wako walistahili,ulitamani leo Hamza (RIP) na Abdul (RIP) ndio wawe wenye kuelezea historia ya nchi hii,unaamini Julius hajui historia ya nchi hii.Ni dhahiri moyo wako unatoa machozi kwani historia haiko kama unavyotaka.Uongozi ni riziki itokayo kwa Mola!
Haswaaa[emoji851][emoji851][emoji851]

Mzee anaumizwa sana na hili. Wakati Nyerere anajifunza a e i o u na ABCD.....Z na kuzungumza lugha ya malkia wao walikuwa wanageuza tu mikeka sakafuni na kukuna nazi

Ndio imeshakuwa sasa. Baba wa Taifa la Tanzania (sio Tanganyika) ni Mwl. Julius Kambarage Nyerere.
 
Nilikuwa Dubai, nilipigiwa simu na BBC kutaka kunihoji hapohapo nilikuwa Tanga nikifuatilia katika TV......

Visa vya kutunga tunga vina shida zake
Huyu Mzee juzi alisema ana Degree ya Historia na ninaweza kumquote, Naomba unisaidie kumuuliza Mohamed Said hili swali:-

1) alisomea Chuo kipi hiyo degree?

2) Alimaliza mwaka gani?
 
Kishindo,
Hapana ndugu yangu sina sababu ya kusema uongo.

Bahati mbaya wewe unadhani hayo ni makubwa si yangu naamua kutunga.

Mie si mgeni wa yote hayo nikae kitako kuyatamani na kuyatunga katika fikra.

Angalia picha niko BBC Glasgow mwaka wa 1991.

Jitulize nisome upya.

BBC walikuwa wanataka kunihoji ugonjwa wa Mwalimu yuko London.

Tanga sasa Mwalimu kesha fariki mimi nafuatilia matangazo ya mapokezi ya mwili wake katika radio siko tena Dubai.

Ukipenda kunifahamu ingia hapa: mohamedsaidsalum.blogspot.com

View attachment 1786755
Kumbe blog, nikajua una Website kabisa kwa miaka yote hiyo

Wanazuoni wa Masjidul na Madrassat mnashindwa kumfungulia Mzee Website bado anatumia Blog

Innallilah wa inna illah Rajiun
 
Huwa anafanya hivyo lakini kamwe hawezi kuuficha ukweli kuwa :-

JK Nyerere was :-

- A born-to be a LEADER

- A Talented LEADER

- An EDUCATOR

- ACADEMICIAN

- A TEACHER

- MWANAHARAKATI MZALENDO ZAIDI

- MKATOLIKI MZURI

Ndio alipokelewa na familia ya akina Mzee Sykes na Waswahili wengine, lakini hawakuwa na Elimu zaidi ya Ilmu Akhera, hawakujua kuzungumza kiingereza, hawakujua management yoyote.

Jiulize tu: kama walikuwa tayari wana uwezo wa Mali na akili kwanini hawakuanza kupigania Uhuru na kumpata Baba wa Taifa kabla ya Nyerere?

Nyerere alizaliwa kuwa kiongozi, alikuwa na kipawa cha uongozi.

Na kwa Bahati nzuri AFRICA na DUNIA inafahamu hivyo.

Wanaofahamu hii Habari ya Mohamed Said ni Wasoma madrasa wa magomeni na Kariakoo na wale wanaosikiliza Redio Imaan na Nur

Usije na kejeli we mgalatia usie na akili, umeskia we nguchiro??

Ukijifanya una kejeli, wengine tuna kejeli zaid yako,

Unaposema wasoma madrasa wa magomeni huko sasa ni kutoka nje ya mada na kukashifu msingi wa iman yetu,

Madrasa ni sehemu takatifu kwetu sisi,usikejeli,that's a place ambapo Qur an hufundishwa,that's a place ambapo maarifa kuhusu Mtume wetu,kipenz chetu Muhammad Hufundishwa,that's a place ambapo civilization yetu sisi waislam Hufundishwa,sasa unapokuja na maneno yako ya kejeli hata kuchamba hujachamba zako asubuh kama hii inabid ujiangalie Sana,

Katika nada hii hakuna sehem hata moja sisi umeona tumeukashifu ukristo wenu we mla Haram,

We as muslims we have been taught to be intelligent,to be Smart,to obey the law,to respect everyone,but if comes someone stupidy like you put your dirty hand On our side we just send you to the cemetery,so mind your tongue
 
Back
Top Bottom