Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
- Thread starter
- #261
Ndugu zanguni hebu someni hii:
MENGI BWANA ABBAS ALINIELEZA NA MENGI BALOZI AMEINGIANAYO KABURINI HAKUNAMBIA
"Tuko kwenye khitma ya Abbas Sykes Msikiti wa Makuti, Kisiwandui Zanzibar niko bega kwa bega na Sheikh Ibrahim Moeva.
Sheikh Moeva na Abbas Sykes wote wametumikia Tanzania nchi za nje na wakifahamiana vyema.
Nimefahamiana na Sheikh Ibrahim Jeddah mwaka wa 1997 na aliyenijulisha kwake alikuwa Balozi Ramadhani Kitwana Dau siku hizo bado hajawa Balozi.
Basi Sheikh Ibrahim akanambia kuwa jamaa wangependa kusikia wasifu wa Balozi Sykes.
Nimeingiwa na hofu hapo hapo.
Kipi kimenitia hofu?
Nimepata uoga kwa kuwa ikiwa kweli nataka kumweleza Abbas Sykes kwa haki ya kumweleza ni lazima nieleze uhusiano wake au uhusiano wao yeye na kaka zake Abdulwahid na Ally na Zanzibar ndani ya chama cha TANU na ASP wakati wa kupigania uhuru wa Zanzibar miaka ya 1950.
Ninatetemeka.
Ishapigwa fatha na khitma zinakusanywa.
Siwezi kukataa kuzungumza.
Lakini najua unyeti wa historia ya Zanzibar.
Ilikuwa kila ninapolileta suala la Zanzibar katika mazungumzo yangu na Bwana Abbas pale Majlis ghafla atakuwa kimya na ataniangalia na "blank face," kama vile sipo pale mbele yake hanioni.
Ali Mwinyi Tambwe alipata kumfukuza mtu nyumbani kwake kwa kumuuliza habari za Zanzibar.
Kipi kilimghadhibisha Ali Mwinyi Tambwe?
Hamza Aziz tukiwa kwenye Majlis yetu yeye alikuwa akiniambia, "Tafiti Mohamed utajua mimi nimekula kiapo mimi nina miaka 74 sasa watanifunga hawa siwezi jela mimi ''raise some dust."
Kwa maneno mengine Hamza Aziz alikuwa ananiambia kuwa hilo somo ninalotaka kusomeshwa na yeye ni somo gumu sana kwa mwalimu na mwanafunzi pia.
Nikasimama kuzungumza.
Nikaeleza maingiliano ya kidugu yaliyokuwapo baina ya wazee wetu Tanganyika na wenzao Zanzibar kiasi cha Sheikh Hassan bin kuwa katika uongozi wa juu wa TAA na kushiriki katika kuasisi TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.
Nikaeleza na yaliyopita bila ya kueleza yale yaliyopita yalikuwa kitu gani.
Hapa nikasimama na kuomba dua Allah awasamehe wazee wetu kwa makosa waliyofanya.
Sikuamini masikio yangu.
Msikiti mzima uliitika, "Amin," kwa sauti ya uchangamfu na ya juu.
Hakika historia ya Zanzibar inataka moyo kuieleza.
Abbas Sykes ndiye aliyekuwa akimpelekea fedha Karume katika mifuko kutoka TANU kusaidia ASP.
Wakati ule Abbas Sykes alikuwa Mweka Hazina Msaidizi wa TANU, Mweka Hazina alikuwa Iddi Faiz Mafungo.
Sijajua kwa nini TANU hawakumtuma Iddi Faiz.
Iddi Faiz Mafungo alikuwa pia ni Mweka Hazina wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika.
Usafirishaji wa fedha hizi ulikuwa siri kubwa na vyombo alivyotumia vilikuwa vya wavuvi.
Abdul Sykes na Dossa Aziz ndiyo walimchukua Nyerere kwendanae Zanzibar kumjulisha kwa Karume.
Inasemekana usiku wa mapinduzi Karume alikuwa amejificha nyumbani kwa Abbas Sykes.
Damu nyingi ilimwagika katika mapinduzi tena bila ya sababu za maana kwani Wamakonde wakata mkonge kutoka Kipumbwi walioingizwa kwa siri Zanzibar kusaidia mapinduzi waliua watu ilhali serikali ya Mohamed Shamte ilikuwa tayari ishaanguka zamani.
Baadhi ya waliouliwa katika mapinduzi na baada ya mapinduzi walikuwa jamaa, ndugu na marafiki wa wazee wetu.
Abbas Sykes alikuwa amehifadhi mengi kifuani kwake.
Baadhi niliyajua."