Hivi humu katika wachangiaji wa JF hakuna madaktari wa binadamu humu? Kuna hali inayoitwa Depression, sijui tafsiri yake kwa kiswahili, hali inayomfanya muathirika kuvuruga mfumo mzima wa kemikali katika mwili wake hivyo kusababisha kupanda kwa Msukumo wa damu (BP), ambayo nayo inasababisha kupanda na kushuka bila mpangilio kwa kiwango cha sukari mwilini!... Depression inasababishwa haswa iwapo muathirika hakupata nafasi ya kutatua msongamano wa mawazo yalokuwa yanamkabili!
Kwa mtizamo wangu naona machungu ya kuvunjika ndoa yake na kunyimwa nafasi ya kujitetea/kujielezea ndiyo chanzo kikuu cha Depression, (kama hiyo ndiyo hali iliyomsibu). Hali hiyo ikimpata mtu mwenye roho ndogo na kutopata msaada wa kitaalamu kwa wakati muafaka, kila gonjwa lilokuwemo na lisokuwemo litafumka, na ndiyo maana wengine huishia kujitundika kitanzi kama sio kunywa dawa ya panya!
Katika nchi zinazokubali dubwana hili "Depression", wamefikia hatua hata ya kuwa na trained psychologists, psychitrists, na Counsellors, wenye mafunzo maalum kuwasaidia watu wenye matatizo hayo!
Kwa wenye Imani, tukumbuke; Kila mtu anazaliwa kwa siku yake, na atakufa kwa siku yake Mw'mungu alomjaalia, kwani hakuna liwezekanalo ila kwa kuwezeshwa na mwenyezi Mungu! Kifo ni kifo tu, ila sababu ya kufa ndiyo inayozua maswali na majibu mengi! Tusiwape kichwa sana hao wanaojitia madaktari wa nguvu za giza, mpaka ikafikia "kunguru kuogopa ubawa wake"! Mwenyezi Mungu ndio mjuzi wa yote, yaliyo dhahiri na yaliyojificha.
Mwenyezi Mungu Ailaze pema peponi Roho ya ndugu yetu Amina Chifupa, Yeye ametangulia, nasi tunafuatia.
Poleni wafiwa, na wote wenye uchungu katika hili, ila mwenyezi mungu anapotupatia kifo ni sawa tu anatukumbusha sote tumo safarini, na aliyemchukua kwanza ndiye aliyempenda zaidi, Kazi ya mwenyezi Mungu haina makosa, tuwe na subira, yeye ndiye hakimu mkuu!