Buriani Hassan Chikusa msomi mkimya

Jili jibu lako ni la kishenzi mno. Hii nchi haina mitaa ya waislamu wala wakristo. Hata huko unapopataja kunaweza kufunguliwa mabucha ya kitimoto na usifanye lolote. Ni vile tu kuheshimiana ila hakuna sheria inayokataza. Ficha upumbavu wako wewe mzee.
 
Mama...
Mimi sioni kama kuandika historia ya uhuru wa Tanganyika na mchango wa Waislam kuwa ni udini.

Udini ni kule kuifuta historia hii na kupachikwa historia ambayo siyo sababu tu historia hiyo imejaa Waislam.

Mimi sijapata kuhisi hata kidogo kuwa sina thamani.
Nina sababu za kusema hili.

Wanaokuja kunijibu wanakuja na matusi na kejeli.
Hii si dalili ya dharau.

(''Jili jibu lako ni la kishenzi mno. Hii nchi haina mitaa ya waislamu wala wakristo. Hata huko unapopataja kunaweza kufunguliwa mabucha ya kitimoto na usifanye lolote. Ni vile tu kuheshimiana ila hakuna sheria inayokataza. Ficha upumbavu wako wewe mzee'').

Mambo kama haya yanasababishwa na husda na wivu.

Husda na wivu ndivyo vilivyosababisha kufutwa kwa historia ya Waislam katika historia ya TANU.

Ushahidi upo.
Kufuta historia ya watu ni uovu uliopitiliza.

Hii ni historia ya kizazi kizima na nilipoandika kitabu cha Abdul Sykes nilianza na historia nyakati za babu yangu Salum Abdallah mwishoni mwa 1800.

Historia hii imechoma hisia za wengi na imefurahisha wengi.

Kitabu changu kimekurejesheni darasani upya si kuisoma historia ya Julius Nyerere peke yake bali kuisoma upya historia nzima ya Tanganyika kuanzia 1900.

Matokeo yake ni haya kuwa kitabu cha Abdul Sykes kimefuta ile historia iliyopenyezwa na ikaaminika kuwa ndiyo ukweli.

Nakueleza kuwa Manzese akiishi mjomba wangu Sheikh Pazi na Shomari Lupindo ni kukufahamisha kuwa Manzese ni kwetu kwa asili.

Heshima yangu inapanda kila uchao ninaponyanyua kalamu kuandika kama hivi.

Vyombo vya habari vya ndani na nje haweshi kunifanyia mahojiano siku zote.

Hivi karibuni nimekamilisha ''documentary'' ya historia ya uhuru na imaenza kurushwa.

Hii ni dalili ya mtu anaedharauliwa na JF na jamii?
Picha hiyo hapo chini nikihojiwa na TBC.

Kipindi kikirushwa mtakiona:

 


''Mji wa Dar es Salaam katika miaka ya 1920 ulikuwa umegawanyika katika sehemu nne: Kariakoo, Gerezani, Kisutu na Misheni Kota.

Sehemu ya ukazi wa asili ilikuwa Kisutu. Kisutu ina msikiti wa zamani kuliko yote katika Dar es Salaam - Msikiti wa Mwinyikheri Akida, unaokaribia takriban miaka mia moja hivi.

Vilembwe wa Sheikh Mwinyikheri hadi leo wangali wakiuhudumia msikiti wa mzee wao na msikiti huo bado uko chini ya uangalizi wao.

Kariakoo ilikuwa sehemu ya kuandikisha wapagazi wakati wa Vita Kuu Vya Kwanza.

Jina lenyewe ëKarikaooí linatokana na jina la Kizungu, ''Carrier Corps.''

Misheni Kota ilikuwa sehemu iliyotengwa makhsusi na Waingereza kwa ajili ya Wakristo.

Wakati ule Wakristo hawakuwa wengi Dar es Salaam, kwa ajili hii walitengewa sehemu yao maalum ya kuishi ili wasichanganyike na Waislam.

Misheni Kota ilikawa sehemu ya kuishi Wakristo kiasi ambacho hata mitaa yake ilipewa majina ya sehemu katika Tanganyika ambako Wamishionari walikuwa wamejipenyeza na kuweka maskani.

Majina ya mitaa kama Masasi, Likoma, Ndanda, Muhonda, Muheza na Magila imedumu hadi sasa.

Hizi ni sehemu ambazo Ukristo ulishamiri.

Misheni Kota ndiyo sehemu pekee katika Dar es Salaam ambapo Wamisionari walifanikiwa kujenga kanisa.

Wakristo walitengewa katika sehemu hii kuwa makazi yao.''

(Kutoka kitabu cha Abdul Sykes).

 
Kwanini wakristo walitengwa eneo lao..kwanini waislamu hawataki kuchanganyika na wakristo.?

#MaendeleoHayanaChama
 
Kwanini wakristo walitengwa eneo lao..kwanini waislamu hawataki kuchanganyika na wakristo.?

#MaendeleoHayanaChama
Wakoloni katika hila zao waliwagawa wananchi ili wapate kuwatawala vyema.

Lakini wazee wetu walikuwa watu wenye akili sana.

Ukisoma historia ya harakati za TANU katika kupigania uhuru utakutana na mengi waliyofanya hawa wazee wangu katika kuwaunganisha wananchi.
Julius Nyerere kisha waunde TANU 1954?

Unajua kwa nini Nyerere ilikuwa lazima akae nyumbani kwa Abdul Sykes Kariakoo na si Mission Kota kwa John Rupia?

Unajua vipi TANU walikivuka kizingiti cha Kura Tatu kupitia mpango uliotengenezwa Tanga kati ya Nyerere, Amon Kissenge, Sheikh Abdallah Rashid Sembe na Mwalimu Kihere?

Unajua kwa nini Sheikh Suleiman Takadir Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU alifukuzwa chama mwaka wa 1958?

Waingereza hawakuwa na ujanja mkubwa hivyo.

Mzee bin Sudi aliiona Tanganyika huru na Tanzania akafa mwaka wa 1972 baada ya kusoma hotuba ya kumkariisha Jaffar Nimeiry ofisi ya TANU Lumumba akiwa na mwenyeji wake Mwalimu Nyerere.


Mzee bin Sudi
 
Sheikh,Mabucha yanayouza nguruwe sasa hivi iwe kavu o roast yapo au hakuna?
 
Utaendaje kuharibu biashara ya watu kisa nguruwe.

Kuna watu wanahitaji kuelimishwa, kwani hii ni nchi ya kiarabu
Myahudi...
Ninaposoma kama hivi najifunza mengi na kukubali ukweli kuwa nyakati zimebadilika sana.

Wakati tunakua Dar es Salaam Wakristo walikuwa wakitaka kuchinja kuku wanampa Muislam kwa kuchelea kuwa Muislam asishindwe kula nyumba ya Mkristo.

Leo mtu anauliza kwani Tanzania ni nchi ya Kiarabu?

Mikutano ya TANU wakati wa kupigania uhuru ilikuwa ikifunguliwa kwa dua na msomaji alikuwa Sheikh Suleiman Takadir.
 
Kwa hiyo tuendelee kuishi kwa mpangilio wa kikoloni kwenye nchi huru?
 
Wewe mzee ipo siku lazima nikulishe kitimoto rost na ndizi mbili ili uache huu udini wako.
 
Hata mm nakubaliana na wewe swala la kuchinja kuku, tilikua tunawapa waislam wachinje ila kwakua umekubalina na mabadiliko basi tusonge mbele pamoja kwa amani
 
Ama kwel sasa mbona hapa sudan karb na royal girrafe hotel kama unaelekea temeke hospital kutokea sudan upande wa kulia kuna msikiti afu kuna uchichoro hapo hapo msikitini ni kama dakika moja tuu kutoka msikitini unakutana na nyumba za wahaya wanajiuza😇🤣🤪🤪
 
Ubarikiwe sana mzee wangu,vitu unavyo tupa hapa ni adimu kwakweli
Amin.
Na mleta mada alikuwa smart. Hakuwa mstari wa mbele katika sakata hilo na hivyo akasalimika.
Kuta...
Haikuwa kuwa uwe mbele ndiyo ukamatwe.

Wala hakuna katika waliokamatwa ambao mimi nilikuja kuzungumzanao waliojuta kwa kukamatwa na kufungwa si katika sakata hili au la Mwembechai.

Kuna historia kubwa sana ambavyo yapaswa kufahamika kwa nini nchi ilifikia pale ilipofika.
 
Assnte. Tunaisubiri kwa hamu hiyo historia ili tuelewe vipi nchi yetu ilifikia pale ilipofika.
 
BURIANI. KWA HAKIKA NI PIGO KUBWA KWA SISI TULIOMFAHAMU KUPITIA MITANDAO NA MAANDIKO YAKE JAPO KWA UCHACHE. NISEME ALIKUWA MTU MUUNGWANA ALIYEHESHIMU KILA MTU. PIA ALIIJUA HISTORIA NA MATUKIO MBALIMBALI YA NCHI HII VYEMA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…