Buriani: Malika wa Mwisho wa Tanganyika, Elizabeth wa Pili wa Uingereza, amefariki dunia

Buriani: Malika wa Mwisho wa Tanganyika, Elizabeth wa Pili wa Uingereza, amefariki dunia

Siwezi kubishana na wewe kwa Sababu unaonekana Hilo vazi la u much know huwezi kuvua pi naomba nikupe ushauri mtu mzima akivuliwa nguo huchutuma na kukusaidia hilo jina CHARLES kuandika CHALE ulikosea ila kwa Sababu hutaki kuabika unashupalia ujuaji.
Chars ukiwa na hela kapuku utaitwa chale

Njoo mtaani kwetu Charles wote ni chale
 
Malika Elizabeti wa Pili

220908114827-01-queen-elizabeth-2015.jpg


Elizabeth Regina

830862-1537871872.jpg


Elizabeth Regina with Julius Kambarage Nyerere of Tanzania. Royal Tour of Tanzania, 1979.





Malika wa Mwisho wa Tanganyika, Elizabeti wa Pili wa Uingereza, amefariki dunia leo Septemba 8 2022 huko Kasri la Balmoral, Uskochi, Uingereza.

Malika Elizabeti amefariki akiwa mtawala aliyetawala Uingereza kwa muda mrefu kuliko watawala wote.
Amekuwa mtawala wa Uingereza kwa zaidi ya miaka 70, kuanzia mwaka 1952. Akiwaandika mawaziri Wakuu 15 Uingereza.

Ni mkuu wa nchi pekee aliyekuwa amesalia aliyewahi kupigana vita vikuu vya pili vya dunia.

Uingereza inafanya siku kumi za maombolezi za kitaifa.

Mwanamfalme Chale anakuwa Mfalme Chale wa Tatu.

Elizabeti wa Pili alikuwa Malika wa kwanza na wa mwisho wa Tanganyika kati ya mwaka 1961 na 1962 kabla Tanganyika haijawa Jamhuri.

Tunamshukuru kwa mema yote aliyofanya na mifano izuri aliyotuachia.

Kwa makosa yake yote tupate kujifunza.
Apumzike kwa AMANI
 
Siwezi kubishana na wewe kwa Sababu unaonekana Hilo vazi la u much know huwezi kuvua pi naomba nikupe ushauri mtu mzima akivuliwa nguo huchutuma na kukusaidia hilo jina CHARLES kuandika CHALE ulikosea ila kwa Sababu hutaki kuabika unashupalia ujuaji.
Mkuu.

Sijaanza mimi leo haya mambo.

Niko hapa tangu namsiliza Paulo Sozigwa anaitangaza Singapore kwa Kiswahili kama Singarpura.

Tangu David Wakati alivyomuita Henry Kiisunger "Kisinja".

Unamjua hata Paulo Sozigwa ni nani? Unamjua David Wakati ni nani?

Nakutajia wazee wako ambao leo hawapo ambao wangeweza kutupa historia nzuri zaidi ya huyu Malika aliyetutoka.

Sipendi kufanya siku ya msiba huu leo izae ubishi mdogo kati yangu nawe.
 
Chars ukiwa na hela kapuku utaitwa chale

Njoo mtaani kwetu Charles wote ni chale
Kwetu wote tumeanza makapuku. Hata hao watoto wa machifu. Na Nyerere mwenyewe kwaweka wote sawa, tuwe na nchi ya watu sawa.

Unaenda Ikulu, unaonea na Nyerere vizuri mpaka unamuomba tausi, na Nyerere asivyo na akili nzuri anakuitia mlinzi wa Ikulu na yeye mwenyewe rais wa nchi anakuahidi kukupa tausi. Mpaka leo namdai tausi wangu mzee yule!

Mpaka kukua kwa kaka Makongoro Charles Nyerere tulikuwa tunaenda sherehe za kwao Ikulu tunamuita "Kaka Mako" au "Kaka Chale".

Muulize Grimey Magombe, mtoto wa marehemu Balozi George Magombe, anazijua parties hizo za Nyerere tulizoenda miaka hiyo ambao tumeijua historia ya Ikulu ya Tanzania kabla hatujazaliwa kwa sababu mama zetu walitembea corridors za Ikulu tangu tuko tumboni na kabla hatujazaliwa.
 
Elizabeti wa Pili alikuwa Malika
Nimejaribu kuhesabu ni mara ngapi umetumia hili neno. Hivi inawezekana kuna 'key' kwenye 'keyboard' inayosababisha hili, au ni 'software' inayotumika?

On the other hand, kuna watu wamenufaika na uwepo wa Commonwealth iliyoshiriki katika kuwezesha kupata wataalam katika nyanja mbalimbali toka nchi zinazoendelea.

Hili litakumbukwa daima kwa shukrani nyingi.
 
Rest In Peace while we are using her soul walahi [emoji2972]
 
Tunaomba mfano wa mema yake aliyotufanyia Tanganyika.
Moja ni hii:
Tanganyika ilipopata uhuru wake ilikuwa haina wataalam (sio wa kutosha bali hakuna kabisa) katika nynja mbalimbali za kitaaluma. Mfuko wa Commonwealth na British Counsil zilisaidia sana kuwapata wataalam hawa.

Sasa pengine swali lako hapa litakuwa ni nani aliyenufaika, nchi au hao waliopewa nafasi. Hilo litakuwa ni swali 'valid' kabisa linalohitaji kujadiliwa kivyake.
 
Nimejaribu kuhesabu ni mara ngapi umetumia hili neno. Hivi inawezekana kuna 'key' kwenye 'keyboard' inayosababisha hili, au ni 'software' inayotumika?

On the other hand, kuna watu wamenufaika na uwepo wa Commonwealth iliyoshiriki katika kuwezesha kupata wataalam katika nyanja mbalimbali toka nchi zinazoendelea.

Hili litakumbukwa daima kwa shukrani nyingi.
Wakati Mfalme Hirohito wa Japan aliyetambuliwa kama Mungu-Mtu na watu wake wa Japan alivyohutubia taifa lake kuwaelewesha kwamba wameshindwa vita viikuu vya Pili Vya Dunia alipolihutubia taifa hilo, kulielewesha kwamba taifa hilo limepigwa kivita na kuliambia taifa lake kwamba amekubali kushindwa vita, watu wengi wa Japan walimsikiliza, lakini wachache sana walimuelewa.

Moja ya sababu nikwamba alitumia Kijapan cha awali sana, cha daraja la juu sana, Wajapani wa kawaida wa muda huo hawakumuelewa.

Umenikumbusha jambo hili, mtoto wa Upanga ninayejua Kiswahili cha Maliki na Malika.

Maliki ni mmiliki wa kiume wa himaya, na Malika ni mmiliki wa kike wa himaya.
 
Pia historia inatuambia kwamba "Shilling" kwa kiswahili "shillingi "ni neno lililotoholewa kutoka lugha ya kiingereza, ambayo kwa wakati huo ilikuwa na thamani karibu sawa na pound ya Uingereza (1 £ = 0.05 shilling). Ilirahisisha sana biashara kati yetu na mataifa yaliyotumia GBP (Great British Pound) Baada ya hapo kutokana na matukio ya vita na sera za kiuchumi wakati huo ndio zikapelekea thamani ya shilingi yetu kuporomoka, Hadi leo hii ( £ 1 = TZS 2675)
 
Back
Top Bottom