Buriani: Malika wa Mwisho wa Tanganyika, Elizabeth wa Pili wa Uingereza, amefariki dunia

Siwezi kubishana na wewe kwa Sababu unaonekana Hilo vazi la u much know huwezi kuvua pi naomba nikupe ushauri mtu mzima akivuliwa nguo huchutuma na kukusaidia hilo jina CHARLES kuandika CHALE ulikosea ila kwa Sababu hutaki kuabika unashupalia ujuaji.
Chars ukiwa na hela kapuku utaitwa chale

Njoo mtaani kwetu Charles wote ni chale
 
Apumzike kwa AMANI
 
Siwezi kubishana na wewe kwa Sababu unaonekana Hilo vazi la u much know huwezi kuvua pi naomba nikupe ushauri mtu mzima akivuliwa nguo huchutuma na kukusaidia hilo jina CHARLES kuandika CHALE ulikosea ila kwa Sababu hutaki kuabika unashupalia ujuaji.
Mkuu.

Sijaanza mimi leo haya mambo.

Niko hapa tangu namsiliza Paulo Sozigwa anaitangaza Singapore kwa Kiswahili kama Singarpura.

Tangu David Wakati alivyomuita Henry Kiisunger "Kisinja".

Unamjua hata Paulo Sozigwa ni nani? Unamjua David Wakati ni nani?

Nakutajia wazee wako ambao leo hawapo ambao wangeweza kutupa historia nzuri zaidi ya huyu Malika aliyetutoka.

Sipendi kufanya siku ya msiba huu leo izae ubishi mdogo kati yangu nawe.
 
Chars ukiwa na hela kapuku utaitwa chale

Njoo mtaani kwetu Charles wote ni chale
Kwetu wote tumeanza makapuku. Hata hao watoto wa machifu. Na Nyerere mwenyewe kwaweka wote sawa, tuwe na nchi ya watu sawa.

Unaenda Ikulu, unaonea na Nyerere vizuri mpaka unamuomba tausi, na Nyerere asivyo na akili nzuri anakuitia mlinzi wa Ikulu na yeye mwenyewe rais wa nchi anakuahidi kukupa tausi. Mpaka leo namdai tausi wangu mzee yule!

Mpaka kukua kwa kaka Makongoro Charles Nyerere tulikuwa tunaenda sherehe za kwao Ikulu tunamuita "Kaka Mako" au "Kaka Chale".

Muulize Grimey Magombe, mtoto wa marehemu Balozi George Magombe, anazijua parties hizo za Nyerere tulizoenda miaka hiyo ambao tumeijua historia ya Ikulu ya Tanzania kabla hatujazaliwa kwa sababu mama zetu walitembea corridors za Ikulu tangu tuko tumboni na kabla hatujazaliwa.
 
Elizabeti wa Pili alikuwa Malika
Nimejaribu kuhesabu ni mara ngapi umetumia hili neno. Hivi inawezekana kuna 'key' kwenye 'keyboard' inayosababisha hili, au ni 'software' inayotumika?

On the other hand, kuna watu wamenufaika na uwepo wa Commonwealth iliyoshiriki katika kuwezesha kupata wataalam katika nyanja mbalimbali toka nchi zinazoendelea.

Hili litakumbukwa daima kwa shukrani nyingi.
 
Rest In Peace while we are using her soul walahi [emoji2972]
 
Tunaomba mfano wa mema yake aliyotufanyia Tanganyika.
Moja ni hii:
Tanganyika ilipopata uhuru wake ilikuwa haina wataalam (sio wa kutosha bali hakuna kabisa) katika nynja mbalimbali za kitaaluma. Mfuko wa Commonwealth na British Counsil zilisaidia sana kuwapata wataalam hawa.

Sasa pengine swali lako hapa litakuwa ni nani aliyenufaika, nchi au hao waliopewa nafasi. Hilo litakuwa ni swali 'valid' kabisa linalohitaji kujadiliwa kivyake.
 
Wakati Mfalme Hirohito wa Japan aliyetambuliwa kama Mungu-Mtu na watu wake wa Japan alivyohutubia taifa lake kuwaelewesha kwamba wameshindwa vita viikuu vya Pili Vya Dunia alipolihutubia taifa hilo, kulielewesha kwamba taifa hilo limepigwa kivita na kuliambia taifa lake kwamba amekubali kushindwa vita, watu wengi wa Japan walimsikiliza, lakini wachache sana walimuelewa.

Moja ya sababu nikwamba alitumia Kijapan cha awali sana, cha daraja la juu sana, Wajapani wa kawaida wa muda huo hawakumuelewa.

Umenikumbusha jambo hili, mtoto wa Upanga ninayejua Kiswahili cha Maliki na Malika.

Maliki ni mmiliki wa kiume wa himaya, na Malika ni mmiliki wa kike wa himaya.
 
Pia historia inatuambia kwamba "Shilling" kwa kiswahili "shillingi "ni neno lililotoholewa kutoka lugha ya kiingereza, ambayo kwa wakati huo ilikuwa na thamani karibu sawa na pound ya Uingereza (1 £ = 0.05 shilling). Ilirahisisha sana biashara kati yetu na mataifa yaliyotumia GBP (Great British Pound) Baada ya hapo kutokana na matukio ya vita na sera za kiuchumi wakati huo ndio zikapelekea thamani ya shilingi yetu kuporomoka, Hadi leo hii ( £ 1 = TZS 2675)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…