Buriani Mzee Ruksa: Ni Deng Xiaoping Wetu wa Mageuzi ya Kiuchumi, Demokrasia, Haki za Binadamu na Uhuru wa Habari. Asante kwa Ruksa Zako, Pumzika!

Buriani Mzee Ruksa: Ni Deng Xiaoping Wetu wa Mageuzi ya Kiuchumi, Demokrasia, Haki za Binadamu na Uhuru wa Habari. Asante kwa Ruksa Zako, Pumzika!

Wanabodi
View attachment 2923058Siku ya leo, tunampunzisha Mzee wetu, Rais Mtaafu wa Tanzania, Mzee Ali Hassan Mwinyi, kwa jina maarufu la Mzee Rukhsa, kwenye nyumba yake ya malalo ya makao ya milele.

Mara ya Kwanza Kulisikia Jina la Ali Hassan Mwinyi.
Kwa mara ya kwanza jina la Ali Hassan Mwinyi, nililisikia mwaka 1977 nikiwa darasa la 3 shule ya msingi, wakati huo akiwa ni Waziri wa Mambo ya Ndani wa serikali ya Nyerere, alipolazimika kujiuzulu kutokana na kashfa ya vifo vya watuhumiwa wawili wa mauaji ya vikongwe, huko Mwanza mwaka 1976.

Mwinyi hakuwa peke yake aliyejiuzulu kutokana na kashfa hiyo, bali Makamo wa pili wa rais na Waziri Mkuu, Rashidi Mfaume Kawawa, pia aliondolewa!, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, anyeshughulikia Usalama wa Taifa, Peter Siyovelwa aliondolewa!. Wakafuatiwa na watendaji wakuu wa vyombo vya usalama Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Emelio Mzena, akastaafishwa kwa manufaa ya umma!, Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Samweli Pundugu akastaafishwa kwa manufaa ya umma, na Kamishna Mkuu wa Jeshi la Magereza pia akapumzishwa.

Mwalimu Nyerere alikuwa sio mtu wa mchezo hata kidogo!, kwani baada ya kuwafagia kule juu, fagio la chuma, likatua mjini Mwanza, likaanzia kumfagia Mkuu wa Mkoa Peter Kisumo, akaenda na maji, RPC wa Mwanza, RSO, OCD, na DSO wa Mwanza, kwanza wote wakafutwa kazi, kisha wakarejeshwa vijijini kwao, kwa kusombwa na Land rover 109 usiku usiku na kurudishwa kwenye their places of domicile na mwisho wa siku walikuwa kushitakiwa kwenye ile kesi maarufu, "Kesi ya Mauaji Mwanza" ya mwaka 1976. Mtu pekee aliyesalimika kati ya hao washtakiwa ni mtu mmoja tuu, aliyeitwa Andrew Mayalla, na salama yake, mdogo wake anayetwa Mathew Kasanga, kumuwekea wakili mahiri wa wakati huo, Wakili Murtaza Lakha, kumtetea kaka yake, lakini wengine wote, walikwenda na maji na walikula mvua za kutosha!. Ni kupitia tukio hilo ndipo nilipoanza kulisikia jina la Ali Hassan Mwinyi. Hiki kisa cha Kesi ya Mauaji Mwanza pia nilikihadithia kwenye bandiko hili TISS Ikanushe tuhuma za uvamizi, utekaji, utesaji na mauaji!. Wasijadiliwe na Bunge kwa uwazi bali wachunguzwe, wakithibitika wafumuliwe!

Sijui uwajibikaji wa aina hii ya enzi za Nyerere, ulikuja kupotelea wapi, siku hizi watuhumiwa wanakufa mikononi mwa polisi, and no body cares!.

Tukio hilo lilileta mageuzi makubwa nchini mwetu, kwanza Idara ya Usalama wa Taifa, ilifumuliwa na kusukwa upya kwa kufanyiwa mabadiliko makubwa, ikaletwa sheria ya usalama wa Taifa, ya 1976, Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976 na katiba mpya ya mwaka 1977.

Jina la Ali Hassan Mwinyi, nikaja kukutana nalo tena shule ya msingi, jijini Dar es Salaam, tukisoma na mtoto wake Hussen Mwinyi (Dr)aliyenitangulia madarasa mawili. Baada ya shule ya Msingi nikajiunga shule ya sekondari ya Tambaza, ile mwaka 1985 Rais Mwinyi anakuwa Rais wa Tanzania, yule mtoto wake Hussein Mwinyi alikuwa anasoma PCB Tambaza! alikuwa darasa moja na mtoto wa Malecela, Seche. Kitendo cha mtoto wa rais na mtoto wa Makamo wa Pili wa Rais na Waziri Mkuu John Malecela kusoma shule moja, na halikuwa jambo dogo!, sasa ndio nikazidi kumfahamu Ali Hassan Mwinyi kwa karibu, wakati huo hapo Tambaza pia tuko na mtoto wa Nyerere na Mtoto wa Mkapa, darasa moja.

Mwanzo wa Mwinyi Kutwa Mzee Ruksa.

Wakati Mwinyi anachukua urais ile 1985, hali yetu ya Uchumi ili dhollfu bin taaban, baada ya vitavya Kager ana Mwalimu Nyerere kutangaza miezi 18 ya kufunga mikanda, mambo kiukweli yalikuwa magumu, tumekula unga wa Yanga, kutoka Marekani ambao kule kwao ni chakula cha mifugo!, Watu wamevaa magunia, sandarusi hadi sisi wanafunzi nchi nzima tumevaa uniforma ya kitambaa cha madurufu, ambacho nip amba chafu ya kutupa!.

Mahitaji muhimu yote ni kwa resheni kupitia maduka ya kaya, tulikuwa tunapanga foleni siku nzima kusubiria kuuziwa kilo mbili mbili za sukari, hivyo Watoto wote mnatumwa, ili kuwahi foleni, watu walidamka asubuhi na kupanga mawe, gari linaweza kuja saa 10 jioni au siku nyingine kutoka bila bila, haliji kabisa.

Nchi za mabeberu zilimpa Mwalimu Nyerere masherti magumu ya kutupa misaada, ndipo Mwalimu akaamua kuliko kukubali misaada ya masherti na kugeuka nyuma akageuka jiwe, bora aachie ngazi, kwa mtindo wa kung’atuka na kumpisha Ali Hassan Mwinyi. Hivyo Mwinyi aliipokea nchi ikiwa kwenye dhiki kubwa!.

Baada ya ya kuingia rais Muislamu, kukaibuka vikundi vya Waislamu wenye siasa kali, kwanza waligomea Nguruwe wasichinjiwe mahali pamoja, na wanyama wengine kwasababu nguruwe ni haramu kwa Waislamu,
na isiuzwe bucha zile zile za nyama ya kawaida.

Vikundi hivyo vikaleta vurugu za kulazimisha nyama ya nguruwe ipigwe marufuku kwasababu ni haramu, na kuanzishwa mihadhara ya kashfa, kwa wanazuoni wa Kiislamu kuikosoa Biblia na kusema nguruwe hata kwenye Biblia ni Haramu. Vurugu hizo zikapelekea kuvamia mabucha ya nguruwe na kuvunja kisha kukimbilia kujificha misikitini kulikopelekea vurugu za Msikiti wa Mwembecha miaka kadhaa baadae.

Rais Mwinyi akatangaza rukhsa mtu yoyote kula kitu chochote, hakuna ruhusa ya mtu mwingine yeyote kuingilia uhuru wa mtu wa dini nyingine yoyote kula chochote, “Ruksa” na huo ukawa ndio mwanzo wa kuitwa Mzee wa Ruksa, wale wahuni kwa kisingizio cha dini walishughulikiwa kikamilifu, ikiwemo Msikiti wa Mwembechai Kuvamiwa, tena ikatokea mmoja wa wana vuguvugu hawa ni mshikaji wangu sana wa deski moja sekondari ya Tambaza, akiitwa Hassan.

Baada ya kuzifungulia hizo ruksa, alikuja kufungulia ruksa nyingine nyingi za biashara, Uchumi, akaruhusu mitumba, akaruhusu Chai Maharage, akalipindua Azimio la Arusha lililoweka miiko ya uongozi na kuleta Azimio la Zanzibar ambalo liliruhusu viongozi kufanya biashara na kumiliki mali na hapa sasa ndio viongozi wa umma wakaanza kuwa matajiri na kuupindua uchumi wetu kutoka uchumi wa kijamaa na kuingia kwenye uchumi wa kibepari wa nguvu ya soko, market economy.

Ruksa nyingine kubwa Rais Mwinyi aliyotuachia ni ruksa ya mfumo wa vyama vingi vya siasa nchini Tanzania kiasi kwamba sifa ya Baba wa demokrasia Tanzania inamstahili kabisa!, Mwinyi ndie Deng Xioping wetu!.

Japo Rais Mstaafu, Ali Haasan Mwinyi, Mzee wa Rukhsa, ametutoka kwa kutangulia mbele ya haki, huku nyuma Watanzania tunaendelea kuzifaidi rukhsa zake, tutanzienzi milele, na tena sio tuu ametuachia Rukhsa, pia ametuachia na kale ka copy pale Zanzibar!, cha mtu rahimu kama yeye!.

Akina sisi, tayari tumeisha mshauri Mama, kama hoja Hivyo kama HII sauti ni sauti ya kweli, na kama vipi 2025, ataona ni parefu, hakuna ubaya, akikapisha kale ka Copy kule kaje huku kutufungulia ruksa nyingine zote zilizobakia!.

Buriani Ali Hassan Mwinyi, Mwendo Umeumaliza.

inna lillahi wa inna ilayhi rajiun
(إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّ إِلَيْهِ رَاجِعُونَ‎)

Paskali.
Kaka Paskali kwa heshima na taadhima swala Mwembe chai halihusiani na Mwinyi lilitokea 1998 kipindi cha Mkapa, watu wameumizwa pale kwa dhulma si sawa kusema hivi kwa kebehi.
 
Maisha yalikuwa yanatisha sana

Leo viatu vya plastic vimejaa kariakoo hata kama vinaisha mapema lakini vimesaidia watu wengi

Leo kariakoo zimejaa nguo feki za kusukuma siku hata kama zinachakaa mapema zinasaidia

Nchi imetoka mbali sana ,Mnaenda kutafuta mafuta ya taa ,Leo mafuta ya taa yatakuwa yamebaki vijiji vichache sana

Usiku ni mwendo wa tochi tu ukiwa unatembea barabarani,Maana nyumba nyingi hakuna umeme

Radio ni moja tu ya kusikiliza,Taarifa ya habari wazee wanakuwa makini kusikiliza na wako punctual sana na muda
Lakini watu walikuwa wanaishi peaceful !
Tena very happy !!
Au nasema uongo ndugu zanguni wahenga wenzangu ???!!!

Vijana wengi wamekaririshwa !!
Lakini ukweli utabaki palepale !
Leo kila kitu kipo lakini hawana peace of mind completely 😅😅😅🙏🙏 !
Maisha ni Rangilangire !
Enzi zile tulienjoy sana 😅🙏🙏
 
Kiranga

Mama yangu aliniambia baba yako alifuatwa na usalama wa taifa nyumbani na wakaondoka naye kisa anaonekana tu ana maendeleo fulani.

Na hicho kipindi mzee alitaka kununua gari, mama anasema na laiti angelikuwa ameshalinunua halafu usalama ndiyo wamemdaka hali ingekuwa mbaya kwa baba yenu.

Kwa sababu kuna ndugu yetu mmoja alifilisiwa na alikamatwa kabisa na aliwekwa ndani. Walichimbia hela nyengine chini ya ardhi ili wasionekane wana visenti angalau.
Nakumbuka mzee alitoka ulaya alikuja na gari ilibidi gari tuliokuwa nalo tuliuze kwanza, Tumevaa kunfu shoes, chacha cha ugali wa yanga, kupanga foleni duka la ushirika na wauza sigara barabarani eti wana kamatwa eti wahujumu uchumi!
 
Back
Top Bottom